YAPO MATUKIO MENGI TU AMBAYO HUTABILI KIFO.Habari wana Jf.
Naandika bandiko hili baada ya kufanya utafiti Kwa muda mrefu.
Mbwa, paka, bundi wanapolia usiku Kwa sauti ya ajabu kama sauti za wanadamu wanaolia Kwa uchungu hutabiri kitu.
Utafiti umenithibitishia juzi mbwa na bundi walilia sana usiku Kwa mfululizo Jana tumezika MTU mtaani kwetu. Hali hii imekuwa ikitokea Mara Kwa Mara wanyama na ndege huyo wanapolia.
Mbwa hulia Kwa kuweka mdomo juu.Paka hutoa sauti isiyo ya kawaida Kwa kubana koo lake. Bundi hutoa mlio Kwa sauti nene yaani bass.
Mwenye zaidi karibuni [emoji250] [emoji240] [emoji211]
Nikiwa naishi Mbeya, kulikuwa na mzee mmoja, alikuwa na matatizo ya akili, alikuwa na ngómbe wengi, siku anafariki hospitali [ni mbali na nyumbani kwake] ngómbe walilia usiku kucha.
Tukio kama hilo likajirudia tena mwaka huu nikiwa Magu, Mwanza, jamaa wana ngómbe nyumbani kwao, yeye ni dereva wa bodaboda, akpata abiria akampeleka mbali na mji, kule wakamuua na kumtupa porini, ngómbe wao walilia usiku kucha, kesho yake asubuhi maiti ikaokotwa.
Hapo ndo patanishindaItabidi uwe wapiga na kapicha tuone hiyo mivurugano ya mapaka wakiwa heat
Sure, nilikua ni paka jike siku likilia Kama binadamu hata ufunge milango na Madirisha lazma litoke, likirudi tayar Lina mimbaWewe ni mjinga na imani zako.
Paka wanaliaga hizo kelele wakiwa ktk HEAT.
uwe unaitumia google pia kutafuta utafiti wa kisayansi na majibu yake kutoka kwa wabobezi waliofanya utafiti.
Yule mzee wetu naye kwani hana ng'ombe? Natamani ng'ombe wake walie usiku kuchaNikiwa naishi Mbeya, kulikuwa na mzee mmoja, alikuwa na matatizo ya akili, alikuwa na ngómbe wengi, siku anafariki hospitali [ni mbali na nyumbani kwake] ngómbe walilia usiku kucha.
Tukio kama hilo likajirudia tena mwaka huu nikiwa Magu, Mwanza, jamaa wana ngómbe nyumbani kwao, yeye ni dereva wa bodaboda, akpata abiria akampeleka mbali na mji, kule wakamuua na kumtupa porini, ngómbe wao walilia usiku kucha, kesho yake asubuhi maiti ikaokotwa.
imani tu hizo. kuna siku bundi lilikuja likalia mlangoni kwangu usiku, likatoka likapanda juu ya paa likaendelea kulia, likatoka likaenda kwenye mti fulani mbele ya nyumba yangu likaendelea kulia,
Dadek! nikaona linanizoea nikatoka na boonge la jiwe nikalitupia na kulikemea likakimbia zake sikuumwa na kichwa wala kalio mwaka wa pili sasa!
Alafu baadae unapiga goti kusali! Au unafikiri ukiwa unatumia fake ID unakuwa si wewe? Unajua dhambi ya kutamani mtu afe ni sawasawa kabisa na aliyeua? Ndio maana tuliagizwa ukimtamani tu mwanamke tayari umezini nae moyoni ....acheni kujitia dhambini kwa ushabiki maandazi wa kisiasa ....Yule mzee wetu naye kwani hana ng'ombe? Natamani ng'ombe wake walie usiku kucha