Mh. Jaji sinde wariba
Tukiwa tumebakisha miaka takribani mmoja, taifa
letu liingie tena katika mchakato wa uchaguzi wa
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na
Uchaguzi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar; nafikiri ni wakati muuafaka sasa wa
kuanza kufikiri viongozi wa namna gani
wanahitajika katika taifa letu hasa wakati huu
ambapo nchi yetu ipo katika mawimbi ya
mabadiliko ya fikra hasa kutoka mabadiliko
makubwa ya Katiba katika historia ya Taifa letu.
Ni matarajio yetu kuwa uchaguzi wa mwaka 2015
pengine utakuwa na historaia ya pekee; upekee
wa uchaguzi huu ni matarajio ya wananchi wengi
kuwa uchaguzi huu utafanyika katika kipindi
ambacho taifa litakuwa limekwisha pata Katiba
yake mpya;
swali ambalo tuanalojiuliza sasa ni je Katiba hiyo
itakuwa imekizi matakwa ya Taifa ambalo linataka
kusonga mbele kimaendeleo?
Kama taifa litakuwa limefanikiwa kupata Katiba
bora basi hatuna budi tupate viongozi ambao kwa
kweli nao watakuwa bora katika kuongoza Taifa
letu kuelekea kwenye maisha bora kwa kila
mtanzania. Ni ukweli ambao haupindiki kuwa
Katiba bora ni msingi wa maendeleo ya nchi
kwani ni msaafa wa sheria na kanuni sahihi
kufuatwa na itamlazimisha kiongozi kuongoza
kwa uwajibikaji; kuonyesha uzalendo na kuwa
mfano bora kwa viongozi wengine.
Pengine katika msingi huu tutahitaji kiongozi
ambaye anauelewa mpana wa kuielewa Katiba ili
aweze kuisimamia kwa dhati kabisa; tutahitaji
viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi,
kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi
wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa
linawapa. Kwa hivyo tutahitaji RAIS pamoja na
mambo mengine awe na UWEZO kuongoza kwa
usahihi.
Vile vile tunahitaji viongozi wajao katika serikali
zetu mbili wawe ni watu wa WATU; viongozi
ambao wataweza kuona matatizo ya wananchi
wao ni yao na yanawakera wanawanyima usingizi,
yana wafanya waongeze nguvu ya uwajibikaji wa
kusimamia rasilimali za Taifa. Nasi kama
wananchi tuwe na uwezo wa kuwapima kwa
watakacho kifanya wakiwa madarakani.
Pengine tutahitaji kidogo aina ya viongozi wetu
wawe wakali japo sio sahihi katika nchi ya
kidemokrasia kutumia msemo huu lakini wakati
mwingine ile tuweze kupiga hatua ya maendeleo
tutahitaji viongozi wenye mawazo ya kidikteta ili
tuweze kubadilisha kidogo maadili ya utendaji
kwa Watanzania hasa viongozi wetu katika
mawizara na idara zake:Tunahitaji Maraisi katika
serikali zetu mbili ambao wanaweza
kuwawajibisha mara moja watendaji wake ambao
wanashindwa kuwajibika, tuwapate viongozi
ambao wanaweka pembeni huruma na urafiki
ambao hauna faida kwa Taifa;
Nafikiri itakuwa ni jambo la busara kama sisi
kama watanzania na wapiga kura tukiweza
kuepuka tabia ya kuwachagua viongozi wetu kwa
Mazoea, Mkumbo na kwa kutumia Hisia na
mapenzi binafsi juu ya wagombea. Nafikiri umefika
wakati tuwachagua viongozi wetu kwa upeo wao
wa kuona mambo mbalimbali nauwezo wao wa
uongozi hapa nazungumzia uzoefu wa kiongozi
kabla ya kuchaguliwa kuwa rais je amefanikiwa
kwa kiasi gani katika idara ambayo amewahi
kuongoza?
kama taifa tunafahamu kuwa taifa letu bado
linaogelea sana katika tope nzito la matumizi
mabaya ya rasilimali ya Taifa Rushwa na Ufisadi
basi tunahitaji Rais ambaye analiona hili kuwa
Lazima tukubali kuwa mabadiliko yoyote ya
kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga
kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi
kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa na ufisadi.
Kiongozi wetu aweze kuliona hili na kuwa tayari
kupambana nalo akiamini kuwa Tanzania yetu
tatizo la rushwa limeshaota mizizi:Watanzania
wengi kwa mamilioni wamepoteza matumaini na
hali zao za maisha lakini Maraisi wetu wapya
watakuwa tayari kulitatua tatizo hili na
kuwachukulia sheria wale wote ambao
wamehusika katika uchafu huu,
Tunahitaji vile vile kiongozi ambaye ataweza
kuyatekeleza kwa vitendo manemo haya ya
Mheshimiwa Yusuph Makamba "maendeleo ya
Watanzania yataletwa na wao wenyewe, kwa
kufanya kazi. Watanzania wamekuwa wavivu wa
kufanya kazi na kwamba kila kitu wanategemea
kitafanywa na serikali … Watanzania wataendelea
kulia umaskini kwa kuwa hatuna tabia ya
kushirikiana na kufanya kazi," . Kauli hii ni nzito
kiongozi wetu anayetaka kuongoza taifa hili
lazima awe kuwahamasisha wananchi bila
kuogopa kwa kuwaeleza ukweli huu bila kuogopa
kukosa kura katika kipindi kingine cha uchaguzi.
Daima tunapofikiria kuwachagua viongozi wa juu
wa Taifa letu tunayakumbuka maneno ya Baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi sema kuwa kazi
ya urais ni ngumu na inahitaji busara na kuchukua
maamuzi magumu, ili kuweza kutimiza haki
wananchi wanyonge " walala hoi "; aliendelea
kushauri kuwa "Ole wale wanaokimbilia Ikulu,
wanakimbilia nini, Ikulu hakuna biashara ya
kufanya, Ikulu ni mahali patakatifu na kama kuna
mtu anadhani kuwa kukaa Ikulu ni raha basi
angeniuliza mimi katika kipindi cha miaka 21
niliyokaa Ikulu nimefanya biashara gani,Ikulu ni
mzigo mzito"
Mwandishi Nyenyembe aliwahi andika kuwa "Kwa
maana hiyo mtu anapoamua kuulilia urais,urais sio
pambo la nchi,urais ni jalala, urais ni chumba cha
kuhifadhia maiti,urais ni njaa,urais ni
magonjwa,urais ni bakuli la kukingia machozi ya
watu wanyonge wanaolia kila siku wakihitaji
msaada na kama hawapati anayetazamwa hapo ni
rais"