Hakuna kigezo cha ukanda , ukabila wala udini.
Vigezo viwe kwenye sifa (merits) za muombaji kama elimu, uzoefu, uadilifu, uchapakazi, n.k.
Hizo sifa ni mifumo tu ya Kibabiloni na kikoloni ambayo haina manufaa kwa jamii zaidi ya ubinafsi na ufahari tu wa familia zao.
Tangu Uhuru tumewapa nafasi kubwa wasomi wengi waliosoma uzeeni kwa lengo la kupata vipato vikubwa lakini sio kwa lengo la kutuletea maendeleo kama Taifa.
Matokeo yake ni watu kukimbilia kwenye siasa na kujiwekea sheria za kuwapa Mishahara mikubwa ,kuwapa fursa zaidi za kusafiri kwenda Ulaya na kujilimbikizia Mali huku waliopo chini wakiendelea kuishi kwa maslahi duni sana.
Ofisi moja mtendaji mkuu kabisa anayewahi kufungua Ofisi na kuchelewa kufunga ofisi analipwa laki 3 ,hana usafiri wa umma, hana nyumba ya serikali ,bima daraja la kawaida ana familia kama wao lakini wasomi wenye PhD na Maprofesa hawajali hilo na hawana mpango kabisa wa kuboresha maisha ya hao wanaowaita wakimbia umande. Wasomi hao wanachowaza ni kujiwekea mazingira mazuri ya kupiga pesa tu na kutembelea magari ya kufahari kwa fedha za umma.
Waislama na Uislam una mambo Mengi mazuri sana sana lakini kuna tatizo sana kwa waislam wenyewe kusimama upande wa dhulma na kupigania vyeo na kuweka unafiki Mbele.
Uislam na Dini ya kiyahudi na Kikristo na dini za asili vimekua mstari wa Mbele kupigania usawa na utu lakini wasomi ndio watu walioleta matabaka yasiyozingatia ubinadam.
Yani mtu anasomeshwa na jamii kwa lengo la kuitumikia jamii matokeo yake anakua ni Bwana mkubwa na jamii inayolipa kodi inakua ni watumwa wake.
Uongozi ni kipaji sio PhD lakini kwa Afrika kiongozi uongozi umekua ni dili la kupata utajiri na maisha mazuri ndio maana Wasomi wanakimbilia huko kwa CV zao lakini Rohoni hawana karama hiyo ya uongozi wala hawana mipango ya kumkomboa mtu wa chini.
Nchi zote zilizoendelea kama Kuweit, Saud Arabia, Ujerumani,China, Qatar , Japan, Marekani ,Uingereza, Urusi, Uholanza, Denmark, Norway ,Libya ya zamani, Israeli ,Uturuki n.k. Wasomi wote wanafanya kazi za kitaalam kwa ajili ya kujenga nchi zao na kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi wao.
Tanzania PhD sasa zinakimbilia madaraka na kisiasa tu. PhD gani kwenye maofisi ya umma ya kutoa huduma ,ujasiriamali , kilimo binafsi kuunganisha ushirika wa vikundi binafsi na biashara binafsi , hizo PhD hazifanyi kazi vizuri na kuleta tija na ajira binafsi Bali ni kwenye siasa tuu ndio zinajifanya ndizo zinazojenga nchi?
Wasomi wa PhD miaka 60 ya Uhuru mpaka sasa bado tunatumia Elimu yenye mitaala ya Kikoloni. Mitaala inayowaandaa watu kukimbilia PhD za Historia na Kiswahili na Kilimo lakini mtu hana hata robo heka ya shamba ,lengo lake aajiriwe apate mshahara mkubwa akeshe baa na walevi ndio anajiona kamaliza kutumia kipaji alichojilazimishwa kupitia elimu ya Kikoloni. Elimu isiyozingatia vipaji vya watu.
Woga wa Wasomi waliokua wameandaliwa na wakoloni wamesababisha wasomi halisi wabaki na vipaji vyao binafsi bila kupata vyeti vinavyothibitisha uwezo wao mkubwa waliojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Waacheni watu wa taasisi mbalimbali watoe maoni yao kuelekea uchaguzi mkuu ili watakao ingia madarakani wajue kuwa wanaongoza binadam waliopewa vipaji na imani tofauti katika kulitumikia taifa lakini cha msingi ni kuzingatia haki na usawa.