Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Unajua mkuu, mimi hapo ndo naona kweli tunaviongozi vilaza, kwasababu hawajui kwamba kuuchimba mkwara huu waraka, ndo wanazidi kuupa umaarufu na kuusambaza! Bora wangeunyamazia usingeshika kasi kama ilivo sasa, nakwambia saa hizi hata hardcopy ikiuzwa kwa elfu 5 watu wataununua tu, pamoja na uvivu wetu wa kusoma, tunausoma tu, yaani they are doing a great job, bila kujua, tena wacha waendelee kuupinga, ili uzidi kusambaa kwa kasi ya ajabu!

Kuna mtu mmoja alinambia, ukitaka wanao wale karanga mbichi kwani ni nzuri kwa afya, Ziweke sehemu, afu wambie hizi karanga msizile, ila ukitaka wasizile, wambie lazima mle hizi karanga na mzimalize!, Sasa naona serikali inatwambia tusizile hizi karanga lol!


Mafisadi wameshikwa pabaya sana .Walidhani ni utani vita ina anzia huko huko vigangoni hadi Parokiani ambako ndiko ziko kata kibao .Na hasa Wabunge wa CCM wakristo wachafu ndiyo watakao umia sana maana .

Mafisadi ninhatari hata kwa maendeleo ya watu kokote .Majuzi kuna mkuu mmoja mwanae anasoma hapa Kowaki Gals ambayo iko chini ya Fr.James Conrad .Basi alifika hapo katika kuonyesha yeye ni nani alimwaga 1m kama mchango bila ya kuombwa .Sister mkuu wa shule alipokea lakini akawa na mashaka kwamba ilikuwa ni hongo maana binti yake hana uwezo darasani.Wakati wa mitihani ya mwisho maana pale ni mchujo kama seminarini sister alitaka kufa na pressure maana alipokea pesa ya jamaa na mtoto akili hakuna.Ikawa bahati binti akafikisha marks kwenye line kabisa .Sister alikuwa amesha umwa maana hakujua ajibu nini mbele ya fisadi yule jina lake ninalo .Kama mtoto angerudo home wakati ni miezi 3 kafika Kowaki na kumwaga pesa yake .

Hii ni hatari kubwa .
 
Sindio hawa walio ongea na Mungu 2005, wakashuka toka mbigun, wakatuambia JK ni chaguo la Mungu? sasa chaguo la Mungu linashindwa vipi ku-deal na mafisadi?

Siwezi amini tena wakina pengo, wafunge midomo yao na wa-keep their houses in order, ufisadi, uzizi, ushoga, utapeli nk, nimwingi sana kanisani. tekelezeni neno la Mungu mjisafishe na msafishe kanisa kabla hamja wa-JURGE wenzano.

Nani kati yenu hana dhambi?
 
Kuna baadhi ya Watoto wa viongozi wa zamani wanaojidanganya sana kwa kudhani kuwa Kama mzazi alikuwa au ni kiongozi basi na Mtoto ni kiongozi, ........ 'God Damn it'

Sasa Mtu kama Nape amefikia sehemu anataka Kukemea Ilani hii ya Cathoric. Nape real... I will live to see your influence. Kumbuka mfupa uliomshinda fisi (you know him) Mbwa hauwezi.

Kwa ufupi nimeisoma ilani hiyo yote jana baada ya kuona mabishano makali yakiendelea, ninacho weza kusema ni kuwa Ilani iko wazi na haina ubaguzi wala misigi ya Kidini,

Wanaoilalamikia wana lao jambo na wanadhihirisha kuwa Tanzania bado ina viongozi Bongolala.

Aliyesema "miafrika ndivyo tulivyo" hakukosea kabisa.
 
Siri nzito ilani ya Kanisa Katoliki

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Julai 1, 2009
rC.jpg

bul2.gif
Yahoji mamlaka ya Rais kuteua mawaziri

bul2.gif
Yapendekeza wagombea binafsi isipokuwa urais


WAKATI Ilani ya Uchaguzi ya Kanisa Katoliki ikitoa vipaumbele na mwongozo wa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na Uchaguzi Mkuu wa 2010, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), nalo linaandaa tamko la kuwaandaa waumini kuwawajibisha watawala, imefahamika.
Kiongozi mmoja mwandamizi wa KKKT, amelithibitishia Raia Mwema wiki hii kwamba tayari vyombo vya juu, Baraza la Maaskofu na Halmashauri Kuu ya Kanisa hilo, kwa pamoja vimeridhia uandaaji wa tamko hilo zito litakalolenga chaguzi za viongozi wa dola katika ngazi ya Serikali za Mitaa 2009 na Serikali kuu 2010.
"KKKT nao wako katika mkakati wa kuandaa tamko lenye sura ya kuwaelekeza waumini wake kuamka na kuwawajibisha watawala katika kila ngazi, tangu vitongoji hadi Taifa. Wanasema kwamba wanazuoni maarufu wa vyuo vikuu mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, wanadiplomasia na wanaharakati wanashiriki katika kukusanya takwimu," kinaeleza chanzo chetu cha habari kilicho karibu na maandalizi ya tamko hilo.
Hayo yakijiri, Waislamu nao wameelezwa kujipanga ili kuhakikisha kuwa Rais, wabunge na madiwani hawachaguliwi kwa misingi ya kidini, uamuzi ambao umeelezwa kwamba umekuja baada ya mipango ya makanisa kuandikwa katika magazeti hivi karibuni.
Wanazuoni wa Kiislamu pamoja na mashekhe 15 wameunda jopo ambalo pamoja na mambo mengine, litaratibu na kusimamia mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu ujao kwa maslahi ya Waislamu.
Jopo hilo lililozinduliwa katika hoteli ya Starlight, hivi karibuni, linaongozwa na Sheikh Mohamed Idd, ambaye alinukuriwa akikemea ubaguzi wa kidini katika masuala yote ya uchaguzi.
Tayari uongozi wa juu wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, umeelezea masikitiko yake kwa jinsi viongozi wa dini zote wanavyouangalia kwa mtazamo hasi utawala wa sasa, ikiwa ni pamoja na viongozi na waumini wa Kikiristo kuhisi kwamba uongozi wa sasa unapendelea Waislamu huku kwa upande wao Waislamu wakiona kiongozi wa kutoka dini yao haonyeshi kuwasaidia. Kauli hiyo imetolewa hadharani mwishoni mwa wiki.
Katika vijitabu vya "Ilani, Mapendekezo ya Vipaumbele vya Kitaifa" ya Kanisa Katoliki pamoja na "Mada za Kuongoza Maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2010", maandiko ambayo yameandaliwa kitaalamu na ‘Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT), kwa baraka zote za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), waumini wamepewa miongozo ya kufahamu vipaumbele vyao kabla ya kushiriki chaguzi zilizo mbele yao.
Sehemu kubwa ya nyaraka hizo za Kanisa Katoliki, mmoja utakaochapishwa katika toleo lijalo la Raia Mwema, zinakosoa maeneo karibu yote ya Serikali ikitoa vipaumbele vikiwa na mapendekezo ya jinsi ya kuboresha maisha ya Watanzania katika sekta zote muhimu ikiwa ni pamoja na sheria na haki za binadamu; uchumi; elimu; afya na ajira.
"Kwa sababu chaguzi za mwaka 2010 haziko mbali tunaona ni muhimu kupendekeza vipaumbele vyetu kama jamii tukiwaambia viongozi wetu wajao yale ambayo tungependa yafanyike kwa ajili ya jamii yetu. Katika uchaguzi hatupigi kura tu, tunapaswa kueleza makusudio yetu kwa yale tunayofikiri kuwa muhimu kwa Taifa," inaeleza sehemu ya utangulizi wa Ilani ya Kanisa Katoliki, ulioandikwa na Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani, Askofu Mkuu wa Tabora, Paul Ruzoka.
Kwa umakini mkubwa, Ilani hiyo ya Katoliki imekuwa ikisisitiza kuwaelekeza Watanzania wote na si waumini wao pekee ambao wametajwa kama walengwa wakuu wa waraka huo kutokana na wote kuguswa na mambo yatakayofanywa na viongozi.
"Tunatoa mwaliko kwa wote na kuwasihi Watanzania wote kufikiri kwa makini changamoto kuu zinazokabili nchi yetu na wananchi wake wengi ambao ni masikini wa mali, waliotengwa na wasio na uwezo. Kuzishughulikia changamoto hizi kunahitaji kuweka vipaumbele sahihi na njia sahihi za ufumbuzi ambazo zinashughulikia kikamilifu matatizo ya umasikini, utenganisho wa kijamii na hali ya kukosa uwezo kwa Watanzania wengi," inaeleza sehemu ya maelezo ya ‘madhumuni/lengo la Ilani na kuendelea.
Katika kuonyesha kwamba lengo si kuelekeza chama ama mtu maalumu, madhumuni ya Ilani hiyo yanaeleza kwamba itakuwa "mwongozo kwa mtu binafsi kuchagua chama na mgombea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2009 na Uchaguzi Mkuu wa 2010."
Pamoja na kuzungumzia haja ya kuifanyia marekebisho Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ilani hiyo imeweka suala la ‘hadhi ya utu wa binadamu' kama kipaumbele cha kwanza, ikisisitiza kuwapo kanuni za kimaadili na weledi (meritocracy) katika vigezo au sifa za kuwapa watu kazi na kupandishwa vyeo. Kigezo hicho kinaashiria kuwapo malalamiko ya upendeleo katika ajira na utoaji nafasi za ajira na uongozi.
"Pana haja ya kuunda Baraza la Mapitio ya Katiba. Katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kuna njia kadhaa za kuwezesha suala kutekelezwa; Mahakama ya Kikatiba, chamba ya pili katika Bunge na Mkutano wa Katiba. Tunapendekeza paundwe Baraza la Wazee wanaoteuliwa na sekta ya kijamii, ama wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo hiki kingechaguliwa na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake kulingana na katiba yenyewe. Kisibanwe na Serikali," inaeleza.
Kutokana na matukio ya matumizi makubwa ya fedha katika chaguzi, Ilani hiyo imependekeza kuwapo kwa kanuni za marekebisho na udhibiti na kuwezesha uwazi wa kisheria kuhusiana na upatikanaji wa fedha za chama ama wagombea pamoja na kupendekeza kuwapo kwa kanuni za udhibiti na marekebisho katika kuchagua wagombea kutoka ndani ya vyama kwa lengo la kusaidia mchakato mzima wa kidemokrasia.
Pendekezo lingine la kikatiba lililoguswa na Ilani hiyo ya Katoliki ni pamoja na pendekezo la kutaka kuwapo kwa wagombea binafsi katika ngazi zote isipokuwa ile ya urais na kuikumbusha Serikali, "kuheshimu kanuni ya kuwa Serikali haina dini na kutoruhusu taasisi za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi ikitoa mfano wa suala la la Mahakama ya Kadhi na uanachama wa OIC.
Kutokana na kukithiri kwa matukio ya kifisadi, Kanisa Katoliki katika Ilani hiyo limependekeza kuwapo uwazi katika uteuzi na kufanyika kwa mapitio ya "mamlaka ya Rais katika kuwateua mawaziri, idadi ya wizara, na pia uwezo na uhuru zaidi wa bodi za usimamizi wa mashirika ya huduma za umma," na kuwapo kanuni na taratibu za uongozi za kuondoa wale wanaothibitika kutumia vibaya nafasi zao.
Maeneo mengine yaliyoguswa kwa kina, sehemu kubwa ikiwa ni kukosoa mfumo wa sasa ni pamoja na mfumo wa kisheria; viwanda, biashara na fedha; uchumi; elimu; afya; ajira na hifadhi ya jamii, huku ikitoa mapendekezo mbadala yenye lengo la kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na nchi kupiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo.
Habari zinasema vijitabu hivyo vya Kanisa Katoliki vimesambazwa nchi nzima na kuuzwa kwa bei nafuu na hata kugawanywa bure kwa watu wote wakiwamo waumini wa dini nyingine, lakini vimeibua mjadala mkubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwamo waumini wa madhehebu mengine, huku baadhi ya watu wakitafsiri kwamba Kanisa Katoliki linalenga kusaidia watu maalumu kuingia madarakani.
Hata hivyo, uongozi wa Kanisa hilo ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ulitoa ufafanuzi kwamba kanisa hilo linatimiza wajibu wake wa kitume wa kuwaelimisha waumini wake na Watanzania wengine kuhusu haki zao na si kutaka kumsimika mtu ama kumwangusha kiongozi yeyote.
Kauli ya Kardinali Pengo na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini kuhusiana na suala hilo ilitafsiriwa kwa namna tofauti na baadhi ya vyombo vya habari, chombo kimoja kikieleza kwamba sasa kanisa hilo linajipanga kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, katika kampeni za uchaguzi mkuu ujao wa 2010, tafsiri ambayo nayo imepingwa na viongozi wengi wa kanisa hilo wakisema hawataelekeza mtu bali wanachofanya ni kutoa elimu ili uamuzi uwe ni wa wananchi wenyewe.
Jana Jumanne tukienda mtamboni suala hilo liliingia bungeni kupitia kwa Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM) Manju Salum Msambya, aliyerejea waraka huo akitaka Serikali kutoa tamko akisema unalenga kuwaelekeza waumini wao kuchagua viongozi maalumu ambao unaweza kuwafanya waumini hao kuchagua viongozi kutoka dini yao pekee.
"Tusiifikishe nchi pabaya. Ukitoa waraka wa kichungaji unatoa sababu ya waumini kujielekeza kuchagua muumini mwenzao. Ni hao hao waliowahi kusema kwamba tusichanganye dini na siasa, leo hii wao ndio wanaofanya siasa. Kuna waziri mmoja wa serikali hii hii ya CCM ambaye aliunga mkono waraka huo. Nchi hii ni yetu sote, hakuna mwenye hati miliki hata Rais wa nchi," alisema Msambya akichangia bajeti ya Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba.
hs3.gif
 
Wakatoliki waliwaita 'vigogo' kuandaa ilani

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Julai 15, 2009
rC.jpg

bul2.gif
Wamo wa mahakama, wabunge

bul2.gif
CCM ilialikwa lakini haikuhudhuria


bul2.gif
Mafisadi waelezwa hawatapona

WAKATI mjadala mkali ukiibuka kuhusiana na nyaraka zilizotolewa na Kanisa Katoliki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, imefahamika kwamba baadhi ya vigogo ndani ya serikali na vyama vya siasa walishirikishwa katika hatua za awali za maandalizi yake.
Raia Mwema limefahamishwa kwamba maandalizi ya nyaraka hizo ikiwa ni pamoja na Ilani ya Mapendekezo ya Vipaumbele vya Taifa, yalifanyika kwa kuwapo vikao vya pamoja kati ya wanataaluma wa kanisa hilo na wadau mbalimbali kutoka serikalini na sekta nyingine.
Nyaraka hizo ambazo tayari zimekabidhiwa ofisi nyeti nchini, ambazo ni Ikulu, Mahakama, Bunge, Ofisi ya Waziri Mkuu na vyama vya siasa, kwa ajili ya kufanyiwa kazi, zimeibua mjadala zaidi baada ya kuanza kuandikwa na Raia Mwema baadhi wakikerwa na jinsi taarifa kuhusiana na nyaraka hizo zinavyoripotiwa.
Ndani ya nyaraka hizo, pamoja na mambo mengine, kumesisitizwa kwamba kutenda haki ni zaidi ya kufuata sheria na taratibu, na watawala sio mabosi mbele ya watu.
Baadhi ya washiriki katika vikao vya maandalizi wanatajwa kuwa ni pamoja na Jaji Mkuu Augustino Ramadhani, baadhi ya wabunge, maofisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na baadhi ya vyama vya siasa. Hata hivyo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho chama tawala hakikushiriki licha ya kualikwa kama chama tawala.
Mjadala wa kwanza wa maandalizi hayo unaelezwa kufanyika Mei, mwaka huu na kwamba kutakuwapo na muendelezo wa mijadala na vikao katika siku zijazo kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama Cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT), Joseph Ibreck, kati ya Agosti na Septemba, mwaka huu, makundi ya kijamii yatapata fursa ya kujadili juu ya mrejesho (reflection) wa ilani hiyo. CPT ndio waliokuwa waratibu na waandaaji wa nyaraka hizo kwa Baraka zote za Kanisa Katoliki.
"Kalenda inaonyesha kuwapo kwa forum (jukwaa la majadiliano) Agosti au Septemba, mwaka huu kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi, NGOs, wanahabari," alisema Ibreck na kuongeza kuwa;
"Kwa bahati mbaya tumekuwa tukinyanyasana sisi wenyewe (Watanzania) na si mtu kutoka nje ya nchi…kwa nini? Kwa hiyo lengo la ilani hii ya vipaumbele ni hadhi ya utu wa mwanadamu, marekebisho ya Katiba, uongozi wa umma na mengine."
Kwa mujibu wa Ibreck, Kanisa Katoliki linasisitiza kuwa suala hilo si la kidini bali ni la kiimani.
"Hili si suala la kidini kwa kuwa udini ni sawa na ukabila ni ubaguzi. Hili ni suala la imani, na katika imani sote tunaamini Mungu, lakini kwenye dini tunatakiwa kujitambua kama watu wa mfumo fulani na taratibu mahsusi kwa hiyo tunajiweka katika makundi, '' alisema.
Alipoulizwa kuhusu Kanisa Katoliki kuhusika katika kutoa kauli kali kuhusu umasikini wa Watanzania, na hasa kwa kuhoji; ''uchumi na siasa vipo kwa madhumuni gani?'' Ibreck alisema Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kutoa kauli kali zaidi kuliko msimamo huo wa kanisa.
''Hatujaeleza kwa ukali ni masuala yenye hoja za msingi kwa kila Mtanzania, na tumeitwa kutoa ufafanuzi na hasa pale awali kulipojitokeza kikundi kilicholenga kupotosha ukweli, lakini sasa wengi na hasa viongozi wameelewa lengo letu.
''Mwalimu Nyerere alikuwa akitoa maneno makali zaidi kuhusu umasikini wa Watanzania na pia kuhusu ufisadi. Ni mambo yaliyokuwa yakimkera.
''Mwadhana Polycarp Kardinali Pengo amekwishaeleza kuwa kanisa halitawalinda mafisadi na anatambua kati ya waumini wapo watu wa aina hiyo.
''Kwa hiyo ni kuipigania jamii ibaki salama, watu wasinyanyasane na kubaki wakinung'unika na kulaumiana, utu wa kila mtu upewe hadhi inayostahili.
''Unajua tatizo kubwa nchini ni kwamba watu wenye sifa za kuwa viongozi bora hawajitokezi, sasa tunataka kuamsha dhamira, watu wajitokeze kuchaguliwa na kuchagua pia,'' alisema.
Ilani ya Mapendekezo ya Vipaumbele vya Kitaifa inazungumzia marekebisho ya Katiba, suala ambalo limekuwa likipigiwa kelele na wadau mbalimbali nchini kwa muda mrefu.
Katika mapendekezo yake ya marekebisho ya Katiba, ilani hiyo inaeleza kuwa Katiba ni zaidi ya sheria, ni dira`ya kimaadili na maelezo ya kifalsafa ya tunu na kanuni watu wanazotaka kuzizingatia katika maisha yao ili kuwakikishia amani, haki na kuheshimiana na kuvumiliana katika kuwa na maoni tofauti.
Imeelezwa kwamba hakuna chama cha siasa wala serikali ya wakati huu wanaoweza kihalali kutumia Katiba kwa faida zao za kisiasa.
Inapendekezwa Baraza la Mapitio ya Katiba. Katika mifumo mbalimbali ya kisiasa, kuna njia kadhaa za kuwezesha suala hili kutekelezwa: Mahakama ya Kikatiba, Bunge na Mkutano wa Katiba.
Pia inapendekezwa kuundwa kwa Baraza la Wazee, wanaoteuliwa na sekta za kijamii, ama wanaochaguliwa na taasisi mbalimbali za kijamii, kidini na wanazuoni. Chombo hicho kichaguliwe na kuhakikishiwa uhuru watendaji wake na Katiba yenyewe, kisibanwe na serikali.
Inapendekezwa kuwekwa kanuni za udhibiti wa upatikanaji wa fedha za chama ama mgombea, kuchagua wagaombea ndani ya chama kufanyike kwa uwazi na kwa demokrasia zaidi.
Kuanzisha mfumo wa kiuwiano katika uwakilishi badala ya sasa wa mwenye kupata kura nyingi kuwa ndiye mshindi. Kuruhusu wagombea binafsi isipokuwa Rais.
Kuheshimu kanuni ya kuwa serikali haina dini na kutoruhusu taasisi zake za kidini kuwa sehemu ya mfumo wa nchi na kulinda haki ya watoto ambao hawajazaliwa.
Wakati hayo yakiendelea, kuna habari kwamba baadhi ya watendaji ndani ya serikali wameelezea kukerwa kwao na taarifa zinazonukuu nyaraka hizo za kanisa, wakielezea kwamba zinapotoshwa bila kutoa ufafanuzi mwanana.
Kwa mfano, watendaji hao wanazungumzia kutotajwa kwa udhaifu wa serikali katika nyaraka hizo, ambazo kwa sehemu kubwa zinaelezea udhaifu katika mfumo wa kiutendaji na utoaji huduma na kutoa mapendekezo ya mambo ya kurekebishwa ikiwa ni pamoja na Katiba ya sasa kufanyiwa marekebisho.
Hofu kubwa imejengwa kwamba kwa sasa waraka huo umejengewa mazingira na picha kama vile ni shambulio la Kanisa Katoliki dhidi ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
"Pamoja na ufafanuzi wa Kardinali Polycarp Pengo, uliofuatiwa na ule wa Rais Kikwete aliyezungumzia uhusiano mzuri ulioko kati ya Serikali yake na dini mbalimbali katika hotuba yake ya mjini Songea, Wilaya ya Kilindi, Mkoa wa Tanga wakati anazindua Hospitali Teule ya Wilaya ya Kilindi mwishoni mwa mwezi uliopita, bado juhudi za kupotosha uhusiano huo zimeendelea," anaeleza mmoja wa watu ndani ya serikali (ambaye hakupenda kujitambulisha) katika taarifa yake aliyoituma Raia Mwema.
"Picha inayojengwa ni kwamba Kanisa Katoliki limeishambulia Serikali ya Kikwete katika Waraka huo kwa sababu mbalimbali, kuanzia kwenye madai ya rushwa na mambo mengine. Kwamba Kanisa Katoliki halimtaki Rais Kikwete na kuwa halitamuunga mkono katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani. Kwamba Kanisa Katoliki linaandaa viongozi wake kwa ajili ya kukamata madaraka katika uchaguzi huo wa mwakani," anaendelea kulalamika ofisa huyo wa Serikali.
Mtendaji huyo, aliye ndani ya duru la wasaidizi wa karibu wa Kikwete wa sasa, ameendelea kulalamika kwamba kumekuwapo na upotoshwaji wa makusudi unaohusisha pia uamuzi wa Serikali kufuta misamaha ya kodi kwa baadhi ya vifaa vya matumizi ya dini na adhabu dhidi ya viongozi wa dini kwa sababu ya Waraka huo.
"Kwa nini dini zote nchini ziadhibiwe kwa sababu ya Waraka uliotolewa na madhehebu ya Wakatoliki ni jambo ambalo hata halielezwi kwa sababu halina maelezo yoyote yenye mantiki kwa hata mtu mjinga," anasema.
Hata hivyo, hofu imeelezwa kuwaingia serikalini baada ya kuelezwa kwamba wapo baadhi ya viongozi wa Serikali ambao sasa wameanza kulitisha Kanisa Katoliki kutokana na Waraka huo.
"Waraka wa mwaka huu, uliotolewa Januari hata kama wakubwa wameugundua majuzi tu, siyo wa kwanza kutolewa na Kanisa Katoliki tokea kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa. Kanisa Katoliki lilitoa Waraka wa kwanza wa namna hiyo mwaka 1995, likatoa wa pili wa namna hiyo mwaka 2000, na Waraka wa sasa ni wa tatu. Na wala hakuna tofauti kubwa katika Nyaraka zote hizo tatu," anaendelea kueleza mtumishi huyo wa serikali.
Raia Mwema limekuwa likiandika taarifa zilizonukuu maandiko hayo huku likichambua vipaumbele vilivyotajwa ikilinganishwa na hali ya sasa serikalini katika utendaji na utoaji huduma.
 
Ni kweli waraka umeshika kasi .baada ya TEC kufanya mabadiliko ya uongozi mwishoni waliamua kueneza kasi ya waraka huo .Leo hii nimesikia LIVE toka Parokia ya Mwanjelwa Padre akisema kuhusu huu waraka .Kasema copy zimeisha lakini kanisa limeamua kuuchapa kwa kasi na kila muumini azingatie atafute muda asome na viongozi wa take charge kuutafasiri kwa waumini .Leo hii nimesikia habari hizi kwenye Radio Maria katika ibada ya shukrani ya mtu kuulamba Upandre tokea Mwanjelwa .

Kazi sasa
 

Quote:
Bull​



tekelezeni neno la Mungu mjisafishe na msafishe kanisa kabla hamja wa-JURGE wenzano.

Nani kati yenu hana dhambi?



​




Mkuu unamaana gani hapo???
__________________
MASANILO NENO LA MUNGU LINASEMA NITAPIGANA NAO WANOPIGANA NANYI...NITWALAANI WALE WAWALAANIO..NITAWABARIKI WALE WANOWABARIKI...HAKUNA HAJA YA KUBISHANA NA HUYO JAMA HAPO JUU
 
Sindio hawa walio ongea na Mungu 2005, wakashuka toka mbigun, wakatuambia JK ni chaguo la Mungu? sasa chaguo la Mungu linashindwa vipi ku-deal na mafisadi?

Siwezi amini tena wakina pengo, wafunge midomo yao na wa-keep their houses in order, ufisadi, uzizi, ushoga, utapeli nk, nimwingi sana kanisani. tekelezeni neno la Mungu mjisafishe na msafishe kanisa kabla hamja wa-JURGE wenzano.

Nani kati yenu hana dhambi?

Tatizo hapa ni kuto kuelewa, ukimzaa mtoto si huwa unafurahia?? Na baadaye akija kuwa mla unga utamlaumu Mungu au utapambana ili mtoto wako aache kula unga?? Tumia akili hapa. Serikali ya JK ni sawa na mtoto anazaliwa, wazazi wanafurahi lakini baadaye mtoto huyo huyo anakuwa mbwia unga, na makanisa sasa ni wazazi wanapambana ili mtoto aache kula unga!!!
 
Tatizo hapa ni kuto kuelewa, ukimzaa mtoto si huwa unafurahia?? Na baadaye akija kuwa mla unga utamlaumu Mungu au utapambana ili mtoto wako aache kula unga?? Tumia akili hapa. Serikali ya JK ni sawa na mtoto anazaliwa, wazazi wanafurahi lakini baadaye mtoto huyo huyo anakuwa mbwia unga, na makanisa sasa ni wazazi wanapambana ili mtoto aache kula unga!!!


Very well said Magezi chukua 5 zinngine baadaye na uzidi kukanyaga mafuta twende
 
Pengo hakikisha unapata feedback to kila Jimbo na uhakikishe kule kwenye kigango changu ujumbe unafika maana wana taabika wale watu na hawana pa kutokea .Kama umeamua sasa basi hii ndiyo kazi hasa ya kitume , usirudi nyuma.

KWELI LUNYUNGU TUKO NYUMA YAKO................LEO HIIIIIIIIII NIMESIKITISHWA SANA KUMUONA KWENYE TV NAPE NNAUYE BAADA YA KUHAIDIWA ULAJI KWA KILA UCHAGUZI LEO HIII ANATHUBUTU KUTAMKA VIONGOZI WA DINI ACHANENI NA SERIKLI...KAMA NI MAFISADI WAOOMBEENI WAMJUE MUNGU NA SI KUWASEMA KWENYE MADHABAHU.......LOH!!!!!!!!!! SHAME NNAPE KWA HIYO ANASEMA TUWAACHIE SERIKALI KAMA MAFISADI NI HIYO HIYO SERIKALI.............,,JAMANI TUPELEKE TENA KESI HUKO....LOH
Dawa ya watu kama hawa ni kufunga siku saba na kumwomba Mungu awapatilize. Muda si mlefu ujao Mola atatushindia vita hii, zetu sala
 
I wish waraka kama huu ungekuwa unasambaa misikitini. Maana watanzania wote tunatakiwa kutambua hii nchi ni yetu sote. Misikitini na Makanisani kunachangia sana kuleta mabadiliko. Hata historia inaonesha, may be sasa tunaweza kuona mwanga kuwa kuna watu at least wanaweza kufanya effort ya kuinusuru nchi.
 
Huyo Pengo kwanza awakataze wanawake kwenda makanisani kisha awaeleze wanapokuwa wawe wamevaa mitandio kufunika vichwa vyao ,ee ndio maana yake awaandalie mwongozo huko kwanza na kuwafundisha neno la Mungu.Awakataze wanawake kuvaa nguo za kiume,
Deuteronomy 22:5:The woman shall not wear that which pertains to a man, neither shall a man put on a woman's garment, for all that do so are an abomination to the Lord your God.

Apinge Mawaziri wanawake na hata kuwaruhusu kuhubiri kwenye makanisa.Azuie wanawake walioolewa kuhudhuria makanisani ,maana yeye kama mwanamme atakuwa anawakodolea macho.

Matthew 6:5-6:
And when thou prayest, thou shalt not be as the hypocrites are: for they love to pray standing in the synagogues and in the corners of the streets, that they may be seen of men. Verily I say unto you, They have their reward.


Kama haitoshi azuie watoto kutumia jina la baba pia awazuie wale wa Tanzania wanaotumia jina la Baba kumwita Nyerere hayo ndio mafundisho ya Bibilia ,


Matthew 23:9:

And call no man your father upon the earth: for one is your Father, which is in heaven

wacheni mipango yenu ,msiwe na pupa kuingilia mambo ya wengine wakati kumbe hata dini yenu hamjui inawafundisha kitu gani.
 
Tatizo hapa ni kuto kuelewa, ukimzaa mtoto si huwa unafurahia?? Na baadaye akija kuwa mla unga utamlaumu Mungu au utapambana ili mtoto wako aache kula unga?? Tumia akili hapa. Serikali ya JK ni sawa na mtoto anazaliwa, wazazi wanafurahi lakini baadaye mtoto huyo huyo anakuwa mbwia unga, na makanisa sasa ni wazazi wanapambana ili mtoto aache kula unga!!!


Mkuu
Hapa wachungaji wangetuambia wanamchagua au JK nichaguo la wachungaji, nisinge laumu, tunajua wao wanaweza kosea kama anyokosea mzazi, lakini wachungaji walituambia JK ni chaguo la Mungu!!

Mungu alishachagua wengi hapo nyuma, walionyesha umahir wao, uaminifu, hekima na busara za hali ya juu. Mungu wawezi chagua kitu alfu watu wa Mungu wamkatae, kama wakina pengo wanavyo mkataa JK. Hapa kuna mawili either Mungu alikosea au watu wa Mungu ndo wenye matatizo. sasa chaguo hili nanai kakosea?


Chaguo la Mungu nikitu ingine, haliwezi kushindwa na kazi yake, hawezi kushirikiana au kuwaonea haya mafisadi, chaguo la Mungu nimtu clean asiye na utata.

Mzazi hajui atazaa mtoto wa aina gani, Mungu anajua, kamwe hawezi kuwachaguli watu mtu au nabii mbovu alfu baadae aka regret.



Na ndo maana siwaamini tena hawa wachungaji, wamenitekeleza pamoja na kura yangu, sasa hawaweziniambia kitu, mpaka watuombe radhi wa TZ
 
Mkuu
Hapa wachungaji wangetuambia wanamchagua au JK nichaguo la wachungaji, nisinge laumu, tunajua wao wanaweza kosea kama anyokosea mzazi, lakini wachungaji walituambia JK ni chaguo la Mungu!!

Mungu alishachagua wengi hapo nyuma, walionyesha umahir wao, uaminifu, hekima na busara za hali ya juu. Mungu wawezi chagua kitu alfu watu wa Mungu wamkatae, kama wakina pengo wanavyo mkataa JK. Hapa kuna mawili either Mungu alikosea au watu wa Mungu ndo wenye matatizo. sasa chaguo hili nanai kakosea?


Chaguo la Mungu nikitu ingine, haliwezi kushindwa na kazi yake, hawezi kushirikiana au kuwaonea haya mafisadi, chaguo la Mungu nimtu clean asiye na utata.

Mzazi hajui atazaa mtoto wa aina gani, Mungu anajua, kamwe hawezi kuwachaguli watu mtu au nabii mbovu alfu baadae aka regret.



Na ndo maana siwaamini tena hawa wachungaji, wamenitekeleza pamoja na kura yangu, sasa hawaweziniambia kitu, mpaka watuombe radhi wa TZ
Aloo wewe umewapiga na chini kabisa,aisee kuna watu JF wanakumbukumbu ,yaani inabidi sasa Makadinali na Maaskofu wawaombe radhi WaTz kwa kuwapandisha mkenge.Kabla hawajaungwa mkono na uzushi mpya.
 
Huu waraka wanaoupinga si lazima wawe mafisadi. Lakini kama umeishiwa utasema ni mafisadi, ni haki yao kama vile wanaouunga mkono. Lakini yetu macho na masikio, tunaweka kumbukumbu muhimu kwa huu waraka kama ile iliyowahi tolewa nyuma. Historia itatuambia.
 
Mkuu
Hapa wachungaji wangetuambia wanamchagua au JK nichaguo la wachungaji, nisinge laumu, tunajua wao wanaweza kosea kama anyokosea mzazi, lakini wachungaji walituambia JK ni chaguo la Mungu!!

Mungu alishachagua wengi hapo nyuma, walionyesha umahir wao, uaminifu, hekima na busara za hali ya juu. Mungu wawezi chagua kitu alfu watu wa Mungu wamkatae, kama wakina pengo wanavyo mkataa JK. Hapa kuna mawili either Mungu alikosea au watu wa Mungu ndo wenye matatizo. sasa chaguo hili nanai kakosea?


Chaguo la Mungu nikitu ingine, haliwezi kushindwa na kazi yake, hawezi kushirikiana au kuwaonea haya mafisadi, chaguo la Mungu nimtu clean asiye na utata.

Mzazi hajui atazaa mtoto wa aina gani, Mungu anajua, kamwe hawezi kuwachaguli watu mtu au nabii mbovu alfu baadae aka regret.



Na ndo maana siwaamini tena hawa wachungaji, wamenitekeleza pamoja na kura yangu, sasa hawaweziniambia kitu, mpaka watuombe radhi wa TZ

Inabidi ukanoe bongo lako mazee..u-gret thinka sidhani kama ndio huu..labda u-gret-sinker!

Wachungaji wanaponena kuwa Fulani ni chaguo la Mungu wanatumia the simplest of the logic kuwa kila mamlaka imeidhinishwa na Mwenyezi Mungu, na si vinginevyo kama akili yako ya 'u-gret-sinker' unavyotaka kupotosha..
 
Inabidi ukanoe bongo lako mazee..u-gret thinka sidhani kama ndio huu..labda u-gret-sinker!

Wachungaji wanaponena kuwa Fulani ni chaguo la Mungu wanatumia the simplest of the logic kuwa kila mamlaka imeidhinishwa na Mwenyezi Mungu, na si vinginevyo kama akili yako ya 'u-gret-sinker' unavyotaka kupotosha..

Wangetamka hayo baada ya JK kushinda ingekuwa sawa, walitamka kabla hajashinda, walijuaje kama Mrema, Mbowe, Lipumba sio chaguo la Mungu manake alikuwa JK hajapata hayo mamlaka ya uRais.
 
Huyo Pengo kwanza awakataze wanawake kwenda makanisani kisha awaeleze wanapokuwa wawe wamevaa mitandio kufunika vichwa vyao ,ee ndio maana yake awaandalie mwongozo huko kwanza na kuwafundisha neno la Mungu.Awakataze wanawake kuvaa nguo za kiume,
Deuteronomy 22:5:The woman shall not wear that which pertains to a man, neither shall a man put on a woman's garment, for all that do so are an abomination to the Lord your God.

Apinge Mawaziri wanawake na hata kuwaruhusu kuhubiri kwenye makanisa.Azuie wanawake walioolewa kuhudhuria makanisani ,maana yeye kama mwanamme atakuwa anawakodolea macho.

Matthew 6:5-6:
And when thou prayest, thou shalt not be as the hypocrites are: for they love to pray standing in the synagogues and in the corners of the streets, that they may be seen of men. Verily I say unto you, They have their reward.


Kama haitoshi azuie watoto kutumia jina la baba pia awazuie wale wa Tanzania wanaotumia jina la Baba kumwita Nyerere hayo ndio mafundisho ya Bibilia ,


Matthew 23:9:

And call no man your father upon the earth: for one is your Father, which is in heaven

wacheni mipango yenu ,msiwe na pupa kuingilia mambo ya wengine wakati kumbe hata dini yenu hamjui inawafundisha kitu gani.
__________________


MKUU MWIBA YAKALE YAMEPITA TAZAMA YAMEKUWA MAPYA....HAYO UNAYOONGELEA NI MAMBO YA AGANO LA KALE ...UNAKUMBUKA NGURUWE HARAMU AGANO LA KALE...LAKINI UNAJUA AGANO JIPYA LINASEMAJE....KITOKACHO NJE NI NANJISI NA SI KIINGIACHO....MEANS RUKSA HOTSEAT........
NINI MAANA YAKE...UKO SAWA YOTE NI MAANDIKO LAKINI LAZIMA UJUE TUMEZALIWA UPYA TUNATAKIWA KUISHI NA AGANO JIPYA UKICHUKUA KIPENGELE KIMOJA KIMOJA AGANO JIPYA UTAKUWA MUUMINI WA DINI YOYOTE......MUNGU AKUTIE NGUVU ENDELEA KUTAFUTA NA KUJUA MAANDIKO ZAIDI UPATE UFAHAMU WA YESU KRISTO HAKUNA KITU CHEMA KMA HEKIMA NA UFAHAMU WA MUNGU
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom