Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,976
Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba,

Ulitueleza kuwa "wananchi walio wengi" walitaka
Serikali 3, japokuwa Takwimu zenyewe nazo zina ukakasi mwingi! Hatujasikia kuwa ukilieleza Bunge wakati wa kuwasilisha Rasimu kuwa "wananchi walio wengi" wakitaka "Nchi 3!"
Sasa hayo ya
"Nchi 3" umeyapachika kwenye Ibara ya 64 (1) ya Rasimu uliyatoa wapi?
Au kwako
"Nchi" na "Serikali" ni kitu kile kile ukiamini tu wananchi 37,000 waliotaka "Serikali 3" walimaanisha "Nchi 3?"

=========
ADDITIONAL 1
=========
Ibara ya 64 inayozungumzia kuhusu
Nchi Washirika (Nchi 2) inasema kama ifuatavyo (hiyo nchi ya 3 imeelezwa kwenye Ibara ya 1):
"(1) Kwa mujibu wa Katiba hii, Nchi Washirika ni Tanganyika na Zanzibar.
(4) Nchi Washirika zitatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii na Katiba zao.
(5) Nchi Washirika zitakuwa na hadhi na haki sawa ndani ya Jamhuri ya Muungano na zitatekeleza majukumu yao kwa mambo yote yasiyo ya Muungano katika mamlaka ya Nchi Washirika kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba za Nchi Washirika."

Ibara nyinginezo zinazozungumzia Zanzibar na Tanganyika kama "Nchi" ni hizi zifuatazo: Ibara ya 1, 44 na 60 (3).

==========
ADDITIONAL 2
==========
Ukitaka kujua kuwa hizo "Nchi Washirika" zina HADHI SAWA na "Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" soma Ibara ya 8 (4) inayosema kama ifuatavyo:

"Sheria yoyote, mila, desturi au uamuzi wowote wa chombo cha dola, Ofisa wa Serikali au chombo binafsi ni sharti afuate na kuendana na masharti yaliyomo kwenye Katiba hii na kwamba Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote ambao hautawiana au kwenda sambamba na masharti ya Katiba hii utakuwa batili."

Hapa zinapozungumziwa Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote maana yake ni Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote wa Jamhuri ya Muungano (ie katika mambo ya Muungano) na sio Sheria, Mila, Desturi au uamuzi wowote wa "Nchi Washirika." Zaidi ya hapo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijatajwa kuwa ni
KUU kupita Katiba za Nchi Washirika! Sasa unawezaje kuwa na MAFAHALI WATATU (3) katika zizi moja? Kwa wapenda Muungano watakubaliana na mimi kwa hili!

Hapa ndio lilipo BOMU la kuulipua Muungano wetu, amini usiamini! Kama Muungano utavunjika (endapo Rasimu hii itakuwa Katiba) basi ni kupitia Ibara hii ya 8 na nyingine nilizotaja hapo juu!
 
Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba,

Ulitueleza kuwa "wananchi walio wengi" walitaka Serikali 3, japokuwa Takwimu zenyewe nazo zina ukakasi mwingi! Hatujasikia kuwa ukilieleza Bunge wakati wa kuwasilisha Rasimu kuwa "wananchi walio wengi" wakitaka "Nchi 3!"
Sasa hayo ya "Nchi 3" umeyapachika kwenye Ibara ya 64 (1) ya Rasimu uliyatoa wapi?
Au kwako "Nchi" na "Serikali" ni kitu kile kile ukiamini tu wananchi 37,000 waliotaka "Serikali 3" walimaanisha "Nchi 3?"

Endelea kuweweseka tu! Tanganyika is back, it's a irreversible reaction!
 
You haveb zero thinking capacity bro

Sijakataa kuwepo kwa hiyo Tanganyika yenu mnaoililia utafikiri itawaongezea fedha mifukoni kumbe mtashtukia ufisadi uko pale pale hauogopi neno Tanganyika, nazungumzia maoni ya wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 3?
 
Sijakataa kuwepo kwa hiyo Tanganyika yenu mnaoililia utafikiri itawaongezea fedha mifukoni kumbe mtashtukia ufisadi uko pale pale hauogopi neno Tanganyika, nazungumzia maoni ya wananchi walitaka Serikali 3 au Nchi 4?

Sawa kwa tusi lako kwa Watanganyika!

Swali ni kweli Rais wa Jamuhuri ya watu wa Zanzibar akija Tanganyika hupigiwa mizinga 21! Na akiwa Zanzibar pia hupigiwa hiyo hiyo mizinga 21?
 
Sawa kwa tusi lako kwa Watanganyika!

Swali ni kweli Rais wa Jamuhuri ya watu wa Zanzibar akija Tanganyika hupigiwa mizinga 21! Na akiwa Zanzibar pia hupigiwa hiyo hiyo mizinga 21?

Mimi nauliza juu ya maoni ya "wananchi walio wengi!" Je, walitaka "Nchi 3" au "Serikali 3?" Hayo ya mizinga yaanzishie Topic yake tutachangia!
 
Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba,

Ulitueleza kuwa "wananchi walio wengi" walitaka Serikali 3, japokuwa Takwimu zenyewe nazo zina ukakasi mwingi! Hatujasikia kuwa ukilieleza Bunge wakati wa kuwasilisha Rasimu kuwa "wananchi walio wengi" wakitaka "Nchi 3!"
Sasa hayo ya "Nchi 3" umeyapachika kwenye Ibara ya 64 (1) ya Rasimu uliyatoa wapi?
Au kwako "Nchi" na "Serikali" ni kitu kile kile ukiamini tu wananchi 37,000 waliotaka "Serikali 3" walimaanisha "Nchi 3?"

tume ya warioba haikuwa inachukua idadi bali uzito wa hoja kwakuwa muda ulikuwa mdogo wa kuchangia dk.3 na ndiyo maana mwenzio akishazungumzia muungano sisi wengine tunazungumzia mambo mengine lakini mkitaka rejea ipo rejea tume ya nyalali,ya kisanga ya shelukindo n.k.
 
Mimi nauliza juu ya maoni ya "wananchi walio wengi!" Je, walitaka "Nchi 3" au "Serikali 3?" Hayo ya mizinga yaanzishie Topic yake tutachangia!

Ni utumwa kukataa asili yako, mimi na wewe na watz bara wote asili yetu na babu zetu waliishi Tanganyika. Mkwawa, Rumanyika, Sina, Chabruma, Mirambo, Mkama Ntare, Burito, Makongoro na Julius Kambarage Nyerere walipambana na wakoloni wakiipigania Tanganyika. Sio Tanzania!
 
mbona ni rahisi tu nchi moja yenye serikali 3

Nashukuru mkuu! Kumbe hajajipanga na hoja yake. Ni km wana-ccm na uchache wa waliotoa maoni ktk tume ya Rais kuhusu muungano. Wanasahau Rais Kikwete alichaguliwa na wa-Tanzania m5 kati ya m45?! Je uhalali wake uko wapi wa kuwa Rais?
 
Tatizo lenu ccm mnajitoa ufaham kwa kujaribu kupotosha maon ya wananchi wanao taka Tanganyika yao huku mkiwa mmekunywa viroba, Ibara ya 64(1) hii hapa nioneshe neno nchi hapo au km umeleta lasim ya congo sawa
 
Attachments

  • 1396326808774.jpg
    1396326808774.jpg
    84.7 KB · Views: 211
Ni utumwa kukataa asili yako, mimi na wewe na watz bara wote asili yetu na babu zetu waliishi Tanganyika. Mkwawa, Rumanyika, Sina, Chabruma, Mirambo, Mkama Ntare, Burito, Makongoro na Julius Kambarage Nyerere walipambana na wakoloni wakiipigania Tanganyika. Sio Tanzania!

Asili yangu nimezaliwa Tanzania sio Tanganyika! Pia zaidi ya 90% ya wananchi wote wamezaliwa baada ya Muungano, 10% tu ndio walioonja Utanganyika!
 
Tatizo lenu ccm mnajitoa ufaham kwa kujaribu kupotosha maon ya wananchi wanao taka Tanganyika yao huku mkiwa mmekunywa viroba, Ibara ya 64(1) hii hapa nioneshe neno nchi hapo au km umeleta lasim ya congo sawa

huenda alijichanganya akanukuu rasimu ya ccm ya mafichoni na si ile ya tume ya Warioba
 
Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba,

Ulitueleza kuwa "wananchi walio wengi" walitaka Serikali 3, japokuwa Takwimu zenyewe nazo zina ukakasi mwingi! Hatujasikia kuwa ukilieleza Bunge wakati wa kuwasilisha Rasimu kuwa "wananchi walio wengi" wakitaka "Nchi 3!"
Sasa hayo ya "Nchi 3" umeyapachika kwenye Ibara ya 64 (1) ya Rasimu uliyatoa wapi?
Au kwako "Nchi" na "Serikali" ni kitu kile kile ukiamini tu wananchi 37,000 waliotaka "Serikali 3" walimaanisha "Nchi 3?"

Acha kujidharirisha, huenda umenukuu rasimu ya mafichoni ya lumumba, lakini kwenye rasimu ya tume ya Warioba hakuna kitu unachokizungumza
 
Serikali mbili ndio chaguo la wananchi wengi.
Twende kwenye kura ya maoni mkaabike na serikali zenu kumi hizo.
 
Asili yangu nimezaliwa Tanzania sio Tanganyika! Pia zaidi ya 90% ya wananchi wote wamezaliwa baada ya Muungano, 10% tu ndio walioonja Utanganyika!

Kwani Wazanzibar wao hawamo kwenye hiyo 90% ?mbona wanajulikana kwa utambulisho wa kabla ya 1964?wana hadi vitambulisho vya ukaazi vya kuwatofautisha na Watanzania wengine? hizo hoja mufilisi angalia sehemu ya kutoa usi copy na ku paste tu toka kwa vilaza wenzio
 
Walioba anachekesha sana ndani ya rasimu yake yapo mambo mengi anajipinga yeye mwenyewe mzee waajabu sana huyu.
 
Back
Top Bottom