Kaka mswahili, ninaacha shughuli zabgu nyingina muhimu kwangu binafsi ili nikujibu hoja na shutuma zako moja baada ya nyingine, kwa faida yako na faida ya watanzania wenzangu humu ndani,
1. Zitto kafungua NGO ya kitapeli Kigoma anamemuweka mbele mzazi wake kama mwenyekiti,yaani anatumia advantage ya maumbile (physical appearence) mama yake ili wafadhili wasaidie NGO yake(wapatwe na huzuni).
Kaka huu ndio ninaoita uzandiki. Sikatai uhusika wa Zitto katika kuanzishwa kwa ile NGOs lakini ni makosa kumshutumu Zitto kuwa amemtumia mama yake. Alichokifanya Zitto ambacho nategemea hata wewe unapaswa kufanya ni kutumia ujuzi wake alioupata kutokana na sacrifices ambazo mama yake alitoa kumfikisha hapo alipo, kumsaida mama yake na watu wengine kuanzisha na hata kuendeleza hiyo NGO. Lakini hiyo haiwezi kuwa ushahidi wa kum-demonize Zitto na mama yake.
2. ilikuwaje ukaunganisha jina langu na lake kwenye post yako huko nyuma? kwa tafsiri yako umesema kuwa, mswahili ni mtu ovyo ovyo au waislamu wasio na mipango ni watu ambao hawatakiwi wapuuzi hawana maana.
Kaka nadhani nilikuwa wazi kuhusu hilo kuwa nilifanya ili kukuchokonoa lakini vilevile kukuonyesha kuwa una mapungufu Fulani. Sijasema kuwa wewe ni hovyohovyo bali nilisema kuwa unavyobehave hapa unasaidia kuhalalisha prejudice za watu ambao wanapenda kunasabisha USWAHILI na tabia hovyohovyo na bahati mbaya mara nyingi katika jamii yetu tunapenda kujumuisha waswahili na waislam na uswahili na uislam.
3. tena umempinga Tanzania kwa kunifananisha na Es , ukasema ni kumshushia heshima mzee Es, kwani mswahili hadhi yangu ni ndogo sana kwenye jamii nakubali.
Kaka sijasema kuwa haddi yako ni ndogo kaka. Najitahidi sana kuepuka tabia ya kukejeli binadamu wenzangu (kama ufanyavyo wewe na mama Zitto) isipokuwa nilikuwa natofautisha aina ya michango yako hapa na michango ya Mzee Es. Kama unavyojua pale nionapo Mzee Es anakosea huwa sikosi kumkosoa kama nifanyavyo kwako hapa lakini huwa najitahidi kuwa ukusoaji wangu uwe unalenga kujenga zaidi ya kubomoa. Na hiyo ndio principle ninayojitahidi kuijenga katika maisha yangu kaka.
4. Sakata la Nssf kuhusisha waislam si mahala pake jee sheikh Khalifa hamisi ni padri? huyo ndio alikuwa kwenye mstari wa mbele akiwa na Mzee Mengi kumpinga Manji na upande wa manji kulikuwa na sheikh Basaleh. sikuona Dau kuhusika na waislamu labda wewe umeamua tu kumtoa Dau kafara (kaka yako) kama ambavyo Zitto Kabwe, anayefurahi kumuona mama yake yuko hali ile ili mambo yake yawe muswanu kwa wajerumani.
Kaka please sio mimi niliyemtoa kafara Dr DAU ila michango kama yako katika ule mjadala ndio kwa maoni yangu imekuwa ikihalalisha prejudice zilizotuzunguka katika jamii yetu kwa kila mtu kujiona yeye ndiye mstaarabu na wengine ni hovyohovyo. Kaka I was born, raised, grow up and up to know I am surviving in that dreadful environment so I know how painful and destructive it is for our country kaka. But siamini kama approach yako inajenga bali naona inazidi kubomoa. Na katika mjadala ule nadhani kuwa ilimbomoa Dr DAU zaidi ya kumjenga. Huhitaji kuwa political psychologist kugundua hilo. Na kama wajerumani wametambua umuhimu wa Zitto katika siasa zetu na za afrika kwa ujumla sio kwa sababu ya maumbile ya mama yake bali kwa sabau ya sacrifice alizotoa mama yake kumjenga Zitto na hawa wengine kumuona na kutoa michango yao pia.
5. ukiendelea nitatoa zile PM unazonitumia za kinafiki ili wanabodi wakujue wewe mnafiki kiasi gani. tena kanzu hii uliyovaa inakufaaa sana wachache tunaokujua kama umebadilisha kanzu.
Kaka kama kuna vitu ambavyo siviogopi ni kutoa mawazo yangu. Na kama nilivyosema hapo nyuma mimi siamini tabia ya kujifichaficha lakini ktumia jina la Tanzanianjema ambalo kwangu ni zaidi ya codename tu ni kuheshimu protocola za JF. Nilikutumia PM nikiamini wewe kama mswahili bado una hekima, stara na ustaarabu wa kutambua nini maana ya uungwana lakini nasikitika kuwa unachofanya nini tofauti na fikira zangu. Kama unajisikia kutowa hizo PM ambazo nilikutumia mwanzoni na kama protocol za JF zinaruhusu kutowa toa kaka. Lakini ukumbuke kutoa mlolongo mzima ikiwemo response zako. Na kama utashindwa na administrator wataruhusu mimi niko tayari kukusadia kuzitoa.
6. 1-tulileta fact kuwa Zitto kafukuzwa chuo Zanzibar wakajichanganya mmoja anasema alinyimwa scholarship, Mkumbo naye anasema kulikuwa Zanzibar university hakuna debate nyingi. Kweli mtu kashamaliza mwaka ataacha chuo kuhamia kingine akaanze upya mwaka wa kwanza sababu tu kule anakotoka hakuna midahalo mingi?. Jamani huu ni uongo,ina maana chadema hawajui thamani ya muda? na kama kule alitumia scholarship ya mwaka wa kwanza haoni kama ameharibu pesa za watu?
Kaka i wish kulikoa na anything to call facts. Lakini hivi kweli unaweza kuhoji uamuzi wa mtu kuhamia UDSM hata baada ya mwaka mmoja kutoka katika Zanzibar University kule Tunguu. Ina maana wewe hujui mapungufu makubwa ya kiutendaji yaliyopo pale Tunguu haswa kutokana na ule mkono wa wale wafadhili wake. Ina maana hujui matatizo ya scholarship za wale jamaa wa kutoka Sudan katika chuo hiki? Hivi kweli kwa dhati kabisa unaweza kulinganisha debate za UDSM na Zanzibar University? Ina maana kama mwanao atataka kufanya hivyo kuhama Zanzibar Univeristy kwenda UDSM utamkataza? Kati ya kupoteza muda na kufuata wingi wa maarifa nini kipaumbelea kwako? Unataka kila mtu akimbilie kupata bora degree na sio degree bora halafu kesho uje lalamika kuhusu utendaji wa watu ambao hawakuwa na guts za kutumia muda na fedha nyingi ili mradi wapate elimu iliyobora na yenye kuongeza maarifa kuliko just a degree? Si wewe ndiye uliyemrecognise Kitila kumshauri Mbowe kwenda kukaa darasani? Hapo ulikuwa hauoni suala la kupoteza muda na fedha? Ama ni huu urithi tuliochiwa na wakoloni wa DEVIDE AND RULE ndio ilikupelekea kurecognise huwo mchango wa Kitila
7. Kichuguu akaleta hoja lemavu (samahani Zitto zijalenga kwako nimekosa neno mbadala ndio nitatumia neno hilo)kuwa Udsm hawapokei waliofukuzwa, jibu Zitto alianza upya haku mention kama alisoma ZNZ. alidanganya kuwa ni form six tu.
Kaka mswahili jaribu kutafuta data kwanza kabla ya kutoa hoja. UDSM haipokea mtu aliyekuwa discontinued kutoka chuo kingine ama hata palepale mpaka huyo mtu atimize miaka miwili baada ya kuwa discontinued. Na kama suala la kufukuzwa mbona Zitto ana shahada ya umahiri wa kufukuzwa na sio mlimani tu na hata katika elimu yake ya sekondari. Na wewe ukiwa kama jamaa yake ama ulikuwa na mahusiano ya kifamilia naye hapo nyuma ulipaswa kujua kuwa mara zote hizi Zitto amefukuzwa kutokana ama na misimamo yake ama nafasi yake kama kiongozi kusimamia kile anachoamini ni haki za waezake.
8. Option ya sasa ni kuja na udini hii ameiweka wazi Kichuguu kule kwenye silencing MP, na Tanzania Njema kaiweka juu.lengo kutugombanisha waTanzania. mimi nina marafiki zangu humu si waislam lakini tunakubaliana na kupeana hoja mbali mbali kwa heshima.
Kaka lengo langu sio kuwagombanisha watanzania bali kuwa tayari kutambua mapungufu yetu na kwako wewe kutambua mapungufu yako katika uchangiaji wako humu. Uchangiaji ambao naamini kuwa mara nyingi umekuwa sio mzuri kwa jamii yetu. Ni muhimu kucritisize mambo lakini tunapanswa kuwa responsible na criticism zetu na tuwe tunalenga kujenga na sio kubomoa jamii yetu. Zaidi mimi naamini umuhimu wa self criticism na ndio maana nilitolea mifano hiyo nikijua kuwa utaweza kuitumia kujiangalia wewe mwenyewe na kutambua mapungufu yako badala ya kujaribu kutumia mapungufu yaw engine kujipa moyo kuwa wewe uko safi. Kuhusu Dr DAU kama nilivyowahi kusema hapo mwanzoni naamini kuwa yeye binafsi hana hatia na kuna ushahidi wa kimaandishi ni jinsi gani aliyokuwa akipinga ule uozo wa Manji na juhudi zipi alizochukua hadi ile safari yake kule
..ambako aliishia kuvunjwa moyo namtu aliyemtegemea kuzui huo unyangau
9. sasa huo udini uko wapi? Inajulikana nyinyi nguvu zenu si Zitto bali kutetea reputation ya chama chenu. jamani kama siasa mmeshindwa fanyeni shughuli nyingine.
Kaka jitahidi kujipusha na hii sumu mbaya kuwa kila mtu anayekosoa matendo ya chama tawala ama anamtetea mtu tunatakiwa na wenye nchi kumuojna kama mpinzani basi naye mpinzani. Hiyo ni sumu kali ya kisiasa katika jamii yetu ambayo kwa maoni yangu ni moja ya sababu za zinazodumaza ujenzi wa demokrasia makini katika nchi yetu. Nilishaweka wazi kuwa Zitto ni mtu wangu wa karibu sana na nathamini mchango wake katika kujenga upinzani makini lakini sio kuwa nafunga macho pale ambapo naona yeye binafsi anaharibu ama wao kama taasisi wanaharibu. Lakini hilo halinifanyi mimi kuwa mwana CHADEMA, changanua hoja zangu lakini usikimbile kunihusihsa na makundi ambayo mimi sina mahusiano nayo. Labda kama unataka kusema kila mtu aliye na muono tofauti na ule wa Tanzania ni CCM na CCM ni Tanzania ni mwana CHADEMA.
Asalam Aleykum kaka
.
Tanzanianjema
Tanzania Njema.
Imebidi nije kukujibu kwanza kabla ya kwenda kulipa kiporo kwa mkuu wako kule kwenye Taifa stars.
1.Kuhusu NGO ya Zitto Kabwe umejaribu kudanganya umma kama unavyozidi kutuvuruga, suala la zitto kuwa na NGO si tatizo aweke wazi, lakini wanakuja wafadhili huweki wazi, kwao unawaambia hapa kuna mama mmoja ana hali fulani ana NGO yake na wenzake, nimeifuatilia naona wako makini naomba muwasaidie huo ndio ulaghai au utapeli, wale wanasaidia wakijua wanasaidia watu baki kwa recommendation ya Mbunge Zitto.
kumbe wanamsaidia mama Zitto na Zito mwenyewe.Anamtumia Mama yake kama chambo cha kupata misaada ya NGO yake.Mheshimiwa umewahi kusikia Celtel au BP wanaanzisha mashindano na kuweka bayana mtu mwenye ndugu kwenye shirika hili asishiriki.
2. Unasema kuna prejudice za watu ambao wanapenda kunasabisha uswahili na tabia ovyo ovyo na bahati mbaya mara nyingi tunapenda kujumuisha waswahili na waislamu au uswahili na uislam,maneno yako hayana mantiki unafanya nini huko au unapoteza pesa za watu tu?
naomba nikuulize Tanzania Njema watu kama Charles Hilal, Rupia. Isack sepetu, Jaji Augustino Ramadhan, Tido Mhando, Charles Boniface, Peter Tino,stephen Nemes Masajage,Kingunge Ngombare,professor Penina Mlama n.k si waswahili?ni waswahili zaidi ya Zitto kabwe au Shaibu Akwilombe,na tafsiri hiyo uliyoitoa hapo juu kuwa uswahili ni uislam sijaiona kwenye kamusi yeyote ya kiswahili labda iwe Zito katoa kamusi yake ambayo mimi sijaiona.
3- unasema nina tabia ya ajabu ya kukejeli watu kama mama ziito. Mimi sijamkeli mama zitto, nimekuwa nikilalamikia tabia yake chafu ambayo haina mahusiano na maumbile, wewe unasema uko karibu sana na Zito basi utayajua yafuatayo 1992 mwezi may mama huyu alimlaghai mtu alichukua pesa zake akijifanya ni wakala wa tiketi za ndege kesi husika ni tiketi ya kwenda Syria.
kuna kesi nyingine ya huyu mama na Karim Immu mwalimu wa shule ya gongoni Tabora, hii 1993. na buguruni Polisi ndio kwenye mafaili mengi ya huyu mama.
au unataka kutake advantage ya hali yake ili awe anawakosea watu na kutumia kinga ya maumbile yake? tukimwambia awe anasema mnanionea kwa ajili ya maumbile yangu?.
Zitto muulize zaidi yeye hakulelewa na huyu Mama, kwani alimuacha Kigoma na yeye kuja Dar kufanya ujanja wake. kusingizia kuwa mama huyu aliteseka sana kumlea Zitto, sio kweli labda matezo ya kubeba ujauzito. malezi mengine hakumlea, alikuwa kama kuku wa kienyeji mara mama mkubwa bi Kabwe, mara kwa bibi, mara kwa kina Lihei hayo ndio malezi ya Zitto.
4-Es amewahi kuandika thread yenye Maudhui Nyerere na Lucy Lameck, jee Tanzania njema maneno yaliyokuwa mle ni mepesi? hadi jinsi walivyokuwa kwenye faragha aliweka Es, kumbuka aliyeandikwa ni baba yetu wa taifa na adm aliiondoa.mimi sijafika huko. sijawahi kusema Mama Zito anafanya nini kitandani na siwezi. sijui umetumia mizani gani kunihukumu baina yangu na Es.
lakini itakavyokuwa Es ni mtu wangu huwezi kutugombanisha. zaidi sijaja kushindana hapa bali kuweka wazi uovo ndani jamii. nakuomba unifanye wa mwisho katika league table yako kwenye hii forum muhimu kwangu watu wajue nini kinaendelea.
5- umedai nilimbomoa DR.DAU,naomba ujue mimi sina mkataba nae hapa wa kumjenga. na mimi kama mswahili sina uwezo wa kumjenga mtu, nadhani kama yeye au yeyote si msomi na mchapa kazi asitegee mswahili atamjenga, mtu anajijenga kwa utendaji wake si michango ya mswahili au Tanzania njema humu. na umezidi kusema kuwa naboa jamii jeee Zito na tabia zake chafu anajenga jamii?na kama nilimboa Dau kwani Kittlya,Mbowe na Zitto nawajenga? ndugu Tn huo si ndio upendeleo? samahani siko hapa kumfanyia mtu kazi.
6-unasema unaomba ruksa kwa Adm ili uweke PM. SWALI Zitto aliomba ruhusa kwa mfanya kazi wake nakuweka mkataba wao wa kazi na mshahara hapa jambo forum? kuwa anamlipa laki tano. yaani hana hata siri za kazi au sheria za kazi. mkataba wa wao wawili kaja kuuweka hapa wa nini? unasema protocol haziruhusu. kwenye mshahara wa msaidizi ziliruhusu? tuache kudanganyana.
7- umesema Zanzibar University kulikuwa na mapungufu ya utendaji. hii ni sababu ya tatu ya wewe kwenda Udsm, swali ulipokuwa unaendaa Znz ulikuwa hujui position ya chuo hadi ulipoenda kwenye mdahalo? jee tukuamini wewe, Kitila au Bi sent 50 ambao nao walikuja na sababu tofauti?. unasema huwezi kulinganisha Znz university na Udsm. mimi nakulinganisha na wanafunzi uliOkuwa nao intake moja Znz university.
nataja wafutao ABDALLAH anafanya phd Birmingham university U.K na ni lecturer IFM, Fatma Khalfan ni Lecturer wa sheria baada ya kushinda scholarship ya jumuia ya madola na hizo nafasi zilikuwa 2 kwa nchi nzima amefanya masters yake Warwick university U.K kati ya vyuo mahiri duniani kwenye fani ya sheria, Mariam Karama huyu ameshinda zawadi kwa kufanya vizuri master yake U,K na amepata CPA. hao ilikuwa umalize nao Znz kama ni mapungufu uliyosema wenzako wamepita na kufanya vizuri, wapo wengi ila nakuonesha kuwa Zitto ni muongo.ama kweli mchagua jembe si mkulima.
chuo ulichofanya Ujerumani hakina thamani yeyote na huwezi kujilinganisha na hao niliowataja hapo juu.tena Zitto ulipokuwa Ujerumani ulikuwa unasaidiwa na binti Lwamo. huko siendi kwa sasa ila nakuonesha kuwa nakujua kama shilingi.
na kusema Udsm kuna midahalo (debate) jee kuna digrii ya debate?
Unajigamba kuwa ulikuwa ukisimamishwa shule nyingi tu, hiyo ni kuonesha kuwa makuzi yako ya utoto yaliathiri hadi tabia yako shuleni, pole si sifa njema hii.
8.Hapa umefanya U-TURN na kusema kuwa Dau hauhusiki hata chembe na kashfa ya Manji,jee ni nani aliyeka post huko nyuma na kuuliza vipi kaka Dau na mamilioni yaliyopotea NSSF? juzi umepost maelezo hayo,leo unasema maneno mengine kabisa au ni kuchanganyikiwa na ugoni? mizimu ya Mpakanjia imeanza kukupotezea kumbukumbu?
9- umesema niwe tayari kukubali mapungufu yangu. jee Zitto yuko tayari kuja kueleza mapungufu yake? au kazi yako kuoneshea wenzio vidole tu?
10- umemalizia kwa kunihusia nisikimbilie kukuhusisha na makundi ambayo huna mahusiano nayo. vipi uliwahusisha waislam na uswahili wangu? vipi ulimuhusisha unaye dai kaka yako Dau na mswahili? vipi ulihusisha jina langu na uovyo ovyo? na ukasema si kila anayepinga pinga au kukosoa ni mpinzani, jee mbona umsema kila mswahili ni muislam? acha hizo tupo macho tunawamulika!