Wapinzani na Gen Z wa Tanzania wanataka wasiadhibiwe wanapodhalilisha CCM, jambo ambalo CCM wamelikataa na kupelekea Wapinzani kulalamika kila mara

Wapinzani na Gen Z wa Tanzania wanataka wasiadhibiwe wanapodhalilisha CCM, jambo ambalo CCM wamelikataa na kupelekea Wapinzani kulalamika kila mara

Pakome

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2024
Posts
1,541
Reaction score
916
Wapinzani na Gen Z wa Tanzania wanataka wasiadhibiwe wanapodhalilisha Chama Cha Mapinduzi CCM, jambo ambalo CCM wamelikataa na kupelekea Wapinzani kulalamika kila wanapoadhibiwa

Nimefuatilia historia ya CCM ya zaidi ya miaka thelathini iliyopita

Niligundua jambo moja kubwa sana

Tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa uanzishwe July 1, 1992 Chama Cha Mapinduzi CCM kimekuwa mhanga wa kudhalilishwa na Wapinzani

Wanachama wa CCM na viongozi wao wamekuwa wakitukanwa matusi ya nguoni na kashfa chafu ikiwemo

Wezi
Mafisadi
Wadhalimu
Matapeli

Pamoja na kwamba Chama Cha Mapinduzi CCM kilifanya kazi kubwa sana ya kuleta Uhuru wa Tanganyika December 9th, 1961 pasipokumwaga damu kilipokuwa kikiitwa Tanganika African National Union ( TANU ) kikiongozwa na Mwl Julius Kambarage Nyerere

Kashfa ambazo hazina ushahidi wa Kisheria

Vyama vya Upinzani vimekuwa vikijiweka kundi la Malaika na Watakatifu hawapendi kukosoana wenyewe kwa wenyewe na huwa hawataki kukosolewa na CCM kwasababu wao ni Watakatifu pamoja na kwamba tumeshuhudia jinsi walivyofilisi vyama vyao wenyewe kwa kashfa zile zile wanazotuhumu CCM kila mara ikiwemo Ufisadi uliopelekea kuanguka kwa vyama vingi vya upinzani na hata vingine kufutika kwenye dunia ya siasa

Katika historia ya CCM tangu 1992 viongozi wao hawapendi kutusi viongozi wa upinzani hadharani lakini wapo viongozi wa Upinzani wanaotusi CCM hadharani matusi mengine machafu yasiyofaa hata kutamkwa ( Sijaambatanisha ushahidi kwasababu matusi yanadhalilisha utu )

CCM imekuwa ikivumilia sana udhalilishaji huu kwa zaidi ya miaka 30 na kadiri wanavyozidi kuvumilia ndivyo tabia hii inazidi kushamiri

Sikuwahi kuona CCM ikisifiwa na Wapinzani kwenye utekelezaji wa sera zake sana sana itaambulia matusi

Hayati John Pombe Magufuli pamoja na kutekeleza sera za Chama Cha Mapinduzi ikiwemo kununua ndege bado Wapinzani kupitia Tundu Lissu walikosoa manunuzi ya ndege na kumdhalilisha hadharani kuwa alifanya maamuzi mabaya pamoja na kashfa nyingine chafu za Udikteta

Jambo la kustaajabisha ndege zile zile ndizo zimerudisha heshima ya Taifa na hata Wapinzani wamekuwa wakipanda kwa mara kwa mara

Je, Watanzania wanataka kuongozwa na Malaika?? Kwasababu kila raisi wa CCM hawamtaki na hawataki CCM ikosoe viongozi wao, watu wenye antisocial personality ( psychopathy )

Ugomvi wa kisiasa wa Tanzania umesababishwa na CCM kukataa kudhalilishwa na kuamua kujibu mashambulizi makali

Endapo CCM wangekubali kudhalilishwa pasipokuchukua hatua kali basi tusingeona mgogoro wa kisiasa kwasababu upande wa CCM usingekuwa ukijibu mashambulizi yanayolalamikiwa kuwa yanaitesa nchi

Baada ya CCM kujibu mashambulizi makali sana Wapinzani wakaanza kulalamika na kupaza sauti zao wakidai kuwa wanateswa na kuonewa na CCM

Wanachokitaka wapinzani pamoja na Gen Z ni kuwa hata kama wataidhalilisha CCM na Serikali yake kwa kiwango chochote kile basi wasiadhibiwe jambo ambalo CCM wamekataa na kupelekea mgogoro mkali wa kisiasa usiokwisha

Tabia chafu kama hizi zinawezakupelekea Serikali kukata tamaa ya kuleta maendeleo kwasababu ya kuamini kuwa hata ifanye jema lipi itaishia kulipwa matusi machafu
 
Kuna TWAHA MWAIPAJA , mashine ina matusi ile , sijui ni binti wa kizaramo 🙂
 
Back
Top Bottom