Wapinzani hawana sifa za Kuongoza nchi. (comparison analysis)

PM,

Hebu fikiria CCM hii ya Jakaya, Mgeja, Mwigulu, Makamba, Makonda, Nape, Mangula, Lowasa, Wassira, Sitta, AshaRose, Meghji, Vuai, Ngeleja,..., etc.,

Bila upinzani wa akina Mbowe, Dr Slaa, Mnyika, Zitto, Msigwa, Mtikila, Lipumba, Mtatiro, Mbatia, Mrema, JamiiForums, ...,etc.

TANZANIA hii ingekuwaje leo

kesho utasikia na yeye anataka kugombea urais
 
Ukitaka kujua chadema haina watu tizama wachangiaji wake mtandaoni wengi hawana hoja za maana zaidi ya matusi ukienda bungeni ndio uozo kabisaa
 
Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayo- base katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika thread hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na ITIKADI na SERA, wamejikita katika kufanya siasa za matukio na UBISHANI. Siasa isiyo endelevu kwani matukio hukoma kwa wakati fulani, hivyo kwa wananchi walio makini hawawezi kuamini katika Chama ambacho chenyewe hakina kitu ama falsafa inayoiamini. Wananchi wanahitaji viongozi wenye falsafa wanayoiamini.

Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.

Maana ya kuwa na Vyama vya upinzani ni kutaka kuwapa wananchi alternative ya Uongozi na falsafa. sio KAZI ya upinzani kupinga kila kitu na sio kazi ya upinzani kusifia serikali, kimsingi kazi ya upinzani ni kutoa the best alternative solution to justify that opposition is the best alternative government in waiting. Lazima upinzani ujijenge kisera, kifalsafa na kiitikadi ambayo wananchi wataona kuwa ni njia ya kufikia Maendeleo na kuwajengea matumaini ya Mafanikio na Maisha Bora (kwani ndio paramount demand ya wananchi - MAISHA BORA)

Na nasema kama Upinzani ungekuwa makini basi Serikali na Chama Kilicho Madarakani nikimaanisha Chama Changu CCM kingekuwa makini zaidi, MWALIMU Nyerere aliwahi kusema maneno ambayo mpaka leo yamewekwa kwenye bango mbele ya Ukumbi wa Mikutano ya NEC (maarufu kama whitehouse) pale Makao makuu dodoma, maneno yale yanasema " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, na Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM "

TANZANIA imekosa UPINZANI MAKINI, upinzani unaojitambua nini unataka na wafanye nini kufikia hicho wanachokitaka. Wachambuzi wa siasa wanapoangalia uimara wa upinzani moja ya kigezo ni kutathimini uwezo wa mawaziri (Viongozi) na watendaji wa Chama tawala na Serikalini yake ukilinganisha na mawaziri Vivuli,na viongozi wa Upinzani. Inatakiwa Shadow Cabinet ioneshe uwezo na matumaini kuliko cabinet. Upinzani uoneshe matumaini na uwezo kuliko CCM.

Wananchi wanaangalia alternative ambayo wapinzani wanakuja nayo, wanafanya comparison analysis ya viongozi hao yaani kwa mfano, kwenye baraza la mawaziri na mawaziri vivuli:
wananchi wanaangalia kambi ya upinzani bungeni kama mfano wa Uwezo wa Viongozi wa Upinzaniti, wanaangalia kati ya:

  • Lema V/s Chikawe kwenye Wizara ya mambo ya ndani, wanajiuliza hivi ni kweli LEMA anaweza kuwa best alternative ya CHIKAWE..,kweli..?
  • Selasini V/s Dr Mwinyi kwenye Wizara ya Ulinzi, wananchi wanawapima kwa uwezo wao.
  • SUGU v/s Dr Mukangara kwenye wizara ya habari, utamaduni na michezo, wananchi wanajiuliza hivi ni kweli SUGU anaweza kuwa bora mbele ya Dr Mukangara hata washawishike kukiondoa Chama kilichomsimamisha Dr Mukangara wakipe Chama kilichowaletea SUGU kama best alternative...,kweli..?
  • Msigwa v/s Lazaro Nyalandu kwenye wizara ya Maliasili.
Wenye v/s Bernard Kamilius Membe kwenye Wizara ya Mambo ya nje.,wananchi wanajiuliza hivi kweli MEMBE akisimama na WENJE..,Wenje anaweza kuonekana bora na kiongozi wa maana mbele ya MEMBE..? wananchi makini wanayaona haya na kuyapima na kisha kufanya uamuzi kupitia sanduku la KURA.

Kwa tathimini hiyo fupi, na hata kwa Uongozi wa juu wa Vyama vya upinzani., mathalani Chama kikuu cha Upinzani yaani Chadema.,ukifanya tathimini kwa Umakini juu ya Aina na Uwezo wa Viongozi wake dhidi ya wale wa Chama Makini CCM, wananchi wanaona matumaini na future bora ya nchi kupitia CCM.

Mathalani tazama mifano hii:
  • Wenyeviti; CHADEMA-MBOWE dhidi ya CCM-KIKWETE
  • Makamu M/kiti: CHADEMA-resigned ARFI dhidi ya CCM-MANGULA
  • Katibu Mkuu: CHADEMA - DR. SLAA dhidi ya CCM- KINANA
  • Naibu K/mkuu: CHADEMA - suspended ZITTO dhidi ya CCM- MWIGULU

Ukiangalia kwa Upande wa Sekretaieti ya CCM
  1. NAPE NNAUYE
  2. MAMA ASHA-ROSE MIGIRO
  3. MAMA ZAKHIA MEGHJI
  4. DR SEIF KHATIBU

Kwa upande wa CHADEMA.
  1. ANTHONY KOMU
  2. JOHN MNYIKA
  3. LEMA GODBLESS
  4. TUNDU LISSU
  5. LWAKATARE
  6. BENSONI KIGAILA
  7. JOHN MREMA

Wananchi makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawapima viongozi wao kwa kutathimini uwezo, maarifa, na uzoefu. kwa tathimini hii ni Vipi watanzania wanaweza kuwapa Upinzani nchi hii., kwa tathmini hii ni wazi CCM itaendelea kuwa Chama bora na kitakachoendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingine hamsini na dahari.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..

Vivaa Vijana Vivaaa.

VIJANA KARIBUNI CCM na kazi iendelee...!!!

Upinzani ni kweli haufai kushika nchi, walahauna uwezo wa kufikirika kushika nchi; kwa sababu ni magenge ya wahuni..Mbowe, slaa akina Lema ni magenge fulani ya wahuni waliopata kibali cha kuiba kwa usafi

CCM kwa upande wake, iliishajifia siku nyingi sana, ina ongoza kwa sbbu hamna upinzani na kwa sbbu haina tena moyo wa kujiuliza wala kuuma pale inapofanya dhambi

CCM sio genge la wahuni bali ni genge la wauji na majambazi

unaposema wapinzani waifuate katiba ya nchi nakushangaa sana, eti ulitaka upinzani kila mmoja aimbe ujamaa na kujitegemea??

una hakika CCM inasimamia itikadi na falsafa zake??

ni nini kimekusukuma kuandika hii post na ukaiita ''compasrison analysis"" ??

CCM mshakufa, na hamna uwezo wa kuwanyooshea vidole wapinzani- hamuishi

wapinzani wao sio wahuni tu bali wanajiua wakijua kuna hatari ya kupoteza 'chakura'-case study Zitto

ACT mpango mzima
 
Ni kosa la makusudi kabisa kuwaita wale wanaohoji uzoroteshaji wa maendeleo na ufishwaji wa wazi wazi wa demokrasia wapinzani, ni kosa kubwa sana....Wapinzani waandamizi wa maendeleo ya wananchi Tanzania ni serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya hawa wasanii walioingia kwenye madaraka kwa mbeleko ya sura!

CCM inayohubiri utawala bora, na demokrasia wakati huo huo ikiwa mbakaji wa kiwango cha juu cha demokrasia nchini,nani kawadanganya kwamba matatizo ya watanzania ambayo kwa kiwango kikubwa yamechangiwa na sera zilizozeeka za CCM yataondoka kwa kuendesha nchi kiubia na wanafamilia wa watawala waliopata appointments sehemu nyingine?

Ni jambo gani kwa mfano Bwanamdogo alisahau kuwafanyia wana Chalinze,ambalo liko kwenye ilani ya Chama ambalo Ridhwani ataenda kulisimamia kwa kutumia ilani hiyo hiyo? Ni nani alimtoa akili bwana Madega ambaye baada ya kutoswa kwenye kura za maoni anageuka mpiga zumari wa Ridhwani? Wana kalenga nao kwanini mkubali kutumiwa kama kandambili ambapo mwisho wenu ni kwenye milango ya bafu tu? Kwanini msitembee peku kabisa ili muwe huru kuzunguka nyumba nzima? Nasema mpeni kura huyu 'mrithi wa kiti cha baba' msiishie hapo na kama mtaona inafaa muoshesheni pia na binti zenu ili mmoja wa watoto wake aje kuchukua jimbo hilo nbaada ya yeye kupata uteuzi mwingine!
 
Hebu soma signature hapo chini labda itatusaidia!
Wise men talk because they have something to say, fools talk because they have to say something"

ngoja niwassaidie wanaweza wakasingizia hawajaona
 
Title yako ilikuwa mzuri sana sema ulichokiandika hakiendani na mtu ambaye tunasema anaweza kujenga hoja kama msosi zaidi ya kucompare watu badala ya utendaji kazi shame on you hopeless thread
 
Title yako ilikuwa mzuri sana sema ulichokiandika hakiendani na mtu ambaye tunasema anaweza kujenga hoja kama msomi zaidi ya kucompare watu badala ya utendaji kazi shame on you hopeless thread
 
there is no way mtu anawza akaniconvincd kwamba ccm wana haki ya kupata nchi mwaka 2015,kwa kifupi ni kwamba hakuna walichofanya ambacho chadema wangeshindwa kufanya tena kwa ubora na ufanisi zaidi na zaidi ya hapo so ccm hawastahili kupata nchi mwaka 2015.not to mention madudu waliyoyafanya na ahadi lukuki wasizozitimiza(you can only see this if you think with open mind).
 
Uludishe sim ya watu ndo uje endelea toka povu apa jukwaani we kibaka
 
Posho ya laki tatu angalau inakupa bundle umejua na kuandika siku hizi

Sent from my iPhone 5 using JamiiForums
 
Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayo- base katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika thread hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na ITIKADI na SERA, wamejikita katika kufanya siasa za matukio na UBISHANI. Siasa isiyo endelevu kwani matukio hukoma kwa wakati fulani, hivyo kwa wananchi walio makini hawawezi kuamini katika Chama ambacho chenyewe hakina kitu ama falsafa inayoiamini. Wananchi wanahitaji viongozi wenye falsafa wanayoiamini.

Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.

Maana ya kuwa na Vyama vya upinzani ni kutaka kuwapa wananchi alternative ya Uongozi na falsafa. sio KAZI ya upinzani kupinga kila kitu na sio kazi ya upinzani kusifia serikali, kimsingi kazi ya upinzani ni kutoa the best alternative solution to justify that opposition is the best alternative government in waiting. Lazima upinzani ujijenge kisera, kifalsafa na kiitikadi ambayo wananchi wataona kuwa ni njia ya kufikia Maendeleo na kuwajengea matumaini ya Mafanikio na Maisha Bora (kwani ndio paramount demand ya wananchi - MAISHA BORA)

Na nasema kama Upinzani ungekuwa makini basi Serikali na Chama Kilicho Madarakani nikimaanisha Chama Changu CCM kingekuwa makini zaidi, MWALIMU Nyerere aliwahi kusema maneno ambayo mpaka leo yamewekwa kwenye bango mbele ya Ukumbi wa Mikutano ya NEC (maarufu kama whitehouse) pale Makao makuu dodoma, maneno yale yanasema " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, na Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM "

TANZANIA imekosa UPINZANI MAKINI, upinzani unaojitambua nini unataka na wafanye nini kufikia hicho wanachokitaka. Wachambuzi wa siasa wanapoangalia uimara wa upinzani moja ya kigezo ni kutathimini uwezo wa mawaziri (Viongozi) na watendaji wa Chama tawala na Serikalini yake ukilinganisha na mawaziri Vivuli,na viongozi wa Upinzani. Inatakiwa Shadow Cabinet ioneshe uwezo na matumaini kuliko cabinet. Upinzani uoneshe matumaini na uwezo kuliko CCM.

Wananchi wanaangalia alternative ambayo wapinzani wanakuja nayo, wanafanya comparison analysis ya viongozi hao yaani kwa mfano, kwenye baraza la mawaziri na mawaziri vivuli:
wananchi wanaangalia kambi ya upinzani bungeni kama mfano wa Uwezo wa Viongozi wa Upinzaniti, wanaangalia kati ya:

  • Lema V/s Chikawe kwenye Wizara ya mambo ya ndani, wanajiuliza hivi ni kweli LEMA anaweza kuwa best alternative ya CHIKAWE..,kweli..?
  • Selasini V/s Dr Mwinyi kwenye Wizara ya Ulinzi, wananchi wanawapima kwa uwezo wao.
  • SUGU v/s Dr Mukangara kwenye wizara ya habari, utamaduni na michezo, wananchi wanajiuliza hivi ni kweli SUGU anaweza kuwa bora mbele ya Dr Mukangara hata washawishike kukiondoa Chama kilichomsimamisha Dr Mukangara wakipe Chama kilichowaletea SUGU kama best alternative...,kweli..?
  • Msigwa v/s Lazaro Nyalandu kwenye wizara ya Maliasili.
Wenye v/s Bernard Kamilius Membe kwenye Wizara ya Mambo ya nje.,wananchi wanajiuliza hivi kweli MEMBE akisimama na WENJE..,Wenje anaweza kuonekana bora na kiongozi wa maana mbele ya MEMBE..? wananchi makini wanayaona haya na kuyapima na kisha kufanya uamuzi kupitia sanduku la KURA.

Kwa tathimini hiyo fupi, na hata kwa Uongozi wa juu wa Vyama vya upinzani., mathalani Chama kikuu cha Upinzani yaani Chadema.,ukifanya tathimini kwa Umakini juu ya Aina na Uwezo wa Viongozi wake dhidi ya wale wa Chama Makini CCM, wananchi wanaona matumaini na future bora ya nchi kupitia CCM.

Mathalani tazama mifano hii:
  • Wenyeviti; CHADEMA-MBOWE dhidi ya CCM-KIKWETE
  • Makamu M/kiti: CHADEMA-resigned ARFI dhidi ya CCM-MANGULA
  • Katibu Mkuu: CHADEMA - DR. SLAA dhidi ya CCM- KINANA
  • Naibu K/mkuu: CHADEMA - suspended ZITTO dhidi ya CCM- MWIGULU

Ukiangalia kwa Upande wa Sekretaieti ya CCM
  1. NAPE NNAUYE
  2. MAMA ASHA-ROSE MIGIRO
  3. MAMA ZAKHIA MEGHJI
  4. DR SEIF KHATIBU

Kwa upande wa CHADEMA.
  1. ANTHONY KOMU
  2. JOHN MNYIKA
  3. LEMA GODBLESS
  4. TUNDU LISSU
  5. LWAKATARE
  6. BENSONI KIGAILA
  7. JOHN MREMA

Wananchi makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawapima viongozi wao kwa kutathimini uwezo, maarifa, na uzoefu. kwa tathimini hii ni Vipi watanzania wanaweza kuwapa Upinzani nchi hii., kwa tathmini hii ni wazi CCM itaendelea kuwa Chama bora na kitakachoendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingine hamsini na dahari.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..

Vivaa Vijana Vivaaa.

VIJANA KARIBUNI CCM na kazi iendelee...!!!

Dogo tuliza boli ili upate hekima na uelewa kwanza. Hiyo Kasi mpya yako haitokufikisha kokote.
Siku moja jamaa alipanda ndege halafu Pilot alifanikiwa kuipaisha kisha akatangaza kwamba hajui kuendesha na wala hajui namna ya kutua wala hajui kusoma ramani ya kule tuendako.
Utajisikiaje kama na wewe ni abiria katika chombo hicho cha usafiri.

Kiongozi mmoja mkubwa katika serikali hii ya chama chako alihojiwa alipokuwa ziarani Ufaransa ka nini Nchi hii ni Maskini wakati ikijinasibu kuwa na raslimali kedekede. Alijibu bila aibu kwamba hata yeye hajui kwa nini Tanzania ni Maskini.
Sasa dogo inabidi utambue kwamba Umaskini wa Nchi hii ni wa kutengenezwa sio wa lazima. Miaka 52 ya Uhuru bado tunapita Dunia nzima na bakuli la kuomba misaada. Lipo Tatizo kubwa kwenye akili ya watawala wa sasa ambao wanatoka kwenye Chama chako.

Wakati Mh. Sumaye amemaliza Degree yake Havard University aliporejea nchini alikiri kwa Kinywa chake kwamba sasa anajua kwa nini NCHI YA TANZANIA ni maskini, kumbuka huyu amekuwa Kiongozi wa shughuli za serikali Bungeni miaka kumi.

Sasa wewe ungekuwa wa maana sana kama ungetumia muda mwingi kufafanua kwa nini chama chako kinashindwa kutuingiza kwenye nchi yenye asali na maziwa badala ya kuwashambulia hao wapinzani wako.
 
Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayo- base katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika thread hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na ITIKADI na SERA, wamejikita katika kufanya siasa za matukio na UBISHANI. Siasa isiyo endelevu kwani matukio hukoma kwa wakati fulani, hivyo kwa wananchi walio makini hawawezi kuamini katika Chama ambacho chenyewe hakina kitu ama falsafa inayoiamini. Wananchi wanahitaji viongozi wenye falsafa wanayoiamini.

Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.

Maana ya kuwa na Vyama vya upinzani ni kutaka kuwapa wananchi alternative ya Uongozi na falsafa. sio KAZI ya upinzani kupinga kila kitu na sio kazi ya upinzani kusifia serikali, kimsingi kazi ya upinzani ni kutoa the best alternative solution to justify that opposition is the best alternative government in waiting. Lazima upinzani ujijenge kisera, kifalsafa na kiitikadi ambayo wananchi wataona kuwa ni njia ya kufikia Maendeleo na kuwajengea matumaini ya Mafanikio na Maisha Bora (kwani ndio paramount demand ya wananchi - MAISHA BORA)

Na nasema kama Upinzani ungekuwa makini basi Serikali na Chama Kilicho Madarakani nikimaanisha Chama Changu CCM kingekuwa makini zaidi, MWALIMU Nyerere aliwahi kusema maneno ambayo mpaka leo yamewekwa kwenye bango mbele ya Ukumbi wa Mikutano ya NEC (maarufu kama whitehouse) pale Makao makuu dodoma, maneno yale yanasema " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, na Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM "

TANZANIA imekosa UPINZANI MAKINI, upinzani unaojitambua nini unataka na wafanye nini kufikia hicho wanachokitaka. Wachambuzi wa siasa wanapoangalia uimara wa upinzani moja ya kigezo ni kutathimini uwezo wa mawaziri (Viongozi) na watendaji wa Chama tawala na Serikalini yake ukilinganisha na mawaziri Vivuli,na viongozi wa Upinzani. Inatakiwa Shadow Cabinet ioneshe uwezo na matumaini kuliko cabinet. Upinzani uoneshe matumaini na uwezo kuliko CCM.

Wananchi wanaangalia alternative ambayo wapinzani wanakuja nayo, wanafanya comparison analysis ya viongozi hao yaani kwa mfano, kwenye baraza la mawaziri na mawaziri vivuli:
wananchi wanaangalia kambi ya upinzani bungeni kama mfano wa Uwezo wa Viongozi wa Upinzaniti, wanaangalia kati ya:

  • Lema V/s Chikawe kwenye Wizara ya mambo ya ndani, wanajiuliza hivi ni kweli LEMA anaweza kuwa best alternative ya CHIKAWE..,kweli..?
  • Selasini V/s Dr Mwinyi kwenye Wizara ya Ulinzi, wananchi wanawapima kwa uwezo wao.
  • SUGU v/s Dr Mukangara kwenye wizara ya habari, utamaduni na michezo, wananchi wanajiuliza hivi ni kweli SUGU anaweza kuwa bora mbele ya Dr Mukangara hata washawishike kukiondoa Chama kilichomsimamisha Dr Mukangara wakipe Chama kilichowaletea SUGU kama best alternative...,kweli..?
  • Msigwa v/s Lazaro Nyalandu kwenye wizara ya Maliasili.
Wenye v/s Bernard Kamilius Membe kwenye Wizara ya Mambo ya nje.,wananchi wanajiuliza hivi kweli MEMBE akisimama na WENJE..,Wenje anaweza kuonekana bora na kiongozi wa maana mbele ya MEMBE..? wananchi makini wanayaona haya na kuyapima na kisha kufanya uamuzi kupitia sanduku la KURA.

Kwa tathimini hiyo fupi, na hata kwa Uongozi wa juu wa Vyama vya upinzani., mathalani Chama kikuu cha Upinzani yaani Chadema.,ukifanya tathimini kwa Umakini juu ya Aina na Uwezo wa Viongozi wake dhidi ya wale wa Chama Makini CCM, wananchi wanaona matumaini na future bora ya nchi kupitia CCM.

Mathalani tazama mifano hii:
  • Wenyeviti; CHADEMA-MBOWE dhidi ya CCM-KIKWETE
  • Makamu M/kiti: CHADEMA-resigned ARFI dhidi ya CCM-MANGULA
  • Katibu Mkuu: CHADEMA - DR. SLAA dhidi ya CCM- KINANA
  • Naibu K/mkuu: CHADEMA - suspended ZITTO dhidi ya CCM- MWIGULU

Ukiangalia kwa Upande wa Sekretaieti ya CCM
  1. NAPE NNAUYE
  2. MAMA ASHA-ROSE MIGIRO
  3. MAMA ZAKHIA MEGHJI
  4. DR SEIF KHATIBU

Kwa upande wa CHADEMA.
  1. ANTHONY KOMU
  2. JOHN MNYIKA
  3. LEMA GODBLESS
  4. TUNDU LISSU
  5. LWAKATARE
  6. BENSONI KIGAILA
  7. JOHN MREMA

Wananchi makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawapima viongozi wao kwa kutathimini uwezo, maarifa, na uzoefu. kwa tathimini hii ni Vipi watanzania wanaweza kuwapa Upinzani nchi hii., kwa tathmini hii ni wazi CCM itaendelea kuwa Chama bora na kitakachoendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingine hamsini na dahari.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..

Vivaa Vijana Vivaaa.

VIJANA KARIBUNI CCM na kazi iendelee...!!!

Kijana umeahidiwa nini? Mwenzio Mwigulu kajitahidi sana kapata. Sasa na wewe umeanza. Nape alianza na Lowasa enzi ya UVCCM akapewa kwanza ukuu wa wilaya kisha katibu mwenezi. Umetumia saa nyingi sana kuelezea hofu ulonayo juu ya chama kinachowanyima usingizi. Pole sana, tunakusubiri bungeni tukupime hoja zako wewe na wachache wa upinzani
 
haka kajamaa tangu kateuliwe kwenye bunge la katiba kanajiona kama kapo karibu na watawala nako ni katawala. kumbe ni kachumia tumbo ,

ndo maana kameanza kuiponda CDM ili kapewe cheo, kwani ili upande cheo ndani ya CCM ni lazima uwatukane sana CDM,

pole sana kijana hizo 300,000 Tsh kwa siku unazopewa zinakuzuzua??

sisi huku mtaani hizo 300,000 Tsh kwa siku tunazipata kilaini kwa kufanya kazi halali,

hatuhitaji kujikomba kwa watawala ili watulambishe makombo kama ulivyo wewe,

umepost utumbo tu. we tuambie unaijua vizuri itikadi na falsafa ya CCM??
 
Hata CCM walikuwa wapinzani na watarudi kwenye nafasi yao ya upinzani. Wajiandae kisaikolojia.
 
Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayo- base katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika thread hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na ITIKADI na SERA, wamejikita katika kufanya siasa za matukio na UBISHANI. Siasa isiyo endelevu kwani matukio hukoma kwa wakati fulani, hivyo kwa wananchi walio makini hawawezi kuamini katika Chama ambacho chenyewe hakina kitu ama falsafa inayoiamini. Wananchi wanahitaji viongozi wenye falsafa wanayoiamini.

Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.

Maana ya kuwa na Vyama vya upinzani ni kutaka kuwapa wananchi alternative ya Uongozi na falsafa. sio KAZI ya upinzani kupinga kila kitu na sio kazi ya upinzani kusifia serikali, kimsingi kazi ya upinzani ni kutoa the best alternative solution to justify that opposition is the best alternative government in waiting. Lazima upinzani ujijenge kisera, kifalsafa na kiitikadi ambayo wananchi wataona kuwa ni njia ya kufikia Maendeleo na kuwajengea matumaini ya Mafanikio na Maisha Bora (kwani ndio paramount demand ya wananchi - MAISHA BORA)

Na nasema kama Upinzani ungekuwa makini basi Serikali na Chama Kilicho Madarakani nikimaanisha Chama Changu CCM kingekuwa makini zaidi, MWALIMU Nyerere aliwahi kusema maneno ambayo mpaka leo yamewekwa kwenye bango mbele ya Ukumbi wa Mikutano ya NEC (maarufu kama whitehouse) pale Makao makuu dodoma, maneno yale yanasema " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, na Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM "

TANZANIA imekosa UPINZANI MAKINI, upinzani unaojitambua nini unataka na wafanye nini kufikia hicho wanachokitaka. Wachambuzi wa siasa wanapoangalia uimara wa upinzani moja ya kigezo ni kutathimini uwezo wa mawaziri (Viongozi) na watendaji wa Chama tawala na Serikalini yake ukilinganisha na mawaziri Vivuli,na viongozi wa Upinzani. Inatakiwa Shadow Cabinet ioneshe uwezo na matumaini kuliko cabinet. Upinzani uoneshe matumaini na uwezo kuliko CCM.

Wananchi wanaangalia alternative ambayo wapinzani wanakuja nayo, wanafanya comparison analysis ya viongozi hao yaani kwa mfano, kwenye baraza la mawaziri na mawaziri vivuli:
wananchi wanaangalia kambi ya upinzani bungeni kama mfano wa Uwezo wa Viongozi wa Upinzaniti, wanaangalia kati ya:

  • Lema V/s Chikawe kwenye Wizara ya mambo ya ndani, wanajiuliza hivi ni kweli LEMA anaweza kuwa best alternative ya CHIKAWE..,kweli..?
  • Selasini V/s Dr Mwinyi kwenye Wizara ya Ulinzi, wananchi wanawapima kwa uwezo wao.
  • SUGU v/s Dr Mukangara kwenye wizara ya habari, utamaduni na michezo, wananchi wanajiuliza hivi ni kweli SUGU anaweza kuwa bora mbele ya Dr Mukangara hata washawishike kukiondoa Chama kilichomsimamisha Dr Mukangara wakipe Chama kilichowaletea SUGU kama best alternative...,kweli..?
  • Msigwa v/s Lazaro Nyalandu kwenye wizara ya Maliasili.
Wenye v/s Bernard Kamilius Membe kwenye Wizara ya Mambo ya nje.,wananchi wanajiuliza hivi kweli MEMBE akisimama na WENJE..,Wenje anaweza kuonekana bora na kiongozi wa maana mbele ya MEMBE..? wananchi makini wanayaona haya na kuyapima na kisha kufanya uamuzi kupitia sanduku la KURA.

Kwa tathimini hiyo fupi, na hata kwa Uongozi wa juu wa Vyama vya upinzani., mathalani Chama kikuu cha Upinzani yaani Chadema.,ukifanya tathimini kwa Umakini juu ya Aina na Uwezo wa Viongozi wake dhidi ya wale wa Chama Makini CCM, wananchi wanaona matumaini na future bora ya nchi kupitia CCM.

Mathalani tazama mifano hii:
  • Wenyeviti; CHADEMA-MBOWE dhidi ya CCM-KIKWETE
  • Makamu M/kiti: CHADEMA-resigned ARFI dhidi ya CCM-MANGULA
  • Katibu Mkuu: CHADEMA - DR. SLAA dhidi ya CCM- KINANA
  • Naibu K/mkuu: CHADEMA - suspended ZITTO dhidi ya CCM- MWIGULU

Ukiangalia kwa Upande wa Sekretaieti ya CCM
  1. NAPE NNAUYE
  2. MAMA ASHA-ROSE MIGIRO
  3. MAMA ZAKHIA MEGHJI
  4. DR SEIF KHATIBU

Kwa upande wa CHADEMA.
  1. ANTHONY KOMU
  2. JOHN MNYIKA
  3. LEMA GODBLESS
  4. TUNDU LISSU
  5. LWAKATARE
  6. BENSONI KIGAILA
  7. JOHN MREMA

Wananchi makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawapima viongozi wao kwa kutathimini uwezo, maarifa, na uzoefu. kwa tathimini hii ni Vipi watanzania wanaweza kuwapa Upinzani nchi hii., kwa tathmini hii ni wazi CCM itaendelea kuwa Chama bora na kitakachoendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingine hamsini na dahari.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..

Vivaa Vijana Vivaaa.

VIJANA KARIBUNI CCM na kazi iendelee...!!!

Eti vipi umesema? Ujamaa na kujitegemea? Sawa ni lipi katika hili limetekelezwa na chama chako? Na jee hayo mafanikio ya maisha bora na mafanikio yametekelezwa kwa kipindi cha miaka 53?
Hivyo kwako wewe kuifanya siasa kuwa ajira zenu ndio iwe kigezo cha kuaminiwa na wananchi? Ukweli ni kuwa mnajenga mtafaruku tu kwani mnafanya kama muwezavyo wananchi wasifanye mabadiliko wanayoyahitaji!
 
Hicho ndo umeenda kujifunza Dodoma? kimsingi huna hoja wala mantiki juu ya nini hasa ulitaka kuzungumzia.In short wewe si mtu sahihi wa kuwasemea wananchi,wewe ni kiongozi wa CCM isiyo na dira wala mwelekeo (chama cha KIJAMAA KISICHOKUWA NA MJAMAA HATA MMOJA NA WEWE UKIWEMO MCHUMIA TUMBO TU),Unekuwa mfuatiaji wa mambo ungekuwa unajua itikadi,falsafa na sera za vyama vingine ikiwemo CDM,Lakini tunajua kuwa si utamaduni wa wana CCM KUJISOMEA,HATA HUKO DODOMA MMEENDA KULEWA,KUWATAJILISHA MACHANGUDOA NA KUPIGA KURA TU.

'Sio kawaida wana ccm kujisomea" Unamaanisha nn?
Mtazamo wa Paulo kwa maana ya ushindani wa kisera kupitia vyama vya siasa ni sahihi.
 
Paul Makonda
Hebu rudisha simu ya watu uliyokwapua then ndo uje hapa JF.
Huna tofauti na Chris Lukosi mwivi wa rambi rambi
 
Last edited by a moderator:
Sasa wewe ni Paul Makonda, una jipya gani la kuwaelimisha watanzania wakati bado na wewe mwenyewe wajifunza ni kuelewa tu kumekuwa kugumu maana Mungu katuumba tofauti....Omba sana usije ukashtuka umechelewa
 
Eti vipi umesema? Ujamaa na kujitegemea? Sawa ni lipi katika hili limetekelezwa na chama chako? Na jee hayo mafanikio ya maisha bora na mafanikio yametekelezwa kwa kipindi cha miaka 53?
Hivyo kwako wewe kuifanya siasa kuwa ajira zenu ndio iwe kigezo cha kuaminiwa na wananchi? Ukweli ni kuwa mnajenga mtafaruku tu kwani mnafanya kama muwezavyo wananchi wasifanye mabadiliko wanayoyahitaji!

Mafanikio ni nini? Miaka 53 nyuma kulikuwa kuna hii mitandao ya kijamii?
CCM imefanya maendeleo makubwa.
watu walikuwa wanapeleka ujumbe kwa barua wanakaa zaidi ya wiki taarifa haijafika.
Maendeleo ni going process. Hata mataifa endelevu hawajafika mwisho.
 
Achana na huyu bhana. Si anajua mwisho wake ni 2015 ije ccm ya EL au CDM. Alijichanganya kumtukana EL sasa anaona Kama kwa bahati mbaya CDM ikakosa kuchukua nchi ambayo is only 15% anafahamu EL atamfungia jiwe la kusagia na kumtosa baharini.
 
Back
Top Bottom