Uchaguzi 2020 Waraka wa Uchaguzi wa Shura ya Maimamu Tanzania

Status
Not open for further replies.
Kama asilimia kubwa ya wasomi ni wakristo, ni wazi asilimia kubwa watakuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira, labda kama waajiri wataanza kuangalia kigezo cha dini badala ya vigezo vya taaluma, hapo ndo mzani unaweza kuwa sawa.....
 
Teuzi na upandishwaji vyeo lazima vifanyike kwa kuangalia sifa na vigezo vya mtu husika.
Lazima viwe 'based on merits' siyo sifa ya udini au ukabila.

Neno teua au (teuzi) halikwepi upendeleo kuondoa hizo hisia ni bora likatumika neno ( ajira) kuwe na kamati maalum ya kuajiri hizo teuzi
 
Mnataka mtafuniwe na kumezeshwa kabisa yakhee?
Kwa juhudi zetu tungekuwa hutupiganii mafanikio yetu tungeshapotea ila tunapambana ingawa mnaturudisha nyuma, na kupigania yako haimaanishi unyamaze unapambana huku unasema
 
Kama asilimia kubwa ya wasomi ni wakristo, ni wazi asilimia kubwa watakuwa kwenye mfumo rasmi wa ajira, labda kama waajiri wataanza kuangalia kigezo cha dini badala ya vigezo vya taaluma, hapo ndo mzani unaweza kuwa sawa.....
Tatizo hata hao waislam (wachache kwa mujibu wao) waliosoma wakianza kuchomoza wanarudishwa angalia Gaudencia na timu yake walivyotoa waislam 11 UDOM na kuweka wakristo
 
Tatizo hata hao waislam (wachache kwa mujibu wao) waliosoma wakianza kuchomoza wanarudishwa angalia Gaudencia na timu yake walivyotoa waislam 11 UDOM na kuweka wakristo
Hapo ndo penye tatizo, na kuna taasisi ambazo kama mtendaji mkuu ni mwislamu au maafisa utumishi ni waislamu wanawakandamiza watumishi ambao ni wakristo, niliwahi kulisikia nssf hili.....ni bora sasa taratibu zifuatwe ili kuondoa hii mikanganyiko ya kidini maana haiwezi kuleta tija yoyote katika jamii..
 
Hapa tulipaswa kuanza kujiuliza ilikuaje wote nafasi hizo walikuwa waislamu? Halafu ndo tuje ktk mjadala wa pili. Lakini pia tungeanza na uwiano Uliokuwepo na Uliopo wa wafanyakazi wa dini hizi mbili hapo UDOM. maana hizi kelele huwezi zisikia UDSM au MZUMBE.
 
Hao unaosema wanalialia ndiyo Majority walioanzisha harakati za kumng'oa mkoloni, wakati huo Wakiristu wengi wakiwa ni watoto watiifu wa mkoloni.
Baada ya Uhuru badala ya kuwa treated fairly, bahati mbaya yule mtu waliyemuamini kuwa atakuwa fair kwa wote akasimika mfumo unaofavor watu wa dini yake nchini, mfumo ambao ni pasua kichwa kwelikweli, Vitengo vyote muhimu kajaza watu wa dini yake, Maraisi wauslamu walipojaribu kuwa fair kwa wote wanakutana na barua kali za kichungaji zenye maonyo yaliyofichika ya kutishia kuvuruga amani ya nchi iwapo zitafanyika reforms za haki nchini.

Ndiyo maana hata mkuu wa mkoa wa Dar es salaam anasema nchi hii iko chini ya Kanisa. Yuko sahihi, anazungumza ukweli mchungu.

Kwa hiyo waache waislamu waendelee kulialia kwa sababu wanabaguliwa katika ajira, na teuzi za kuitumikia nchi.

Wewe huwezi kuelewa feelings za waislamu kwa sababu ni mnufaika wa mfumo, hapa unachokifanya unatetea maslahi yako na watoto na wajukuu zako.

But Fahamu kwamba, Wanaosimamia mfumo wa ajira na utumishi na teuzi za kiserikali nchini ni dhahiri wako too biased against Muslims.

Unaweza kuwabeza waislamu, lakini hawako radhi na jinsi mambo yanavyofanywa.

Unaweza wewe kama wewe ukapuuza madai haya lakini waislamu in majority wanayaunga mkono na hawapendezwi na hali hii. Sasa chagueni tu muendelee na business as usual au muaddress madai haya ya waislamu, Msipoyaddress basi hili ni bomu linalosubiri kupasuka, It is a matter of time
Hahaha, huu Uzushi wa wafuasi wa Mwamedi huwa inashangaza sana

Sasa baada ya kumuondoa Mkoloni mkaishia wapi?

Teh teh teh......
 
Kumbe huwa mnahesabu, ? na kuweka asilimia, wengine hatujawahi kufikiria hayo kabisa.
Hapo ndipo utajua wana muda wa hovyo

Badala wakutane kujadili namna ya kujikomboa kiuchumi na kielimu wao huwa wanatafuta kulaumu tu.
 
Katika waraka huu;

Kwanza niupongeze maana umeandaliwa kisomi sana na lengo lake mahsusi ni kutoa rai kwa umma wa watanzania kuelekea uchaguzi mkuu Oct 2020. Hongera kwenu waandaaji.

Pili yaliyomo ndani yake nayaunga mkono kwa zaidi ya 80% maana yamegusa uhalisia wa sura ya taifa letu la Tanzania. Yameelezwa kiungaubaga bila hofu wala kificho wala kuonea upande kweli yamebalance. Japo, binafsi ninaweza kuargue juu ya nafasi za uteuzi katika usawa; hapo sidhani kama tutaweza kupata mlinganyo sahili kwa kutumia kigezo cha udini bali hekima yapaswa kutumika katika kutatua hili ingawa sura yake hili jambo kuna kitu linakielezea. Katika kuepuka hili nashauri mabadiliko ya kikatiba na kumpunguzia mamlaka ya kiuteuzi rais na badala yake teuzi hizo zifanyike kwenye vyombo vingine vya kimamlaka kama tume za ajira n.k

Waraka huu, umeelezea pia jinsi vitendo ambavyo sio vya kawaida kutokea kwenye jamii ya watanzania kama kupotezwa kwa watu hasa wanaonekana wapinzani wa serikali na wengine hata kuuawa. Kushindwa kuliongelea tukio baya kabisa lilitokea Dodoma maeneo ya bunge la kushambuliwa kwa Mh Tundu Lisu limetia doa waraka huu aidha kwa kusahaulika ama bahati mbaya.

Ushauri wangu; kweli siasa ni maisha ya watu na hakuna namna jamii inaweza kwepa ukweli huu. Vivyo hivyo makundi au taasisi mbalimbali zitoe nyaraka kama hizi zenye kuamsha ari kwa wanajamii na viongozi katika jamii yetu itasaidia sana. Mungu awabariki.
 
Mi niliwah kuwa na kesi mahakama ya ardhi pale mwananyamala. Hakim alikuwa anaitwa Mohamed.nilikuja kugundua Alikuwa mlokole wa kufa mtu. So jina lisikuhakikishie din ya mtu
Kitali,
Yawezekana lakini uwezekano wa kumkuta Mkristo au Muislam ambae ana jina si la dini yake ni mdogo sana.

Sasa ikiwa tutakuwa tunakwepa kuwa lipo tatizo tutakuwa tunajitengenezea wenyewe tatizo kubwa sisi wenyewe huko tunakokwenda.

Nyerere katika hotuba yake ile aliyotoa hoja hiyo alikuwa kajiingiza kwenye mtego wake mwenyewe kwa sababu ukweli unajulikana.

Prof. Njozi katika kitabu chake kilichopigwa marufuku kuingizwa Tanzania, "Mwembechai Killings..." kafanya uchambuzi wa tatizo hili kwa kirefu na kwa kutoa ushahidi kiasi cha kujiuliza ni kitu gani kilimfanya Nyerere aseme maneno yale ilhali anaujua ukweli?
 
Kitali,
Maana yangu si hiyo kuwa wapewe vyeo.

Hofu yangu ni kuwa ile hali ya kupigania uhuru itarejea upya Waislam watapambana na serikali yao kudai kile walichokipigania chini ya TANU.

Kwahili nakuunga mkono mzee Said

Check and balance nimuhimu sana katika afya na uhai wa Taifa letu.
 
Kitali,
Maana yangu si hiyo kuwa wapewe vyeo.

Hofu yangu ni kuwa ile hali ya kupigania uhuru itarejea upya Waislam watapambana na serikali yao kudai kile walichokipigania chini ya TANU.
Kazi mnayo kwa mawazo hayo.
 
Kwahili nakuunga mkono mzee Said

Check and balance nimuhimu sana katika afya na uhai wa Taifa letu.
Check and balance ya kweli itakuja tu kwa njia ya kikatiba siyo kwa maono ya Rais aliyeko madarakani ambaye katiba ya sasa haimlazimishi kufuata hicho wnachotaka hawa kina shura ya maimamu.
 
Hapo ndo penye tatizo, na kuna taasisi ambazo kama mtendaji mkuu ni mwislamu au maafisa utumishi ni waislamu wanawakandamiza watumishi ambao ni wakristo, niliwahi kulisikia nssf hili.....ni bora sasa taratibu zifuatwe ili kuondoa hii mikanganyiko ya kidini maana haiwezi kuleta tija yoyote katika jamii..
Hiyo nssf inayolalamikiwa ilikuwa na 69% ya watumishi ni wakristo, kisa boss mkuu muislam imekuwa shida na angalia alivyotolewa muislam akawekwa mkristo huku ahadi zikitolewa hamtakaa mpate mkurugenzi muislam milele
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom