Wapinzani hawana sifa za Kuongoza nchi. (comparison analysis)

Baada ya kukupa jina hilo sasa kwa ufupi sana naomba nigusie huu ujinga wako uliosema:

  1. Wapinzani ni Watanzania kama Watanzania wengine walioko kwenye chama chako cha Mafisadi-CCM.Hivo wana HAKI ya kikatiba kuongoza nchi saa yoyote kama Watanzania watawapa ridhaa hiyo kwa kupitia UCHAGUZI ULIO HURU NA WA HAKI. Kumbuka: Tangu Tanzania iingie kwenye mfumo wa vyama vingi hakuna mwaka wowote ambao nchi imefanya Uchaguzi ulio huru na Haki! Hili ni jambo liko wazi na halina ubishi.
  2. Hueleweki unaposema KATIBA IKO WAZI KUWA SERA KUU ni SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA! Hivi kwa akili yako bado unafikiri nchi hii inaendeshwa kwa sera ya Ujamaa na Kujitegemea kweli???Naona unaota ndoto za Alinacha za mchana kweupe. Hebu waulize hao vizee wako kina Kingunge Ngombare kama kuna kitu kama SIsa ya Ujamaa na Kujitegemea!! Baba wa Taifa hili kabla hajaondoka aliwahi kuhoji mbele ya hao vibabu wa CCM kwamba kwanini WALIAMUA KULIZIKA AZIMIO LA ARUSHA KULE ZANZIBAR na kuamua KUKUMBATIA SIASA ZA KIBEPARI NA UTANDAWIZI? Sina hakika ulikuwa wapi kipindi lakini nafikiri ulikuwa shule. Mwalimu alisema kuwa kwa wakti huo kuongelea habari za AZIMIO LA ARUSHA ilikuwa ni kama kuonekana ''mwendawazimu''!!!Kwa hiyo usitake kupotosha watu hapa kila Mtz anajua Azimio la Arusha lilishazikwa ZANZIBAR hata kabla Baba wa Taifa kuiaga dunia.
  3. Unaposema kuwa CCM wanajipambanua kwa ITIKADI na SERA na kuwa Wapinzani hawana Itikadi wala Sera ni kutaka kuwatukana Watanzania walioko kwenye vyama vingine tafauti na CCM yako. Haya ni mawazo MFU na ya kipuuzi kwa kufikiri kuwa vyama vingine vyote havina sera wala itikadi. Hivi vyama vimesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa na vina Katiba zake ambazo zimeweka wazi ITIKADI na SERA zake ambazo zinakubalika kisheria ndani ya nchi hii na kila chama huelimisha na kutangaza sera zake wakti wa Chaguzi mbalimbali na kwenye majukwaa ya siasa. Pengine nikukumbushe tu kwamba kuna SERA ambazo CCM wamekuwa wakiziiga toka upinzani kwa vile wanaona zinafaa na wanazikubali. CHADEMA ilishaweka msimamo katika sera zake kwamba ELIMU BURE inawezekana katika nchi hii na vilevile VIFAA vya ujenzi kama Saruji na Mabati zinaweza kuuzwa kwa bei nafuu ili kuwawezesha Watanzania kuwa na nyumba bora. Tumeona CCM wakizifanyia kazi sera kama hizi kwa mlango wa nyuma! Naamini hili unalijua.
  4. Katika porojo au propaganda zako umesema kuwa Tanzania imekosa UPINZANI MAKINI. Hii si kweli hata kidogo. Pengine nikukumbushe tu kwamba kwa sasa wewe upo Dodoma kwenye Bunge Maalumu la Katiba Mpya. Hapa sitaki ubishi wa kitoto na wa kijinga. Ukweli utabaki palepale kwamba WAZO LA KATIBA MPYA LIMETOKANA NA ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO-CHADEMA mwaka 2010. Mwenyekiti wako Kiwete alifanya kudandia HOJA hii kwa vile haikuwahi wala haijawahi kuwa kwenye SERA,ITIKADI wala ILANI ya Uchaguzi ya CCM!! Sasa kama KATIBA MPYA imetokana na MAWAZO YA WAPINZANI, hivi kwa akili yako nani anayefaaa kuongoza nchi hii, ni CCM au UPINZANI?????
  5. Mwisho ni hili la kulinganisha kati ya KUB(Kambi ya Upinzani Bungeni) kwa maana ya BARAZA LA MAWAZIRI wa serikali ya CCM na BARAZA KIVULI LA KUB. Kwa Watanzania wenye kupenda ukweli na uwazi Bunge la JMT siku hizi linachangamushwa na HOJA motomoto toka kwa Mawaziri Vivuli wa CHADEMA. Huu ni ukweli ulio wazi kabisa na hakuna sababu ya kubishana. Laiti kama kungelikuwa na sheria ya kuruhusu Mawaziri vivuli wa KUB kupewa nafasi ya kukalia hizo ofisi za Wizara husika japo hata kwa robo tu ya kipindi cha miaka 5 ya serikali inayokuwa madarakani, basi watu wangelishuhudia mabadiliko ya ajabu sana. Lakini kwa vile nchi hii imelaaniwa kutokana na sera mbovu za CCM, kila kitu hata kama ni kizuri kutoka upinzani kitakataliwa tu!!!

Kwa hoja zangu hizo 5 naamini utakubaliana nami kuwa yote uliyoongea ni pumba na upuuzi mtupu. Kumbuka Tanzania ni yetu sote na hakuna mwenye HATI MILIKI ya kutawala nchi hii milele. Lazima kuna siku CCM itaondoka madarakani,sijui imebakia miaka mingapi hata hivo dalili zote zinaonyesha huo mwisho wa CCM umekaribia sana kuliko vile wana CCM wanavyodhani. Watz tunajua kuna mikakati,mbinu tena chafu zinazofanywa na CCM usiku na mchana kuhakikisha kwamba uoinzani haupati nafasi ya kuongoza nchi hii. Huu ni udikteta wa kihuni tu lakini mwisho wake umekaribia.

Watz tunaaamini kama Bunge hili la Katiba litakuwa makini na likakubali kupitisha RASIMU-2 ya Katiba Mpya ya Tanzania kulingana na Matakwa, Maoni na Mawazo ya Watanzania walio wengi basi tutarajie mabadiliko makubwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015. Kama Katiba sasa itakubali kuwa na TUME HURU YA UCHAGUZI ambayo haihitaji kuripoti kwa Mwenyekiti wa CCM NA kwamba Mwenyekiti wa Tume na Mkurugenzi wake wanateuliwa na chombo kisichokuwa chini ya Rais na hawawajibiki kwake, basi UCHAGUZI utakuwa HURU na HAKI na CCM hawataweza kuitumia Tume ya Uchaguzi kuchakachua matokeo ya Urais na Ubunge ili waendelee kukaa madarakani! That moment is coming my friend Paul Muk*nd*!!

Sijui utakimbilia wapi ewe usiye na haya pale utakaposikia Rais akiapishwa toka chama kingine kabisa tafauti na CCM yako! Wazungu wanasema, ''Always THINK POSITIVE and ACCEPT CHANGES! If you resist Changes, the Changes will automatically change you by force''.
Ndugu umeandika mengi sana lakin kwa bahati mbaya umeandika vitu visvyo na msingi na pengine vilivyo nje ya thread ambayo mleta mada ameianzisha. labda nikusaidie kwa ushauri wa bure.,jitahidi kabla haujacomment sehemu hakikisha umesoma na kuelewa vizuri hiko ambacho unataka kukijadili na kuchangia. kazi njema.
 
tetetetetetetetetetetetete.........HAKA KAJAMAA BWANA, YAANI KUMSEMA LOWASA VIBAYA NA KUUNGWA MKONO NA BAADHI YA WAZEE WA CCM SASA KAMEANZA KULEWA SIFA,tetetetetetetetetete.......kwiikwiii. KANAJIONA KANAJUA SANA.
Acha kumjadili mtu, jadilini hoja yake ya udhaifu wa upinzani na uimara wa CCM.,sio kuishia aka kajamaa kanajiona bora na kamelewa sifa.
 
Sasa umeshasema upinzani hauna uwezo wala mipango ya kuongoza nchi. Halafu unamalizia na "ACT mpango mzima". Sasa ACT sio wapinzani?
Watu wengine sijui walienda shule kufanya nini!!!

mkuu Tuko umeelewa vizuri sana namaanisha nini, labda kama mwenzetu ni 'wale' wa kutafsiri neno kwa neno ningeandika ''upinzani uliopo''

kuhusu shule sijaenda mkuu, usinipe sifa, ulichosema ndio sahihi kabisa
 
Najiuliza maswali mengi lakini moja kubwa ambalo linasumbua kichwa changu ni swali kuwa thread kama hizi zinasomwa na vijana na makamanda hewa wa chadema.

kila nikisoma kwa kutuliza kichwa naiona hekima kubwa ya kiongozi wangu Makonda na naona kupotea kwa waziwazi kwa vijana wa chadema.
 
Najiuliza maswali mengi lakini moja kubwa ambalo linasumbua kichwa changu ni swali kuwa thread kama hizi zinasomwa na vijana na makamanda hewa wa chadema.

kila nikisoma kwa kutuliza kichwa naiona hekima kubwa ya kiongozi wangu Makonda na naona kupotea kwa waziwazi kwa vijana wa chadema.

Juliana Shonza, nimekufundisha hapo UDSM. Hebu soma hiyo tittle ya uzi huu mara mbili imekaa sawa? Comparison analysis ndio nini? Na nMODS wameacha makusudi makosa ili Kummumbua kijana makonda. Shonza na digrii yako umeshindwa umeshindwa kumsahihisha huyo bosi wako haraka kabla utupu wake haujaonekana?
Uniashia tu kumsifia? Inaonekana nyie walamba viatu mmeambiwa viongozi wenu wakiongea lazima muwasapoti la sivyo hakuna posho. Maana hakuna ulichochangia zaidi ya kumsifu huyo makonda wako. Halafu we mwananmke sijui km utakuja kuolewa tena! Ushajiloga tayari.
 
Kama viongozi wenyewe ni wa KALIBA ya kwako basi CCM haina viongozi.

Ukiangalia kwa umakini hujui hata Chama Chako kinafuata itikadi gani,kwa UJAMAA hamko mlishatoka huko na ndiyo sababu mliua Azimio la Arusha ,makazalisha Azimio la Zanzibar yaani Azimio la kuchukua chako Mapema,hivyo kwa usahihi kabisa hujui hata unaloongea.

Kwa Lema anaweza kuwa mbadala wa Chikawe ndiyo sababu Chikawe aliweza kufanya kazi naye vizuri sana na SIASA za CHIKAWE huziwezi hata siku moja.

Chikawe anajua nini maana ya vyama vya vingi vya siasa,anaelewa umuhimu wa vyama vya siasa kwa TAIFA lake.Chikawe aliweka TAIFA mbele chama baadaye na katika uongozi wake tuliona Polisi wakiwaheshimu na kufanya kazi na Wapinzani bila ugomvi japo ulikuwepo kwa kiasi kidogo.

Leo Itikadi na sera ya CCM ni chuki,visasi na ubaguzi ukiongezea na wizi wa raslimali za TAIFA.

Hivyo in short hakuna mwanaCCM ambaye anafaa kuwa kiongozi sababu wote ni wale wale wezi wa RASLIMALI zetu.

Hebu jiulize kwanini mnakimbizana na wapinzani kila kukicha??Kwanini hamtaki kukosolewa??Kwanini hamuukubali ukweli?

Jibu lake ni sababu mko busy kutafuta ulaji na kujilimbikizia mali.As for you huna hata moral authority ya kumkosoa Mpinzani awae yote.Hebu jichunguze kuanzia ngazi ya shule hadi hivi leo.

Tuhuma zote za kupewa mali na GSM hujazitolea maelezo,je unayo moral authority ya kusema upinzani??Haya vyeti vyako je??

Mdogo wangu angalia kabla hujaanza kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako anza kutoa Boriti kwanye jicho lao.

Usidhani watanzania ni wapumbavu,jua tunaakili sana kuwaangalia si kwamba tunaukubali upuuzi mnaoufanya
 
Ni kosa kubwa sana kuifananisha kampuni ya wachaga na ccm. Hawa ungepaswa uwafananishe na kampuni kama mohamed enterprises, au ipp ya mengi au TANAPA sio mbaya

Nadhani umepotea njia,hicho chama cha majangili nacho unakiita ni chama kweli??Na siku hizi nasikia mnaitwa Chama Cha Masogange
 
falsafa ya ccm ni ipi...?

itikadi ya ccm ni ujamaa na kujitegemea kama ulivyosema, nataka nikuulize unatumia microscpe ya aina gani kuoana hyo itikadi, na mm nitafute hyo microscope niweze kuona?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom