Warioba: Mimi na Salim urais basi

Warioba: Mimi na Salim urais basi

Hata mimi natamani saaana kuona warioba anakabidhiwa nchi walau kwa miaka mitano tu ili kuturejeshea misingi ya taifa

Warioba akiwa Rais ,tumshinikize amteue Dr Salimu awe waziri mkuu,hapa Majizi yote kama haya yaki na Lowassa ,Werema,Chenge ,yaki Rostam yatakimbia nchi.

Tutakuwa tumefanikiwa kupata viongozi waadilifu katika ngazi ya juu na hakuna atakae thubutu kufanya ufisadi kama huu wa IPTL
 
Kama si warioba bas awe salim a. Salim kwa maono yangu
 
Anaweza kushinda akiungwa mkono na ukawa pia atagawa vipande vipande ccm
 
Wanajamvi;

Nadhan ingekuwa ni kitu cha maana sana kama wanaUKAWA wangemsimamisha jaji Warioba katika mbio za kusaka urais wa nchi hii.Hii yote ni kutokana na uadilifu na uzalendo alionao huyu mzee.
CCM na tamaa zao wamemdhalilisha sana...na huu ndio wakati wa kuweka maslahi ya taifa letu mbele bila kuangalia tofauti zetu za kivyama.
Naamin kabisa kwa moyo wa dhati sidhani kama Mzee Warioba anaifikiria tena CCM ya sasa ya wapiga dili wa Lumumba.
Nawasilisha...
 
Bora wewe umekuwa mkweli kuwa Waryoba ni UKAWA.

Kwa kukusaidia zaidi ni kwamba UKAWA ni Umoja wa Katiba ya Wananchi. Hii ina maana kila anaye tetea katiba inayotokana na mawazo yaliyotolewa na wananchi, ni mwana UKAWA.
Sasa tumia akili kujiuliza nanai anastahili kuitwa UKAWA
 
Kuwa UKAWA haihitaji kuthibitishwa na yeyote. Mtu yeyote anayetaka maoni ya wananchi ndiyo yawe dira ya uandaaji wa Katiba ya nchi ni UKAWA. JAJI WARIOBA ni UKAWA namba 1.

Kama Warioba angekubali lingekuwa jambo la hekima sana awe Rais kipindi hiki cha mpito (2015-2020) ambacho kazi kubwa kuliko zote iwe ni kupata katiba ya kwanza ya Watanzania. Baada ya hapo apumzike kwa heshima zote.

Kwaajili ya umoja wa kitaifa, asaidiwe kwenye nafasi za juu na Dr. Slaa, Prof. Lipumba, Mbowe, Seif Sharif Hamad, Prof. Safari, Mbatia na wote wenye mawazo chanya juu ya upatikanaji wa katiba ya Watanzania. Kwaajili ya kuwaonesha wananchi unafiki wa CCM, wawaingize kwenye serikali ya Umoja Lukuvi na Wasira.

Iko wazi mkuu kwa hali ilivyo WARIOBA NI UKAWA hajathibitishwa tu
 
kwani kuwa UKAWA ni lazima upate nembo ya TBS?kwi kwi kwi te teh.poleni yenu mnaomchukia.......
 
Wadau, sio wazo wala mchango, wala si kitu cha kufikirika ila kwa uhahika kabisa Napenda kuwashauri vyama vyote vinavyounda ukawa, kua jibu sahihi la katiba ya tanzania, na ili kuleta mapinduzi katika taifa ili muweke tofauti, tamaa na matakawa yenu kichama na kumsimamisha Jaji Joseph Sinde Warioba kuwania uraisi kwenye uchaguzi mkuu mwakani. Sisi wapenda maendeleo, wapenda haki na usawa, wapenda tanzania mpya tutakua nyuma yenu. Tafadhari zingatieni hilo....najua humu ndani viobgozi wa cuf, chadema, nccr, na vyama vyote vinavyounda ukawa wapo msipuuzie hili.

NB: kwa msisitizo zingatieni hili.
 
Dah angefaa sana ni kwa vile amezeeka...lakini pia yule mzee ni ccm damu na hawezi kutoka..sema ccm siku hizi inaendeshwa na wahuni akina nape na majangili .,
 
I stil believe kua ukawa stand a chance ya kumshawishi Jaji Warioba as long as wewe na nia ya dhati to do that.
 
CCM ya baba zetu sio hii ya sasa. Ile utajiri ilikuwa disqualification factor no. 1. Leo sii ajabu mabilionea wanatangaza wazi kugombea uongozi hata urais. Warioba anafaa, awe kama Mandela wetu umri is just a number. Wenye umri mdogo ndio hao wana kamatwa na AK47 hotelini.
 
CCM ya baba zetu sio hii ya sasa. Ile utajiri ilikuwa disqualification factor no. 1. Leo sii ajabu mabilionea wanatangaza wazi kugombea uongozi hata urais. Warioba anafaa, awe kama Mandela wetu umri is just a number. Wenye umri mdogo ndio hao wana kamatwa na AK47 hotelini.

Nakubaliana na wewe 100%.
 
Back
Top Bottom