Umesema kama mwanamume inkubu ya nini kuogopa? yule mtoto wa kike kasema watakula na kufanya karamu na iwe karamu yao ya mazikoni! Yule mbwa ninae tumaini kumuumbua kutakapo pambazuka amesema hatuwezi kuwashambulia sababu tu wachache! bwana mkubwa makenzie ana watu ishirini na kuna watu watano wako makumazahn kisha kuna watu weupe watano wanatosha kabisa tazama vita vitapiganwa hivi wakati mwangaza unaanza kuangazia pembe za ng'ombe si kabla wala baada (makumazahn wewe ni mzee na mwerevu wa mambo ya vita!
Unalijua lile boma waliloweka kambi niliiona asubuhi! Akachora chini hapa kuna mlango mkubwa umezibwa kwa miiba inkubu mimi na yule mkazi mwenye kifua kipana ni mtu jasiri tutasimama hapo na mashoka yetu.
Bougwan na watu wake kumi waende penye mlango mdogo wamuue yule mlinzi anaeshika zamu bila kufanya sauti kisha watu wengine waliobaki wagawanywe kwa makumazahn na bwana mkubwa kisha utakapo fanya sauti ya mlio wa ng'ombe wewe makumazahn basi waanze kushambulia lakini wakimuangalia yule mtoto wa kike basi kwa milio ya bunduki ya makumazahn na kwa makelele ya sauti ya juu ya ukuta ya watu wa bougwan basi wajivuni wale kwa pombe nyingi walizo kunywa na kwa hamaki ya kuamshwa usingizini watajikusanya na kuelekea lango la miiba basi hapo watatukuta na inkubu hilo ndio shauri langu makumazahn kama nawe una shauri jema liseme.
Basi hapo nikawaambia maneno mengine wasio yaelewa kisha wote tukakubaliana na mbinu za yule mzulu nikamtania aah mzee simba unajua jinsi ya kuvizia na jinsi ya kuuma unajua pahala pa kushika na mahala pa kushika akajibu ndio makumazahn vita vitakuwa vyema.
Guasa...
Mwaga vitu kaka mwaga...
Umenirudisha 1963 Kinondoni Primary School...na mie mkutubu
wa darasa na ''time keeper'' mgonga kengele.
Bibi yangu
Mwantum biti Rajabu alikuwa ana kibiashara chake
pale shule akiuza maharage kipimo kikombe cha kahawa.
Hela yake mwenyewe kaifunga kwenye upande wa khanga.
Likibaki rojo lile ni la waume zake mimi na rafiki zangu tunakwenda
kusafisha sufuria.
Hatukusikia kipindupindu wala nini...
Hapo nyumba juu kuti chini tope.
Iko siku nilipata hamu ya kwenda kuangalia shule yangu.
Siku nzima sikuwa na raha najiuliza kulitokea nini?
Maua tuliyokuwanayo pale shule hakuna...
Madarasa hayana milango wala madirisha, makabati tuliyokuwa tunawekea
vitabu hivi vya Msloopogas maktaba ya darasa hakuna hata hilo kabati...
Nimebakia nimeduwaa...
Yarabi nini kimetokea?
Na hii wala haikuwa shule ya matajiri.
Tukisoma sisi watoto wa watu wa kawaida kabisa.
Kulikuwa na timu kali ya kabumbu, net ball, riadha tukiongoza mkoa wa Dar
Salaam.
1966 darasa zima limepasi kwenda sekondari.
Nikamkumbuka Mr. Romenesko mwalimu Peace Corps mwalimu wetu wa
Kiingereza aliyetufunza kucheza base ball na mwalimu wa riadha...