Waraka mfupi wa maombi, toka kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jami kwenda kwa Waziri wa Afya

Dat4

Member
Aug 24, 2022
96
148
Copy and Pasted

WARAKA WA MAOMBI YA KUPEWA FURSA YA KUJIENDELEZA KIELIMU KWA KOZI NYINGINE ZA AFYA KWA KUTUMIA CHETI CHA UHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII (COMMUNITY HEALTH WORKER).

Kwa Waziri wa afya

Katibu mkuu wizara ya Afya,

Mkurugenzi wa idara ya mafunzo wizara ya afya
,

Kwanza kabisa tunapenda kutoa shukrani za dhati na za kipekee kwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha huduma za afya na kuhakikisha watanzania wote wanapata Huduma bora za afya nchini, kwa kuendelea kujenga vituo vya afya, Hospitali na zahanati mbalimbali nchini sambamba na utoaji wa ajira kwa kada zote za afya ili kuhakikisha wananchi wanapata Huduma bora kabisa

Vile vile kwa ufupi tunapenda kutambulisha kada ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii iliyopo ndani ya kada za afya ambayo wahitimu wake huajiriwa katika taasisi za afya, Hospitali, vituo vya afya na zahanati kama Health assistant

Ndg Mhe.
Bila kupoteza wakati na kwa umuhimu mkubwa Tunapenda kuleta maombi yetu kwako kama ifuatavyo:

Katika mwaka wa masomo 2015/2016. Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Baraza la elimu na vyuo vya ufundi NACTE kwa sasa (NACTVET) ilianzisha kozi ya uhudumu wa Afya ngazi ya jamii yaani (Community health worker) mojawapo ya sifa ya kujiunga na kozi hii ni wahitimu wa kidato cha nne wenye ufaulu wa kuanzia masomo manne (4) na somo la Baiolojia likiwa ni lazima. vile vile sifa nyingine ya kusoma kozi hii ilikua ni wale waliopitia mafunzo ya uhudumu wa afya (Medical attendants) nao waliweza kuruhusiwa kusoma kozi hii kama equivalent qualification.

Kozi hii ilituandaa kufanya kazi katika sehemu kuu tatu (3) yaani vituo vya kutolea huduma za afya, ustawi wa jamii na ndani ya jamii husika (katika vijiji).

Kozi hii ilitoa wahudumu wa afya ngazi ya jamii katika awamu nne yaani 2015/2016, 2016/2017, 2017/2018 na 2018/2019, ilipofika mwaka 2019 mwezi mei Baraza la elimu ya vyuo vya ufundi NACTE lilitoa tangazo la kusitishwa kwa kozi hii, hadi pale itakapotangazwa tena.

Mara baada ya kozi ya community health worker kusitishwa tumeendelea kuajiriwa katia taasisi za afya ikiwemo Muhimbili,KCMC, bugando na hospitali za mikoa na wilaya, vituo vya afya na zahanati, Tunaishukuru sana serikali na wizara ya Afya kwani inaendelea kuwaajiri wahudumu hawa kwa hakika tunatambua juhudi zote zinazofanya na viongozi wa serikali ya Tanzania,

Ndg Mhe,
Pamoja na nia njema ya wizara ya afya na serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumekuwa na changamoto kwetu ya kushindwa kujiendeleza kielimu na kuongeza ujuzi kazini kwa kozi yoyote ile ndani ya kada za afya mara baada ya kozi ya community health kufutwa. tunapenda kuleta mbele zako ombi moja tua ambalo ni:

Tunaomba Cheti cha Community Health Training (CHT) kutoka NACTVET kiruhusiwe kutumika kama equivalent qualification kujiunga na kozi zingine za afya kuanzia ngazi ya NTA LEVEL 4

Ndg Mh kipekee kabisa tunaomba kuwasilisha maombi haya mikononi mwako, kwani kulingana na kwamba hakuna muendelezo wa kada ya community health ngazi ya NTA level 5 mpaka 6 hivyo tunaomba cheti cha CHT kitumike kama equivalent qualification ya kujiunga na kozi zingine za afya kwanzia hatua ya kwanza ya NTA level 4, mfano kusoma kozi ya uuguzi na ukunga kwaanzia ngazi ya NTA level 4,5 na hadi 6 kwa kutumia cheti cha ChT kama equivalent qualification, ili na sisi tuweze kuongeza ujuzi kazini na kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa jamii kama lilivyo lengo la wizara ya afya,

Tuwapo katika utekelezaji wetu wa majukumu hususa ni katika ngazi ya vituo vya afya na zahanati tunafanya shughuli nyingi za kuhudumia wagonjwa hivyo tungependa rasmi kuwa qualified kwa kupewa fursa ya kujiendeleza na ujuzi kazini hususa ni kwa kada za uuguzi ambapo tupo katika kundi hilo.

Rejea Jedwali la mwaka 2015/2016 linaloonesha kozi kozi ambazo tungeweza kuendelea nazo baada ya kuhitimu kozi ya Community health
IMG_20230925_182207.jpg
MWISHO
Ndg Mhe
Tunamaliza kwa kutoa shukrani kwako na kwa wizara ya afya kwa kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa kwa wananchi na kwa weledi mkubwa kutoka kwa watumishi wa kada ya afya wenye vigezo na mafunzo mbalimbali ya utoaji huduma, Ni imani na matumaini yetu kuwa myatafanyiwa kazi ndani ya muda muafaka.

IMEANDALIWA NA WAHUDUMU WA AFYA (HEALTH ASSISTANTs) WALIOUNGANA KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII
 
Back
Top Bottom