Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Mimi naomba kuuliza swali kwa Askofu Kilaini na WanaJF mahakama ya kadhi na OIC zinahusiana vipi na Ufisadi naombeni jibu tafadhali.

Pili ndani waraka unasema katiba iheshimiwe naomba kama kuna mdau anayo katiba atuwekee tuanze kichambua maana kama waraka ulivyosema kuwa katiba imetungwa na wananchi na pia katiba isielekee upande mmoja iangalie pande zote mbili vinginevyo ilo ikae kimya. Tunaomba katiba wakubwa.

Mwisho upande fulani naungana na Kingunge kwamba msijijidai kutupaka mafuta huu ni unafiki wa kanisa katoliki unajulikana dunia nzima wanataka kutuwekea serikali ambayo inafata maelekezo yao ili iprotect interest za kanisa. Mara nyingi hiyo strategy huishia katika machafuko. Kama mlikuwa mnaupinga ufisadi mbona mlikurupuka alipochaguliwa JK na kumsifu kuwa ni chaguo la mungu??? five years later mnaleta muongozo wa kuchagua viongozi huu si unafiki. Mlikuwa wapi nyuma na hata huo muongozo mlioutoa mwaka 2005 mbona ulitoka kimya kimya sembuse huu au kwavile mnajua jamii inachukia ufisadi ndio mnajidai kuleta unafiki sasa hivi???

Naomba mwongozo waheshimiwa.
 
Rai yangu kwa wasomi wenzangu hapa bodini .
Badala ya kukaa na kujadili utumbo wa hawa jamaa wa mjengoni Idodomya tafadhalini naomba tufanye kazi moja na kwa kasi na uaminifu na kujutuma .Tusipoteze muda wa kubishana tufanye kazi ya kitume sasa .Wenzetu wamesha fanya moja na sisi tuongeze kasi ya kuusambaza waraka huu kuanzia Vyuoni , high schools na vijijini .Kila mmoja wetu anatoka kijijini hapa tumia kila njia mpe mtu anaye elewa anawez kuusoma na kutafasiri vilivyo .Iwe ndiyo kazi yetu tuachane na maneno .Sote tuungane kwa kuwa tunakubaliana na tuusambaze na hata kuulizia feedback .
 
Bado tuna kazi kubwa nchi hii! Kama hii ndiyo level ya uelewa wa watu wetu, sioni ni jinsi gani tutajikwamua kutoka kwenye makucha ya mafisadi.

Ni rahisi, angalia huyu bnhai alijiunga lini hapa JF. Kutokana na michango yake hapa, I am 90% convinced kwamba ni kati ya wale wachache waliotumwa kujaribu kuyeyusha na kupotosha hoja za msingi hapa JF. Wana kazi moja tu, kujaribu ku-divert hoja na kulinda maslahi ya Mafisadi.

Tiba
 
Mwalimu walimwogopa kumbe hawakumheshimuuu....ndo chanzo cha unafiki wao viongozi waaandamizi wa CCM na serikali mpaka leo...

muda wao kuumbukaa umewadiaaaa.....

mwongozoo huu nimeusomaa hauna chembe ya udini hata kidogo zaidi ya ukweli mtupu..

U shall know the truth and the truth shall set u free...

Hapo umenena!!! Pia tujiulize swali la msingi: Inakuwaje mtu asiye na dini wala kuelewa misingi ya kidini na majukumu ya viongozi wa dini kuhoji bila mantiki???

Uchungu wa mwana aujuaye mzazi na Kingunge hana uchu wa dini ila tunajua ana uchungu na mwanaye na ndiop maana kammilikisha rasilimali na kumtoa gerezani kila alipokuwa akigonga raia wema mabarabarani wengine wameacha yatime mitaani!!!!!!!!!

Kingunge mzee, rest in pieces---dont stir the tea which is not yours!!!!
 
hana lolote huyo anatetea maslahi ya mafisadi,Nyerere kafa mara tu na yeye kawa bepari.sasa anajua kuwa viongozi wa dini wanaweza kuwa na sauti kubwa kuliko wapinzani.ni bora angekaa kimya.
 
Ni rahisi, angalia huyu bnhai alijiunga lini hapa JF. Kutokana na michango yake hapa, I am 90% convinced kwamba ni kati ya wale wachache waliotumwa kujaribu kuyeyusha na kupotosha hoja za msingi hapa JF. Wana kazi moja tu, kujaribu ku-divert hoja na kulinda maslahi ya Mafisadi.

Tiba
Nimecheka saana nilivyosoma hoja ya Tiba. Watu mnaogopa saana kuwa critisized. Eti alijiunga lini? Sio hoja ya msingi. Nimekuwa nikisoma saana JF for years sasa. Nikaona naguswa kuweka mkono. Sina lengo la kudivert attention ila nataka tuwe fair. Weka hoja kama na wewe ni msafi otherwise kaa kimya. Ukiiba wewe sawa ila wengine hapana. No way kama wanaweza hasa wawatenge na mafisadi tuone kama hao mafisadi watapumua. Mbona wao wanawakumbatia? Tuzibe mianya yote ya kwnye uongozi hadi kwenye dini.
 
Hongera sana kanisa katoliki kwa mwongozo huu: Tunaomba uende hadi vijijini ikiwezekana ufike hata kwenye shule na vyuo: Ufike wakati ambapo kila mtu anajua wajibu wake alionao ili mafisadi wafutwe kwenye ramani watanzania: Mungu tunakuomba uongoze elimu hii.
 
Wiki jana niliandika barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais Kikwete na kuiweka kwenye JamiiForum siku ya Ijumaa. Barua hiyo ilikuwa katika lugha ya Kiingereza. Pamoja na mambo mengine nilimwomba Rais na serikali yake wasichukulie waraka wa kanisa katoliki kama mzaa. Mimi ni mkatoliki na kiongozi wa ngazi fulani hivyo najua kinachoendelea. Wakatoliki wana mtido wa kufanya mambo yao kimya kimya na kupitia katika waraka huo kuna ujumbe mahususi na mzito. Jambo nililomwomba Rais wetu kupitia vyombo vyake achunguze kiini cha waraka huo. Kwa nini sasa na si wakati mwingine? Hizo semina zinaelekeza tu yale yaliyomo kwenye waraka au kuna mengine zaidi ambayo hayakuandikwa kwenye waraka? Rais akipata jibu atajua jinsi ya kutatua tatizo hili. Ili nataka kusema kwamba Mzee Kinguge asipoteze muda wake kushauri kanisa katoliki kwa lolote maana kanisa haliendi hivyo. Angetaka angewasiliana na viongozi wa kanisa faragha na sio kupitia Bungeni. Ushauiri wake umepitia sikio la kushoto na kutokea sikio la kulia!



Hapa nimechoka , wewe ni kiongozi wa juu wa Kikristo ama Kanisa katoliki ? Kama ni mkatoliki then utakuwa unajua how the system it works maana JK anajua hilo .Una wasi wasi na waraka na wewe pia ? wasi wasi ni nini ? Kuona kama nilicho andikwa ndicho kina kuwa preached ama kuna mengine zaidi hayakuandikwa ? Je kama yako ambayo hayakuandikwa yeye na watu wake hao watayajuaje ?
 
Mafisadi payroll at work!!!!!!!

Tiba
Utanihukumu upendavyo lakini ukweli utabaki bali tunataka kuhakikisha kila fisadi anamulikwa alipo. This tym hadi kwenye sadaka, EPA, meremeta nk
 
Mkuu, umefanya kazi takatifu. Ilikuwa kidogo na mimi niutume tena hapa JF.

Waraka huu unapaswa kutunzwa hala tuanze kuujadili na kuusambaza utakapokaribia uchaguzi! Tena hakuna haja ya kuomba copyright maana nasikia wakatoliki wamekubali uchapishwe na usambazwe na yeyote anayeweza kuusambaza. Ukizani nabisha piga simu kwa walioundaa yaani Chama Cha Wanataaluma Wakatoliki na namba yao hii hapa (022-2127675)

Mdanganywa, ni ukizani nabisha au ukidhani nadanganya? mdanganywa bana!!!
 
Mtumie MJJ kwenye cheche aanze kuutoa maramoja sio kusubiri

Samahani dada Mage sikufafanua zaidi. Niliposema tusubiri hadi uchaguzi unapokaribia sikuwa na maana tuache majadiliano au kuusambaza sasa hivi. Nilikuwa na maana kwamba nawajua wabongo tutapiga kelele sasa hivi lakini ikipita miezi miwili kimya kama vile hakuna kilichokuwa kinaongelewa.

Na kama ni hivyo basi zitakapoanza kampeni tutumie na njia hiyo pia maana ni nzuri kila mmoja kuujua kwa kupata message kwa simu yake. Achilia mbali MJJ kuutoa RAIA MWEMA wameshaanza kuutoa tangu toleo la wiki hii.

Hebu nikumbushe MJJ ni nani?
 
Kingunge nyamaza, hakuna mantiki kwa kila unachosema. Kwanza niwaunge mkono wote mnaoukubali waraka huu makini wa kanisa katoliki, kama serikali haitaki kuelimisha watu namna nzuri ya kupata viongozi safi kwanini kanisa lisitoe elimu hiyo adimu na ya lazima kwa wananchi wote. Halafu hajui kuwa katika inatoa uhuru wa watu kupata habari!

Kingunge alikuwa kimya wakati CCM inaingiza udini kwenye ilani ya chama na yeye akiwa mmoja ya watu waliyo tunga ilani ya CCM ambayo iliahidi kuwapa waislamu mahakama ya kadhi huku akijua ni ukiukwaji wa katiba! Sasa leo anashutumu kanisa katoliki linalotaka kuelimisha wauumini wake wasichague mafisadi! Aache kelele asubiri hukumu yake na mafisadi wenzake!

Mimi ni si muumini wa katoliki lakini naaunga mkono waraka huu, na nimeshapata mialiko kadhaa ya kwenye makanisa ya katoliki vijiji kuufundisha huu waraka na nitaenda! Mafisadi wajiandae kuanguka kwa kishindo!

Mimi nitasambaza kwa message za simu. Kila siku verse moja kwa watu 20. Ninaowahafamu. Kutembea hadi vijijini sina uwezo huo. Lakini simu zinafika. Mafisadi kaeni chonjo.
 
Mimi naomba kuuliza swali kwa Askofu Kilaini na WanaJF mahakama ya kadhi na OIC zinahusiana vipi na Ufisadi naombeni jibu tafadhali.

Pili ndani waraka unasema katiba iheshimiwe naomba kama kuna mdau anayo katiba atuwekee tuanze kichambua maana kama waraka ulivyosema kuwa katiba imetungwa na wananchi na pia katiba isielekee upande mmoja iangalie pande zote mbili vinginevyo ilo ikae kimya. Tunaomba katiba wakubwa.

Mwisho upande fulani naungana na Kingunge kwamba msijijidai kutupaka mafuta huu ni unafiki wa kanisa katoliki unajulikana dunia nzima wanataka kutuwekea serikali ambayo inafata maelekezo yao ili iprotect interest za kanisa. Mara nyingi hiyo strategy huishia katika machafuko. Kama mlikuwa mnaupinga ufisadi mbona mlikurupuka alipochaguliwa JK na kumsifu kuwa ni chaguo la mungu??? five years later mnaleta muongozo wa kuchagua viongozi huu si unafiki. Mlikuwa wapi nyuma na hata huo muongozo mlioutoa mwaka 2005 mbona ulitoka kimya kimya sembuse huu au kwavile mnajua jamii inachukia ufisadi ndio mnajidai kuleta unafiki sasa hivi???

Naomba mwongozo waheshimiwa.

Katiba hii hapa nimei-attach kila member aisome.
Halafu unaweza ku-click website yake kwenye mabano yafuatayo ili wasio JF members waweze kudownload: (http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf)

Ukishaipata katiba hii isambaze sambamba na nyaraka hizo za kanisa. Maana moja maazimio ya kanisa ni watu wajue katiba ambayo inafundisha haki zao. Unaona ilivyosaidia hata wewe umeomba katiba ambayo ulikuwa huijui na tumekupa. Sasa kwa mchakato huu wa kanisa wengine kama wewe watapata zaidi ya katiba.

Sambaza waraka wa kanisa. Sambaza katiba ya nchi.
 
Nilimshangaa Fisadi mkuu KINGUNGE NGOMBALEMWILO kulishambulia Kanisa katoliki lilipotoa taratibu ya kuwafundisha washiriki wake jinsi ya kutochagua mafisadi katika uchaguzi ujao mwakani (2010) . Katika uchaguzi ujao tunataka kupata akina DANILE, YUSUFU wa nyakati hizi, wenye tabia kama ya akina DANIEL , MUSA NA YUSUFU waliotajwa kwenye Biblia na Quran.

Hatutaki Mawaziri Makanjnnja, Hatutaki mbabaishaji, Hatutaki rais Msanii, Hatutaki rais ama waziri mhuni. Hatutaki Kiongozi wan chi anayelinda mafisadi, Hatutaki Kiongozi wa nchi anayeishi angani, Hatutaki kiongozi KINYONGA anayesema hiki leo , kesho anasema hiki, Hatutaki Kiongozi anayerubuni NCHI WAHISANI KUTOA FEDHA ZA MISAADA KUNEEMESHA MAFISADI AKIWEMO YEYE NA MKE WAKE huku Watanzania maskini wakifa kwa kukosa Tsh 1000/- ya kununua dawa ama kukosa Tsh 5000/- za kumwona Daktari, ama kukosa nauli Tsh 500/- kkwenda hopitali, huku mafisadi yakiishi kama yapo peponi. Watoto wa Maskini wanasoma katika SECONDARI ZA YEBO YEBO Huku watoto wa Mafisadi wakiwapo wa Karumekenge (JK) wakisoma ughaibuni. Watoto wa maskini walipa kodi wakikosa shule kwa kukosa fedha ya kulipia ada secondary na vyuo vikuu Huku watot wa mafisadi wakitanua MAJUU. Huku mafisadi wametunza feddha zao nje ya nchi zikinufaisha UCHUMI WA MATAIFA YA MAGHARIBI.

Huu UPUUZI na UNYAMA ndio unautetea KINGUNGE?. Kwamba Watanzania wasifundishwe kuleta MAPINDUZI YA AMANI YA KUWANYIMA KURA MAFISADI HAWA MWAKANI????. KINGUNGE WATU WAMEKUDHARAU KUPITA UKOMO.

KIBABUUUUUU KAMA WEWE TULITEGEMEA UWE UMEACHA UONGOZI WOWOTE MAANA UMESHAFIKIA KWENYE UMRI WA KUANZA KUVIA KUFIKIRI (MENTAL LITHERGY).

Kingunge umesahau kuwa wewe ni fisadi wa kutupwa kama ifuatavyo:

(1) Wewe ulilipotezea taifa mwelekeo na kuliwekea rais ALIYEFULIA KICHWANI. . Kingunge umesahau kuwa ulifanya hivyo baada ya kuhongwa dola million moja za Kimareakani mwaka 2005 ili umpitishe Karumekenge(JK). Fehda hiyo ni sawa na TSH Tsh billion 14 ambazo zingeweza kusomesha watoto wa maskini wapatao 20000 katika secondari. KIBABU WEEEEEE, Hiyo ndiyo misingi ya kujenga umoja wa kitaifa unaoupigia kerere na kulilaumu Kanisa Katoliki linapotaka kuelimisha Watanzania Walete Mapinduzi ya amani mwakani (2010) . KIBABU uwage na aibu kama busara haipo. Yaani kama busara imekuishia as per too being aged, basi tunakusihi UWE NA AIBU.

(2) KINGUNGE ukiwa umejiunga na ufisadi na upiga debe wa ufisadi huku ukiimba umoja wa kitaifa(AIBU) Unalipotezea taifa hili zaidi ya Tsh billion 980 kwa mwaka kupitia kampuni yako ya ulinzi jijini na kampuni ya kituo cha ushuru wa mabasi ya stand ya Ubungo (UBUNGO TERMINAL) uliyohongwa na KARUMEKENGE (JK) Baada ya kufanikisha kumwingiza madarakan kuanzia faulo na rafu ulizochangia kuanzia kwenye kura za maoni ambazo ULIFANIKISHA KUMG’OA NA KUMCHAFUA DR. AHAMED SALIM . Hivyo ulihongwa kwanza dolla 1,000,000/- kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyilo cha sakata la kura za maoni. Na uliahidiwa kupewa kampuni ya ulinzi jijini na UBUNGO TERMINAL. Hivyo wewe kingunde ni tapeli na fisadi la kutupwa. Tunakuomba kama ukanushe tukuanike zaidi maana hiiltuliyotoa ni WARM-UP tu ya ufisadi wako.

KWA HIYO KIBABU TUNAKUOMBA UNYAMAZE KABISA , UWAACHE WATANZANIA WAELIMISHANE JNISI YA KULETA MAPINDUZI YA KWELI ILI KILA MTANZANIA AFAIDI KWA MATUNDA YA RASILIMALI TELE MNAZOZICHEZEA NA MAFISADI.

Kingnge kumbe wewe ni wa ovyo. Unatetea mafisadi na kuucheza ufisadi na kudai Roman Catholic Move ya kuelimisha watu kwa amani juu ya ufisadi wenu na jinsi ya kuwang’oa kwa amani , wewe unaona ni kupoteza amani. Hujui kuwa chanzo ya CIVIL WARS huwa ni mafisadi wachache (5% ya taifa )kumiliki mali ya taifa na kuwaacha maskini wengi (95%) wakiishi kama wako jehanamu?

KINGUNGE NAKUKUMBUSHIA MAFISADI WANAOITAFUNA NCHI HII NA KUELEKEA UVUJAJI WA AMANI BAADAYE NI HAWA WAFUATAO:

(i) A..F. Magoma Mhasibu feki SUA .
Alilip[otezea taifa hili zaidi ya Tsh millioni 21,532,000,000/-kati ya mwaka 1995 na 2009.
Pinda na Karumekenge (JK Mrisho) wnalifahamu hilo. Wamelilea na kulilinda

(ii) PROFESA PETER MSOLLA –WIZARA:SAYANSI NA TEKNOLOGIA
Kalipotezea taifa zaidi ya Tsh 30,569,176,000/- tangu akiwa SUA hadi hapo alipo.Baba wa mafisadi (JK) analifahamu hilo)i.e. Mkitaka details tunazo.

(iii) DR. JUMA NGASONGWA
Alilipotezea taifa hili zaidi ya Tsh billioni 45 kifisadi kupitia wanyama pori na misitu yetu akiwa waziri husika wakati wa awamu ya tatu

(iv) Ndugu KAPUYA
Kalipotezea taifa zaidi ya Tsh 35 billioni kwa ubia wake na mine za nzega na Arusha . Pia kwa bendi yake aliyodanganya kuwa ni ya jeshi akiwa waziri ya ulinzi.

Hili ni kanjanja ama fisadi ambalo lina mzizi mrefu wa urafiki na JK Tangu wakiwa kijiweni Kinondoni. Fisadi huyu ana kampuni ya madini Nzega na Arusha ambay humwingizia zaidi ya billoni 200 kwa mwaka, kinyume cha katiba ya nchi. Alitumia ndege ya jeshi kuzalishia mali za familia yake, alianzisha bendi iliyokuwa inamzalishia fedha rukuku kwa wiki (Millioni 1.5) akiwa waziri wa ulinzi, bendi hiyo ilipandikizwa kama chombo cha jeshi la wananchi akachota VIJISENTI MABILLIONI. Huyu naye hafai kushika nafasi hiyo. Anatakiwa akamatwe na kufilisiwa

(v)ROSTAM AZIZ. Huyu ni kanjanja hatari sana, alilifirisi taifa hili kwa biahsahra haramu aliyofanya mkataba wa kibishara na Japan ambao hazitozwi ushuru, Ameipotezea nchi yetu zaidi ya billioni 200. Ni mwasisi wa wizi wa fedha za BOT kupitia EPA akitumia kampuni feki na mufilisi ya KAGODA (Billioni 40) akishirikiana na fisadi lililokubuhu- Benjamin Mkapa. Ni rafiki kipenzi cha mzee Kanjanja /cheka cheka Huenda dili hilo ni lao. Anamilki makampuni makampuni manane, lakini yale saba jina anayamilki kijasusi kwani jina lake halipo. Makampuni hayo ni haya yafuatayo:
Africa Tanneries Limited
Tanzania Leather Industries Limited
Wember Hunting Safari Limited
Tanzania Packages Manufacturers Limited
Dowans
Kamppuni ya kagoda
Isenegeja Limited (ijulikanayo kama THE NEW HAGARI LIMITED –NHL) iliyonunua Magazeti ya The African, Dimba, Bingwa, Rai, Mtanzania na chuo cha uandishi wa habari (MAMET)

(vi) MEGHJI
Alilifirisi taifa zaidi ya Tsh billion 20 kwa vitalu vya uwindaji haramu vya wanyama pori akiwa waziri husika wa wizara hiyo. Pia humo ailikuwa na vitaru haramu vya familia yake pia na vya ndugu zake. Karumekenge analifahamu hilo , lakini kutokana na maslahi binafsi amekauka.

(vii) KINGUNGE NGOMBALEMWILO
Huyu amelipotezea taifa hili zaidi ya Tsh 130 billion kupitia kampuni yake ya ulinzi jijini na kampuni ya kituo cha ushuru wa mabasi ya stand ya Ubungo (UBUNGO TERMINAL) aliyohongwa na KARUMEKENGE (JK) Baada ya kufanikisha kumwingiza madarakan kuanzia faulo na rafu alizochangia kuanzia kwenye kura za maoni ambazo WALIFANIKISHA KUMG’OA NA KUMCHAFUA DR. AHAMED SALIM . Hivyo alihongwa kwanza dolla 100000/- kabla ya kuingia kwenye kinyang’anyilo cha sakata la kura za maoni. Na aliahidiwa kupewa kamuni ya ulinzi jijini na UBUNGO TERMINAL. Hivyo kingunde ni tapeli na fisadi la kutupwa.

(viii) ABDALLAH KIGODA
Kalipotezea taifa zaidi ya Tsh 6.1 trillion kwa sakata la EPA, RADA, MIKATABA MIBOVU YA MADINI, UUZAJI FISADISHI WA MASHIRIKA YA UMMA NA KUJIKABISHISHA KIWIRA AKIWA NA MRS MKAPA NA B.MKAPA.

(a)Wizi wa zaidi ya Tsh* Trillioni 5, 97 BOT kwenye kampeini za uraisi na ubunge zilizotuwekea rais mufilisi. Kigoda anatakiwa asimame kuelekea kizimbani na kujibu wizi huo ulioifilisi nchi* ikawa kama dampo la umasikini
(b) Uporaji fedha za* taia hili kupitia ununuzi wa rada feki Tsh 50 billioni ambayo akiwa na Mkapa na Mramba waliishupalia kama ruba
(c) Uuzwaji angamizi wa mashirika ya umma na viwanda kwa hila zote, kwani hata yale yaliyokuwa yakijiendesha kwa faida kubwa yaliuzwa kwa bei ya tupatupa (throw away prices)
(d) Kushiriki mikataba mibovu ya madini alilipotezea taifa zaidi ya Tsh mia tisa- kwa kipindi chote Hivyo huyu ni fisadi lililokubuhu.

(ix) Edward Hosea (TAKUKURU- Taasis ya kukuza na kurutubisha rushwa)
Kalipotezea taifa zaidi ya Tsh billion 298.2 kupitia kulinda RICHMOND, EPA (BOT), kuharalisha vitalu haramu vya uvunaji wanyama pori,kupitisha mikataba feki kama ya TICS, TRL, MIKATABA MIBOVU YA MADINI PAMOJA NA MADUDU MENGINE MENGI. Kanjanja hilo bado linakumbatiwana KARUMEKENGE na TARISHI WAKE (PINDA).

(A): Amekomba zaidi ya billioni 140 kwa kupokea rushwa nene na kutoa taarifa feki kwenye uchunguzi wa RICHMOND , sakata la Buzwagi, mikataba mibovu ya madini, sakata na hujuma za wahindi kupanga kwenye nyumba nzuri za National Housing kuliko wazawa, Sakata la DOWANS na hujuma nyingine nyingi. Ni fisadi anayetakiwa ajiuzuru mara moja.. Pia lilikuwa kwenye kamati ya kuchunguza wizi wa fedha za BOT (kupitia EPA), Je fisi anaweza kumchunguza fisi mwezie au kujihukumu mwenyewe? NEVER!!!!. Hiyo ni danganya tot
(B) Inaaminika kuwa amekuwa akila fedha hizo na wakubwa ama kupitisha miradi/ feki ya wakubwa kama vile TICS, TRL , Vitalu vya uvunaji wanyama pori na mikataba mingi ya kifisadi ndiyo maana bado anakumbatiwa na JK.. Huyu naye ni nyang’ao linalositahili kukamwatwa na kufilisiwa baada ya kuwekwa ndani/jeli kwa kesi inayofanana na ubakaji wa mali za umma.

(x) ANDREW CHENGE
Kalipotezea taifa zaidi ya Tsh trillion 133.7 kupitia yafuatayo> EPA, RADA FEKI, NDEGE FEKI YA RAIS, MIKATABA MIBOVU YA MADINI, UUZWAJI TUPATUPA WA MASHIRIKA YA UMMA, UFICHAJI FEDHA NJE YA NCHI, KULA RUSHWA NZITO NZITO KWA MATAPELI WA KIHINDI N.K.

(a) Akiwa mwanasheria mkuu wan chi, alihararisha wizi wa zaidi yaTsh Trillioni 133 BOT kwenye kampeini za uraisi na ubunge zilizotuwekea rais mufilisi. Chenge anatakiwa asimame kizimbani na kujibu wizi huo ulioifilisi nchi* ikawa kama dampo la umasikini
(b) Uporaji fedha za* taia hili kupitia ununuzi wa rada feki ununuzi wa Rada na Ndege ya feki ya rais Tsh 90 billioni kwa ujumla wake alishauri vibaya kwa maslahi yao (yeye, Mramba na Mkapa) badala yan maslahi ya taifa
(c) Uuzwaji angamizi wa mashirika ya umma na viwanda kwa hila zote, kwani hata yale yaliyokuwa yakijiendesha kwa faida kubwa alishauri yauzwe kwa bei ya tupatupa (throw away prices)
(d) Kushiriki mikataba mibovu ya madini kama vile Nzega gold mine, Geita gold mine, Buhemba gold mine, Bulyankulu ngold mine, Kahama mine , Buhemba mine, Melelani Tnzanzanite mine alilipotezea taifa zaidi ya Tsh Trillioni 18/- kwa kipindi chote .
(e) Imeficha fedha lukuku ndani na nje ya nchi kwa ufisadi wa kinyonyaji, hatufai.
(f) Inaaminika kuwa aliwahi kuizidi esrikali ya Tanzania zaidi ya billioni 15 na analielewa hilo. Hivyo huyu ni fisadi mufilisi, ni kibaka wa kodi za walala hoi. Kwa maneno mengine amekunywa damu ya watanzania na kuwaacha wakiwa na upungufu wa damu (anaemic natioi),Hana tofauti na vibaka wa viungo vya ALBINO.. Tunashauri akamatwe na kufirisiwa..

Karamagi, Lowassa na Msabaha wamelipotezea taifa zaidi ya Tsh 1,824,000,000/- kwa mwaka Kwa kukwepua Tsh 152,000,000/- kwa siku. Na hapo Kikwete anawasifia ni wahanga wa kisiasa. Bora wafirisiwe tu, maana tukisema wafikishwe mahakamani ni danganya toto tu. Maana kesi zao ni zile zile za kina MAHALU , Kesi Ambazo zimetawaliwa na kupigwa tarehe hata kama ushahidi uko wazi.Lowassa, Karamaji na Msabaha mnasubiri nini kuachia uongozi mlionano , maana kama ni kunuka ni mnuko wa uozo mbaya fisadishi. Pia Karamagi ndiye kingunge wa wizi wa mali ya taifa hili kwa kulipotezea takribani Tsh 205,596,500,400/- kwa kampuni yake ya TICS bandarini Dar-es salaam.

Masha, fisadi la EPA na vitambulisho vya kitaifa, anasemekana kuipotezea Tz zaidi ya billioni 40 kutokana na ufisadi wa EPA, pia ilikuwa amejiandaa kulipotezea Taifa zaidi ya Tsh 200,000,000,000/- kwa mkataba mufilisi wa vitambulisho vya taifa. Watanzania na Tanzania wanahujumiwa kila kukicha na mafisadi ambayo yanaishi kama yapo peponi. Is high time sasa tuwamulike kenge hawa.Hivi ni halali kenge ama mbweha kujichanganya na watanashati wa kimaadili? . Ama kweli ukijipaka harufu mbaya , harufu ya uozo ukakubali kujipaka kwa muda mrefu huwa inafikia wakati unaizoea unajisikia kama hunuki. Viongozi wa andamizi wa ngazi zote hadi kichwa cha state wamejipaka harufu ya ufisadi na kuvaa ufisadi hadi kutosikia harufu mbaya inayotoa kichefuchefu kwa kila mtanzania. Wanadai Chama ni kisafi isipokuwa wanachama wake ni mafisi. Hivi ukikuta baba mwenye nyumba, mkewe na watoto ni walevi, wagomvi, wezi , UTASEMA KUWA FAMILIA HIYO NI NZURI SANA ISIPOKUWA MWANAUME, MWANAMKE NA WATOTO TU NDIO WABAYA. Hapa nadhani hata taihira atkucheka kwani atakuwa nafuu kifikra.

(xi) Karamagi,
amelipotezea taifa zaidi ya Tsh 9,824,000,000 Kwa ufisadi wa RICHMOND, DOWANS na TICS akiwa. TICS ni wazi KATUMEKENGE amejifichamo

(xii)E. Lowassa
Amelipotezea taifa zaidi ya Tsh 1,824,000,000 Kwa mwaka wake wa RICHMOND

(xiii) Msabaha
Amelipotezea taifa zaidi ya Tsh 1,824,000,000 Kwa mwaka wake wa RICHMOND

(xiv) MASHA,-wizara ya wizi wa ndani
Amelipotezea taifa zaidi ya Tsh billion 458.7 kwa kampuni yake inayodaiwa ni kampuni ya jeshi la wana na sakata la vitambulisho fisdadishi vya taifa.

(xv) Pro/ MAGHEMBE
Amelipotezea taifa zaidi ya Tsh 130,000,000/- kwa kulea wauzaji wa mitihani ya NECTA na uuzaji wa vyeti bandia. Pia ameamua kujenga taifa la mazezeta kwa kuachia mitahani iliyovuja kutahini wanafunzi. He could the most dangerous figure in our national. Cha ajabu Karumekenge akisikia hayo anacheeeeekaaaa hovyo hvoyo (hopelessly).

Maghembe , waziri wa Elimu NA UFISADI
Ameruhusu watu waliochini yake kukwapua zaidi ya Tsh 80,000,000/- kwa kuuza mitihani ya kidato cha nne mwaka 2008.
(a) Alidanganya kuwa mitihani mingine haikuvuja isipokuwa mtihani wa Hisabati tu. Hii si kweli kwani mitihani yote ilikuwa imezagaa mithili ya maswali ya masomo kama Historia, Vivics, Geografia, Kiswahili yalikuwa yanafungiwa kwenye karatasi walizokuwa wakiuzia maandazi na vitumbua akina
(b) wanafunzi ambao hawakusoma masomo takribani Chemistry, Physics walipewa credits kwenye masomo hayo kwenye matokeo yao, wanafunzi ambao (e.g. Wilaya ya Serengeti), wanafunzi ambao hawakuwa na History walijikuta wana alama ya B ama C kwenye matokeo yao.
(C) Almost kila wilaya ilipewa mtihani wake tofauti, huku maghembe akinadi kuwa mitihani haikuvuja. YA Kama mitiani mingine haikuvuja , ni kwa nini sasa alisambaza mitihani tofauti kila wilaya ama mkoa nchini?.
(d) Wanafunzi ambao walifeli masomo yote walijikuta wameandikwa wamepasi masomo mawili au matatu. Inakuwaje mwanafunzi amefeli masomo yote saba ama manane (i.e. 8 Fs or 7Fs) anaandikiwa pass ya masomo mawili? Huu ni usanii wa hali ya juu sana.
(e)Inasemekana kwamba baada ya Maghembe na katibu wake kugundua kuwa mitihani yote imevuja, alichokifanya ni kutafua mbinu za kubaki madarakani. VIPI?. Ujanja aliotumia ni kuihakikisha shule nyingi zinafelishwa ili kuhakikisha uongo wake kuwa mitihani haikuvuja , pia aliiamrisha NECTA itoe namba tu kwenye matokea . Hivyo matokeao yakatoka kwenye internet yakiwa yana namba tu bila majina ya watahiniwa. Hii ilimsaidia kuficha uozo wake na uozo wa NECTA na Wizara yake kwa ujumla.Kutokana na hayo, hivi kwanini NECTA, KATIBU MKUU WA WIZARA HINYO NA MAGHEMBE WASIJIUZULU?

Otherwise, wanatujengea taifa la mazezeta. Kikwete na Pinda wamekauka, huenda wanapenda taifa liendeshwe kiukoo kwani watoto wao na wajukuu wao wako ACCESSIBLE KWENDA KUSOMA NJE ZA NCHI na kujiandaa kuja kutawala taifa hili kwa miaka nenda rudi (infinite time period) MAGHEMBE UNASUBIRI NINI KUJIUZURU?

(xvi) WILLIAM NGEREJA:
Ameeendela kulipotezea taifa Tsh 35,561,602,550/-Kwa mwaka kupitia kukumbatia ufisadi wa mikataba mibovu ya madini, utapeli wa vigogo wa TANESCO, DOWANS, IPTL, APR, KIWIRA POWER RESOURCE, SONGAS n.k.

Waziri wa Nishati na Madini anahusishwa na ufisadi kwa kukumbatia ama kufumbia ufisadi ufuatao:

(a) Takribani Tsh 798,950,604,900..75 zimekuwa zikipotea kwenye secta ya madini kwa kupitia mikataba mibovu na fisadishi ya madini yetu yanayoporwa na wachimbaji kutoka mataifa ya kibeberu. Ngereja analifahamu hilo lakini yeye amefumba macho na kujifanya haoini HUKU AKIFAIDI CHA JUU katika uharamia huo. Si rais ama Waziri mkuu anayejali ama kupata presha ya moyo ama matumbo. Wako kimya wakijua kuwa taifa hili either limelogwa hadi kuwa taifa la mambumbumbu ambayo hayasikitiki ama kuhoji juu ya uharamia huu ambao unatukfanya (80%) TUISHI MAISHA YA KUBAHATISHA AMA KUBANGAIZA HUKU WAHESHIMIWA HAWA WANAISHI MURUA KIASI CHA KUSHINDWA KUTOFAUTISHA KATI YA PEPONI PAO NA MAISHA YA PEPONI –MBINBUNI

(b) Takribani zaidi ya Tsh 700 millioni .kwa siku ama Tsh 255,500,000,000/- kwa mwaka zinasagwa kupitia TANESCO ambayo huwalipa wazalishaji feki wa umeme kwa kupitia mikataba ya makampuni feki na fisadishi wakiwemo marais wasitaafu. Hapa Dr. Rashidi –mkurugenzi mtendaji wa TANESCO wnashirikiana na Ngereja kuliangamiza taifa, otherwise kama wangekuwa wanafanya kazi kwa manufaa ya taifa hii wangekuwa wamepeleka hoja bungeni ya kuyafutia mikataba makampuni fisadishi haya, ama wangekuwa wametangaza kuacha kazi kwa kushindwa kuwajibika. Makampuni yanayolitafuna taifa hili kwa kuikaba koo TANESCO na watanzania kwa ujumla ni haya yafuatayo:

(i) IPTL hutafuna Tsh 5.6 billioni kwa mwezi (Tsh 3.8 billioni kwa gharama za uwekezaji na Tsh 1.8 billioni kwa kuitunza mitambo i.e. capacity charge) ,ama Tsh millioni 284 kwa siku. .Hapa haijalishi tumepata umeme ama hatujapata, tumetumia umeme ama hatujatumia!!!!, Mkataba huu fisadishi ulisainiwa mwaka 1995 na aliyekuwa wazairi Wizara ya Nishati na Madini wakati huo, sasa ni kingunge wa mambumbumbu wa taifa hili.
(ii) DOWANS dada RICHMOND inalipwa Tsh 156 millioni kwa siku ama Tsh 4,740,000,000/- kwa mwezi bila kujali uchakavu wa mitambo yao na bila kujali kutokuzalisha kwao umeme. Kuna kuwadi mmoja kutoka nchi za magharibi alitamuka wazi wazi kuwa watanzania toko kwenye dozi nzito iliyoroga viini vya kufikiri (centres of thinking and reasoning) BILA KUJALI KUWA HUYU NI MAAMUMA AMA NI PROFESA.
(iii) SONGAS yenye mkataba angamizi wa miaka 20 hupora Tsh 264 millioni kwa siku ama Tsh 7,928,000,000/- kwa mwezi bila kujari wamezalisha au hawakuzalisha umeme , lazima TANESCO walipe. Viongozi wa TANESCO ngazi za chini wakipiga kelele hushushwa vyeo ama kuhamishiwa porini, hivyo waliopo sasa wamenyamaza na kuwaachia watanzania waamue kama sauti ya umma. Masikini wana TANESCO hawa hawajui kuwa watanzania WAMEJIDHIRA.
(iv) ASTON POWER RESOURCES (APR) ya Mwanza hulipwa Tsh 76 millioni kwa siku ama Tsh 2,280,000,000/- kwa mwezi . Napo bado pana mgao wa umeme nchini
. (v) AGRECO hunyofoa na kufyonza Tsh 62 millioni kwa siku ama Tsh 1,860,000,000/- kwa mwezi, napo bado kuna mgawo wa umeme mkali, na bahati mbaya zaidi zaidi ya 89% ya Watanzania hawatumii umeme hasa vijijini ambako wanatumia vibatari ama vijinga vya moto, bado nao wanakumbwa na zahama hii ya kulipa kodi inayonufaisha mafisadi ya ndani na nje ya nchi.
(vi) KIWIRA POWER RESOURCE hufyonza na kufisadisha Tsh 300 millionni kwa silu ama kupora Tsh 9,000,000,000/- kwa mwezi bila haya. Kingunge wa kampuni hii hana aibu, kwani mwaka 1995 alipita nchi nzima akiwahadaa Watanzania , viongozi wa dini , hata Maaskofu wake kuwa yeye ni msafi (clean) na angepambana na rushwa na wala rushwa , kumbe alikuwa akivuna laana tu , kwani kudanganya umma masikini kama huu wa kitanzania , pia ukadanganya viongozi wako wa dini ni kuvuna laana ambayo inafukuta,

(c ) Ngereja bila aibu amesikika akiipigia filimbi DOWANS kwamba richa ya ukweli wa wazi wazi kuwa vifaa vya DOWANS ni vichakavu, yeye ameishupalia esrikali ivinunue ili kulinusuru taifa hili na giza akidai kuwa mabwawa yetu yamekauka. JAMANI , HATA MWEHU HUWA NA AKIBA YA FIKIRA YA KUJUA SASA NI WAKATI WA MASIKA AMBAPO KUNA MVUA YA KUTOSHA. Hili nalo linafaa kuwashawishi Ngereja na Rashidi kuachia ngazi ili taifa liweze kutembea kimwelekeo wa kusaka maendeleo ya umma .

(d) Ngereja alisema wazi kwa Watanzania kwamba Serikali imeendelea kunadi kuwa mtaji inayowekeza serikali kwa suala la umeme ni Tsh 50 millioni kumbe kinyemela zinatolewa Tsh 36,000,000,000/- .
Kwa hiyo kutokana na hujuma hizo ambazo Ngereja amezikumbatia ama kuzinyamazia huku taifa likiporwa kila kukicha , anakuwa ni sehemu ya ufisadi akishirikiana na Fisadi Dr. Rashid wa TANESCO, wote hawa wawili hawastahili kuendela na nyasifa hizo.

(xvii) BENJAMINI MKAPA
Kalipotezea taifa zaidi ya Tsh Trillion 98.5 kwa miaka yake akiwa ikulu kwa miaka 10 (1995-2005) kwa kupitia uanzishaji wa EPA,, Kampuni zake (ANGEN, fosnik, TANPOWER,) Ndege feki ya rais, RADA, utupaji wa mashirika ya umma, kushiriki mikataba mibovu ya madini kwa masrahi yake binafsi,kuweka rais pandikizi-karumekenge, kuendelea kuienzi kampuni angamizi ya ITPL

(xix) WASIRA-Waziri wa kilimo na chakula.
Alikiua kilimo tangu miaka ya sitini kwa kujali maslahi yake binafsi. Ikiwemo kula fedha ya mbolea ya ruzuku waka 2008. Sasa amekiua kilimo kwa kusambaza mbolea angamizi ya Minjingu hufanya mimea ivie ama kuzuia kukua ikichanganywa na mbolea zingine kama vile CAN, TAP, TSP,SA, UREA. Mbolea ya minjingu imewaliza wakulima wengi.

(xx) MWANYIKA , MWANASHERIA MKUU TANZANIA,
Amekomba zaidi ya billioni 987 kwa kupokea rushwa nene na kutoa taarifa feki kwenye uchunguzi wa RICHMOND , sakata la Buzwagi, mikataba mibovu ya madini, sakata na hujuma za wahindi kupanga kwenye nyumba nzuri za National Housing kuliko wazawa, Sakata la DOWANS na hujuma nyingine nyingi. Ni fisadi anayetakiwa ajiuzuru mara moja.. Pia lilikuwa kwenye kamati ya kuchunguza wizi wa fedha za BOT (kupitia EPA), Je fisi anaweza kumchunguza fisi mwezie au kujihukumu mwenyewe? NEVER!!!!. Hiyo ni danganya tot(B) Inaaminika kuwa amekuwa akila fedha hizo na wakubwa ama kupitisha miradi/ feki ya wakubwa kama vile TICS, TRL

Ameifilisi nchi kwa kusaini mikataba FISADISHI alimradi tu akajari masilahi yeke binafsi. e,g,BOT, RADA, RICHMOND, DOWANS, UNUNUZI WA NDEGE YA RAIS, ubinafishaji TRL, IPTL . Alilipotezea taifa zaidi ya Trillioni 15. ANASTAHILI AKAMATWE NA KUTIWA NDANI. LAKINI KIKWETE BADO ANAWAIMBISHA HALELUYA . It is too un-Islamic and un-Godliness.

(xxi) WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI/UVIVU
imeoza mpaka kwenye visigino tukisema imeoza hadi kichwani tutakosea. Hebu fikiria , Botswana ina ng’ombe millioni tatu na nusu , lakini inaingiza pato la taifa kiasi cha 80% GDP. Tanzania ina ng’ombe 18.5 million, lakini inaingiza pato la taifa kwa asilimia 4.9% tu. Hivi pinda huoni kuwa hapo panahitaji kusambaratishwa na kuundwa upya. Kumtoa Diallo peke yake haikutosha, mimi nachukulia kuwa ilikuwa chuki ya kibinafsi kati ya diallo na bosi wako. Maana aliacha mapapa yanayotafunafedha za walipa kodi kwa kudai wanatuma mamia ya millioni kila mwaka kudai zinakwenda kuboresha sherehe kama vile
(a)maonyesho ya nane nane
(b)wiki za maziwa
(c)maonyesho ya sabasaba
(d) Safari za nje ya nchi za makatibu wakuu. Kurugenzi, na marafiki wa vigogo hao waliopo wizarani.

Nasema kuwa Safari hizo zote matunda yake ni ziro kama sio kwenda kupata mitaji haramu na material fisadishi. Kwani mifugo na mfugaji mwenyewe wamebaki vile vile kama miaka ya 1820 AD. Sehemu zingine ambazo zinatafuna fedha ni makongamano, washa na seminar zailizoanza tangu miaka ya 60 lakini hadi leo mifugo imebaki hafifu isiyokidhi soko la nje.

Wafugaji wamekuwa wakimbizi ndani ya nchi yao , wakifukuzwa kila wanapokwenda bila kutengewa eneo maalumu.?. Ihefu?, Kilombero?, Kilosa?) na kuhamishiwa kwenyhe kanda za ndolobo kama vile Lindi ili mifugo yetu isiweze kuwa na thamani ya soko la nje. Ndugu pinda anayajua haya na bosi wake Karumekenge. Lakini kutokana na ufinyu wa akili zao, wameshindwa kuivunja wizara hiyo ama kuiweka chini ya WIZARA YA ULINZI, yaani iwe ”WIZARA YA ULINZI NA MAENDELEO YA MIFUGO”, na kuwang’oa VINGUNGE WALIOPO HAPO KWA NAFASI ZA UKATIBU MKUU AMA KURUGENZI FISADISHI. Hapo ndipo Mifugo ingezalisha pato linaloeleweka..

Lakini Pinda akipelekewa matatizo hayo ANASHANGAA SHANGAA TU HUKU Bosi wake akiyasikia hayo anacheeeeekaaaa kama kichaa kaokota tambala chafu jalalani.

INATISHA! MASKINI TANZANIA UMEVAMIWA NA VIONGOZI MATAPELI, POLE SANA MTANZANIA!!!!!. Wizara hii ameipiga HATI CHAFU MKAGUZI WA MAHESABU YA TAIFA (CAG), YAANI AMEIPIGA ZIRO. WEWE PINDA HULIONI HILO? Kwa bahati mbaya zaidi , MAGUFULI AMEFUNGA KUFULI KWENYE MIFUGO, AMEJILKITA KWENYE SAMAKI PEKE YAKE. NILISHANGAA SIKU MOJA KUSIKIA KUWA AMEKAMATA KOKOLO ZA UVUVI HARAMU KWENYE MADIMBWI YA SAMAKI HUKO ARUSHA. JE TUTAFIKA?

KWA KUFAFANUA ZAIDI , KINGUNGE TUANAKUPA MAELEZO YA KINA KIREFU KIASI CHA BAADHI YA MAFISADI TULIOWAORODHESHA HAPO JUU:

Ulikoma kukwepua fedha hizo baada ya Prof Peleka (DVC) wa SUA kumshitukia na kulazimisha vibarua wafungue akaunti mwaka 2008.

Ulaji wa Tsh 60,000,000/- kwa kingiza makonteina feki kati ya mwaka 2000 na 2004 . Hujuma hiyo ilikoma baada ya kumtapeli mama Fulani (jina tumelihifadhi) rafiki yake na mama Ana Mkapa . Mama huyo kwa kumtumia Anna Mkapa, polisi walifuatilia hadi kuyaona makonteina yake mawili hapo SUA. Magoma alishauri uongozi SUA wamtoe kafara mhasibu mmoja (Mr. Mkama) kwa kuwekwa mahabusu takribani mwezi mmoja, baadaye fedha hiyo hiyo ikatumika kuhonga polisi na Kumwacha huru Mr. Mkama mpaka leo.

(e) Wizi wa Tsh 442,000,000/- SUA Tarehe 22/4/2006 . Baadhi ya fedha hizo (400,000,000/- ) zilikuwa zimekusanywa kama Pet-cash , zingine Tsh 42,000,000/- zilkuwa malipo ya wafanyakazi, cha ajabu tarehe 22.4.2006 zikatangazwa Tsh 42,000,000/- tu , kwa maana kwamba zile Tsh 400,000,000/- ziliachwa kutangazwa makusudi ili kupunguza makali ya ufisadi huo. Magoma alikutwa na fedha zaidi ya Tsh 80,000,000/- nyumbani kwake siku hiyo ya tukio. Cha ajabu alikamatwa na wahasibu wenzie baadaye akaachiwa baada ya kumhonga polisi aliyekuwa anapeleleza kesi hiyo. Kikwete alipewa taarifa hizo , nafkiri alicheka cheka na baadaye kuunda safari ya kwenda Marekani (USA) kwa bosi wake. Fedha hizo aliongezakununua magari , kujengea majumba ya nguvu wake za watu (e.g. Mama nyabinyili, Mama Magafu, Mama Dowire,Mama demagera,Mama Ngokomwa, Mr Paulo Manumba) na kuvunja ndoa zao na nyingine nyingi ikiwemo ya Mama NICE(huyu ndiye mwenye hasara kwani hajajengewa nyumba, ameishia kuchezewa na kuvunja nyumba tu. Magoma anapractice enzi za Sodoma na Gomora ndani ya taifa linalojiita linafuata siasa za Ujamaa na Kujitegemea.

Wakuu wanafahamu , lakini wamekauka huenda kwa vile nao wana mchozo huo huo, TUSUBIR MUNGU ATOE ADHABU YA MITHILI YA SODOMA NA GOMORA AU ZAIDI KWA TAIFA HILI. Huwezi kuamini kwamba watoto wa masikini wanashindwa kwenda shule, ama masikini kufa majumbani au mbele ya Hospitali kwa kukosa fedha ya kumwona daktari (Tsh 10,000/-) na kukosa dawa huku wengine wanaishi maisha ya KUFURU

(f) Wizi wa Tsh 130,000,000/- Kwa ukarabati hewa na uwekaji furniture hewa wa nyumba anayotakiwa kuishi makamu wa chuo (Vice Chancellor (VC) . Hujuma hiyo ilifanyika mwaka wa fedha 2007/2008. Magoma na VC (Prof Monera) walibuni mradi huo kwa kudanganya kuwa waliingiza furniture mpya na kuikarabati nyumba hiyo. Kwa kweli nyumba hiyo ilikuwa na kila kitu, na ilikuwa haihitaji ukarabati wowote, Kwa hiyo huo ulikuwa ni ufisadi-hujumu. Taarifa hizo wanazo Pinda na Kikwete, wamejikaukia.

Mimi nawashangaa Watanzania wenzangu tumelogwa na nini, maana utakuta watu mitaani wakisifia utendaji wa Pinda ama Kikwete, je wanasifia kwa lipi iwapo wameachia fedha ambayo
(i) ingesomesha Watanzania bure hadi chuo kikuu bure imo mikononi mwa mafisadi as if yanaaishi miaka 500
(ii) Fedha ambayo ingewezesha watanzania watibiwe bure imo kwenye magodoro ya mafisadi
(iii) Fedha ambayo ingenunulia matrekta imefugwa kwenye akakunti za mafisadi Ulaya
(iv) Fedha ambayo ingenunulia mbolea ya wakulima wetu (peasants) imehifadhiwa kwenye mifuko ya wahujumu uchumi ndani na nje ya nchi
(v) Fedha ambayo ingeanzisha kilimo cha kumwagilia na ranchi kubwa za mfano Tanzania na Africa imefunikwa kwenye akaunti fisadishi nje na ndani ya nchi. Cha kushangaza zaidi, watu hawa wanawafahamu, tunawafahamu, tunapishana nao wakiwa kwenye mashangingi yao yaliyopora jasho la walipa kodi.
Tuamke tuyamulike mafisadi haya kwa kutoshabikia ziara zao,ama kwa kuandaa kura zetu vizuri kupigia kura ya NO NO NO KILA FISADI KATIKA NGAZI ZAO ZOTE ZA UNGOZI. NCHI ZA WENZETU HUWA YANAZOMEWA LICHA YA KUNYIMWA KURA.

(g) WIZI WA TSH 200,000,000.00 KATIKA UJENZI WA MGOROFA MAWILi (mabweni ya kulala wanafunzi) badala ya manne kati ya 2007/2008. Plan ya awali ilikuwa kujenga magorofa manne , baadaye Magoma akashauri wajenge gorofa mbili tu ambazo eti ziko modified. Hapo ndipo walikata Tsh 200,000,000/- wakaweka mfukoni na wakubwa wa chuo Gray Mgonja
(A) Alibariki na kuhisika na uporaji wa sh 17,857,616,400/- BOT kwenda kampuni yao ya *Tangold ltd akiwa mkurugenzi wa BOT pia hapo hapo akiwa mkurugenzi wa Tangold ltd kampuni ambyo hikuwa na usajili.
(B) Kunyamazia ufisadi wa uporaji wa trillioni za fedha BOT* kenda kwenye makampuni hewa akiwa mkurugenzi BOT. Pia liko kwenye kamati for determining the corrupt persons in Abusive thefty of BOT, Je fisi anaweka*kumhukumu fisi mwezie au kujihukumu mwenyewe? NEVER!!!!. Hiyo ni danganya toto ya Kikwete ambaye bado anafikiri anaongoza Watanzania wa miaka ya 1960s. Leo nadokeza tu.Mambo haya yanauzi sana
MAFISADI WENGINE NI :
WASIRA-Waziri wa kilimo na chakula. Alikiua kilimo tangu miaka ya sitini kwa kujali maslahi yake binafsi. Ikiwemo kula fedha ya mbolea ya ruzuku m
waka 2008. Sasa amekiua kilimo kwa kusambaza mbolea angamizi ya Minjingu.
-Anna Mkapa na ANBEN YAKE, ushauri mbaya kwa fisadi Mkapa
Sophia Simba , huyu hajui kile anachokifanya, yupo yupo tu kwa vile anakula na bosi wako
SHUKRU KAWAMBWA. MPWA WAKE NA KARUMECHENGE, Ameleta losi kwa Wizara tatu za Tsh 105 billion kwa kushindwa kusimamia watu waliochini yake. Na sasa yuko kwenye wizara ya nne. Yaani amezishindwa Wizara nne tangu azawadiwe uwaziri na Mjomba wake (Karumekenge). Ameshika wizara nne kwa muda wa miaka miwili na nusu tangu mwaka 2006 hadi 2009 na hakuna wizara inayotembea mara tu apewapo tapeli huyo wa ujomba.
 
Last edited by a moderator:
Shy,

You do not sound like an I.T Sepecialist (grin)

This is toooooo looooooooooong!
 
Duu Mjomba anapita pita humu apate ujumbe wake???balaa.....nchi kama haina mwenyewe sasa...maana hata Kikongwe nae amebadilika kabisa yuko upande wao....sio wa wananchi tena....sijui rashid Mafaume yuko wapi na familia yake maana najua anamuunga mkono JK
 
"Hata hivyo, Kanisa Katoliki kupitia Baraza lake la Maaskofu (TEC), limekuwa na utamaduni wa kutoa mwongozo kama huo wakati Taifa linapoelekea Uchaguzi Mkuu, huku kumbukumbu zikionyesha kuwa pia lilifanya hivyo mwaka 2005."

Mzee Kingunge keshapoteza heshima yake kutokana na mambo mengi aliyofanya kinyume na matarajio ya Watanzania walio wengi ambao walikuwa wakizitegemea sauti za 'wazee wenye busara' katika kutoa ushauri mzuri na miongozi kwa faida ya Taifa letu sasa na kizazi kijacho. Katika hili mzee Kingunge amechemsha big time.

Tunaambiwa mwaka 2005 Kanisa Katoliki lilitoa mwongozo kama huo lakini hatukusikia sauti ya Mzee Kingunge akisema kwamba mwongozo huo 'urudishwe'! Why now?

Watanzania wote, iwe kutoka kanisani, msikitini, jamatini, mitaani n.k.wanayo haki ya kutoa mawazo yao ili mradi hawavunji sheria. Wakatoliki kwa mwongozi wao wamevunja sheria gani hata wasakamwe hadi na Mzee Kingunge? Hata kama 'mwongozo' huo wa Kanisa Katoliki utarudishwa kama anavyotaka Mzee huyu ni kipi kitawazuia Wakatoliki kutoa mwongozo huo kwa waumini wao kwa njia ya kusimama madhibahuni na kuusoma na kuuhubiri kikamilifu mpaka uwaingie waumini na kusambaa kwa watu wengine kupitia Wakatoliki?

Alichotakiwa kufanya Mzee Kingunge kama 'mzee mwenye busara' na mshauri mahsusi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi ni kuangalia ni jambo gani limekwenda kombo ama liko kombo nchini lililopelekea Wakatoliki kutoa mwongozo kama huo na manung'uniko mengine ya wananchi kwa ujumla. Akishafanya hivyo, anapaswa kuishauri Serikali ama Chama ili vyote viliwi virudi katika mstari wananchi makanisani, misikitini, majamatini, na wasio na dini wote waridhike na hali halisi.

Mzee Kingunge atafakari kwa nini Miongozo kama hiyo inatolewa kwa wananchi na si kutaka kuisitisha kwa kuwa haiwapendezi watu kadhaa.
 
Nimecheka saana nilivyosoma hoja ya Tiba. Watu mnaogopa saana kuwa critisized. Eti alijiunga lini? Sio hoja ya msingi. Nimekuwa nikisoma saana JF for years sasa. Nikaona naguswa kuweka mkono. Sina lengo la kudivert attention ila nataka tuwe fair. Weka hoja kama na wewe ni msafi otherwise kaa kimya. Ukiiba wewe sawa ila wengine hapana. No way kama wanaweza hasa wawatenge na mafisadi tuone kama hao mafisadi watapumua. Mbona wao wanawakumbatia? Tuzibe mianya yote ya kwnye uongozi hadi kwenye dini.

Mkuu bnhai,

Jibu hoja tafadhali. Wapi huo waraka una mapungufu???? Tujadili hoja hii, tukimaliza utuletee ya kwako ya misamaha ya kodi!!!

Tiba
 
"Hata hivyo, Kanisa Katoliki kupitia Baraza lake la Maaskofu (TEC), limekuwa na utamaduni wa kutoa mwongozo kama huo wakati Taifa linapoelekea Uchaguzi Mkuu, huku kumbukumbu zikionyesha kuwa pia lilifanya hivyo mwaka 2005."

Heri wewe umeona uliona mwongozo wa mwaka 2005. Unajua watanzanzania ukitaka kuwaficha kitu waambie wasome. Hapa wameadi waraka wamepewa na sijui ni wangapi wameshausoma. Kelele zote hizi siajabu kuna wanaozipiga wakati hata kichwa cha habari hawajakisoma.

Binafsi natafuta waraka ule wa mwaka 1999 ambao ulikuwa mkali kupita huu. Niliusoma kwa kuuazima kwa jamaa nikamrudishia na sasa hayupo tena nchini.
Kwa kuwa Mdanganywa ametupa namba ya CPT nitawasiliana nao ili nipate waraka wa mwaka 1999 niwaletee hapa jamvini.

Halafu tutajadiliana hizi kelele za sasa mbon hazikupigwa mwaka 1999 yaani miaka 10 iliyopita.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom