Mkuu aliwahi kutolewa yule mbunge wa Kigamboni CCM, ingawa kwa kiasi kikubwa spika amekuwa na uonevu mkubwa sana kwa wabunge wa upinzani na wakati mwingine bila sababu yoyote ya msingi. Pia amekuwa mtu wa vijembe na mipasho visivyo na tijaSijawahi kuona mbunge wa ccm ametolewa nnje
Wala sijawahi kuona mbunge wa ccm akitukana n'a kuchukuliwa hatua bila shaka adhabu zote pâle bungeni ni kwa ajili y'a wapinzani tu
Kwa mtindo huu kuna haja gani kuhudhururia kwenye futari za majaliwa n'a spika ndugai au tulia Akson ?
Éden kimario
Huyu bora angebaki na kazi yake ya kuchunga nyumbu na nyemela huku kwenye siasa ni ofyo sana. Mnafik mkubwa...the enemy is always closer
Lazima tupigane ili kupunguza kura za ndio kila jambo,fikiria kura za ndio zilivyoruhusu madini yetu kuibiwa
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai ameonyesha kuumizwa na kitendo cha baadhi ya wabunge wa upinzani kutojumuika pamoja na wabunge wenzao katika masuala ya kijamii ikiwepo kususia futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
![]()
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai
Kufuatia jambo hilo Ndugai amewaomba viongozi na wabunge kwa pamoja kuachana na mambo ya kujitenda kwani yanaweza kuleta athari kubwa ambazo hakuna anayehitaji, na kudai kama kuna mambo ambayo yanakwaza basi viongozi hao wanapaswa kukaa pamoja na kumaliza mambo hayo.
"Tumekuwa tukiandaa baadhi ya hizi shughuli siku ile ya bajeti tulipata nafasi ya kupata futari iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu na wageni wote waliokuwepo, mabalozi tulihudhuria pale na ilikuwa imeandaliwa kwa wema kwa kweli. Leo (jana) pia na mimi nimepata nafasi ya kuandaa kama nilivyowataarifu lakini nikajifunza kitu kimoja ambacho sikupenda kukisema lakini ngoja nikiseme hapa kidogo, kuna baadhi yetu wengine wamekatazana rasmi kutohudhuria shughuli kama hizi, sasa mimi sitaki kuingilia uhuru wao, wana haki kufanya hivyo kama wanaona ni sawa lakini mimi mwenzao ningependa kuwashauri tu hasa viongozi wanaofanya mambo hayo kutazama tena njia zao, yako mambo mengine ni ya kijamii tu, ukifika mahali kiongozi unaanza kuwazuia watu hata mambo ya kijamii ujue unaenda mbali kidogo" alisema Ndugai
Spika wa Bunge aliendelea kutoa malalamiko yake dhidi ya vitendo vya baadhi ya wabunge wa upinzani kususia shughuli hizo za kijamii ambazo zinawaweka pamoja na kusema
"Hili bunge linavyoendeshwa labda wabunge wa kambi mbalimbali mnaweza msielewe bunge hili linaendeshwa katika mawasiliano mbalimbali ya sisi kwa sisi endapo kuna jambo linakwaza mpaka linasababisha hata watu wasipate futari kwa pamoja basi ni vizuri viongozi wa pande zote tukakaa tuzungumze na kuondoa vikwazo hivyo kama vipo maana mimi sijui kama vipo lakini kama havipo ni vizuri tuwe tunajumuika kwa pamoja, maana sera hizo zikienea na hakika kabisa na pande zingine nazo zitaanza na hakika matokeo yake italeta mipasuko ambayo hakuna anayehitaji hapa" alisisitiza Job Ndugai
Ndugai alisema kuwa yeye anatambua kuwa wanamjibu na kufanya wanayoyafanya lakini Mungu anajua kuwa wanachokifanya si busara kwa kufanya hivyo na kusema kuwa katika mwezi huu mtukufu wanapaswa kusameheana, kuombeana, kutoa mikono upande wa pili na kufanya ibada kwani si mwezi wa chuki na kubaguana.
Source: EATV
Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
Nafutari ale mwenyewe. [emoji23] [emoji23]Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
Hahahhhaaa...umenikumbusha kipindi najifunza methali kwa kingereza....."that eats you is in your clothes"....
Hizi propaganda mfu zilishapitwa na wakatiChadema wanachukia sana uislam si shangai Mbowe na Lissu kuwashauri wasihudhurie futari...lengo lao ni kuendeleza chuki dhidi ya Uislam
wewe jitathimini sio kila kitu unashabikia. Ukweli uonaonekana kabisa black n white.Spika Ndugai alipokuwa yuko nje akitibiwa na nafasi kuchukuliwa na naibu wake yule Mhe. dada yetu wengi (wapinzani) walimlilia apone haraka na kurejea kwenye kiti chake...sasa wapinzani hao hao wanamuona hafai...Spika Ndugai anafuata sheria,kanuni na miongozo ya Bunge....Mbunge akimshika nguo yule 'askari' wa bunge ni lazima ashughulikiwe tu...Bungeni siyo mahalin pa mchezo mchezo
wewe jitathimini sio kila kitu unashabikia. Ukweli uonaonekana kabisa black n white. I AM SURROUNDED BY IDIOTS kwa sauti ya ........ the lion ...............
Mkiti Mussa Zungu angelikuwa ndiyo spika, bunge lingeendeshwa kwa uweledi mkubwa sana!! Jamaa namkubali sana kwa busara zake. Pamoja na mapungufu yake kipindi cha kura, but he is far better!!Source ya yote haya ni wewe Spika Job Ndugai mwenyewe..
Wewe ndio unaeleta huu mgawanyiko bungeni na mpaka wabunge wa upande mwingine wameamua kuwa wapinzani kwelikweli..
Acha kulia lia..
Be fair kwa wote.
Am sure (kwa mfano) kama Mkiti Mussa Zungu angekuwa ameandaa futari na kuwakaribisha wabunge, wote wangeudhuria..!!
So Ndugai angalia nyendo na matendo yako kwa wapinzani na hasa Chadema then jiulize why??
Hayo Maji wala chochote wasiguse wala kushirikiana na SHETANI Mwana mlaaniwa.Mi nashauri Bungeni kuwepo na kamati ya kuwahudumia wapinzani maji na makabrasha mengineyo. Wahudumu wawe wapinzani. Hali ishachafuka.