Agizo la Rais ni amri

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Juzi Mhe. Rais akiwaapisha Wateule wake alikemea sana wizi unaofanyika Serikalini na baadaye akasema kuwa kuanzia sasa Halmashauri zitapewa fedha kutoka Serikalini kutokana na makusanyo yake.

Mfano kama halmashauri itakusanya 50% basi Serikali itawapa pia 50%.. Agizo la Mhe. Rais ni amri lakini kwa ukweli uanzishwaji wa baadhi za Halmashauri hazikufuata vigezo na hivyo kupelekea kuwa na makusanyo madogo sana.

Tuchukue mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo ilimegwa na kuanzishwa Halmashauri ya Mji wa Bunda na kupelekea mapato yake kupungua kwa kasi kubwa. Pato kubwa la Halmashauri ya Bunda ni samaki.

Kusema ukweli samaki katika Ziwa Victoria ni kama wamekwisha kabisa na hivyo Halmashauri ya Bunda ni mojawapo ya Halmashauri maskini katika nchi hii na hivyo tunamwomba Mhe. Rais kuwa utafiti wa agizo hili ufanyike kwanza ili kufikia uamuzi wa agizo alilolitoa.

Halmashauri kama Bunda, Rorya, Bumbuli n.k. zitaathirika sana. Mwisho, kuanzia sasa uanzishwaji wa Halmashauri ufuate vigezo vinavyotakiwa na siyo kwa tamaa za wachache kupata ubunge.
 
Bunda!home sweet home!!
Kumbe siku hizi ni maskini tena!!

Wasalimie pale DDH hospital,Mtaa wa RTC pale palipokua na MK Bar miaka ya tisini,wape Hi sana kina Mohamedi kesi wale waarabu was pale dairy (deire) karibu na stendi ya zamani,tulinunua maziwa pande zile!MPE Hi Jamil muarabu mmoja hivi mpangaji mwenzetu enzi hizo nikiwa dogo na utundu was kutosha!

Kina mshangi,masaba,katikiro,evarist,makanya,mfungowa mama,evarist,maiko poo,magoli,nyabina,mkwaya,zawadi,makongoro, aiseh hizo kamanda nitazionea wapi tena!!?

Palikua patamu sana miaka Ile kabla ya kusafiri ghafula kuja Kanda ya kati,hasta sijui Mzee Nini kilimtokea aiseh akakatisha utamu wangu wa kukatisha mitaa na kutega njiwa manga sokoni!!
 
Rais wetu anatoa maagizo ambayo hata yeye mwenyewe hayafuatilii
 
Juzi Mhe. Rais akiwaapisha Wateule wake alikemea sana wizi unaofanyika Serikalini na baadaye akasema kuwa kuanzia sasa Halmashauri zitapewa fedha kutoka Serikalini kutokana na makusanyo yake.

Mfano kama halmashauri itakusanya 50% basi Serikali itawapa pia 50%.. Agizo la Mhe. Rais ni amri lakini kwa ukweli uanzishwaji wa baadhi za Halmashauri hazikufuata vigezo na hivyo kupelekea kuwa na makusanyo madogo sana.

Tuchukue mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo ilimegwa na kuanzishwa Halmashauri ya Mji wa Bunda na kupelekea mapato yake kupungua kwa kasi kubwa. Pato kubwa la Halmashauri ya Bunda ni samaki.

Kusema ukweli samaki katika Ziwa Victoria ni kama wamekwisha kabisa na hivyo Halmashauri ya Bunda ni mojawapo ya Halmashauri maskini katika nchi hii na hivyo tunamwomba Mhe. Rais kuwa utafiti wa agizo hili ufanyike kwanza ili kufikia uamuzi wa agizo alilolitoa.

Halmashauri kama Bunda, Rorya, Bumbuli n.k. zitaathirika sana. Mwisho, kuanzia sasa uanzishwaji wa Halmashauri ufuate vigezo vinavyotakiwa na siyo kwa tamaa za wachache kupata ubunge.
Hayo ni maneno ya jukwaani ila kiuhalisia na inavyopaswa kuwa neno la rais si sheria.
Lakini kibongo bongo rais ni above everything practically though theoretically sio
 
Kusema ukweli samaki katika Ziwa Victoria ni kama wamekwisha kabisa na hivyo Halmashauri ya Bunda ni mojawapo ya Halmashauri maskini katika nchi hii na hivyo tunamwomba Mhe. Rais kuwa utafiti wa agizo hili ufanyike kwanza ili kufikia uamuzi wa agizo alilolitoa.
Si walisema jimbo likiwa na mwanaccm kitapelekewa miradi ua maendeleo?

Nini kimetokea?
 
Kusema ukweli samaki katika Ziwa Victoria ni kama wamekwisha kabisa na hivyo Halmashauri ya Bunda ni mojawapo ya Halmashauri maskini katika nchi hii na hivyo tunamwomba Mhe. Rais kuwa utafiti wa agizo hili ufanyike kwanza ili kufikia uamuzi wa agizo alilolitoa.
Samaki wanaishaje wakati kuna maafisa uvuvi wanafanya nini ofcn kwanini wasije na njia za kuhakikisha samaki hawapungui kwa kupandikiza mbegu kwa wingi na kufanya bunda kuwa kitovu ununuzi wa sato na sangara..
Graduates kibao wàpo mitaani kwanini almashauri isiwatumie hao kama semu ya kupa uzoefu kwa malipo kidogo ya kuwawezesha.
maofisi ya serikali mnachekeana sana.
 
Sio kwel kwenye nchi inayoongozwa na sheria na katiba inayojielewa.
Mambo hayo ni katka tawala za kifalme.

Katika nchi za utawala wa kisheria Rais anapingwa, anaweza shtakiwa na kufungwa kama raia yeyote
sasa si ukaishi huko ili uinjoy maisha
 
Back
Top Bottom