Habari wana jf,hivi ni sahihi kwa wapenzi ambao uhusiano wao haujajulikana bado kwa pande zote mbili nikimaanisha kwa mwanamke hawamtambui mwanaume na kwa mwanaume hawamtambui mwanamke,je ni sahihi kuishi pamoja kabla ya kuoana lets say ile mwanamke anaenda kwa mwanaume anakaa hata mwezi sometime mwanaume anaenda kwa mwanamke nae anakaa even week!
Kuishi wawili sio ishu sana. Sasa kama uwezo wa kufunga ndoa haupo mtafanyaje? Na mpaka mkaishi pamoja it is obvious nyumbani mnajulikana otherwise taarifa zingefika polisi kuwa kuna mtu kapotea.
Mazingira ya sasa yana discourage vijana kuoa maana ndoa ni mitaji. Sasa kama huna hela ufanyaje?
Ndoa ni kuhusu watu wawili na kwa mtazamo wangu mm, siku mnapofanya mapenzi kwa mara ya kwanza ndio siku mlifunga ndoa.
Na kama nia yenu ni kufunga ndoa basi hata muishi pamoja still mtafunga ndoa ni swala la maamuzi tu.