Rais Samia mrudishe Balozi Polepole kutumika ndani ya nchi bado anahitajika

Ngungenge

JF-Expert Member
Jun 11, 2016
2,863
3,192
Nakushukuru sana Rais kwa kuwa unasoma na kufuatulia mambo yote yanayoendelea nchini na Mimi Ngungenge nimebahatika kuandika maoni machache ambayo ama wewe binafsi au wasaidizi wako walisoma na kuchukua ushauri huo mathalani katika kujenga nchi na chama chetu cha CCM. Niliandika kukuomba;

1. Husein Bashe awe Waziri kamili badala ya Naibu Waziri

2. Nehemia Mchechu arudishwe serikalini kwa kuwautendaji wake utakuwa na manufaa

3. Maoni kadhaa kuhusu uwezo wa Albert Chalamila

Nakushukuru sana na yote kati ya hayo uliyapitisha na wote niliowataja wanafanya vizuri yaani wanajitahidi kuwajibika katika majukumu yao.

Kipekee naomba utambue kuwa nimewahi kuandika makala ya kumpinga, kumuonya na kumshauri kijana wako Humfrey Polepole humu jamvini katika mambo ambayo hayakwenda sawa au aliteleza kwa vile mimi Ngungenge ni black and white huwa silembi mtu anapopotoka au kukengeuka.

Niliwahi muonya, kumkanya na kumpinga Polepole katika kile kinaitwa darasa huru na ile tabia yake ya kuropoka ovyo. Nilifanya hivyo kwa lengo la kumsaidia ili awe mtu bora siku zijazo.

Imechukua miezi kadhaa kwa Polepole kuelewa nini nilikua namshauri na sasa amekuwa mtu safi.

Kimsingi wewe Rais umesaidia kumlea na kumkuza Polepole ili awe mtu bora mwenye diversity ya kuishi katika falsafa mbalimbali.

Licha ya kuwa Polepole alihisi mimi ni adui yake kwa vile tuu sipendi ego yake ya personnal attack ambayo nakiri kuwa sasa ameacha na kuwa mtu wa fact kuliko personality, napenda kuchukua nafasi hii kwa unyenyekevu mkubwa kukuomba umrudishe Balozi Polepole nchini ili akutumikie katika nafasi mbalimbali za Chama au Wizarani Tamisemi na badala yake nafasi yake ya ubalozi apewe mtu mwingine.

Jambo hili litasaidia kuongeza matokeo makubwa ya kiutendaji na kiuenezi wa kazi zako na serikali yako

Naomba utambue kuwa unahitaji watu kama Polepole wawepo katika serikali yako, watu wa maneno na vitendo angalia Albert Chalamila anavyopiga kazi, vipi kama Tamisemi akiwepo Polepole si utaona matokeo maradufu. Polepole anaweza kusimamia, kudhibiti rushwa, kueneza yanayofanywa, kukagua na kukusemea vizuri

Nakuomba sana Rais mrudishe huyu kijana nchini atusaidie, akiwa Cuba ameonesha mabadiliko makubwa. Kwa sasa, bado ni viongozi wachache tuu wanakusemea na kueleweka kwa wananchi. Wengi wanakusemea ama hawaeleweki, ama hawakubariki, ama hawaaminiki. Sasa fanya usajiri huo kwa faida ya serikali yako, chama cheque CCM na nchi yetu kwa ujumla

SAMIA 2025-2030
 
Watanzania akili hakuna ila mnajifanya wajuaji Sana, huyu poleople lini alifukuzwa chamani? Lini alinyang'anywa kadi ya uanachama?

Huyu ni balozi cheo cha ngazi ya juu kwenye wizara ya mambo ya nje, anamuwakilisha rais Cuba wewe unataka arejeshwe kwenye serkali ipi?

USSR
 
Kama unampenda sana Polepole nenda kanywe nae chai, alivyokuwa Mwanaharakati alifanya vizuri, akafika bei akahama Bahari Beach na kwenda Upepo unapovuma, akanunua mabajaji ya biashara kwa fedha za hongo.

Mtu kama huyo hafai kuwa kiongozi wa umma maana anaweza kuuza nchi.
 
Mr slow slow still ni mbogamboga crew, but tangu atuletee calculation za Cambodia kuhusu ile 1.5trl cna hamu nae!!
 
Wapo wengi wenye uwezo mkubwa mno kuliko Polepole. Polepole ameingia chamani baada mapambano makali kuisha mtu huyo hawezi kuwa Bora Zaidi ya waliopambana kufa na kupona.
 
KIla mtu ana nafasi yake
Kupambania chama sio mwisho wa chama bado kuna ukiaji na maendelea
Wapo wengi wenye uwezo mkubwa mno kuliko Polepole. Polepole ameingia chamani baada mapambano makali kuisha mtu huyo hawezi kuwa Bora Zaidi ya waliopambana kufa na kupona.
 
Nakushukuru sana Rais kwa kuwa unasoma na kufuatulia mambo yote yanayoendelea nchini na Mimi Ngungenge nimebahatika kuandika maoni machache ambayo ama wewe binafsi au wasaidizi wako walisoma na kuchukua ushauri huo mathalani katika kujenga nchi na chama chetu cha CCM. Niliandika kukuomba;

1. Husein Bashe awe Waziri kamili badala ya Naibu Waziri

2. Nehemia Mchechu arudishwe serikalini kwa kuwautendaji wake utakuwa na manufaa

3. Maoni kadhaa kuhusu uwezo wa Albert Chalamila

Nakushukuru sana na yote kati ya hayo uliyapitisha na wote niliowataja wanafanya vizuri yaani wanajitahidi kuwajibika katika majukumu yao.

Kipekee naomba utambue kuwa nimewahi kuandika makala ya kumpinga, kumuonya na kumshauri kijana wako Humfrey Polepole humu jamvini katika mambo ambayo hayakwenda sawa au aliteleza kwa vile mimi Ngungenge ni black and white huwa silembi mtu anapopotoka au kukengeuka.

Niliwahi muonya, kumkanya na kumpinga Polepole katika kile kinaitwa darasa huru na ile tabia yake ya kuropoka ovyo. Nilifanya hivyo kwa lengo la kumsaidia ili awe mtu bora siku zijazo.

Imechukua miezi kadhaa kwa Polepole kuelewa nini nilikua namshauri na sasa amekuwa mtu safi.

Kimsingi wewe Rais umesaidia kumlea na kumkuza Polepole ili awe mtu bora mwenye diversity ya kuishi katika falsafa mbalimbali.

Licha ya kuwa Polepole alihisi mimi ni adui yake kwa vile tuu sipendi ego yake ya personnal attack ambayo nakiri kuwa sasa ameacha na kuwa mtu wa fact kuliko personality, napenda kuchukua nafasi hii kwa unyenyekevu mkubwa kukuomba umrudishe Balozi Polepole nchini ili akutumikie katika nafasi mbalimbali za Chama au Wizarani Tamisemi na badala yake nafasi yake ya ubalozi apewe mtu mwingine.

Jambo hili litasaidia kuongeza matokeo makubwa ya kiutendaji na kiuenezi wa kazi zako na serikali yako

Naomba utambue kuwa unahitaji watu kama Polepole wawepo katika serikali yako, watu wa maneno na vitendo angalia Albert Chalamila anavyopiga kazi, vipi kama Tamisemi akiwepo Polepole si utaona matokeo maradufu. Polepole anaweza kusimamia, kudhibiti rushwa, kueneza yanayofanywa, kukagua na kukusemea vizuri

Nakuomba sana Rais mrudishe huyu kijana nchini atusaidie, akiwa Cuba ameonesha mabadiliko makubwa. Kwa sasa, bado ni viongozi wachache tuu wanakusemea na kueleweka kwa wananchi. Wengi wanakusemea ama hawaeleweki, ama hawakubariki, ama hawaaminiki. Sasa fanya usajiri huo kwa faida ya serikali yako, chama cheque CCM na nchi yetu kwa ujumla

SAMIA 2025-2030

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti 2020-2030😂🤣😭😭😭 ...urais wa mkopo ndo aende hadi huko? Labda kama atakuwa rais wa uarabuni
 
Back
Top Bottom