Maajabu ya wabunge wa CCM mkoa wa Mbeya

May 13, 2013
49
12
Ndugu zangu wanajamii forum hasa mnaotoka mkoa wa Mbeya na wale wapenda haki, mimi nawashangaa sana wabunge wa CCM wanaotoka mkoa wa Mbeya, kuna matukio mengi ya kutisha sana yanatokea katika nchi yetu, na mengi ya hayo yamewatokea kwa wenyeji wa mkoa wa mbeya na kibaya zaidi matukio mengine yamewagusa baadhi ya wabunge wetu wa mkoa wa Mbeya.

Karibia wabunge wawili wamelishwa sumu, hawa ni Prof. Mwandosya na Dr. Mwakyembe, pia tumeshudia kifo cha Daudi Mwangosi, Kibanda na Ulimboka na wengine amboa wapo usalama wanakufa hovyo tu. cha ajabu yote haya yanatokea waheshimiwa hawa wamekaa kimya kabisa. swali ambalo napenda kuwauliza ni kwamba, je wanatuachia wosia gani kwa vijana tunaotoka mkoa wa Mbeya?

Je tuachane na siasa? au hii inatokana udhaifu wao binafsi? na kama ni udhaifu wao CCM wanambeya wanatushauri tuchukue hatua gani? napenda kuwasilisha.
 
Ukiingia CCM huwezi kutoka, vumilia humo humo hadi kifo kikuchukue.( cc mwakyembe, EL, Malecela, Sitta; Nape) huwezi kutoka kama uliapa mbele ya mungu kwamba wewe ni CCM na utafia CCM. hata wakufanyaje we vumilia tu. Kuna watu waliamua kuanzisha CCJ wapo wapi? kuna watu walikatwa majina wapo wapi? kuna watu waliambiwa si raia wa Tanzania wapo wapi?
 
Sasa kwanini mliwachagua na mnaendelea kuwachagua? Hao ndiyo taswira yenu, maana ndiyo mliowachagua kuwawakilisha.
 
Koma amisi abhana bhende kitalii... Wabunge wa ccm Mbeya ni mfu kama kilivyo mfu chama chao, afterall matukio yote hayo yamefanywa na serikali ya chama chao wafanye nini sasa,hata akina Mwandosya na Mwakyembe nao wamekaa kimya kulinda chama chao...
 
Hata mimi huwa siwaelewi wameonyesha ni watu dhaifu sana wasio na umoja, hawajiamini na hawana maamuzi..sijui wanataka nini kiwapate zaidi ya yaliyotokea, akina mwakyembe jeuri wanawekea ccm humo humo kwangu mimi afadhali samuel sitta namwona anajisimamia kuliko hawa watu wetu
 
Eti wanajifanya waungwana, wanamfanyia nani ungwana huo wakati wao wanateketea na nchi inateketea. hatuhitaji ushauri wao sana sana waondoke tu hawana jipya hawa.
 
CCM is like a secrety societies(illuminat,skull and bone,freemanson etc) ukishaingia kuna daraja ukifikia huwezi kutoka.and it is real a secrety society maana ukiangalia yanayofanyika nyuma ya pazia kama mauji,kupeana sumu,kuteka etc ili kulinda utawala huwezi amini.ndio maana hao waliokula viapo hawawezi kutoka.thats why they say CCM ina wenyewe,we mwanachama wa kawaida usijidanganye.
 
Koma amisi abhana bhende kitalii... Wabunge wa ccm Mbeya ni mfu kama kilivyo mfu chama chao, afterall matukio yote hayo yamefanywa na serikali ya chama chao wafanye nini sasa,hata akina Mwandosya na Mwakyembe nao wamekaa kimya kulinda chama chao...
naloli bhikukoma amisi bho twebhanabo tukwenda kitali.
 
Ukiingia CCM huwezi kutoka, vumilia humo humo hadi kifo kikuchukue.( cc mwakyembe, EL, Malecela, Sitta; Nape) huwezi kutoka kama uliapa mbele ya mungu kwamba wewe ni CCM na utafia CCM. hata wakufanyaje we vumilia tu. Kuna watu waliamua kuanzisha CCJ wapo wapi? kuna watu walikatwa majina wapo wapi? kuna watu waliambiwa si raia wa Tanzania wapo wapi?

Hakuna aliyenikera kama Dr. Mwakyembe!Pamoja na kulichungulia kaburi na kutuahidi kuwasema waliomlisha sumu, aliishia kunywea mara tu alipopewa cheo cha uwaziri kamili!
Kweli RUSHWA ni janga la KITAIFA
Wanaowaona kuwa mashujaa wa mkoa wa Mbeya ndo haooooo!
 
Nakumbuka yote haya yanayotokea dr mwakyembe alikua wakwanza kutahadharisha taifa kwamba serikali imekodi alshabab kumwangamiza yeye pamoja na watu wanaoonekana kuwa tishio kwa maslahi ya watawala leo hii tumeyaona yakitokea kwake yeye mwenyewe,prf mwandosy,dr ulimboka,absalom kibanda,daudi mwangosi na yule dada aliye kuwa msaidizi wa dr mwakyembe.swali je ni kweli ccm na serikali yake ina wapenda watu wa mbeya?hususan wasomi wa mkoa wa mby?tafakari chukua hatua.
 
Prof.Mwandosya na Mwakyusa hawana la kusema kabisa amewashinda hata Mwambalaswa japokuwa alipita kwa wizi wa kura, Zambi yeye ameamua kuwa katibu mwenezi wa CCM, Dr.Mwakyembe yupo busy kutafuta ministerial legacy ili amfunike Magufuli lakini jitihada zake zinaonekana kugonga mwamba. Mulugo yeye yuko busy na tongue slip ya muungano wa Tanganyika na Zimbabwe kuunda Tanzania huku akijaribu kuiboresha shule yake ya southern highland huku jukumu alilopewa kitaifa la kuinua ubora wa elimu likimshinda. Yule mbunge wa Mbarali alipewa visurufu na mwekezaji mwishowe wananchi wanakosa maji kwani mwekezaji amejenga mifereji inayozungusha maji katika mashamba yake katika bonde la Mbarali na Kapunga. Hadhi ya Mbeya itazidi kushuka endapo hawa watu watarudi 2015, hawana muda wa kuhoji gas yetu inayotoka Mlima Kyejo bila kufaidika wala mgodi wa Kiwira!
 
Mbeya viôngozi kupitia Ccm hovyo sana lakini wananchi wenyewe wanajitambua, kumwangusha mwana ccm vituo 32 kati ya vituo 34 vya udiwani ni ujumbe mzito! Waache akina mwakyembe waendelee kutafuta umaarufu binafsi sisi tutasonga bila wao
 
We waache wanyamaze hivyo hivyo ila siku tukiwapiga chini kabisa ndo watakomo maana hata chama chao hakitawathamini!
 
Hawewezi kusema kitu kwasabau wakipiga kelele wanapewa vyeo halafu wanatulia kama maiti. Jiulize mkwara wa Mwakyembe wakati ule akitoka India kuwa ataweka wazi yote uliishia wapi.Alipopewa uwaziri akaona ndio malipo ya madhira aliyoyapata. Mwenzake Sitta aliyekuwa akimsemea akaonekana mmbeya. Sasa kama waathirika wenyewe hawajisemei nani atawasemea? Yuko wapi Ulimboka? Kibanda naye si ajabu akawa kama Ulimboka
 
Tatizo la nchi hii kwa ujumla, na wala siyo Mbeya peke yake, siyo viongozi bali ni wananchi wapiga kura wanaowachagua hao viongozi wa hovyo. Siku wananchi watakapo amua kuwa hawahitaji wababaishaji ndio utakuwa mwisho wa viongozi wababaishaji nchi hii.
 
Back
Top Bottom