Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

Kwa hiyo kwa maoni ya "wananchi walio wengi" walitaka "Nchi 3," "Territory 3," au unataka kusema nini hasa? Au definition yako inatusaidiaje kujua maoni ya wananchi yalilenga nini?
Acha kuruka ruka. Soma post zangu vizuri.
Walitaka muungano unaofuata mfumo wa serikali tatu, ya Tanganyika, ya Zanzibar na ile ya Muungano. Kimsingi nchi zipo mbili - Tanganyika na Zanzibar. Ukiunganisha hizo nchi mbili unapata "dhana" ya nchi ya tatu kubwa. Kwa hivyo, kwa mambo yasiyo ya muungano, serikali ya Tanganyiaka itakuwa na mamlaka eneo (nchi) ya Tanganyika, serikali ya Zanzibar itakuwa na mamlaka eneo la Zanzibar na serikali ya muungano itakuwa na mamlaka kwa mambo ya muungano katika eneo lote linalojumuisha eneo la zanzibar na eneo la Tanganyika (nchi ya Tanzania).

Ukisema unataka uwepo wa serikali ni lazima uweze kupambanua eneo (nchi) ambalo serikali hiyo itakuwa na mamlaka. Kwa hivyo kama wananchi wamesema wanataka serikali tatu, mantiki inadai kupambanua maeneo ambayo serikali hizo zitakuwa na mamlaka.

"Waumini" wa serikali mbili, bahati mbaya sana hawatoi takwimu ni wananchi wangapi waritaka muundo huo (achilia mbali muungano wenyewe) wakati muungano unaasisiwa. Angalau hawa waumini wa serikali tatu (hata kama ni "wachache") tunaweza kuwatambua mmoja mmoja na hata kupitia taasisi zao kutokana na maoni waliyoyatoa kwa tume ya Warioba.

Kama hoja zimekwisha katika hili, anzisha mjadala mwingine:
 
Kwa jinsi Warioba alivyolichukulia suala hili ni kama la kwake, hiyo kwa sababu ameendelea "kuiwakilisha" Tume hata baada ya kuvunjwa!! Labda anataka kugombea Urais wa Tanganyika, who knows? Na kwa uzoefu nilio nao kuhusu viongozi wa nchi hii, ukiona mtu anakomalia sana jambo ujue liko jambo!
Lets agree to disagree
 
Kwa upande wangu mimi niliiona Hotuba ya Rais Kikwete kama angalizo badala ya msimamo au amri, ndio maana aliwaambia Wajumbe kuwa "mamlaka mnayo nyinyi!" Still watu wana uwezo wa kumpinga Kikwete kwa manufaa ya umma, kama wanavyodai! Ndio maana Kikwete alisema kuwa kama tunataka Serikali 3 basi ziwe imara, je hapa kosa la Kikwete ni lipi? Hata kama asingeonesha msimamo Bungeni, still Sera ya CCM kuhusu Serikali 2 inajulikana! Ni chama gani ambacho hakitaki Sera yake kufanyiwa kazi? Obviously hakuna, kwa hiyo hakuna wa kumlaumu mwenzake! Ndio maana UKAWA wako busy, si kutetea maslahi ya wananchi kama wanavyodai bali ni kucomply na sera zao!

Mkuu wewe sii mgeni na siasa za nchi hii, unajua kwa nini chama cha mapinduzi kilipigania kwa nguvu ya ajabu kuhakikisha kuna kuwa na kura ya wazi? Ni ili kuhakikisha amri iliyotolewa na JK inatekelezwa na anayekwenda kinyume na hilo au sera ya chama anashughulikiwa.
Ingekuwa sera za vyama ndio zinafuatwa kulikuwa na haja gani kuwa na majadiliano mle ndani? Hayo majadiliano yanafanyika ili wajumbe watafakari na wakati mwingine kubadili msimamo kabla ya kura kupigwa.
Naona niachie hapa kwa sasa, ila ni msimamo wangu kuwa hotuba ya ufunguzi na mkakati uliopo sasa wa kumtukana (nasema ni mkakati mahsusi) Mhe Warioba badala ya kuchambua hoja zake ndio sababu za kufanya kazi hii ionekane ngumu na ya hovyo.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Tuko pamoja Mkuu, lakini kwa bahati mbaya Rasimu hii haidumishi Muungano bali imeufanya si kitu kabisa, angalia ADDITIONAL 2 hapo kwenye Post ya Kwanza hapo juu! Kumbuka maneno ya JK kuwa hata kama tunataka Serikali 3 zisiwe tegemezi wala egemezi! Tusiishie kuwa tunataka Serikali 3 tu basi, wanaojadili zaidi wanaonekana kuwa hawataki kudumisha Muungano!!

Ni kazi ya Bunge kuipa Uhai Serikali ya JMT kama ambavyo inafanyika sasa. Hayo mengine yote ni bla blah, Tanganyika is on the way back. Hata watu walete porojo, propaganda, vitisho lakini ukweli uta prevail. Nchi iliyopiganwa na babu zetu vita vya majimaji haiwezi kufutwa kirahisi tu bila kuliliwa na wajukuu. Tanganyika is back!
 
Acha kuruka ruka. Soma post zangu vizuri.

Kama hoja zimekwisha katika hili, anzisha mjadala mwingine:

A simple question that needs a simple answer: Je, mamlaka yenye eneo lazima iitwe "nchi?"YES or NO?
 
Ukianza kueleza neno baada ya neno kwenye rasimu hatutaelewana kwa maana tutafika sehemu na kusema kuwa kwa Kizaramo tunasema hivi while Kikurya ni hivi! Cha msingi hapa ni kuwa kama kuna Zanzibar yenye mamalaka kamili ndani ya Muungano basi na mshirika wake (i.e. Tanganyika/'tz bara') iwe vivyo hivyo.
Je, na hilo halieleweki!?
 
A simple question that needs a simple answer: Je, mamlaka yenye eneo lazima iitwe "nchi?"YES or NO?
Nchi sio mamlaka. Hiyo ni dola. Eneo la mamlaka hiyo ndio "nchi". Unaweza kuwa na "nchi" ambayo haina dola....kama ilivyowahi kuwa Somalia wakati fulani. Huwezi kuwa na dola ambayo haina nchi. Unaweza kukubuka yaliyotoka USSR. Dola ilibaki bila nchi na hivyo kufa.
 
Sijakataa kuwepo kwa hiyo Tanganyika yenu mnaoililia utafikiri itawaongezea fedha mifukoni kumbe mtashtukia ufisadi uko pale pale hauogopi neno Tanganyika, nazungumzia maoni ya wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 3?
Kwani kutokuwepo kwa Tanganyika ndio kumekuongezea hela?
 
Mimi nazungumzia maoni ya Wananchi, ni lini walisema wanataka Nchi 3, hayo maswali yako yanaingiaje hapa?

Upotoshaji hauwezi kuhalalisha serikali mbili ambayo CCM inataka tofauti na mapendekezo ya seikali tatu ambayo yametolewa na kamati ya kukusanya maoni ya wananchi ya katiba mpya.

Kamati ya Warioba imetoa taarifa ya wazi kuwa wananchi walipendekeza serikali 3. Hii inatokana na Zanzibar kujiita nchi katika katiba yake ya mwaka 2010 hivyo kuvunja katiba ya Tanzania ambayo inasema Tanzania ni nchi moja. Warioba alifafanua kuwa kwa vile Zanzibar imejiita nchi, basi Tanzania si nchi moja tena bali ni nchi mbili ya Zanzibar na Tanganyika. Akasema kuwa ukishakuwa na nchi mbili huwezi kukwepa kuwa na serikali tatu, yaani Jamuhuri ya watu wa Zanzibar na serikali ya Jamuhuri ya Tanganyika na ya tatu ni ya Muungano.

Hakuna sehemu ambako tume ya Warioba imewasilisha maoni ya wananchi yanayopendekeza nchi tatu, bali tume imependekeza mambo yawe wazi zaidi yaani nchi mbili, serikali tatu. Ni upotoshaji kusema tume ya warioba imependekeza nchi tatu.
 
Nchi sio mamlaka. Hiyo ni dola. Eneo la mamlaka hiyo ndio "nchi". Unaweza kuwa na "nchi" ambayo haina dola....kama ilivyowahi kuwa Somalia wakati fulani. Huwezi kuwa na dola ambayo haina nchi. Unaweza kukubuka yaliyotoka USSR. Dola ilibaki bila nchi na hivyo kufa.

Kabla ya Zanzibar kuwa "nchi" ilikuwa na dola, right?
 
Kabla ya Zanzibar kuwa "nchi" ilikuwa na dola, right?
Right, Zanzibar haikuwa nchi, na Tanganyika haikuwa nchi. Nchi ilikuwa moja tu, yaani Tanzania, yenye Serikali mbili, ya Zanzibar na Tanzania.
 
Kabla ya Zanzibar kuwa "nchi" ilikuwa na dola, right?
Right, Zanzibar haikuwa nchi, na Tanganyika haikuwa nchi. Nchi ilikuwa moja tu, yaani Tanzania, yenye Serikali mbili, ya Zanzibar na Tanzania. Baada ya Zanzibzar kujiita nchi (kwa kuvunja katiba ya muungano inayotambua nchi moja) unakuwa na nchi mbili ya Zanzibar na Tanganyika. Katika hali hii huwezi kukwepa serikali 3, ndiyo wananchi walivyopendekeza.
 
Kwa jinsi Warioba alivyolichukulia suala hili ni kama la kwake, hiyo kwa sababu ameendelea "kuiwakilisha" Tume hata baada ya kuvunjwa!! Labda anataka kugombea Urais wa Tanganyika, who knows? Na kwa uzoefu nilio nao kuhusu viongozi wa nchi hii, ukiona mtu anakomalia sana jambo ujue liko jambo!
kama vile mnavyo komalia serikali mbili?
 
Kabla ya Zanzibar kuwa "nchi" ilikuwa na dola, right?
Zanzibar haikuwahi kutokuwa nchi (kwa muktadha wa mjadala huu). Dola haiwezi kusimama bila kuwepo nchi.
 
Kikwete alimshambulia Warioba binafsi, pia Shivji kamshambulia Warioba binafsi, kwa kumtajia jina binafsi si kama tume iliyowasilisha maoni ya wananchi. Ndiyo maana analazimika kujibu matusi. Kwenye semina ya Shivji kwa vijana wa CCM iliyopachikwa jina la kongamano la vyuo vikuu, Warioba ametukanwa binafsi kuwa amesalia kuishi miaka kumi tu. Shivji aliyabariki mashambulizi hayo ya wana CCM.
 
kama vile mnavyo komalia serikali mbili?
Hapana mkuu mimi sijakomalia Serikali 2, ila kwa Rasimu hii isiyoeleweka afadhali "shetani unayemjua kuliko malaika usiyemjua!"
 
Back
Top Bottom