Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

je zanzibar ni nchi au serikali? Ukiwa na jibu la swali hili na swali lako litakuwa lishajijibu.

Mimi nazungumzia maoni ya Wananchi, ni lini walisema wanataka Nchi 3, hayo maswali yako yanaingiaje hapa?
 
Mimi nauliza juu ya maoni ya "wananchi walio wengi!" Je, walitaka "Nchi 3" au "Serikali 3?" Hayo ya mizinga yaanzishie Topic yake tutachangia!

Wewe kweli kichwa Boga. Hapo juu kwenye mabano ya kuwasilisha hoja tayari umefafanua kwamba nchi mbili washirika ni ( Tanganyika na Zanzibar), alafu mbele tena unauliza nchi tatu. Sasa unataka kujifanya mawazo yako ni timamu kuliko maoni ya wananchi walio wengi? BTW typing error zipozipo kwenye hiyo rasmu sikumbuki ni ibara gani lakini my point hapa ni kwamba kama iliandikwa nchi tatu ni typing error zinarekebishika.
 
Mtoa hoja mpka sasa akili yake haina akili ya kutambua kuwa NCHI za Tanganyika na Zanzibar ndio zilizoungana, na kuwa Tanzania, na lengo ilikuwa ni kuanza na serikali mbili kuelekea moja, sasa kuna nchi mbili ndani ya nchi moja, zilozoungana, that means rais mmoja hana wawakilishi katika nchi nyingine, mfano: Rais wa JMT anateua wakuu wa mikoa wa Tanfanyika tu, wakati rais wa SMZ anateua wakuu wa mikoa wa Zanzibar, sasa ha wakuu wa mikoa wa Tanganyika ndio wanajiita wa Tanzania, vituko vitupo!!, sasa elewa kuwa kuna haja ya Tanfanyika
 
Tunataka serikali mbili siyo vinginevyo hatutaki mpasuko kwenye taifa letu kwa sababu ya uroho wa madaraka.
Kama hautaki mpasuko dai nchi moja na serikali moja,mbona tayari znz tayari wamejitenga!
 
Buchanan Basi mkuu kama neno nchi linakupa taabu mahali popote palipoandikwa "nchi" weka neno "mbingu"

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Sio linanipa taabu. Kama "wananchi walio wengi" hawakutaka "Nchi 3" bali "Serikali 3, huoni hapo kuna tatizo? Acha kejeli ndugu!
 
Mtoa hoja mpka sasa akili yake haina akili ya kutambua kuwa NCHI za Tanganyika na Zanzibar ndio zilizoungana, na kuwa Tanzania, na lengo ilikuwa ni kuanza na serikali mbili kuelekea moja, sasa kuna nchi mbili ndani ya nchi moja, zilozoungana, that means rais mmoja hana wawakilishi katika nchi nyingine, mfano: Rais wa JMT anateua wakuu wa mikoa wa Tanfanyika tu, wakati rais wa SMZ anateua wakuu wa mikoa wa Zanzibar, sasa ha wakuu wa mikoa wa Tanganyika ndio wanajiita wa Tanzania, vituko vitupo!!, sasa elewa kuwa kuna haja ya Tanfanyika
Hayo unayoyasema yanajibu swali kwamba "wananchi walio wengi" walitaka "Nchi 3" au la?
 
Wewe kweli kichwa Boga. Hapo juu kwenye mabano ya kuwasilisha hoja tayari umefafanua kwamba nchi mbili washirika ni ( Tanganyika na Zanzibar), alafu mbele tena unauliza nchi tatu. Sasa unataka kujifanya mawazo yako ni timamu kuliko maoni ya wananchi walio wengi? BTW typing error zipozipo kwenye hiyo rasmu sikumbuki ni ibara gani lakini my point hapa ni kwamba kama iliandikwa nchi tatu ni typing error zinarekebishika.
Sasa kama unakiri ni typing error kichwa changu kimekuwaje boga? Uwe unarudia kusoma kabla ya kupost ili angalau kuwe na consistency/logic!
 
Sijakataa kuwepo kwa hiyo Tanganyika yenu mnaoililia utafikiri itawaongezea fedha mifukoni kumbe mtashtukia ufisadi uko pale pale hauogopi neno Tanganyika, nazungumzia maoni ya wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 3?

Kijana nadhani ww ni diaspora au ni mkimbizi unajua Tanganyika ikirudi huna chako. Kama Zanzibar bado ipo hai na inaimarika iweje Tanganyika ipotee katika historia? Lazima tuirudishe Tanganyika yetu.
 
Je, "wananchi walio wengi" walisema wanataka "Nchi 3" au "Serikali 3?"
 
Mimi nauliza juu ya maoni ya "wananchi walio wengi!" Je, walitaka "Nchi 3" au "Serikali 3?" Hayo ya mizinga yaanzishie Topic yake tutachangia!

Huwezi ukawa na serikali ambayo haina nchi, na huwezi ukawa na nchi ambayo haina serikali.Ndiyo maana tunataka serikali ya Tanganyika mbayo itafanya kurudishwa kwa nchi ya Tanganyika
 
Nchi Washirika ni Nchi, as simple as that! Otherwise zingeitwa Serikali Washirika!

Context ya "ushirika" umeielewa? Muungano usingepatikana bila ya "ushirika" wa nchi zilizo ungana. Kwa nini Zanzibar itambulike kuwepo kwake na Tanganyika isiwepo? Inaingia akilini kweli?
 
Mnaompinga Warioba na mnaopinga maoni ya wananchi imekura kwenu.Tanganyika ilikufaje Zanzibar ikabaki?
Swali ni kwamba Wananchi wanataka nini exactly, sio nini kilitokea kuhusu unachodai kuwa Tanganyika ilikufaje!
 
Ngoja nikupe tofauti ya nchi na serikali,
1) nchi lazima iwe na mipaka onayotabulika kimataifa, serikali ni mipaka ya ndani kama serikali za vijiji na mitaa
2) nchi razima iwe na uraia, kama passport documents, vitambulisho nk. Serikali haina
3) nchi lazima iwe na bendera yake ya kuitambulisha kimataifa,
4) nchi lazima iwe na wimbo wa taifa inaojitambulisha kimataifa,
5) nchi lazima iwe na kiongozi wake anatetambulika kimataifa, mf. Rais, waziri mkuu, mfalme au hata malkia
 
Asili yangu nimezaliwa Tanzania sio Tanganyika! Pia zaidi ya 90% ya wananchi wote wamezaliwa baada ya Muungano, 10% tu ndio walioonja Utanganyika!

Kwa hiyo hiyo 10% sio raia halali kwa vile Tanganyika imeuwawa? Hiyo hoja ni ya kitoto sana. Hayo ni majina tuu. Kama vile mkoa wa Kagera ulivyokuwa ukiitwa Ziwa Magharibi zamani na usijekuta baadae ukaitwa Kaitaba.
Hivyo Tanzania au Tanganyika ni majina tuu, ukirudisha jina la zamani haibadili maana.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Context ya "ushirika" umeielewa? Muungano usingepatikana bila ya "ushirika" wa nchi zilizo ungana. Kwa nini Zanzibar itambulike kuwepo kwake na Tanganyika isiwepo? Inaingia akilini kweli?
Ndio "maoni ya wananchi walio wengi" au ni maoni yako binafsi? Je, wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 3? BTW Zanzibar kabla ya Marekebisho ya Katiba mwaka 2010 Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ilisomeka kuwa Zanzibar ni Sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani hapo hakukuwa na "ushirika" mpaka ziitwe "Nchi Washirika?"
 
Ngoja nikupe tofauti ya nchi na serikali,
1) nchi lazima iwe na mipaka onayotabulika kimataifa, serikali ni mipaka ya ndani kama serikali za vijiji na mitaa
2) nchi razima iwe na uraia, kama passport documents, vitambulisho nk. Serikali haina
3) nchi lazima iwe na bendera yake ya kuitambulisha kimataifa,
4) nchi lazima iwe na wimbo wa taifa inaojitambulisha kimataifa,
5) nchi lazima iwe na kiongozi wake anatetambulika kimataifa, mf. Rais, waziri mkuu, mfalme au hata malkia
Kwa hiyo hoja yako ni ipi hapa?
 
Kwa hiyo hiyo 10% sio raia halali kwa vile Tanganyika imeuwawa? Hiyo hoja ni ya kitoto sana. Hayo ni majina tuu. Kama vile mkoa wa Kagera ulivyokuwa ukiitwa Ziwa Magharibi zamani na usijekuta baadae ukaitwa Kaitaba.
Hivyo Tanzania au Tanganyika ni majina tuu, ukirudisha jina la zamani haibadili maana.

Sent from my iPad using JamiiForums
Mkuu hapa sio Jina pekee bali kuna move ya kuvunja nchi yetu vipande vipande!
 
Ndio "maoni ya wananchi walio wengi" au ni maoni yako binafsi? Je, wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 3? BTW Zanzibar kabla ya Marekebisho ya Katiba mwaka 2010 Ibara ya 1 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ilisomeka kuwa Zanzibar ni Sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwani hapo hakukuwa na "ushirika" mpaka ziitwe "Nchi Washirika?"

Wewe unaendeleza ubishi usio na maana.......kwa heri bwana!
 
Back
Top Bottom