Utanganyika umepofusha sana akili za watu!
Walioba anachekesha sana ndani ya rasimu yake yapo mambo mengi anajipinga yeye mwenyewe mzee waajabu sana huyu.
tume ya warioba haikuwa inachukua idadi bali uzito wa hoja kwakuwa muda ulikuwa mdogo wa kuchangia dk.3 na ndiyo maana mwenzio akishazungumzia muungano sisi wengine tunazungumzia mambo mengine lakini mkitaka rejea ipo rejea tume ya nyalali,ya kisanga ya shelukindo n.k.
Asili yangu nimezaliwa Tanzania sio Tanganyika! Pia zaidi ya 90% ya wananchi wote wamezaliwa baada ya Muungano, 10% tu ndio walioonja Utanganyika!
Nadhani huyu Mjita ana uhaba wa msamiati wa kiswahili! Wananchi wanataka "Serikali 3", "Majimbo 2 ya Tanganyika na Zanzibar" na "Nchi 1"!Mimi nauliza juu ya maoni ya "wananchi walio wengi!" Je, walitaka "Nchi 3" au "Serikali 3?" Hayo ya mizinga yaanzishie Topic yake tutachangia!
Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba,
Ulitueleza kuwa "wananchi walio wengi" walitaka Serikali 3, japokuwa Takwimu zenyewe nazo zina ukakasi mwingi! Hatujasikia kuwa ukilieleza Bunge wakati wa kuwasilisha Rasimu kuwa "wananchi walio wengi" wakitaka "Nchi 3!"
Sasa hayo ya "Nchi 3" umeyapachika kwenye Ibara ya 64 (1) ya Rasimu uliyatoa wapi?
Au kwako "Nchi" na "Serikali" ni kitu kile kile ukiamini tu wananchi 37,000 waliotaka "Serikali 3" walimaanisha "Nchi 3?"
Nilishaanza kuamini kuwa hakuna wanaotaka kuelewa kwenye Jukwaa hili kumbe wapo tele, hongera sana kwa kuielewa mada hii ndugu yangu Ileje! Kama wananchi walitaka Serikali 3, hayo ya Nchi 3 si kuuziana mbuzi kwenye gunia?Nadhani huyu Mjita ana uhaba wa msamiati wa kiswahili! Wananchi wanataka "Serikali 3", "Majimbo 2 ya Tanganyika na Zanzibar" na "Nchi 1"!
jamani mbona tunapotosha kauli za watu!je ni lini walioba alisema watanzania wanadai nchi tatu...kwa akili ya kawaida hiyo nchi ya tatu inatoka wapi wakati nchi zilizopo ni mbili tu...tuliomsikia walioba alisema kwamba wananchi walio wengi wanataka selikali tatu jambo ambalo linawezekana katika muungano wa nchi mbili,na alipendekeza wakuu wa nchi hizo mbili wawe ni mawaziri wakuu na rais wa muungano awe ni mmoja na awe na nguvu ya kusimamia mambo ya muungano tu...harafu mtu anapokuwa anafanya research lazima awe na sample size.hawezi kuwahoji watanzania wote lazima atumie wawakilishi wa hao watanzania na kuwatengenezea asilimia..kwa hiyo mtu anaposema ni watu 37000 tu ndio walitaka selikali tatu lazima ajiulize ni wangapi walihojiwa ,na hao waliohojiwa ni wangapi walitaka selikali mbili au moja au tatu,na ni asilimia ngapi ya jumla ya watu waliohojiwa..(kwa kifupi unatakiwa ulijue somo la research kwanza na sio kuongea kishabiki)
Ukishamaliza hasira ulizo nazo rudi kwenye mada, ni lini "wananchi walio wengi" walitaka "Nchi 3?" Kama hawakuwepo Warioba kwa nini aliamua kuliingiza kwenye Rasimu?Ungekuwa karibu ningekuchapa bakora. Wewe huoni uongozi wa sasa hivi sio ule wa Nyerere? Wewe hujui kwamba sasa hivi Zanzibar ni nchi inayojitegemea? Hujui huwezi kuingia tena Zenj kama zamani? Awamu ya nne iliachia Wa-visiwani wakatengeneza katiba yao kwa hiyo wao ni nchi kamili.
Wao wanataka muungano wa mkataba au wa maridhiano na bara. Bara ni nchi ya pili ktk muungano hiyo nchi ya tatu unayosema iko mahali gani au ni Zimbabwe ya Mh Mulugo?
Muungano wa serikali mbili ni viongozi wa nchi kufutilia mbali walichoandaa Zanzibar hapo ndipo itawezekana kuendelea na serikali mbili.
Kuzaliwa baada ya muungano haina uhusiano wowote na yanayotokea sasa hivi kwani Tanzania bara aka Tanganyika itabakia ilivyo hadi mwisho wa dunia huna haja ya kuita nchi hii Tanganyika inaweza kuitwa hata Nyerere au Azania na maisha yakasonga mbele.
Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba,
Ulitueleza kuwa "wananchi walio wengi" walitaka Serikali 3, japokuwa Takwimu zenyewe nazo zina ukakasi mwingi! Hatujasikia kuwa ukilieleza Bunge wakati wa kuwasilisha Rasimu kuwa "wananchi walio wengi" wakitaka "Nchi 3!"
Sasa hayo ya "Nchi 3" umeyapachika kwenye Ibara ya 64 (1) ya Rasimu uliyatoa wapi?
Au kwako "Nchi" na "Serikali" ni kitu kile kile ukiamini tu wananchi 37,000 waliotaka "Serikali 3" walimaanisha "Nchi 3?"
=========
ADDITIONAL
=========
Ibara ya 64 inayozungumzia kuhusu Nchi Washirika (Nchi 2) inasema kama ifuatavyo (hiyo nchi ya 3 imeelezwa kwenye Ibara ya 1):
"(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Nchi Washirika ni Tanganyika na Zanzibar.
(4) Nchi Washirika zitatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Nchi Washirika zitakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na zitatekeleza majukumu yao kwa mambo yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Nchi Washirika kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba za Nchi Washirika."
Ibara nyinginezo zinazozungumzia Zanzibar na Tanganyika kama "Nchi" ni hizi zifuatazo: Ibara ya 1, 44 na 60 (3).
je zanzibar ni nchi au serikali? Ukiwa na jibu la swali hili na swali lako litakuwa lishajijibu.Sijakataa kuwepo kwa hiyo Tanganyika yenu mnaoililia utafikiri itawaongezea fedha mifukoni kumbe mtashtukia ufisadi uko pale pale hauogopi neno Tanganyika, nazungumzia maoni ya wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 3?
Uwe na heshima kwa watu wazima,ile ni ripoti ya tume sio ya Warioba nadhani huyu mzee ana umri zaidi ya mzee Mjepodau
je zanzibar ni nchi au serikali? Ukiwa na jibu la swali hili na swali lako litakuwa lishajijibu.Ukishamaliza hasira ulizo nazo rudi kwenye mada, ni lini "wananchi walio wengi" walitaka "Nchi 3?" Kama hawakuwepo Warioba kwa nini aliamua kuliingiza kwenye Rasimu?