Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Waraka: Kanisa Katoliki laandaa waumini uchaguzi 2010

Status
Not open for further replies.
Kusema kweli jamani ukishahudumia jamii ukazeeka sharti ustaafu na kupumzika na wajukuu.Kingunge anang'ang'ania Siasa kwa maslahi binafsi,naona laana ya J.K.Nyerere ya kukiuka maadili na kuwa fisadi inamnyemelea.Wakatoliki wanawaelimisha waumini wao umuhimu wa kupiga kura na kuchagua viongozi waadilifu sasa kinachomtatiza ni nini kama si wasiwasi wa kuchaguliwa watu makini anaohofu watamuuliza alivyojilimbikizia mali.Apige kelele tu lakini alama za nyakati zinaonyesha mafisadi hawatashinda vita dhidi yao bali watashindwa tuu.
 
Wakati mwingine nashindwa kuamini kwamba huyu ndiye Mzee Kingunge yule yule wa miaka ya 60, 70 na 80! Anatia aibu sana, kwa sisi tunaofahamu michango yake katika siasa ya Chama Kimoja na Ujamaa na Kujitegemea hatukutegemea kwamba atageuka kiasi hiki na kushutumu wale wanaojaribu kusaidia Taifa lirudie maadili yanayostahili.
 
Heri wewe umeona uliona mwongozo wa mwaka 2005. Unajua watanzanzania ukitaka kuwaficha kitu waambie wasome. Hapa wameadi waraka wamepewa na sijui ni wangapi wameshausoma. Kelele zote hizi siajabu kuna wanaozipiga wakati hata kichwa cha habari hawajakisoma.

Binafsi natafuta waraka ule wa mwaka 1999 ambao ulikuwa mkali kupita huu. Niliusoma kwa kuuazima kwa jamaa nikamrudishia na sasa hayupo tena nchini.
Kwa kuwa Mdanganywa ametupa namba ya CPT nitawasiliana nao ili nipate waraka wa mwaka 1999 niwaletee hapa jamvini.

Halafu tutajadiliana hizi kelele za sasa mbon hazikupigwa mwaka 1999 yaani miaka 10 iliyopita.

Kumbe kuna mwongozo wa 1999! Now what is the big deal? Mzee Kingunge aone aibu jamani. Nadhani yeye ndiye anayechochea mtafaruku nchini kwa misingi ya dini na si Kanisa Katoliki.
 
Sababu ya kuandikwa kwa waraka ni hali isiyoridhisha ya uongozi katika ngazi mbalimbali nchini. Huyu mzee naona kama si yule wa miaka ile ya ujamaa.Amebadilika na suala la ufisadi linaweza kuwa linamgusa moja kwa moja kwahiyo anatetea maslahi yake. Mi simpi uzito ule niliokuwa nampa miaka ya zamani.
 
bnhai,
Mie ni mtu mpinzani mkubwa sana wa hawa viongozi wa dini. Wengine wao ni wezi na mafisadi. Lakini si kweli kuwa wote ni wezi. Na hata ukija kwenye viongozi wa CCM, si kweli kwamba wote ni MAFISADI.

Viongozi wa dini huchaguliwa kwenye dini zao na wengine huenda shule na kuanza kufanya kazi kama kazi nyingine. Viongozi wa serikali/CCM ni viongozi waliochaguliwa na wananchi. Viongozi wa dini wanaishi kwa SADAKA na michango ya hiari ya waumini na viongozi wa serikali wanaishi kwa kutumia hela za KODI ambazo hukatwa kwa LAZIMA kwa wananchi wote bila kujali dini zao, rangi zao nk. Hapa ndiyo tofauti inapoanza. Sadaka ni hiari na KODI ni lazima.
Kama viongozi wa DINI wanatumia MISAMAHA ya kodi vibaya na kuFISADI kodi, basi ni wajibu wa SERIKALI kwa kutumia Usalama wa Taifa kuchunguza jinsi misamaha hiyo inavyotumika. Sidhani kama Viongozi wa dini watapinga pale serikali itakapoanza kufuatilia kama kweli vitu vilivyosamehewa kodi vinakwenda sehemu husika.

Sasa tunakuja kwa Wabunge. Wao hujipangia kila kitu wanavyotaka na hakuna wa kuwazuia. Wanasheria zao zinazowafanya wasiguswe hata wanapofanya makosa. Wao hukumu yao ni miaka 5 ijayo. Wana pesa na hivyo inakuwa rahisi unapofika uchaguzi, huhonga na kurudi madarakani. Wananchi vijijini hawayajui hayo. Hapo ndipo vyombo vya DINI huwa vinawajibu wa kuwafumbua watu macho. Masanja juzi katoa mfano wa viongozi wa dini waliochangia kubadili mambo kwenye ulingo wa siasa. South Africa kulikuwa na Desmon Tutu, Zimbabwe kulikuwa kuna Abel Muzorewa (kama sikosei), Poland kulikuwa kuna Pope John Paul II, Iran kuna akina Ayatollah nk nk. Hii ndiyo kazi ya viongozi wa dini pale mambo yanapokaa vibaya.

UFISADI Tanzania umefikia hali mbaya na ya kutisha. Kama watu wanaenda BoT na kuchota pesa na hakuna kinachotokea, kweli nchi imefika pabaya. Kama wewe hilo hulioni na unaona misamaha ya kodi ya wanayopewa watu wa dini ndiyo baya kwa sasa, basi nakupa big 5.
 
Tanzania haina dini lakini watanzania wana dini zao,dini ya Kingunge siifahamu sasa mpagani huyu asituharibie nchi yetu.Viongozi wa dini itisheni maombi mumuombee Kingunge aokoke ili asiishie vibaya uzeeni.
 
Ama kweli Tanzania ukitaka ubaya wako uanikwe basi wewe liseme vibaya kanisa katoliki.

Bila shaka kanisa hili linajiona linaweza kuongoza nchi kwa remote control. Kani kimbelembele kila pahala.

Issue ya KADHI wao wanatoa tamko
Issue ya OIC wao wanatoa tamko
uchaguzi 2010, wao wanatoa tamko(warka)
Kufuta misamaha a kodi kwa taasisi za dini na NGO ( wao tamko)

hakika wakatoliki tumewachoka toeni matamko yenu kanisani kwa waumini wenu na msichanganye dini na siasa.

BRAVO KINGUNGE. mengi watasema lakini ukweli unauma
 
Sasa tunasubiri tamko la katoliki toka kwa PENGO kwenda kwa KINGUNGE kama alilolitoa kwa MEMBE kwenye issue ya OIC.
 
Jamani tuwe makini kwa hili.kwnaza napenda kuwapongeza hawa viongozi wa katoliki kwa hii ilani, nimeisoma haina hata chembe ya udini. ina ujumbe unao elimisha raia yeyote wa tz.
Japokuwa kwenye dini huko nako wana mapungufu yao, lakini ni vyema hili wameliweka hadharani kuliko huko nyuma walipokuwa wakitoa ilani yao kimya kimya.
Vilevile ninachokijua ni kwamba tukipata viongozi waadilifu ni rahisi sana kufuatilia ufisadi unaofanyika hata ndani ya kanisa na misikiti na kadhaliaka, hivyo itakuwa rahisi hata kuwaangalia hawa wachunga kondoo wanatumiaje misaada wanayopata.
mie niionavyo hii ilani ni kitanzi kwa wote serikali/dini coz inaongelea uhadilifu.
Je? fisadi akiwa kanisani haruhusiwi kumtaja fisadi aliye serikalini? mwizi kamtaja mwizi mwezie kunanoma gani? ni faida kwa wananchi kujua nani ni mwizi.
Waraka umekaa vizuri je wakatoliki watauelimisha kwa dhati kabisa ili wananchi wauelewe au ndo maneno mengi ila output ni zero kama kawaida yetu? yangu macho na masikio.
 
Mimi naungana na Mh Kingunge kupinga WARAKA huo wa wawakatoliki. Tunafahamu wazi kuwa waraka huo una baraka zote za Pengo, baraza la maaskofu, balozi wa Vatican na hatimaye Papa.

sasa kama hilo baraza lina hamu ya kufanya hao basi wavue majoho yao na kuingia kugombea uongozi wa kisiasa kama alivyofanya Dr Slaa.

HONGERA SANA KINGUNGE

Tatizo sio waraka kuwa na baraka za akina Pengo, suala muhimu je kuna udini? Kiongozi wa dini asiyeipigania jamii anamofanyia kazi dhidi ya ufisadi, rushwa, uonevu, na unyanyasaji huyo ni mwoga na mnafiki! Wakatoliki hawajalazimishwa waraka uingizwe kwenye katiba au utumike serikalini, wao wametoa mwongozo kwa waumini na jamii kwa ujumla, sasa kiherehere cha nini?

Zama hizi tuna kundi la viongozi wababaishaji na wezi wa mchan kweupe, halafu unataka watu wasiseme? Kama serikali inakubali dini ni wadau katika sekta za afya na elimu vipi kuhusu demokrasia na haki? We have to think twice.
 
Binafsi nampongeza sana mzee Kigunge, ameonyesha ukomavu wa hali ya juu sana na uwezo wa kutumia mawazo ya Zamani. Kigunge anajua fika kuwa kwenye "Balance sheet ya CCM Asset"kubwa ni Ujinga uliotamalaki miongoni wa wananchi wa Tanzania walio wengi, Kwa maana hiyo Waraka wa kanisa katoliki ni hatari kwani unaweza kumega sehemu kubwa ya Asset ya CCM,na CCM ikaingia kwenye matatizo makubwa,Ukiangalia umri wake Ghafla itokee Tanzania bila CCM,mustakabari wake yeye utakuwa mashakani kwani anaishi kwa kuegemea mafisadi. Bravo mzee Kingunge Though it is very late,sorry for that mzee Kingunge
 
Jamani tuwe makini kwa hili.kwnaza napenda kuwapongeza hawa viongozi wa katoliki kwa hii ilani, nimeisoma haina hata chembe ya udini. ina ujumbe unao elimisha raia yeyote wa tz.
Japokuwa kwenye dini huko nako wana mapungufu yao, lakini ni vyema hili wameliweka hadharani kuliko huko nyuma walipokuwa wakitoa ilani yao kimya kimya.
Vilevile ninachokijua ni kwamba tukipata viongozi waadilifu ni rahisi sana kufuatilia ufisadi unaofanyika hata ndani ya kanisa na misikiti na kadhaliaka, hivyo itakuwa rahisi hata kuwaangalia hawa wachunga kondoo wanatumiaje misaada wanayopata.
mie niionavyo hii ilani ni kitanzi kwa wote serikali/dini coz inaongelea uhadilifu.
Je? fisadi akiwa kanisani haruhusiwi kumtaja fisadi aliye serikalini? mwizi kamtaja mwizi mwezie kunanoma gani? ni faida kwa wananchi kujua nani ni mwizi.
Waraka umekaa vizuri je wakatoliki watauelimisha kwa dhati kabisa ili wananchi wauelewe au ndo maneno mengi ila output ni zero kama kawaida yetu? yangu macho na masikio.

Mzee nakuomba uisome vizuri hii statement yako haijakaa sawa unaposema haina chembe ya dini tufafanulie zaidi na sio kusifia
 
Ama kweli Tanzania ukitaka ubaya wako uanikwe basi wewe liseme vibaya kanisa katoliki.

Bila shaka kanisa hili linajiona linaweza kuongoza nchi kwa remote control. Kani kimbelembele kila pahala.

Issue ya KADHI wao wanatoa tamko
Issue ya OIC wao wanatoa tamko
uchaguzi 2010, wao wanatoa tamko(warka)
Kufuta misamaha a kodi kwa taasisi za dini na NGO ( wao tamko)

hakika wakatoliki tumewachoka toeni matamko yenu kanisani kwa waumini wenu na msichanganye dini na siasa.

BRAVO KINGUNGE. mengi watasema lakini ukweli unauma

It's just inferiority complex here , why other religion or sect are not giving out their pronouncements ,they can give one , it's free piece of advice to the government , it's high time for churches and mosque to stand upfront to force government to do what is right to its citizen and should not allow to be used by few governments leaders to accomplish their mission!
 
"3) Uongozi wa Umma
- Uwazi zaidi katika michakato yote ya uteuzi katika huduma na ofisi za umma, Tume za umma na bodi za utawala.
Kufanya mapitio ya mamlaka ya Rais katika kuwateua mawaziri, idadi ya wizara, na pia uwezo na uhuru zaidi wa bodi za usimamizi wa mashirika ya huduma za umma."
Mlafi yeyote atakayesoma huu waraka lazima achemke.
 
labda yeye (Kingunge) unamgusa maana waraka wenyewe unaongelea kuchagua viongozi waadilifu na wasiotanguliza rushwa, ufisadi, etc. Hakuna sehemu hata moja ambako waraka huo unaongelea ni kiongozi wa dini gani achaguliwe. Kwa ufupi ule ujumbe unaweza kuwa mwomgozo kwa mtu yeyote yule awe mkristu, mwislam, mpagani, etc. Kiujumla ni kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi na watu wake.
Tunawahitaji wazee kama kingunge watupe busara zao lakini mimi naona apumzike siasa jamani kazeeka.
 
"3)Uongozi wa Umma
-Uwazi zaidi katika michakato yote ya uteuzi katika huduma na ofisi za umma, Tume za umma na bodi za utawala.
Kufanya mapitio ya mamlaka ya Rais katika kuwateua mawaziri, idadi ya wizara, na pia uwezo na uhuru zaidi wa bodi za usimamizi wa mashirika ya huduma za umma."
Mlafi yeyote atakayesoma huu waraka lazima achemke.

Kweli kabisa.... na hii kauli ni applicable kwa dini yoyote ile... hata devil worshipers!!! Na pia inarandana na rai ya watanzania wengi bila kujali dini wala rangi zao
 
watanzania waliochoka na ukandamizaji uliokithiri, let us take action instead of talking too much.
Uchaguzi unakaribia, everybody should play a part in educating our fellow Tanzanians on what is going on in this country.
Wakatoliki wenzetu they have played their part.
Lets work with them in one way or another.
Let us start to campign, encoureging people to vote for the right Leaders.
A good thing is that tuna mwongozo let us print this and distribute. Everybody should know "SIFA ZA UONGOZI BORA".

I am not saying chama kipi tupigie debe, bali ni kiongozi wa aina gani atatukomboa kutoka kwenye utumwa huu.
Ujumbe ni: 1. TAMBUA NA CHAGUA KIONGOZI BORA ANAYETUFAA
2. NENDA KAPIGE KURA.(CAUSE THAT ONE VOTE MATTERS).
IT'S NOT TOO EARLY TO START CAMPAIGNING.

Other people may critisize this message, GOD Bless you all to realize that no outsider will come to fight for our rights but us TANZANIANS.
STOP TALKING TOO MUCH LETS TAKE ACTION!!!!!!!
 
watanzania waliochoka na ukandamizaji uliokithiri, let us take action instead of talking too much.
Uchaguzi unakaribia, everybody should play a part in educating our fellow tanzanians on what is going on in this country.
Wakatoliki wenzetu they have played their part.
Lets work with them in one way or another.
Let us start to campign, encoureging people to vote for the right leaders.
A good thing is that tuna mwongozo let us print this and distribute. Everybody should know "sifa za uongozi bora".

I am not saying chama kipi tupigie debe, bali ni kiongozi wa aina gani atatukomboa kutoka kwenye utumwa huu.
Ujumbe ni: 1. Tambua na chagua kiongozi bora anayetufaa
2. Nenda kapige kura.(cause that one vote matters).
It's not too early to start campaigning.

Other people may critisize this message, god bless you all to realize that no outsider will come to fight for our rights but us tanzanians.
Stop talking too much lets take action!!!!!!!
you are truly a lady!!!!
 
Binafsi nampongeza sana mzee Kigunge, ameonyesha ukomavu wa hali ya juu sana na uwezo wa kutumia mawazo ya Zamani. Kigunge anajua fika kuwa kwenye "Balance sheet ya CCM Asset"kubwa ni Ujinga uliotamalaki miongoni wa wananchi wa Tanzania walio wengi, Kwa maana hiyo Waraka wa kanisa katoliki ni hatari kwani unaweza kumega sehemu kubwa ya Asset ya CCM,na CCM ikaingia kwenye matatizo makubwa,Ukiangalia umri wake Ghafla itokee Tanzania bila CCM,mustakabari wake yeye utakuwa mashakani kwani anaishi kwa kuegemea mafisadi. Bravo mzee Kingunge Though it is very late,sorry for that mzee Kingunge

Wapi? Kametumwa hako kusema aliyosema...hana IQ hiyo amejichokea.
Ndio wote hawa wanaongeza gharama kwenye serikali yetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom