Wapinzani, mkipewa uteuzi kataeni

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,143
2,000
Baada ya hii hujuma ya uchaguzi na ili kuhadaa Ulimwengu na hasa nchi wafadhili, mnaweza kupewa uteuzi lengo likiwa ni kuonyesha kuwa demokrasia ya vyama vingi inaheshimiwa na inapewa nafasi katika utawala huu.

Nachowashauri, ikitokea mmoja wenu au baadhi yenu wamepewa uteuzi wa kuingia Mjengoni au kwingineko, kataeni hizo nafasi kwani itakuwa ni kubariki huu uharamia uliofanywa dhidi yenu na zaidi itakuwa ni kutekeleza kila kinachoitwa divide and rule.

Msikubali hata kidogo.
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,313
2,000
Kwakua uchaguzi umekwisha, na wingi wameshindwa basi sidhani kama wapo watakao kataa teuzi.

Mkuu, wapinzani pia ni watu na wanafamilia zinazo waregemea. Istoshe tu kwamba siasa sio ugomvi na haijawahi tokea adui wa kudumu kwenye siasa.

Na kwakua hili ni swala mtambuka, basi ebu ngoja tuone.
 

Per Diem

JF-Expert Member
Mar 28, 2018
596
1,000
Kamanda Lissu katoa tamko tuingie barabarani, vipi upo wapi nikupitie?
Baada ya hii hujuma ya uchaguzi na ili kuhadaa Ulimwengu na hasa nchi wafadhili, mnaweza kupewa uteuzi lengo likiwa ni kuonyesha kuwa demokrasia ya vyama vingi inaheshimiwa na kupewa nafasi katika utawala huu...
 

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,612
2,000
Nafikiri M.Seif anaweza kupewa king‘ora, na hatokaa wala kukumbuka, ...
 

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,313
2,000
Linapokuja swala la utashi wa mtu mmoja mmoja, familia ni shwala mtambuka zaidi ya siasa.
Hivyo basi, sidhani kama patatokea mpinzani atakae kataa uteuzi wakati hajaweza kudhibiti njaa ndani kwake.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,495
2,000
29,188,347 ndiyo idadi ya wapiga kura ktk daftari kwa uchaguzi wa Tanzania 2020.

Idadi ya waTanzania walioenda kupiga kura kufuatana na matokeo anayotangaza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi toka majimbo machache matokeo yake yaliyosomwa inaonesha ni asilimia ndogo wamejitokeza yaani kiasi cha asilimia 50 ndiyo wamekwenda kupiga kura.

Hamasa ilikuwa kubwa pande za wanaolinda kubaki madarakani kwa miaka mitano mingine na wakati pia hamasa ilikuwa kubwa kwa wale waliotaka kuingia mitano mwanzo kama serikali Mpya kupitia upinzani.

Nini kimepelekea waliojitokeza kuwa 50% ya wapiga kura 29,188,347 huku wengine hawakwenda kupiga kura ? Wapiga kura zaidi milioni 10 kutopiga kura hii inaashiria nini?
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,911
2,000
Hila zako za kutugawa watanzania hazitafanikiwa kamwe! Uchaguzi umepita ni muda wa kufikiria kuijenga Tanzania imara sasa.
 

signale

Member
Sep 17, 2020
22
75
Wakatae wakati waliunga juhudi kwa Kasi vile last time? Actually kuunga juhudi imechangia sana matokeo ya uchaguzi huu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom