Wapinzani hawana sifa za Kuongoza nchi. (comparison analysis)

Wapinzani hawana sifa za Kuongoza nchi. (comparison analysis)

Simu uliyoiba ndo imekupa uwezo wa kuandika sana na uchambuzi wako mfu. Ila unakumbuka ulivyovuruga uchaguzi wa UDSM 2008 na kumfukuzisha Mwanafunzi Ondongo Odwar kwa kuwa tu ni Mganda? Najua hukuishia hapo maana ndo kazi ulyokuwa nayo ya kupeleka hela za wizi ili uwahonge vijana vyuoni wagombee vyeo vya kuwaongoza wanafunzi wenzao kupitia ccm. Hilo ulijui,Mfumo huo ndo unaoutetea hata hapa. Any way , ndoo ukoo wa panya
umenikumbusha huyu jamaa, alikuwa na ifluence sana, sijui yuko wapi now
 
wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.


Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.
Katika red - kumbe aloandika hajui kabisa alichokiandika ...
Hajui alikotoka ...
Hajui aliko na hajui aendako ...
 
Juliana Shonza, nimekufundisha hapo UDSM. Halafu we mwananmke sijui km utakuja kuolewa tena! Ushajiloga tayari.
Mkuu MCFM40, japo ndoa hupangwa na Mungu na sio na binaadamu, ila kuna binaadamu wengine wenye kauli za kuumba, hivyo sio vizuri kutoa laana kwa binaadamu mwenzako no matter what she did, msamehe binti mfungulie hicho kifungo, muondolee laana ya kutoolewa watu tucheze harusi, jinsia ya kike sio wenzetu, wao wana limitations of time umri unazidi kusonga!.

Paskali
 
Nadhani umepotea njia,hicho chama cha majangili nacho unakiita ni chama kweli??Na siku hizi nasikia mnaitwa Chama Cha Masogange
Vipi mkuu kasharipoti kituoni?

Au badoanaficha ngada kwanza
 
Kama viongozi wenyewe ni wa KALIBA ya kwako basi CCM haina viongozi.

Ukiangalia kwa umakini hujui hata Chama Chako kinafuata itikadi gani,kwa UJAMAA hamko mlishatoka huko na ndiyo sababu mliua Azimio la Arusha ,makazalisha Azimio la Zanzibar yaani Azimio la kuchukua chako Mapema,hivyo kwa usahihi kabisa hujui hata unaloongea.

Kwa Lema anaweza kuwa mbadala wa Chikawe ndiyo sababu Chikawe aliweza kufanya kazi naye vizuri sana na SIASA za CHIKAWE huziwezi hata siku moja.

Chikawe anajua nini maana ya vyama vya vingi vya siasa,anaelewa umuhimu wa vyama vya siasa kwa TAIFA lake.Chikawe aliweka TAIFA mbele chama baadaye na katika uongozi wake tuliona Polisi wakiwaheshimu na kufanya kazi na Wapinzani bila ugomvi japo ulikuwepo kwa kiasi kidogo.

Leo Itikadi na sera ya CCM ni chuki,visasi na ubaguzi ukiongezea na wizi wa raslimali za TAIFA.

Hivyo in short hakuna mwanaCCM ambaye anafaa kuwa kiongozi sababu wote ni wale wale wezi wa RASLIMALI zetu.

Hebu jiulize kwanini mnakimbizana na wapinzani kila kukicha??Kwanini hamtaki kukosolewa??Kwanini hamuukubali ukweli?

Jibu lake ni sababu mko busy kutafuta ulaji na kujilimbikizia mali.As for you huna hata moral authority ya kumkosoa Mpinzani awae yote.Hebu jichunguze kuanzia ngazi ya shule hadi hivi leo.

Tuhuma zote za kupewa mali na GSM hujazitolea maelezo,je unayo moral authority ya kusema upinzani??Haya vyeti vyako je??

Mdogo wangu angalia kabla hujaanza kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzako anza kutoa Boriti kwanye jicho lao.

Usidhani watanzania ni wapumbavu,jua tunaakili sana kuwaangalia si kwamba tunaukubali upuuzi mnaoufanya
Hahahaha.... Hivi hili povu lote unaweza kuthubutu hata kumtolea mwenyekiti wako Mbowe aliyemkaribisha Lowassa mlezi wa mfumo mbovu wa ccm?
 
Hahahaha.... Hivi hili povu lote unaweza kuthubutu hata kumtolea mwenyekiti wako Mbowe aliyemkaribisha Lowassa mlezi wa mfumo mbovu wa ccm?

Kama ni POVU chukua ukafulie hiyo KAPUTULA yako
 
Vipi mkuu kasharipoti kituoni?

Au badoanaficha ngada kwanza

Wewe ulizoficha umeshazitoa??Maana baada ya Masogange aka Agnes kukutwa na NGADA umekuwa mdogo kama piriton.Umejihenyesha kuja na threads kama kumi hivi.
 
Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayo- base katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote.

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika thread hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na ITIKADI na SERA, wamejikita katika kufanya siasa za matukio na UBISHANI. Siasa isiyo endelevu kwani matukio hukoma kwa wakati fulani, hivyo kwa wananchi walio makini hawawezi kuamini katika Chama ambacho chenyewe hakina kitu ama falsafa inayoiamini. Wananchi wanahitaji viongozi wenye falsafa wanayoiamini.

Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.

Maana ya kuwa na Vyama vya upinzani ni kutaka kuwapa wananchi alternative ya Uongozi na falsafa. sio KAZI ya upinzani kupinga kila kitu na sio kazi ya upinzani kusifia serikali, kimsingi kazi ya upinzani ni kutoa the best alternative solution to justify that opposition is the best alternative government in waiting. Lazima upinzani ujijenge kisera, kifalsafa na kiitikadi ambayo wananchi wataona kuwa ni njia ya kufikia Maendeleo na kuwajengea matumaini ya Mafanikio na Maisha Bora (kwani ndio paramount demand ya wananchi - MAISHA BORA)

Na nasema kama Upinzani ungekuwa makini basi Serikali na Chama Kilicho Madarakani nikimaanisha Chama Changu CCM kingekuwa makini zaidi, MWALIMU Nyerere aliwahi kusema maneno ambayo mpaka leo yamewekwa kwenye bango mbele ya Ukumbi wa Mikutano ya NEC (maarufu kama whitehouse) pale Makao makuu dodoma, maneno yale yanasema " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, na Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM "

TANZANIA imekosa UPINZANI MAKINI, upinzani unaojitambua nini unataka na wafanye nini kufikia hicho wanachokitaka. Wachambuzi wa siasa wanapoangalia uimara wa upinzani moja ya kigezo ni kutathimini uwezo wa mawaziri (Viongozi) na watendaji wa Chama tawala na Serikalini yake ukilinganisha na mawaziri Vivuli,na viongozi wa Upinzani. Inatakiwa Shadow Cabinet ioneshe uwezo na matumaini kuliko cabinet. Upinzani uoneshe matumaini na uwezo kuliko CCM.

Wananchi wanaangalia alternative ambayo wapinzani wanakuja nayo, wanafanya comparison analysis ya viongozi hao yaani kwa mfano, kwenye baraza la mawaziri na mawaziri vivuli:
wananchi wanaangalia kambi ya upinzani bungeni kama mfano wa Uwezo wa Viongozi wa Upinzaniti, wanaangalia kati ya:

  • Lema V/s Chikawe kwenye Wizara ya mambo ya ndani, wanajiuliza hivi ni kweli LEMA anaweza kuwa best alternative ya CHIKAWE..,kweli..?
  • Selasini V/s Dr Mwinyi kwenye Wizara ya Ulinzi, wananchi wanawapima kwa uwezo wao.
  • SUGU v/s Dr Mukangara kwenye wizara ya habari, utamaduni na michezo, wananchi wanajiuliza hivi ni kweli SUGU anaweza kuwa bora mbele ya Dr Mukangara hata washawishike kukiondoa Chama kilichomsimamisha Dr Mukangara wakipe Chama kilichowaletea SUGU kama best alternative...,kweli..?
  • Msigwa v/s Lazaro Nyalandu kwenye wizara ya Maliasili.
Wenye v/s Bernard Kamilius Membe kwenye Wizara ya Mambo ya nje.,wananchi wanajiuliza hivi kweli MEMBE akisimama na WENJE..,Wenje anaweza kuonekana bora na kiongozi wa maana mbele ya MEMBE..? wananchi makini wanayaona haya na kuyapima na kisha kufanya uamuzi kupitia sanduku la KURA.

Kwa tathimini hiyo fupi, na hata kwa Uongozi wa juu wa Vyama vya upinzani., mathalani Chama kikuu cha Upinzani yaani Chadema.,ukifanya tathimini kwa Umakini juu ya Aina na Uwezo wa Viongozi wake dhidi ya wale wa Chama Makini CCM, wananchi wanaona matumaini na future bora ya nchi kupitia CCM.

Mathalani tazama mifano hii:
  • Wenyeviti; CHADEMA-MBOWE dhidi ya CCM-KIKWETE
  • Makamu M/kiti: CHADEMA-resigned ARFI dhidi ya CCM-MANGULA
  • Katibu Mkuu: CHADEMA - DR. SLAA dhidi ya CCM- KINANA
  • Naibu K/mkuu: CHADEMA - suspended ZITTO dhidi ya CCM- MWIGULU

Ukiangalia kwa Upande wa Sekretaieti ya CCM
  1. NAPE NNAUYE
  2. MAMA ASHA-ROSE MIGIRO
  3. MAMA ZAKHIA MEGHJI
  4. DR SEIF KHATIBU

Kwa upande wa CHADEMA.
  1. ANTHONY KOMU
  2. JOHN MNYIKA
  3. LEMA GODBLESS
  4. TUNDU LISSU
  5. LWAKATARE
  6. BENSONI KIGAILA
  7. JOHN MREMA

Wananchi makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawapima viongozi wao kwa kutathimini uwezo, maarifa, na uzoefu. kwa tathimini hii ni Vipi watanzania wanaweza kuwapa Upinzani nchi hii., kwa tathmini hii ni wazi CCM itaendelea kuwa Chama bora na kitakachoendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingine hamsini na dahari.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..

Vivaa Vijana Vivaaa.

VIJANA KARIBUNI CCM na kazi iendelee...!!!


Kweli maendeleo yetu bado yako mbali sana tena sana, kama haya ndiyo mawazo yetu na bado tunadhani chama kinaweza kuongoza na kuleta mapinduzi ya kiuchumi ya nchi, basi tunahitaji kujitafakari sana namna tunavyofikiri/kutafakari na kutafsiri maana sahihi ya maendeleo na ni nani anapewa jukumu hilo la kuleta maendeleo hayo. Na tena ni ugongwa usio na tiba kujivunia watu walio ndani ya chama kama waleta mapinduzi ya kiuchumi, nani asiyewajua wanasiasa, wanamacho kama kunguru, miguu yao miepesi kama kurungu, mioyo yao inambio kuliko maji yapitayo kwwenye mbomba kwa pressure na ni wepesi kubadilika kama ntaa ikutanapo na joto. Hao ndiyo walete maendeleo?

Sio CCM wala CHADEMA wala NCCR wala chama chochote kitaleta maendeleo yatakayoonekana kwa mtu mojamoja mipakani na ndani ya nchi ya Tanzania, baali ni taasisi zilizoimara, zilizojengwa kimalengo, kimkakati na kimfumo kuleta maendeleo. zilizotiyari kufikiri kwa fikra itayoishi na sio kwa mujibu wa hisia na mihemko ya kisiasa.
 
Wewe ulizoficha umeshazitoa??Maana baada ya Masogange aka Agnes kukutwa na NGADA umekuwa mdogo kama piriton.Umejihenyesha kuja na threads kama kumi hivi.
Alaaa... Kumbe nabishana na mtoto!

Kwaheri masomo mema!
 
CCM NA UJAMAA KWELI WEWE AKIRI IKO? Unajua maana ya ujamaa? Shame on you.
 
Mkuu wa mkoa mheshimiwa kabisa, Paul Makonda, ulitakiwa kuandika Comparative analysis na sio comparison analysis.

Watanzania wanataka authentication ya vyeti vyako, vyeti vimefanya mambo mengi yasimame, nasimama na wewe kwa mambo mengi, lakini kama utashindwa kuonyesha uhalali wa elimu na majina yako, hutakuwa na moral authority kwenye nafasi adhimu uliyopewa kulitumikia taifa.
 
Back
Top Bottom