Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Wangapi wanamkumbuka Umsolopagaas?

Moja ya vitabu vizuri vilivyowahi kuburudisha na kuchangamsha akili wakati ule ni vile vya bwana Msa (Mohamed Said Abdullah). Kuna mtu anakumbuka SIRI YA SIFURI? Au niko mwenyewe?
Kisima cha Giningi,Mzimu wa Kale,Duniani kuna Watu,
 
Unakumbuka ,, unakumbuka Mkuu siku ulipoelekeza risasi yako kwenye sikio la Nyati aliyekuwa anashambulia unakumbuka?

Yaah hizi ni baadhi ya kauri za huyu jamaa mlinzi wa Ngazi kuu . hakika ni simulizi nzr sn.
 
Nakufa,nakufa,wapo wapi wale wakuu waliotangulia mbele??siwaoni,wewe upo makumazahn??au umekwisha nitangulia sehemu ya mbele nisiyoijua mimi?,mahali panapozungukazunguka??Nasikia harufu ya damu,Naitwaaa!Ndipo alipoiinua inkosikazi yake,akaizungusha ,Ikawa kama inayotoa nuru ya dhahabu,,

Duh unanipeleka mbali sanaaaaaaaa tu
Msolopa gazi mwana wa kazi anavuka Maji ya shingo bila ya kulowa pu*********
 
Nakufa,nakufa,wapo wapi wale wakuu waliotangulia mbele??siwaoni,wewe upo makumazahn??au umekwisha nitangulia sehemu ya mbele nisiyoijua mimi?,mahali panapozungukazunguka??Nasikia harufu ya damu,Naitwaaa!Ndipo alipoiinua inkosikazi yake,akaizungusha ,Ikawa kama inayotoa nuru ya dhahabu,,
Nakufa !nakufa !lakini kitakuwa kifo cha kifalme! wako wapi waliotaka kuipanda ngazi kuu ?mbona siwaoni !upo wapi makumazahn? au umekwisha nitangulia katika sehemu ya kiza ninayo elekea ?damu inapofusha macho na sehemu inazunguuka! nasikia sauti ya maji! kisha akalitizama shoka lake la vita na kusema kwa heri inkosikazi! hapana tumeishi pamoja kwa muda mrefu hakuna mtu wa kuweza kukushika kisha akalizunguusha juu ya kichwa chake na kufanya mduara basi hapo alilishusha katika mwamba ule mtakatifu pigo moja lenye nguvu lile shoka likavunjika na baadhi ya sehemu ya ule mwamba hali ya kuwa nae akianguka huku kashika kipini cha shoka lile basi hivyo ndivyo alivyokufa yule mzee mzulu.
 
Unakumbuka ,, unakumbuka Mkuu siku ulipoelekeza risasi yako kwenye sikio la Nyati aliyekuwa anashambulia unakumbuka?

Yaah hizi ni baadhi ya kauri za huyu jamaa mlinzi wa Ngazi kuu . hakika ni simulizi nzr sn.
Yule mtu wa tatu alinifanya nimtizame zaidi na kugundua huyu si mkazi ila ni mzulu halisi kinywa cha ucheshi cha kizulu na macho madogo ya kahawia ila makali kama mwewe! japo kuwa nilikuwa sijamuona kwa muda wa miaka 12 nilimtambua na kumsalimia kwa sauti ndogo kwa lugha ya kizulu hujambo umslopogaaz basi yule mtu mkubwa nusura shoka lake la vita lianguke kaanza kunisalimia aah mkuu! mkuu baba! Makumazahn mwindaji akeshae hodari mwepesi rafiki muaminifu ambae risasi zake hazikosi shabaha muuwaji wa simba mla tembo mkuu ! mkuu baba !ama kweli ile methali ya kikwetu isemayo milima haikutani ila binadamu hukutana ni ya kweli kabisa na tena yenye busara tizama alikuja tarishi kutoka natal akalia na kusema makumazahn amefariki na nchi haitomuona makumazahn tena lakini tizama leo hii baba yangu katika nchi ngeni tena yenye harufu mbaya kama hii namuona tena makumazahn hakika ndie yeye bila shaka! Manyoya ya mzee mbweha yamekwisha ingia mvi! Lakini macho na meno yake bado ni makali vilevile kama zamani! Mkuu baba unakumbuka namna ulivyo pitisha risasi penye jicho la nyati aliekuwa akishambulia?
 
mwamba mtakatifu ulipo vunjwa kwa pigo lililo nyooka !! ama kitabu hiki kilikuwa kitamu - hutaki kukiacha
Tulikuwa tumekaa mezani ni huzuni iliyotawala hata yule bibi mackenzie hakuja kujumuika nasi. Niseme sikuweza kula na ni ujio wetu umesababisha maafa kwa wenyeji wetu nikaomba radhi na kutoka nje nilikuwa nimekaa kwa muda mchache mara nikasikia sauti ya mwango kufunguliwa kisha kuna kitu kikapita kikiviringika mbele yangu na kutulia mbele kidogo nikajishauri nikifuate basi nikakishika kilikuwa ni kilaini tena chenye uvungu nikakiinua juu ili niweze kuona katika nuru ya mbalamwezi loh!
Kilikuwa ni kichwa cha mtu ndio kwanza kikatwe!
Mimi ni mtu niliezoea kuona mambo mengi ya ajabu lakini lazima nikiri nilichefukwa na roho nikajaribu kumuita inkubu kwa sauti ambayo nilidhani ni ya kawaida sikuweza kwani walitoka wote nikawa sina budi kuwaonyesha bwana mackenzie alifadhaika sana mara wakati tunajadili akaingia mmoja kati watu tulio watuma na kusema baba ujiaze moyi wajivuni wanatujia nao wapo katika boma la zamani la ng'ombe!
Mackenzie akauliza mtoto yu salama? ni mweupe kama theluji lakini mzima nimemuona kazunguukwa na maadui kila upande.
Wakati yule mtu akihadithia mara tukasikia mlango ukigongwa kwa nguvu nikamuamuru umslopogaaz aende akaangalie akasema anamuona mtu mmoja mkono wa kuume kashika mkuki na mkono wa kushoto ana kapu nikamwambia mruhusu aingie! Mlango ukafunguliwa kisha yule mtu asiingie kama dakika tano kukawa kimya kisha akaingia mtu mmoja kama umslopogaaz alivyoeleza nae alikuja kwa hatua za dharau na kujiamini kisha akaukita mkuki wake ardhini na kulitua kapu chini kisha akasema tarishi wa kwanza tulie mtuma hakuongea akacheka kwa dharau huku akionyesha kile kichwa cha mtu walie muuwa nami sikuwa na budi kumsifu hali ya kuwa kazunguukwa na maadui.
 
Back
Top Bottom