Wanyakyusa ni wahanga wa CCM?

Wanyakyusa ni wahanga wa CCM?

Status
Not open for further replies.
Utamaduni wa hawa watu unanifurahisha sana, the way wanavyoishi na mambo wanavyochukuliana, ila tatizo wanawake wao wanapenda sana kujipodoa!
 
Tuliwahi kuweka hii list huko nyuma;

Mwaikambo (Gibbons)
Mwandosya
Mwangosi
Ulimboka
Kibanda
Mwakyembe
Mwaibabile (alikuwa mwandishi jembe sana Songea, akafungwa kwa "nyaraka za siri za serikali")
Kibona
Mwakipesile (aliuwawa Rungwe)
Jwan Mwaikusa


Nawashauri machifu wa Kinyakyusa wajenge Mnara wa Kumbukumbu kuwa-enzi vijana wao
Usisahau Eli Anangisye (wakati wa Nyerere)
 
Kule Mwabepande pamefanana na majina yao ndo maana wanapenda kwenda kuwafanyia finishing huko...............!

kaka unapokuja mtandaoni tena huku kwa wanatafakuri jitahdi kujua unachokiandika,,kule sio 'mwabepande' ni 'mabwepande'. Nilikuwa kwa obama.....Kumbe ni.....Kwani hlo ni jina lako kama unajina zuri weka hapa.
 
Asante mkuu, ila umemsahau na babu yangu Chief Mwansasu.
Machifu watasikia kilio cha wana wao.

...Hapana Mkuu huyo siwezi kumsahau kwani akina Andy, Mpeli tulifahamiana nao vyema na hasa baada ya mimi kuoa huko kwenu....Chief Mwansasu alishatajwa na post zilizotangulia............
 
Usisahau Eli Anangisye (wakati wa Nyerere)

Huyu mbali na misimamo yake yenye akili jambo lililomfurahisha/lilimpendeza Nyerere......aliharibu pale alipoanza kushirikiana na akina Kambona......jina lake la Kinyaki ni "Mwalulesya"....nilikuwa nafahamiana naye vizuri. Na hiyo ndio picha yake enzi zile.....dahh!..... Jasusi anaweza kukupa story zake....i guess
 
Last edited by a moderator:
Huyu mbali na misimamo yake yenye akili jambo lililomfurahisha/lilimpendeza Nyerere......aliharibu pale alipoanza kushirikiana na akina Kambona......jina lake la Kinyaki ni "Mwalulesya"....nilikuwa nafahamiana naye vizuri. Na hiyo ndio picha yake enzi zile.....dahh!..... Jasusi anaweza kukupa story zake....i guess

Ogah,
Hata mimi nilifahamiana na marehemu Anangisye baada ya kumaliza masomo yake Makerere. Daah, tumetoka mbali.
 
Leka mbuke kumyitu kwa mwakalili ngabhalalusye abhasololi pi isyeto lya babu gwangu Mwanjonde, ilopa hili abhikuhomba, naloli ngubhabhula sika sunga hisi, amukuketa...!

papo bhalipakutusenganya pambwani apa!
 
Ogah,
Hata mimi nilifahamiana na marehemu Anangisye baada ya kumaliza masomo yake Makerere. Daah, tumetoka mbali.

Shikamooni wazee!.. Maana huyo mnayemsema wewe na jasusi nilimsoma gazetini. Kama mliwahi kumwona bila shaka mna miaka 50+
 
Haya mabo mbona yamekua na utata kwa ndugu zetu wanyaki, mimi lidhani wanawindwa na nondo tu kumbe ni zaidi ya hapo. Lakini mbona TISS wamejazana wao, 2015 inabidi tumuingize mmoja wao magogoni ili kuokoa kizazi hiki.
 
JK alipigwa mawe Chunya, wilaya mojawapo ya mkoa wa Mbeya, na sio Rukwa.

Ila nakumbuka hata enzi za Nyerere, Wanyakyusa wa Kyela katika kupinga mpango wa operation maduka ya ushirika na kufungwa maduka binafsi miaka ya 1970, walimzomea Abdu Jumbe. Alisema TANU oyee wakasema ziii! Kwa enzi za Nyerere kuwa na ujasiri huo halikuwa jambo la kawaida, lakini Wanyakyusa waliweza! Nyerere aliwatetea akasema hakuamrisha maduka binafsi yafungwe, Kawawa aliyafunga kwa kutomwelewa alichomaanisha!
Sasa si malizia baada ya iyo tafrani watu walikamatwa hasa ring leaders na kuwekwa jela Rungwe.Wana kyela waliandamana mpaka Gereza la Rungwe.Nyerere alibidi amwambie kawawa achia hao watu.Jamaa wakatolewa jela.
Achana na wanyaki ustaarabu waliuanza kitambo mpaka Nyerere alichoka mfano kutenga maeneo ya kufuga na kulima hakuna mapigano kati ya wakulima na wafugaji mpaka leo
 
Si dhani kama kibamba ni Mnyakyusa, nilijua ni mnyalu au Msagala wa pale kijiji cha Mahenge karibu na kitonga ukitoka Ruaha Mbuyuni maana nilioneshwa nyumba nikaambiwa ni ya kwake.
Niko na Nyumba maeneo ya Pugu Dsm does that mean mimi ni Mzalamo?
 
Ha ha haaa.Anajiita mnyakyusa lakini ni mndali.
Mndali ni mnyaki ila tunasema Balyendile Indali kule milimani
Kwa kifupi wote walikuwa njia moja wakitokea moro ila kuna mahara waligawana kwa kupita njia tofauti
 
Huyo wa polisi chang'ombe alikuwa anaitwa Ekson Ahombile Kapyela Kibanda, alikuwa Baba mdogo wa Eng.Norman Kapyela, baba yake Absalom Kibanda
Ndo uzuri wa JF watu wana nondo za kufa mtu.
Unajua wanyaki ni lango nazani kuna haja ya Mwalimu Mwakasege kuliombea hili lango
 
>Ukweli tutaendelea kuusimamia bila kumjali wala kumuogopa mtu yeyote
>Kifo aliumbiwa mwanadamu, na hata wauwao nawao watakufa pia.
>LUKA 12:4 "Msiwaogope wauao mwili tu,bali mwenyeuwezo wa kuua mwili na roho"
>UJASIRI,UKWELI,UZALENDO NA KUJITAMBUA KWETU NDICHOCHANZO
>KYALA ALENANUSWE MWE.

Amen naona ujobhile ghosa
 
Haya mabo mbona yamekua na utata kwa ndugu zetu wanyaki, mimi lidhani wanawindwa na nondo tu kumbe ni zaidi ya hapo. Lakini mbona TISS wamejazana wao, 2015 inabidi tumuingize mmoja wao magogoni ili kuokoa kizazi hiki.
Tulijazana TISS enzi za Mwangonda mmasiku aga jwanio aje KUTISS bhalangani naloli abha!Bhakamanya nesi bhikowomba
 
Ndg. zangu WanaJf, salamu zenu wote na poleni na majanga mbalimbali yanayotokea nchini hivi sasa. Baada ya kutumikia kifungo cha mwezi mmoja hapa JF baada ya kutumia lugha kali dhidi ya ndugu zetu Waislam kwa mauaji ya Wakristo sasa nimefunguliwa. Nawashukuru sana wote walionifungia kwani wasingefanya hivyo nilikuwa na hasira sana wakati ule, pia nawashukuru kwa kunifungulia kutoka lupango.

WanaJF naomba sasa nirudi kwenye maada, huwa nakaa najiuliza kwanini mateso, unyanyasaji na vifo vinawakumba WANYAKYUSA tu? Je kuuwawa kwa Prof. Jwani Mwaikusa na David Mwangosi, mateso dhidi ya Dr. Stephen Ulimboka, Absalom Kibanda, Dr. Harrison Mwakyembe na Prof. Mark Mwandosya kutaisha lini?

Hivi wanaoratibu mipango ya kuwaondoa (eliminate) WANYAKYUSA wanafikiri wanaweza kuwatuliza au kuwaangamiza kabisa WANYAKYUSA kwa mfumo huu, hivi inawezekana ukawanyamazisha WANYAKYUSA kutetea raslimali za nchi yao? Kwanza nawapa pole kwani watambue tu kuwa ujasiri wa WANYAKYUSA katika kutetea nchi yao haufundishwi darasani ni wa kuzaliwa nao na watabaki hivyo hadi mwisho wa dunia hii. Napenda kuwakumbusha tu wanaopanga mipango hii kuwa kuwatokomeza WANYAKYUSA hapa nchini ni sawa na kuhamisha bahari kwa kikombe cha chai.

Hata hivyo napenda kujua hii mipango ni mpaka lini?
 
We mwenyewe humjui adui wa mnyakyusa ni nani? Kamuulize Prof.Mwandosya rafiki yake Mwakasendo wa kijiji cha Ijoka alikufaje? Wanyakyusa wakiamini kwamba hakuna demokrasia na haki ya kuonesha kipaji chako katika mfumo tuliopo wataacha kuuliwa hovyo lakini sasa kujifanya rafiki wa adui ndiko kunawagharimu.Hii haijaanza leo,kwa wanaojua historia ya Elly Anangisye hawashangai haya.Siku si nyingi watatoa kauli moja,kama nawe ni mmojawapo mulika uone adui yako kabla ya kuwauliza watu...Nenkukwe!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom