Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

Warioba, Wananchi Walitaka "Serikali 3" au "Nchi 3?"

Kikwete alimshambulia Warioba binafsi, pia Shivji kamshambulia Warioba binafsi, kwa kumtajia jina binafsi si kama tume iliyowasilisha maoni ya wananchi. Ndiyo maana analazimika kujibu matusi. Kwenye semina ya Shivji kwa vijana wa CCM iliyopachikwa jina la kongamano la vyuo vikuu, Warioba ametukanwa binafsi kuwa amesalia kuishi miaka kumi tu. Shivji aliyabariki mashambulizi hayo ya wana CCM.
Okay, umesomeka ila jaribu kutetea hoja zaidi kuliko kutetea mtu! Huyo Warioba, mimi na hata wewe tutakufa kesho au keshokutwa, lakini Tanzania itaendelea kuwepo! Tujadili kwa ustaarabu hata kama hatukubaliani. After all "wananchi walio wengi" ndio wataamua kwa referendum!
 
piga uwa garagaza ni serikali 2 tu mengineyo tutayaboresha hatutaki kuivunja nchi yetu hadi sasa NAUNGA HOTUBA YA RAIS WANGU KIKWETE .......YALIO MENGI YANAZUNGUMZIKA
 
Tatizo lako umetafsiri utafikiri Warioba anavyochanganya "Serikali 3" na "Nchi 3" akifikiri ni kitu kile kile!
hakuna shida, najua unachuki binafsi na Mzee Warioba, kila kitu warioba, warioba utafikiri tume nzima alikuwa pekeyake, Alafu kwa nini wewe na wenzako mnaiogopa sana Tanganyika? Kelele zote hizi kisa Tanganyika tuuu.
 
Warioba yupo nyumbani kwake anamwagilia maji maua yake. Si mlipitisha sheria ya kifuta Tume ya kuratibu maoni ili wasiwe sehemu ya bunge la katiba? Sasa mtapiga ramli mpate majibu.
 
Uzuri hatima ya muundo wa muungano ni ijumaa,kitaeleweka na labda longolongo itapungua watu waanze kujadili masuala ya msingi.
 
Mzee warioba anakazi sana ya kuwaelimisha watanzania wote na viongozi wao maana hamna wanachoelewa maskini
 
Mkuu, on the contrary nampenda sana Warioba, sina chuki naye hata kidogo, lakini sitaki kuwa mnafiki kwa kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa! Pale alipofanya vizuri nitamsifu na pale alipokosea nitamkosoa!
Kuhusu Tanganyika, sio kwamba naichukia ila nilitaka kujua juu ya "maoni ya wananchi walio wengi" kuhusu "Nchi 3!" Kuuliza hilo tu nimekuwa na chuki na Warioba? Halafu mimi sijaona wajumbe wengine wa Tume wakifunua midomo yao zaidi ya Warioba, ndio maana amemjibu hata Shivji! Katika mazingira hayo ndio maana mtu wa kumpelekea ujumbe ni Warioba, yeye ndio atawajulisha wenzake! Mbona akipewa sifa hasemi tuzipeleke kwa Tume? Lawama ndio anaona ni za Tume. Hata hivyo, kuhusu Tume nayo, imevunjwa, maadam msemaji wake bado anatetea hoja tutaendelea kujibu/kutoa hoja kwake!
 
Mzee warioba anakazi sana ya kuwaelimisha watanzania wote na viongozi wao maana hamna wanachoelewa maskini

Ni kweli mimi sielewi hili suala la "Nchi 3" kalitoa kwa "wananchi walio wengi" au la? Anielimishe!
 
Uzuri hatima ya muundo wa muungano ni ijumaa,kitaeleweka na labda longolongo itapungua watu waanze kujadili masuala ya msingi.

Bado tutaibua hoja zingine kuwa 1.katiba imebeba mambo mengi mno ambayo yanatakiwa yawekwe kwenye Sheria 2. Mbunge akiumia na hayupo kazini miezi 6 eti aachishwe Ubunge 3. Kuwa na Mahakama ya Juu ya Muungano huku haipo kwenye orodha ya Mambo ya Muungano, nk.
Mambo mengi hayajakaa sawa kusema kweli!
 
Warioba yupo nyumbani kwake anamwagilia maji maua yake. Si mlipitisha sheria ya kifuta Tume ya kuratibu maoni ili wasiwe sehemu ya bunge la katiba? Sasa mtapiga ramli mpate majibu.

Anamwagilia maua huku akimjibu Prof Shvji pamoja na kwamba Tume imeshavunjwa!
 
Kama Zanzibar iliwekwa na kupewa mamlaka ya kuitwa serikali ya mapinduzi; bas na Tanganyika lazima irudishwe na isimame kama serikali inayojitegemea.
 
Kama Zanzibar iliwekwa na kupewa mamlaka ya kuitwa serikali ya mapinduzi; bas na Tanganyika lazima irudishwe na isimame kama serikali inayojitegemea.

Hilo la Serikali sio tatizo maana "wananchi walio wengi" walitoa maoni kutaka hizo Serikali 3 kama Warioba na Tume yake wanavyodai! Tatizo ni lile la "Nchi 3," "wananchi walio wengi" walitoa mawazo lini?
 
Back
Top Bottom