Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

Waraka wangu kwa JWTZ, Watanzania

Kama yeye kidume kweli hayo majeshi yake aliyoyapeleka mpakani na DRC aue wanajeshi wa JWTZ tujue anatisha...

Tunachopingana hapa ni ushamba wa kukimbilia vita, huu ni ushamba mkubwa tutafaidikaje hasa na vita hii wewe unaweza kutueleza faida za huu upuuzi? nauita upuuzi kwasababu kama mtanzania naona aibu kubwa kushabikia vita nje ya nchi yangu nikifahamu fika watanzania kwa maelfu wanatekea kwa madawa ya kulevya, kufa kwa kukosa huduma bora za afya, elimu duni na hatuelewi tutatokaje huko. Yatupasa kupigania uchumi wetu na sis kushabikia kagomnvi kasiko na mashiko tena kakikuda kati ya mh kikwete na kagame.
 
Kama yeye kidume kweli hayo majeshi yake aliyoyapeleka mpakani na DRC aue wanajeshi wa JWTZ tujue anatisha...

PK hanasababu yakupigana na tanzania,unakumbuka minister mshikiwabo alisema watanzania waishio rwanda msiwena wasiwasi mjisikie nyumbani kwani sisi wote ni waafrika na wana east afrika,ungejua jinsi pk anawapenda watanzania,tatizo ni dissapointment iliyo fanywa na mtu mmoja tu ambayo inaleta hili joto,pk anajua anao pigana nao mtazania atapigananaye kwa shida ipi labda mkijaribu kuingia anga zake hapo ata wahit.
 
Huu waraka inabidi uhifadhiwe kwani unaweza kutumiwa kama ushaidi wa uchochezi dhidi ya watusi,Hata yule hasan ngeze mwandishi aliye chapisha 10 hutu commandments hivi sasa yuko ananyea ndoo arusha.

Mkuu,

Hiki ndicho wanachofanya wengi wetu hapa jf bila kujua. Rejea pia waraka wa Mtikira ambao nafikiri ndo unafanyiwa kazi. zaidi ikitokea kwa bahati mbaya vijana wa jk waingie Kigari kwa mwono wa wengi hapa nahsi watafanya mabaya zaidi ya 1994 (God forbid). Vita si yakushabia hata kidogo. There is always an option for war.
 
HEBU ANGALIENI ITIKADI ZA HAO WANAOITWA INTERAHAMWE(GENOCIDERS) DHIDI YA WATUSI JE UNAFIKIRI NIHAKI FIB KUWAUNGA MKONO?

[h=1]Hutu Ten Commandments[/h] From Wikipedia, the free encyclopedia
Jump to: navigation, search
The "Hutu Ten Commandments" (also "Ten Commandments of the Bahutu") was a document published in the December 1990 edition of Kangura, an anti-Tutsi, Hutu Power Kinyarwanda-language newspaper in Kigali, Rwanda. The Hutu Ten Commandments are often cited as a prime example of anti-Tutsi propaganda that was promoted by extremists in Rwanda following the 1990 invasion by the Rwandan Patriotic Front and prior to the 1994 Rwandan Genocide.[SUP][1][/SUP][SUP][2][/SUP][SUP][3][/SUP][SUP][4][/SUP] The chief editor of Kangura, Hassan Ngeze, was convicted of genocide and crimes against humanity in 2003 by the International Criminal Tribunal for Rwanda and was sentenced to 35 years' imprisonment.[SUP][5][/SUP]

[h=2]Text[/h]
The Hutu Ten Commandments

1. Every Hutu should know that a Tutsi woman, whoever she is, works for the interest of her Tutsi ethnic group. As a result, we shall consider a traitor any Hutu who

  • marries a Tutsi woman
  • befriends a Tutsi woman
  • employs a Tutsi woman as a secretary or a concubine.
2. Every Hutu should know that our Hutu daughters are more suitable and conscientious in their role as woman, wife and mother of the family. Are they not beautiful, good secretaries and more honest?
3. Hutu women, be vigilant and try to bring your husbands, brothers and sons back to reason.
4. Every Hutu should know that every Tutsi is dishonest in business. His only aim is the supremacy of his ethnic group. As a result, any Hutu who does the following is a traitor:
  • makes a partnership with Tutsi in business
  • invests his money or the government's money in a Tutsi enterprise
  • lends or borrows money from a Tutsi
  • gives favours to Tutsi in business (obtaining import licenses, bank loans, construction sites, public markets, etc.).
5. All strategic positions, political, administrative, economic, military and security should be entrusted only to Hutu.
6. The education sector (school pupils, students, teachers) must be majority Hutu.
7. The Rwandan Armed Forces should be exclusively Hutu. The experience of the October 1990 war has taught us a lesson. No member of the military shall marry a Tutsi.
8. The Hutu should stop having mercy on the Tutsi.
9. The Hutu, wherever they are, must have unity and solidarity and be concerned with the fate of their Hutu brothers.
  • The Hutu inside and outside Rwanda must constantly look for friends and allies for the Hutu cause, starting with their Hutu brothers.
  • They must constantly counteract Tutsi propaganda.
  • The Hutu must be firm and vigilant against their common Tutsi enemy.
10. The Social Revolution of 1959, the Referendum of 1961, and the Hutu Ideology, must be taught to every Hutu at every level. Every Hutu must spread this ideology widely. Any Hutu who persecutes his brother Hutu for having read, spread, and taught this ideology is a traitor.[SUP][1][/SUP]
Hizi commandments ndizo zinatumiwa na watu wengi humu kuendeleza chuki dhidi ya watusi!

na ndizo anazotumia Kikwete. Kwa nini kawaacha FDLR na makundi mengine ya waasi aende M23 pekee? Kikwete anatumiwa na wazungu
 
Manyerere,

Hongera sana kwa kuueleza ukweli mtupu.
Tanzania hatuna cha kupoteza hata kama tutatengwa na hawa wagomvi.
Kwanza, si vema kilazimisha ushirikiano na watu wasiokutakia mema. Najua Tanzania tuna nia ya dhati kushirikiana na jirani zetu, lakini sioni kama Uhuru, Museveni na Kagame wana nia njema na sisi, Tanzania.

Kwa vyovyote vile mwisho wa mtu mbaya ni aibu mbaya; mwisho wa Kagame umekaribia. Hana muda mrefu kabla mambo yake hayajaharibika kabisa. Kuwatendea hiyana Watanzania ni kujiletea tu laana. Na itampata Kagame yeyote yule mwenye nia mbaya na Watanzania.

Viongozi wetu waangalie mambo haya kwa umakini sana.

MUMGU, Baba yetu wa Mbinguni twakuomba ibariki Tanzania na Watu wake.
 
Mkakati uleule unaotumiwa na mafisadi kuepusha maswali magumu kwa wahusika.

Hiki ni kiini macho. Tutaelekeza macho yetu Rwanda ilhali mchwa na majambazi wa kitanzania wakiendelea kuifilisi nchi yetu.

Tutaambiwa tatizo ni Paul Kagame ilhali tuna rais asiyejua kwanini yupo ikulu, mzururaji mahiri, na atakumbukwa (pindi akikubali kutoka madarakani) kwa uongozi wake dhaifu kupindukia.

Waungwana, hiki ni kiini macho. Hivi hamjiulizi UZALENDO wa gazeti la Mtanzania ktk ishu ya DRC/Rwanda unatoka wapi? Kwamba Rostam ana uchungu na Tanzania kiasi hicho? Hawa ni akina Salva Rweyemamu wapo kazini, na wanaelewa udhaifu wa Watanzania: ni rahisi kuwaingiza mkenge!
 
Mniwie radhi kwa urefu wa makala hii, lakini nimeona ni muhimu wakati huu ambao Rwanda, Burundi na Kenya wanapoelekea kutufanya sisi mazuzu. Naomba wana JF mchangie bila jazba.

Safari hii ya Goma ihitimishiwe Kigali

Na Manyerere Jackton, JAMHURI

Meja Khatibu Mshindo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), amekufa katika mapambano nchini DRC. Amekufa kishujaa.

Amekufa akitekeleza maelekezo halali ya Umoja wa Mataifa (UN) yanayolenga kuwafanya wananchi wa Mashariki mwa DRC waonje tunu ya amani.
Kifo cha kamanda huyu kinapaswa kiwe chachu kwa Watanzania na wapenda amani katika Afrika na duniani kote.
Watanzania tuna historia iliyotukuka ya ukombozi wa wanyonge sehemu mbalimbali duniani. Ndugu zetu wa Msumbiji, Angola, Afrika Kusini, Namibia, Comoro, Ushelisheli, Angola na kwingineko wanatambua hilo. Bila kujali umasikini wetu, tulijitoa kwa hali na mali kuhakikisha wanyonge katika mataifa hayo tunawakomboa. Wakati tukihaha kutekeleza dhima hiyo ya kiutu, hatukujali kuachwa nyuma kimaendeleo na majirani zetu kama Kenya au Malawi ambao hawakuhangaika kwa namna yoyote.

Kifo cha Kamanda Mshindo kinapaswa kiwe chachu kwa wapiganaji na makamanda wa JWTZ katika kuhakikisha wananchi wa DRC wanapata amani, wanafaidi matunda ya uhuru, na utajiri wao unabaki kuwanufaisha wao kwanza.

Tumempoteza Mtanzania mwenzetu katika vita ambayo mwasisi wake ni Rais Paul Kagame wa Rwanda. Huyu ni mpenda vita, na ndiyo chimbuko la kundi la waasi wa Kihutu la FDLR. Hili ni matokeo ya ubabe wake alipoamua kushiriki kuwaua Rais Juvenal Habyarimana na mwenzake wa Burundi, Cyprien Ntaryamira. Aprili 6, 1994 ndege iliyokuwa imewabeba viongozi hao kutoka nchini Tanzania ilipigwa kombora wakati ikijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali, Rwanda.
Pamoja na marais hao, wengine waliouawa kwenye shambulizi hilo ni Bernard Ciza (Waziri wa Ujenzi wa Burundi), Cyriaque Simbizi, (Waziri wa Mawasiliano wa Burundi, Jenerali Deogratias Nsabimana (Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda), Meja Thaddée Bagaragaza (Msaidizi wa Rais wa Rwanda-masuala ya kijeshi), Kanali Elie Sagatwa (Mjumbe wa Sekretarieti ya Rais wa Rwanda), Juvénal Renaho (Mshauri wa Rais wa Rwanda wa Masuala ya Kigeni), na Emmanuel Akingeneye ambaye alikuwa Daktari wa Rais wa Rwanda.
Wana anga watatu, raia wa Ufaransa nao waliuawa. Nao ni Jacky Héraud (rubani), Jean-Pierre Minoberry (rubani mwenza) Jean-Michel Perrine (mhandisi wa ndege).
Damu ya watu hawa inamsumbua Rais Kagame.
Taarifa mbalimbali kutoka pande mbalimbali duniani zinamweka mbele kwenye orodha ya waliohusika kwenye mauaji hayo ambayo baadaye yalisababisha kile kilichokuja kujulikana kama mauaji ya kimbari.

Dola ya Bahima

Watanzania tuna sababu zote za kupigana vita ndani ya DRC. Hii ndiyo njia pekee sahihi ya kuvuruga mkakati wa Rais Kagame na rafiki yake, Rais Yoweri Museveni wa Uganda wa kuanzisha Dola ya Bahima. Hii ni dola ya watu wa kabila la Watutsi.
Marais hawa wanaamini Bahima inapaswa kusambaa Rwanda, Burundi, Uganda, sehemu za Tanzania na katika DRC. Tukiwaruhusu waimege DRC, nasi Tanzania tukae mkao wa kunyolewa! Hapa tunapaswa kutambua kuwa kwa huruma yetu tuliwakaribisha maelfu ya wakimbizi wa Kitutsi. Hawa wanajua mengi ya Tanzania. Haitashangaza siku moja wakijiunga na kuanzisha vita kwa madai ya kutaka watambuliwe. Tumeyaona juzi baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaamuru wahamiaji haramu warejee kwao.

Kumetolewa maneno mengi ya vitisho na lawama, kana kwamba ni halali kwa mtu kuishi katika nchi nyingine bila kufuata taratibu. Waliingia nchini mwetu wakiwa na mifugo mingi. Wakajitwalia maeneo makubwa kwa nguvu na kwa hila. Wakawaua wananchi wetu. Wakachoma nyumba na mashamba ya wenyeji. Kama wameweza kufanya hivyo sasa, watashindwa nini hapo baadaye kudai Karagwe na Ngara kuwa ni yao? Tuwe macho sana.

Rais Kagame alihakikisha anaingiza nchi yake kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki, si kwa kutafuta kitu kingine, bali nguvu za kisiasa.

Chokochoko zake zimepamba moto baada ya ushauri wa Rais Kikwete wa kumtaka aketi na waasi ili wamalize tofauti zao kwa mazungumzo. Alichofanya Rais Kikwete ni kutoa ushauri, na si kumshurutisha! Kejeli, matusi na dharau vilivyotolewa baada ya kauli ya Rais Kikwete, vinaashiria kuwa kuna jambo kubwa zaidi ya hilo la kuchukizwa na ushauri aliompa.
Zipo sababu nyingi zinazomfanya Rais Kagame awe mbogo. Nitajaribu kuziainisha hapa kwa ufupi tu. Mosi, Tanzania tunakubalika sana kimataifa. Kwenye diplomasia tumeiacha mbali Rwanda. Hili linamuudhi sana kwani anaamini yeye ni bora na maarufu zaidi.

Kitendo cha Rais Barack Obama wa Marekani kuja Tanzania na kuziacha Rwanda, Uganda na hata Kenya kimewaudhi, na kwa kweli tunaweza kusema hii imekuwa nguzo imara iliyoibua mshikamano na mapenzi ya ghafla miongoni mwao. Rwanda ikijiona kuwa ndiyo nchi inayoinukia kiuchumi kwa kasi, ilidhani ina sifa zote za kuiwezesha kutembelewa na Rais Obama. Uganda ambayo ilikuwa mshirika mkuu wa Marekani, inaona Tanzania imechukua nafasi yake. Imeingiwa wivu! Kenya ambayo inaamini Obama ni wao kwa sababu babake ni Mkenya, imechukizwa kuona ikipigwa kumbo na Tanzania. Hawa watatu-Kagame, Museveni na Kenyatta-wameungana kuichukia Tanzania kwa sababu tu ya kumkosa Obama.

Pili, kinachomsumbua Rais Kagame na washirika wake ni uamuzi wa Tanzania wa kutaka Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama wa EAC liende hatua kwa hatua. Msimamo wa Tanzania umekuwa kwamba maoni ya wananchi ni muhimu mno kabla ya kuchukua uamuzi wowote. Kwao, Tanzania ndiyo kikwazo cha kuwa na serikali moja ya EAC. Hapa ni vema Watanzania wakakumbuka namna Rais Museveni alivyokuwa amejiandaa kuwa Rais wa Kwanza wa Shirikisho la Afrika Mashariki. Sidhani kama ameshaufuta mpango huo.

Baada ya kuona Tanzania tukitaka jambo hili liende hatua kwa hatua, watatu hawa wameungana sasa kutaka shirikisho lao la kisiasa, huku wakiiacha nje Tanzania na Burundi. Wanajidanganya bure. Lakini hapana sababu ya kulumbana nao. Kama wanataka kuanzisha, waanzishe tu. Hakuna haja ya ugomvi. Wakianzisha kutakuwa na nchi mbili-hiyo ya Shirikisho, na Tanzania kwa upande mwingine.

Hapa ni vema kwanza tukatambua kuwa Tanzania ni nchi kubwa. Ukichukua Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya, ukaziweka pamoja, bado ni ndogo kwa Tanzania. Hatuna sababu ya kuogopa.

Tatu, hawa jamaa kiu yao kubwa kabisa ni ardhi ya Tanzania. Ukiacha tamaa ya kutaka kuitawala kanda yote hii, kiu yao ya kweli ni ardhi ya Tanzania. Wamepambana kwa hali na mali kuhakikisha kuwa ardhi inakuwa moja ya mambo kwenye shirikisho. Wanataka Mkenya, Mganda, Mnyarwanda na mwanachama mwingine yeyote, akitaka kuingia Tanzania, basi apewe uraia wa kudumu na apata ardhi bila masharti!

Hoja yetu imekuwa kwamba wao wakija Tanzania watapata ardhi, je, Mtanzania akienda Rwanda au Kenya au Uganda ataipata? Chao chao, chetu chetu sote. Wao hawana mita ya mraba ya ardhi iliyo wazi kwa hiyo wanajua mlengwa na wa kuumizwa hapa ni Tanzania tu. Uroho wao wote ni ardhi ya Tanzania. Hilo tumeapa kuwa haliwezekani. Kama haliwezekani kwa ndugu wa tumbo moja, seuze kwa nchi na nchi? Tukianzisha shirikisho tutapeana nini? Hilo ndilo jambo wanalopaswa kutujibu kwanza. Janja ya kuja kuoa au kuolewa Tanzania haitawasaidia.

Wanachofanya sasa kinatokana na hasira tu

Shirikisho la Rwanda, Uganda na Kenya likianzishwa haliwezi kudumu. Watagombana tu. Rwanda watataka walitawale shirikisho. Hicho ndicho wanachokitafuta. Wakenya hawasumbuliwi na kingine, isipokuwa biashara. Wameingia kwenye mkakati huu kwa sababu wanadhani bandari ya Mombasa inaweza isiwe na maana endapo Rwanda, Uganda na Burundi wataamua kutumia bandari za Tanga na Dar es Salaam; na hiyo nyingine inayojengwa Bagamoyo. Bado ukweli unabaki kwamba kutoka Dar es Salaam hadi katika nchi za Rwanda na Burundi ni karibu mno kuliko kuanzia Mombasa.
Katika mpango huu sidhani kama Burundi itakubaliana nao. Burundi kuwa karibu na Tanzania kuna manufaa makubwa zaidi kwake kuliko kuwa karibu na hayo mafiga matatu.
Harakati hizi zote zinachochewa na Rwanda, na hapa ndipo ninapokuja na sababu ya nne ya Tanzania kuchukiwa. Rais Kagame amechukia mno kuona majeshi ya Tanzania yakiongoza mapambano ya kuwang’oa M23 ambao ni Wanyarwanda. Kwa miaka yote DRC imekuwa shamba la Rwanda. Kagame ameongoza harakati za kuliibia taifa hilo bila huruma. Ameanzisha vita ili amani isiwepo. Anajua DRC ikitawalika, hatapata mwanya wa kwenda kupora rasilimali, hasa madini. Kwa sasa adui yake mkubwa ni Rais Kikwete na Tanzania kwa sababu tunaziba njia yake haramu ya uchumi.

Kuachwa kwetu solemba EAC

Sioni kwanini tusianzishe Jumuiya yetu kwa kuwakaribisha DRC na Burundi. Sisi ni taifa kubwa. DRC ni taifa kubwa pia. DRC na Tanzania tuna rasilimali nyingi mno. Faida za kujitoa EAC ni kubwa kwetu kuliko kuendelea kuhangaika na hawa wapenda vita. Tuwaache waanzishe yao, na sisi tuanzishe yetu. La, hilo kama haliwezekani, tujikite zaidi SADC ambako kuna soko pana kuliko EAC.
Tukijitoa EAC atakayeumia zaidi ni Kenya maana bidhaa na uwekezaji wake mkubwa kauelekeza Tanzania. Soko lake kubwa lipo Tanzania. Wanajidanganya tu.

Tusiendelee kuwabembeleza watu wasiokuwa na shukrani. Tuwatakie heri katika ndoa yao hii mpya ambayo sioni uhai wake. Hizi ni hasira za mkizi ambazo mara zote humnufaisha mvuvi. SADC ni bora zaidi. Tupeleke nguvu zetu kwenye SADC.

Kagame na Museveni walisaidiana kuichukua Uganda. Museveni alimsaidia Kagame kuitawala Rwanda. Sasa wanasaidiana wachukue sehemu ya DRC. Museveni anamsaidia Kagame katika hili. Tutambue kuwa inayofuata ni Tanzania. Si ajabu wale Wanyarwanda waliokuja siku nyingi sasa wakadai wanabaguliwa, na kwa sababu hiyo wakaanzisha vita ya kutaka kutambuliwa au kujitenga na kuwa sehemu ya Rwanda na Uganda (Bahima Empire).

Njia pekee ya kumwondoa Rais Kagame ni hii aliyotusaidia kuiweka, yaani vita. Kuichokoza Tanzania ni njia ya kuelekea ukingoni mwa utawala wake. Amepigana kwa muda mrefu na wasiojua vita. Amejaribu kuitisha Tanzania akidhani atafanikiwa. Kinachotakiwa sasa ni kumwonyesha kazi. Safari iliyoanzia Goma inastahiki ihitimishiwe Kigali. Kama kasahau, arejee kwenye historia ili ajue kilichompata nduli Iddi Amin Dadaa. Buriani Kamanda Khatibu Mshindo.

manyerere@hotmail.com


[/COLOR][/SIZE]
Manyerere safi sana umechambua na kutoa mapendekezo mazuri. Kigali iwe uelekeo. Huyu Rutajumbukirwa ndo Kati ya wale ambao hawajaondoka nchini kurejea kwao lakini zoezi la nyumba kwa nyumba litawatoa tu warudi kwao.
 
na ndizo anazotumia Kikwete. Kwa nini kawaacha FDLR na makundi mengine ya waasi aende M23 pekee? Kikwete anatumiwa na wazungu

Habari ndio hiyo,hizi commandments bado zinafundishwa mpaka sasa huko maporini congo,halafu ndio hao kikwete anasema selikali ya rwanda iongeenao,na hii ideology ndio iliyopelekea hao interahamwe kuua watusi bila huruma kwani hawakua tena na thamani,imagine mtusi hakua na haki kipindi hicho,lakini hi sasa katika selikali ya kagame wahutu wamejazana katika idara mbalimbali za serikali bila ubaguzi,tafuta sehemu yote hautapata mahali pameandikwa mambo ya ubaguzi kwa wahutu yaliyofanywa na watusi,mengi ni maneno ya kutunga tu,lakini ushaidi upo dhidi yahao wahutu wenye msimamo mkali,unategemea mtu mwenye itikadi kama hiyo akiingia kigali kuna mtusi atabaki? lakini ninachojua this time mtusi hatakufa kama ilivyo kua 1994 kwani nao itabidi wajihami.
 
Kwahilo rwanda imelitatua kabisaa kwa FDLR anaye rudi na kuomba msamaha na kujitenga na itikadi za kimbari na kutambulika kua hana hatia ya mauaji anapokelewa na kua integrated in society ndio hao unaosema,sasa hao waliobaki ni wale ambao either wanamakosa makubwa walitenda rwanda au wanaitikadi za kimbali ambazo hawataki kuachana nazo,nafikiri unajua hatakama unakesi ya mauaji ukakiri na kuomba msamaha unaweza hurumiwa au kupunguziwa kifungo,sasa rwanda haiwezi kulazimishwa kuongea na hao wauaji wakati wao hawataki kutubu dhambi zao na kukubali kuachana na hiyo itikadi ya kimbali,hiyo wanyarwanda hawawezi kuikubali nisawa na kupatia zawadi mtu aliye kufanyia ukatili.

Ok, kama hivyo ndivyo hapo kwenye RED, kwanini Kikwete aliposema Rwanda iongee na FDLR yeye Kagame na kagenge chake cha wahuni walimtukana....? Kama utaratibu ni kuomba msamaha, unaonaje FDLR wote waombe msamaha kwa pamoja na kusamehewa na kurudi Rwanda....? Uliyosema sio kweli, Rwanda inatumia porojo za FDLR kusakama wahutu na watutsi wanaompinga Kagame kimawazo na pia unatumia excuse hiyo ili kuendelea kuinyonya Kivu...? Hata Gen. Nyamwasa mmesema yeye pia ni FDLR.....ingawa ni kweli Nyamwasa, Kagame, Kabarebe na wengineo walihusika na mauaji ya halaiki Rwanda na Congo!

Inshallah.....with JWTZ tutakunywa chai Kigali...!
 
Manyerere safi sana umechambua na kutoa mapendekezo mazuri. Kigali iwe uelekeo. Huyu Rutajumbukirwa ndo Kati ya wale ambao hawajaondoka nchini kurejea kwao lakini zoezi la nyumba kwa nyumba litawatoa tu warudi kwao.

Nawewe achakutisha watu kigali wanakaribisha hadi watanzania hakuna matata ni nchi yenye amani na watu wakarimu nenda na wewe ujionee peace people,yani utapigwa na butwaa ukifika utaona aibu kwa yote uliyo yaandika dhidi ya rwanda na wanyarwanda,tatizo umezaliwa tz na kueekea tz tembea uone,labda tu ukiwa mmoja wao hao wauaji ujue utafikishwa mahakamani ukikanyaga mguu wako kigali.
 
Manyerere siku nyingine weka FONT kubwa kaka....

Binafsi sioni sababu ya watu kutukanana na kukejeliana humu jf, maada zinaletwa na zinahitaji kuchangiwa tu unaweza kuwa positive au ukawa negative na ukatoa sababu, hatuwezi kukubaliana wote kwa kila kitu na sehemu yoyote wanapokubaliana kwa kila kitu ujue wana matatizo ya kufikiri.

Mimi kuna sehemu nakubaliana kabisa na Manyerere na kuna sehemu nakataa.... Kenya, Uganda na Rwanda wameanza mikakati yao kwa jina la EAC huku TZ na Burundi zikiachwa nje na nadhani sababu kubwa hapa ni mahusiano yaliyopo kati ya TZ na Rwanda ambapo Kenya ameamua kutumia advantage kupanua soko la bidhaa zake huku akisahau kuwa TZ inatumia sana bidhaa zake, Uganda wenyewe hasa M7 wanahistoria yao na Kagame kwao ni sawa.
Suala la kwenda Kigali kumtoa Kagame siliafiki.
Sioni sababu ya kuendelea na huu uhusiano wetu wa mashaka na kinafiki EAC ningeshauri tusitishe mara moja.
 
Manyerere,

Hongera sana kwa kuueleza ukweli mtupu.
Tanzania hatuna cha kupoteza hata kama tutatengwa na hawa wagomvi.
Kwanza, si vema kilazimisha ushirikiano na watu wasiokutakia mema. Najua Tanzania tuna nia ya dhati kushirikiana na jirani zetu, lakini sioni kama Uhuru, Museveni na Kagame wana nia njema na sisi, Tanzania.

Kwa vyovyote vile mwisho wa mtu mbaya ni aibu mbaya; mwisho wa Kagame umekaribia. Hana muda mrefu kabla mambo yake hayajaharibika kabisa. Kuwatendea hiyana Watanzania ni kujiletea tu laana. Na itampata Kagame yeyote yule mwenye nia mbaya na Watanzania.

Viongozi wetu waangalie mambo haya kwa umakini sana.

MUMGU, Baba yetu wa Mbinguni twakuomba ibariki Tanzania na Watu wake.

Wewe Ngano mungu huwa haingizwi wala hajishughulishi na watu waovu wanaona matatizo kutoka macho yalitiwa boliti wakidhani wakosahihi kushinda yule mwenye kibanzi. Hutaweze kumshirikisha mungu naye akakusikia endapo unafanyama mambo yako kinafiki na kiurongourongo.

Kwanini tukapigane mbona hamtupatii sababu za msingi kabisa genuine beyond reasonable doubt kwamba vita hiyo itakuwa na tija kwa Taifa la tanzania na watanzania? Tunawauliza hawa viongozi wetu wanapata wapi jeuri ya kupigana vita nje ya nchi yetu wakati tunavita mbaya kabisa ya kiuchumi? Je endapo kagame ataamua kupigana moja kwa moja mnaushahidi wakutosha kwamba tutashinda na tukishinda hayo madhara na majeraha ya vita tutayatibu kwa miaka mingapi? Tunafahamu fika wayahudi wanakanchi kadogo sana lakini moto wake unafahamika duniani kote nyuma yake wamarekani wakisupply kila aina ya sophisticated weapon kwa wayahud. Je mnafaham nani yupo nyuma ya kagame au mnakurupuka tuuu. Lakini chamsingi kabisa kagame ametukosea nini sisi watanzania?

Tusiwe wajinga wakukurupukia kila jambo bila kutathimini kama linatija kwetu au tunazunguushwa ili tusahau kashifa na matatizo kibao yanayotusumbua hapa nchini.
 
Ok, kama hivyo ndivyo hapo kwenye RED, kwanini Kikwete aliposema Rwanda iongee na FDLR yeye Kagame na kagenge chake cha wahuni walimtukana....? Kama utaratibu ni kuomba msamaha, unaonaje FDLR wote waombe msamaha kwa pamoja na kusamehewa na kurudi Rwanda....? Uliyosema sio kweli, Rwanda inatumia porojo za FDLR kusakama wahutu na watutsi wanaompinga Kagame kimawazo na pia unatumia excuse hiyo ili kuendelea kuinyonya Kivu...? Hata Gen. Nyamwasa mmesema yeye pia ni FDLR.....ingawa ni kweli Nyamwasa, Kagame, Kabarebe na wengineo walihusika na mauaji ya halaiki Rwanda na Congo!

Inshallah.....with JWTZ tutakunywa chai Kigali...!

Sasa nafikiri unatatizo la kagamephobia,mtu kanitendea makosa badala ya mwenyewe kuja na kuniomba msamaha wewe unaniambia eti niongee naye kama vile ni mimi mwenye kosa? msamaha wajumla haiwezekani kwani hawajawahi kuuomba msamaha,ni jk anayejifanya kua wakili wao,jiulize kwanini nchi kubwa hazithubutu kumwambia pk hayo maneno unafikiri nikwasababu wana muogopa? lahasha wao wanaujua ukweli na uchungu walionao wanyarwanda,kuhusu huyo kayumba kuitwa FDLR nikwa sababu anashirikiana nao kwa sasa,wamejazana GOMA wanapigana begakwabega na FIB,FARDC dhidi ya M23.
 
Manyerere,

Kweli una mawazo ya al-qiada. kweli kuna mfugaji ambaye amewahi kuchoma nyumba na mashamba? huu ni uchochezi kabisa, uliza mtu yeyote kutoka Kagera, hawa watu wanaishi kwa kuliwa. Wanaliwa na police, immigration, idara ya wanyamapori burigi, nk. Walikuja kwasababu kwao hakuna ardhi, huo ndo ukweli, wakati mipaka inawekwa walipewa ardhi kidogo, basi.

Lakini usieneze chuki eti wanachoma mashamba, etc, nenda kafanye utafiti ache jaziba, na usilifanye gazeti lako kuwa la itikadi la ki-nazi, we ni mwandishi wa habari una wajibu wa wananchi, wasomaji na kuleta utengamano wa kijamii na maendeleo sio kuchochea chuki, make makala yako imejaa jazba sana

We mtusi hii discussion kati ya watanzania inakuhusu nini?
 
Nawewe achakutisha watu kigali wanakaribisha hadi watanzania hakuna matata ni nchi yenye amani na watu wakarimu nenda na wewe ujionee peace people,yani utapigwa na butwaa ukifika utaona aibu kwa yote uliyo yaandika dhidi ya rwanda na wanyarwanda,tatizo umezaliwa tz na kueekea tz tembea uone,labda tu ukiwa mmoja wao hao wauaji ujue utafikishwa mahakamani ukikanyaga mguu wako kigali.

We ndio umetembea sana au vita ya huko kwenu ndio ilikuleta Tanzania? Watanzania wanatembea sana lakini katika nchi zenye amani kama ya kwao.
 
Habari ndio hiyo,hizi commandments bado zinafundishwa mpaka sasa huko maporini congo,halafu ndio hao kikwete anasema selikali ya rwanda iongeenao,na hii ideology ndio iliyopelekea hao interahamwe kuua watusi bila huruma kwani hawakua tena na thamani,imagine mtusi hakua na haki kipindi hicho,lakini hi sasa katika selikali ya kagame wahutu wamejazana katika idara mbalimbali za serikali bila ubaguzi,tafuta sehemu yote hautapata mahali pameandikwa mambo ya ubaguzi kwa wahutu yaliyofanywa na watusi,mengi ni maneno ya kutunga tu,lakini ushaidi upo dhidi yahao wahutu wenye msimamo mkali,unategemea mtu mwenye itikadi kama hiyo akiingia kigali kuna mtusi atabaki? lakini ninachojua this time mtusi hatakufa kama ilivyo kua 1994 kwani nao itabidi wajihami.

MukamaMasimba nikushauri tu uache kumshabikia Kagame na kagenge chake cha wahuni...labda kama na wewe ni mmojawapo! Kagame ni mtu dhaifu sana ndio maana hata elimu yake ni ya kuunga-unga.....taarifa zilizopo ni kuwa alikuwa-drop out secondary school, hata mafunzo aliyopelekwa USA kiupendeleo hakumaliza. Hivyo usikubali kuyumbishwa na kiongozi asiye na ufahamu na mbumbumbu...!

Ni kamanda James (Kabarebe) na watu wachache ndio wanaendesha Rwanda sio hata Kagame....! Kamanda James kila mtu anajua ni mwehu, ndio maana pamoja na kutandikwa makofi na Kagame enzi zile Mulindi bado ameendelea kuwa mlamba viatu wa Kagame....tofauti na wenzie wenye kuheshimika ndani ya jeshil la Rwanda...! Ni wehu wake huu Kamanda James aliutumia baada ya kufukuzwa Congo pale alipoenda Ikulu kujifanya anaaga kumbe anataka kumuua Mzee Kabila kwa bastola aliyoficha kwenye kofia kichwani, thanks to mlinzi wa Kabila aliyeamua kumvua kofia na kuiona......! Ni ujasiri huu wa kipumbavu wa Kamanda James alirudi nao Kigali na kumwambia Kagame 'kama unataka kuendelea kuwa kiongozi wetu, niache niandae mashambulizi kuivamia Congo'

Ni Kamanda James na ujinga wake na akina Bizima Karaha na maneno yao ya kipuuzi yalisababisha tena mauaji wa watutsi wasio na hatia Congo....mpaka leo hii kama una shingo ndefu, uwe mrefu mwembamba huwezi kukatiza mitaa ya Kinshasa kwa amani.....wacongoman watakugawana kama fenesi...!

Ni vizuri kama wewe sio mmoja wao uache kumshabikia Kagame na kagenge chake cha wahuni kwa vile anazidi kuweka taswira mbaya ya kabila la watutsi....na kuhatarisha maisha ya wale wasio na hatia...! Nikuhakikishie kuwa mauaji ya halaiki hayatatokea Rwanda kwa vile hata watutsi wanafahamu kuwa adui yao sio wahutu bali watawala wenye tamaa na kukosa ubinadamu kama Kagame.....! Tofauti ya Kagame sasa na ilivyokuwa Habyarimana ni nini...? Cha zaidi Kagame ameua watu wengi zaidi wasio na hatia na pia hataki kuzungumza na waasi, wakati mwenzie angalau alikubali kuzungumza...!

Ni kundi dogo tu la inner-circle ya Kagame na kagenge chake cha wahuni wasiozidi 2,000 ambayo itaathirika kwa sasa

Inshallah....with JWTZ tutakunywa chai Kigali...!
 
Tumeanza kuwatambua watutsi humu JF. Tujadili mada, kejeli na matusi tuviweke pembeni.

Kweli mkuu tujadili mada tu,pia kwa manufaa ya nchi yetu na vixazi vyetu vijavyo. Huwezi kimbilia kuwekeza pasipo na amani ya kweli,huo ni utoto na kujilisha upepo . Watanzania tunasoma mazingira,chekea nyan i Kagame utajavuna mabua, security,political stability.....halafu tutafanya biashara. Anaefikiria kuwa kukimbilia kufanya biashara na kujinufaisha ambako hakuna usalama wa kudumu .
 
Mkuu,

Hiki ndicho wanachofanya wengi wetu hapa jf bila kujua. Rejea pia waraka wa Mtikira ambao nafikiri ndo unafanyiwa kazi. zaidi ikitokea kwa bahati mbaya vijana wa jk waingie Kigari kwa mwono wa wengi hapa nahsi watafanya mabaya zaidi ya 1994 (God forbid). Vita si yakushabia hata kidogo. There is always an option for war.

kwa unyama huu wa rwanda na kiburi cha pk TANZANIA haina jinsi mbali na kuingiza askari rwanda kusimamisha vitisho, dharau, mauji ya halaiki na uporaji wa mali asili ya DRC.
 
Nimesoma waraka wako nimeshindwa kuelewa;

1.0 Kichwa cha habari na content yenyewe. Kwa nini uliamua kuuita waraka kwa JWTZ??

2.0 Vita ni fedha. Kwa hali ya sasa ya Tanzania hatutakiwi kupigana vita yoyote ile. Nchi iliyoshindwa kujitegemea kibajeti tokea uhuru mpaka leo, bado inategemea misaada ku "subsirdise" bajeti yake halafu ikapigane vita!!!

Nashindwa kuelewa mwandishi kama wewe unameshindwaje kuelewa kuwa Tanzania ya JK hali ya uchumi ni mbaya labda kuliko hata Mkapa alipokuwa akiondoka. Kama serikali inashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kukosa fedha itawezaje kugharamia vita ambayo ni ghari kuliko miradi ya maendeleo??? Deni la Taifa kila siku linakuwa kama mimba lakini hatuoni kinachofanyika kisha tukapigane vita!!! Ni jambo la kushangaza sana.

Ukweli kama hujui tukusaidie, serikali ya sasa imebaki kulipa mishahara tu na kupiga propaganda kuwa uchumi unakuwa kwa asilimia fulani huku mwananchi wa chini akizidi kuzama katika dimbwi la umaskini.

3.0 Umeshawahi kujiuliza athari za vita tuliyopigana ya kumng'a Iddy Amini?? Ile vita ilikuwa haikwepeki lakini uchumi wa nchi ulitetereka sana, itakuwaje leo Taifa la kujisifu kwa kupewa misaada tukapigane vita??

Kwangu mimi huu ni waraka wa kishabiki na kipuuzi kabisa.

Ni matumaini yangu kwamba mlete mada amesoma na amekuelewa,uliyoyaongea yana maana tushishabikie vita wakat hali ya uchumi ni mbaya na kweli vita yoyote ile ni gharama,tujikumbushe vita ya kagera ilivyoigharimu hii nchi.
 
mukamamasimba nikushauri tu uache kumshabikia kagame na kagenge chake cha wahuni...labda kama na wewe ni mmojawapo! Kagame ni mtu dhaifu sana ndio maana hata elimu yake ni ya kuunga-unga.....taarifa zilizopo ni kuwa alikuwa-drop out secondary school, hata mafunzo aliyopelekwa usa kiupendeleo hakumaliza. Hivyo usikubali kuyumbishwa na kiongozi asiye na ufahamu na mbumbumbu...!

Ni kamanda james (kabarebe) na watu wachache ndio wanaendesha rwanda sio hata kagame....! Kamanda james kila mtu anajua ni mwehu, ndio maana pamoja na kutandikwa makofi na kagame enzi zile mulindi bado ameendelea kuwa mlamba viatu wa kagame....tofauti na wenzie wenye kuheshimika ndani ya jeshil la rwanda...! Ni wehu wake huu kamanda james aliutumia baada ya kufukuzwa congo pale alipoenda ikulu kujifanya anaaga kumbe anataka kumuua mzee kabila kwa bastola aliyoficha kwenye kofia kichwani, thanks to mlinzi wa kabila aliyeamua kumvua kofia na kuiona......! Ni ujasiri huu wa kipumbavu wa kamanda james alirudi nao kigali na kumwambia kagame 'kama unataka kuendelea kuwa kiongozi wetu, niache niandae mashambulizi kuivamia congo'

ni kamanda james na ujinga wake na akina bizima karaha na maneno yao ya kipuuzi yalisababisha tena mauaji wa watutsi wasio na hatia congo....mpaka leo hii kama una shingo ndefu, uwe mrefu mwembamba huwezi kukatiza mitaa ya kinshasa kwa amani.....wacongoman watakugawana kama fenesi...!

Ni vizuri kama wewe sio mmoja wao uache kumshabikia kagame na kagenge chake cha wahuni kwa vile anazidi kuweka taswira mbaya ya kabila la watutsi....na kuhatarisha maisha ya wale wasio na hatia...! Nikuhakikishie kuwa mauaji ya halaiki hayatatokea rwanda kwa vile hata watutsi wanafahamu kuwa adui yao sio wahutu bali watawala wenye tamaa na kukosa ubinadamu kama kagame.....! Tofauti ya kagame sasa na ilivyokuwa habyarimana ni nini...? Cha zaidi kagame ameua watu wengi zaidi wasio na hatia na pia hataki kuzungumza na waasi, wakati mwenzie angalau alikubali kuzungumza...!

Ni kundi dogo tu la inner-circle ya kagame na kagenge chake cha wahuni wasiozidi 2,000 ambayo itaathirika kwa sasa

inshallah....with jwtz tutakunywa chai kigali...!

hakika tanzania tuna hazina kubwa. Sasa kazi ni moja tu, kumtoa huyu mwehu madarakani.
 
Back
Top Bottom