Hii taarabu ni nzuri sana lazima unaijua ngoja nijaribu kukumbuka manenoNna data base kichwani .....ila hiyo ulioisema sijaijua unless uniambie inazungumzia nini kidogo. Or is it "Kauli natoa" ?
Nataka kunena kuwafahamisha, naona fitina mmeizidisha,
wenyewe tumependana, kuachana ni muhari
FF please upload the song dear... kama unao...
Hii taarabu ni nzuri sana lazima unaijua ngoja nijaribu kukumbuka maneno
samahani maneno siyakumbuki lakini to me its one of the old time best
Usikasirike, hii kiswahili yake, labda utaikumbuka:
Ewe kiumbe wa shani nalipenda umbo lako
Mzuri uso kifani kakuumba Mola wako
Katu humu duniani hapana mfano wako
Ewe ua la peponi waridi lisilo miba
Kwenu kakutoa nani kwenye masikani yako
Bilisi au Ruhani kakuiba kwa wenzako
Mabanati wa peponi hao ndio fani yako
Ewe ua la peponi waridi lisilo miba
........it is all in the date in relation with the words in the song....
Nafikiri wewe unazungumzia TAARABU. Mark the U at the end of the word
Kifo cha mahaba, kina idhilali
hakina haiba, wala afadhali
bali tajikaba, nifilie mbali
kufa kwa mahaba, ni adhabu kali
leo ni msiba, usio mithali
kesho ni adhaba, mbele ya jalali
Ewe mahabuba, niepushe hili
Ni wewe tabiba, hakuna wa pili
Hapanda jadhiba, tajiua kweli
Ni kweli huyasemayo mkuu.Gaijin unapiga propaganda hapa...lol... taarab za sasa zimejaa mipasho sisikiii mirindimo "myororo" kama ilivyokuwa kwa kina Issa Matona, Patricia Hillary, Culture, Shakila etc enzi zao.
We acha tu yaani its too much happiness......lol!! Mie niko poa kabisa ila kale ka issue ka cm, aisee bado mtu wangu nakomaa tu ivoivo! Mmmh.....ila una kumbukumbu wewe duh!.....ndio maana pple zilikumiss!!Kipipi you surprise seems to be a happy one...lolMzima wewe?? vipi ulirekebisha cm na iko pouwa sasa?
Ni kweli huyasemayo mkuu.MOHD ILYAS: NIMESAFI MOYO
Hizo nyimbo zimetungwa na wakongwe wenye kujua nini maana ya utunzi.Hii nyimbo kumbe inawakosha wengi sana..........🙂
Ni kweli huyasemayo mkuu.MOHD ILYAS: NIMESAFI MOYO
Gaijin, please tukandamizie hizi nyimbo kwenye post moja, ni nzuri saaana.
gaijin ile nyimbo inaimbwa kama hivi nadhani
ooh raabi,usinipe mapenzi..
na wapeendwa haakuuna...
ushaikumbuka?
Hizi nyimbo za zamani wadada uzitumia sana kwenye kuboresha mahusiano yao ya kwenye ndoa, na wengine uzitumia kutongozea. ah ah ah ah ah!Kwenye post moja vipi?
Burudika na hii kwanza
Iwapi ile ahadi, wewe uliyo iweka
Umeitupa baidi, huwezi kuikumbuka
Au wafanya kusudi, nipate kufedheheka
Kudanganywa nimechoka, mwenzio ninateseka
Pendo lako nalitaka, nipate kufurahika