Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Hakuna kigezo cha ukanda , ukabila wala udini.
Vigezo viwe kwenye sifa (merits) za muombaji kama elimu, uzoefu, uadilifu, uchapakazi, n.k.
Hizo sifa ni mifumo tu ya Kibabiloni na kikoloni ambayo haina manufaa kwa jamii zaidi ya ubinafsi na ufahari tu wa familia zao.

Tangu Uhuru tumewapa nafasi kubwa wasomi wengi waliosoma uzeeni kwa lengo la kupata vipato vikubwa lakini sio kwa lengo la kutuletea maendeleo kama Taifa.

Matokeo yake ni watu kukimbilia kwenye siasa na kujiwekea sheria za kuwapa Mishahara mikubwa ,kuwapa fursa zaidi za kusafiri kwenda Ulaya na kujilimbikizia Mali huku waliopo chini wakiendelea kuishi kwa maslahi duni sana.

Ofisi moja mtendaji mkuu kabisa anayewahi kufungua Ofisi na kuchelewa kufunga ofisi analipwa laki 3 ,hana usafiri wa umma, hana nyumba ya serikali ,bima daraja la kawaida ana familia kama wao lakini wasomi wenye PhD na Maprofesa hawajali hilo na hawana mpango kabisa wa kuboresha maisha ya hao wanaowaita wakimbia umande. Wasomi hao wanachowaza ni kujiwekea mazingira mazuri ya kupiga pesa tu na kutembelea magari ya kufahari kwa fedha za umma.

Waislama na Uislam una mambo Mengi mazuri sana sana lakini kuna tatizo sana kwa waislam wenyewe kusimama upande wa dhulma na kupigania vyeo na kuweka unafiki Mbele.
Uislam na Dini ya kiyahudi na Kikristo na dini za asili vimekua mstari wa Mbele kupigania usawa na utu lakini wasomi ndio watu walioleta matabaka yasiyozingatia ubinadam.
Yani mtu anasomeshwa na jamii kwa lengo la kuitumikia jamii matokeo yake anakua ni Bwana mkubwa na jamii inayolipa kodi inakua ni watumwa wake.

Uongozi ni kipaji sio PhD lakini kwa Afrika kiongozi uongozi umekua ni dili la kupata utajiri na maisha mazuri ndio maana Wasomi wanakimbilia huko kwa CV zao lakini Rohoni hawana karama hiyo ya uongozi wala hawana mipango ya kumkomboa mtu wa chini.

Nchi zote zilizoendelea kama Kuweit, Saud Arabia, Ujerumani,China, Qatar , Japan, Marekani ,Uingereza, Urusi, Uholanza, Denmark, Norway ,Libya ya zamani, Israeli ,Uturuki n.k. Wasomi wote wanafanya kazi za kitaalam kwa ajili ya kujenga nchi zao na kutoa huduma bora na za kisasa kwa wananchi wao.

Tanzania PhD sasa zinakimbilia madaraka na kisiasa tu. PhD gani kwenye maofisi ya umma ya kutoa huduma ,ujasiriamali , kilimo binafsi kuunganisha ushirika wa vikundi binafsi na biashara binafsi , hizo PhD hazifanyi kazi vizuri na kuleta tija na ajira binafsi Bali ni kwenye siasa tuu ndio zinajifanya ndizo zinazojenga nchi?

Wasomi wa PhD miaka 60 ya Uhuru mpaka sasa bado tunatumia Elimu yenye mitaala ya Kikoloni. Mitaala inayowaandaa watu kukimbilia PhD za Historia na Kiswahili na Kilimo lakini mtu hana hata robo heka ya shamba ,lengo lake aajiriwe apate mshahara mkubwa akeshe baa na walevi ndio anajiona kamaliza kutumia kipaji alichojilazimishwa kupitia elimu ya Kikoloni. Elimu isiyozingatia vipaji vya watu.

Woga wa Wasomi waliokua wameandaliwa na wakoloni wamesababisha wasomi halisi wabaki na vipaji vyao binafsi bila kupata vyeti vinavyothibitisha uwezo wao mkubwa waliojaliwa na Mwenyezi Mungu.

Waacheni watu wa taasisi mbalimbali watoe maoni yao kuelekea uchaguzi mkuu ili watakao ingia madarakani wajue kuwa wanaongoza binadam waliopewa vipaji na imani tofauti katika kulitumikia taifa lakini cha msingi ni kuzingatia haki na usawa.
 
Wanachotaka hawa Maimamu ni usawa katika kugawana keki ya taifa.
Usawa kwa kila kitu kwa raia wote.

Hoja yao siyo dini fulani tu washikie fursa zaidi ya waumini wa dini zingine au wasiokuwa na dini.
Sijui wewe umewaelewaje? labda unifafanulie walikuwa wanakusudia kusema nini hapo kwenye teuzi.

wanataka haki itendeke kama katiba zinavyosema ,hujakosea
 
Waeanza kujitambua itakuwa sio bakwata.
Wa bakwata wapenda ubwabwa wakiongozwa na yule shehe wa mkoa wa Bashite hawawezi kutoa tamko la namna hii. Wao wanasubiri siku ya kuapishwa tu Dom wakale wapige na picha full stop
 
Hao hawatusemei waislamu wote.....hao Wala hawatambuliki KISHERIA kutusemea.

Muislam Mimi SIYATAKI HAYO WAYASEMAYO.
Muislam mimi na wenzangu tulio wengi tunataka kuiona tume HIIHII iendelee kwani iko KISHERIA na haina dosari zozote.......

Waislam tunasemewa na BARAZA letu kuu BAKWATA.

WENGINE WANAKUWAGA WALE WACHOCHEZI WACHACHE.
Jisemee Wewe tafadhali, na usifanye Waislam waonekane hawawezi kung’amua.
Na hilo DUBWANA BAKWATA ni lenu peke yenu.
 
uko mwanzoni wameenda vizuri sana ila waliponza kuongelea mambo ya udini ndo nikajua hawa jamaa ni wapumbavu sana:(:(:(, wanafikiri juu ya uislam na ukristo tu, je vipi wale wasiokua na dini??

Je, vipi juu wale wasioamini juu ya mungu?? wao hawastahili hayo yote??? Hizi dini zinajaza watu upumbavu mwingi sana kichwani, badala ya kuangalia mambo ya msingi we unaangalia eti waslam/wakristo wangap wameteuliwa..Dini nyingine wasemaje???
 
Kean kwa teuz hizo wakristo wamefaidi nini na waislamu wamekosea nini?

Kwan Kuna barabara au shule au hospital nk Za wakritu na Za waislamu?
 
Titi...
Tutafanyaje inapokuwa waumini wa dini moja tu ndiyo wanakuwa na sifa za elimu, uxoefu, uadilifu, uchapakazi nk. kwa hiyo ndiyo wanaoongoza serikali na wengine wako nje?

Katika hali kama hii tunafanyaje?
Mzee nyie ndio mnatakiwa kupotezwa

Umejaa chuki na udini,Mna propaganda za kutaka vita

Na mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi

You are not so safe,Watch your family first

Hii nchi asilimia 90 hawana dini wala vyama..
 
Huyu si PONDA karudi kwa mlango wa nyuma kweli. Wakumbuke huu upuuzi wa udini uliwa-cost sana miaka 1998/1999 kama sijakosea mwaka. Kwenye suala la watumishi wa UDOM kuondolewa kwenye nafasi zao naona hapa huyu mwandishi anataka kutuaminisha kwamba walitolewa kwenye hizo nafasi zao kwa sababu za kidini. Huo ni uzushi maana inavyooneka hata huyu mwandishi hana uhakika na anachokisema zaidi ya majungu tu hana ushahidi wowote. Pili watu hawaajiriwi kwa sababu ya dini yao hakuna mwongozo kama huo hayo madai ni kutojiamini kwao tu.

Tanzania kama Taifa hakuna mtu yoyote anabaguliwa kupata huduma za jamii kwa misingi ya kidini. Raia wote tunapata haki sawa bila kujali tofauti zetu zozote zile maana wote tunachangia kwenye pato la taifa.

WATU WASITUMIE MAJUKWAA KAMA HAYA YA SHURA YA MAIMAMU KWA AJILI YA MASLAHI NA MATAKWA YAO BINAFSI. TENA AMINI NAWAAMBIA HAKUNA KITU KIBAYA KUENDEKEZA UDINI NA UKABILA NI MAJANGA.
 
Hawa wa kuendeleza ushoga na usagaji tatizo lao Muislamu akijitetea na kudai haki ya baada ya kufanywa raia wa daraja la pili hasa katika awamu hii ya tano, ataitwa mdini,gaidi na mchochezi,lakini wao wanapouendekeza inakuwa ni haki yao na zaidi wanatupiga sana kwenye elimu
 
Mzee nyie ndio mnatakiwa kupotezwa

Umejaa chuki na udini,Mna propaganda za kutaka vita

Na mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi

You are not so safe,Watch your family first

Hii nchi asilimia 90 hawana dini wala vyama..
Madu...
Kumtishia mtu maisha yake ni kosa la jinai.

Nikifikisha hiki kitisho chako kwenye vyombo vya sheria utakuwa matatani.

Hatari yake ni kuwa unajihatarishia maisha yako mwenyewe na walio karibu na wewe sababu ni kuwa uliyechomoa upanga kutoka kwenye ala yake ni wewe.

Tuliza akili yako.

Huna moyo wa kustahamili jikalie pembeni utakuwa salama.

Uliyejaa chuki ni wewe usiyeweza kustahamili kusikiliza mawazo ya wengine.

Wala hapa JF hapana vita tunajadiliana kwa heshima na adabu.
 
Huyu si PONDA karudi kwa mlango wa nyuma kweli. Wakumbuke huu upuuzi wa udini uliwa-cost sana miaka 1998/1999 kama sijakosea mwaka. Kwenye suala la watumishi wa UDOM kuondolewa kwenye nafasi zao naona hapa huyu mwandishi anataka kutuaminisha kwamba walitolewa kwenye hizo nafasi zao kwa sababu za kidini. Huo ni uzushi maana inavyooneka hata huyu mwandishi hana uhakika na anachokisema zaidi ya majungu tu hana ushahidi wowote. Pili watu hawaajiriwi kwa sababu ya dini yao hakuna mwongozo kama huo hayo madai ni kutojiamini kwao tu.

Tanzania kama Taifa hakuna mtu yoyote anabaguliwa kupata huduma za jamii kwa misingi ya kidini. Raia wote tunapata haki sawa bila kujali tofauti zetu zozote zile maana wote tunachangia kwenye pato la taifa.

WATU WASITUMIE MAJUKWAA KAMA HAYA YA SHURA YA MAIMAMU KWA AJILI YA MASLAHI NA MATAKWA YAO BINAFSI. TENA AMINI NAWAAMBIA HAKUNA KITU KIBAYA KUENDEKEZA UDINI NA UKABILA NI MAJANGA.
Luriga,
Tuwe na subira tuwape muda waliokusudiwa wasome waraka bila shaka watatoa majibu mathalan kuwa kuwatoa Waislam 11 UDOM na kujaza nafasi zao na Wakristo 11 kulisababishwa na sababu kadha wa kadha nk.

Tusiwe na haraka.
 
uko mwanzoni wameenda vizuri sana ila waliponza kuongelea mambo ya udini ndo nikajua hawa jamaa ni wapumbavu sana:(:(:(, wanafikiri juu ya uislam na ukristo tu, je vipi wale wasiokua na dini?? je vipi juu wale wasioamini juu ya mungu?? wao hawastahili hayo yote??? Hizi dini zinajaza watu upumbavu mwingi sana kichwani, badala ya kuangalia mambo ya msingi we unaangalia eti waslam/wakristo wangap wameteuliwa..Dini nyingine wasemaje???
Hunijui...
Subira waliokusudiwa watakuja na majibu.

Ama kuhusu wasio na dini utapata shida kuwafananisha na Waislam.

Soma historia jinsi Waislam walivyopigania uhuru wa Tanganyika kuondoa ukoloni ili pawe na haki na usawa kisha watafute hao wasiokuwa na dini uangalie walikuwa wapi.

Tanganyika haikuwa na kundi hilo si katika Vita Vya Maji Maji wala katika TAA/TANU.

Hivyo hivyo hii leo kundi hilo halipo.
 
Status
Not open for further replies.
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom