Mutakyamirwa
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 4,942
- 1,360
Mkakati uleule unaotumiwa na mafisadi kuepusha maswali magumu kwa wahusika.
Hiki ni kiini macho. Tutaelekeza macho yetu Rwanda ilhali mchwa na majambazi wa kitanzania wakiendelea kuifilisi nchi yetu.
Tutaambiwa tatizo ni Paul Kagame ilhali tuna rais asiyejua kwanini yupo ikulu, mzururaji mahiri, na atakumbukwa (pindi akikubali kutoka madarakani) kwa uongozi wake dhaifu kupindukia.
Waungwana, hiki ni kiini macho. Hivi hamjiulizi UZALENDO wa gazeti la Mtanzania ktk ishu ya DRC/Rwanda unatoka wapi? Kwamba Rostam ana uchungu na Tanzania kiasi hicho? Hawa ni akina Salva Rweyemamu wapo kazini, na wanaelewa udhaifu wa Watanzania: ni rahisi kuwaingiza mkenge!
Mkuu,
Sijui niku-support kiasi gani nieleweke kwa wengine. Kinachofanyika ni plan za magamba aidha kuzolotesha mchakato wa katiba mpya au kuzua vita vitakavyosogeza utawala dhaifu miaka mingine mbele.