Wandwi amshushua Dk Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wandwi amshushua Dk Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kishongo, Nov 8, 2010.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]ALIYEKUWA mgombea wa ubunge Jimbo la MusomaNMjini, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mustafa Wandwi, amemtaka aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa, kuacha kuzungumza mambo ya kuambiwa bali awe na ushahidi wa kutosha.

  Pia amesifia uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu kwamba ulikuwa wa haki na huru zaidi.

  Akizungumza na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki, alisema kuwa mgombea huyo wa Chadema amekuwa akizungumza mambo ambayo hakuyachambua kwa kina kama kweli yana ukweli wowote na yana madhara gani kwa jamii.

  Alisema kitendo alichokionesha Dk. Slaa cha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, sio cha kiungwana kwa kiongozi mkubwa kama yeye ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kubwa ya
  nchi.

  "Dk. Slaa ana matatizo makubwa ambayo inabidi ajifunze na aache kutumia muda wake kusikiliza mambo ya kuambiwa na kuyaamini, kiongozi mkubwa kama yeye lazima awe na subira na kuyachambua kwa kina yale anayoambiwa kabla ya kuyasema," alisema na kuongeza:

  "Mfano kipindi cha kampeni, wakati ule maboksi na karatasi za kupigia kura yakiletwa nchini, alisema kuwa kuna kontena limeingizwa mkoani Mbeya likitokea Afrika ya Kusini likiwa na kura za wizi.

  “Serikali ilipofuatilia walikuta ni vipodozi, aache kudanganywa na watu wake wa karibu uongo ni adui mkubwa wa nchi yetu ".

  Alisema kuwa kasoro ambazo Dk. Slaa amekuwa akizisema kwa baadhi ya majimbo kuwa maofisa wa usalama waliongia kwenye vituo vya kupigia kura, ni kasoro za kibinaadamu lakini hazikuwa na lengo ya kubadilisha matokeo kwa kuiba kura kama alivyosema mgombea huyo.

  "Kasoro ambazo anazisema Dk. Slaa ni za kawaida lakini kama ingekuwa suala hilo lingetokea nchi mzima basi tungesema CCM ameiba kura lakini kitu kingine ambacho Dk. Slaa anashindwa
  kujua ni kuamini wakati wa kampeni zake, watu waliokuwa wanajaa kuwa ni kura halisi.

  "Kuna wengine tangu wamezaliwa hawajawahi kuiona helkopta kwa kuwa kampeni za kutumia ndege ni chache katika nchi yetu na Bara letu la Afrika pia wengine walikuwa wanahudhuria lakini hawakujiandikisha kupiga kura kura,"alisema.

  Alisema kuwa Dk. Slaa ameshindwa kujua kuwa kampeni zake zilijikita zaidi mjini ambapo wapiga kura ni asilimia 20 ikilinganishwa na asilimia 80 ya wapiga kura wengi ambao
  wapo vijijini.

  "Yeye amesafiri na kufanya kampeni kwa ndege, hakupita vijijini na kuona wapiga kura wake pia mtandao wa Chadema sio mkubwa nchini kama wa CCM na CUF ambao wagombea wao walitumia magari kuwafikia wananchi walio wengi vijijini, “ alisema.

  Wandwi alikiri kuwa vijana wameamua kupiga kura na kuwachagua vijana wenzao kwa maana hiyo hana mpango tena kugombea nafasi hiyo mwaka 2015 kwa kuwa sasa wananchi wanahitaji viongozi vijana ambao wanaamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia.[/FONT]
   
 2. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Rest In Peace Kamanda Mstaafu. This time jamaa wa musoma wame-ku do kweli. Kura ngapi vile uliambulia?? sio 200 vile??? Pole saana, Ndio maana sishangai wewe kuyasema hayo unayoyasema dhidi ya Dr Slaa.
   
 3. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hayo ni maneno ya wafa maji cuf,washaolewa na ccm na kilichobaki ni kupigwa mimba tu wazalishwe mapacha
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wandwi needs to be polite and appreciate slaa's power, hii ya kutafuta u-DC kwa namna hii ngumu bana
   
 5. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Anatafuta kaumaarufu kwamba alikuwepo au alitoa maoni..ni haki yake!
   
 6. M

  Membensamba Senior Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wandwi nakushauri usitafute cheap popularity. Anything cheap is expensive.
   
 7. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haswa tena wameolewa ndoa ya mkeka, nahuyo wa msoma asitafute u supe star kwa jina la Dr Slaa.
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  :rip:
   
 9. F

  Ferds JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Good views bt not credible and unreliable
   
 10. T

  Tanzania Senior Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Who is Wandwi?
   
 11. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mie nasubiri chama kipya kitakachotokana na muungano wa CCM na CUF, maana tayari washa ungana hawa. Hakuna asiyetambua mchango wa Dr. Slaa (Phd) ukombozi wa Taifa hili mikononi mwa CCM.

  Ukimsikiliza Wandwi nawe utakua kama yeye. Dr. Slaa ni mtu makini, mwelewa mzalendo wa kweli na mpiganaji asiyeogopa.
   
 12. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #12
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Slaa sio saizi yake anyamaze kimya
   
 13. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #13
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu ni ccm au???
   
 14. W

  We can JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haichukui hata sekunde kujua mawazo yaliyokufa na yaliyo hai. Zama za kuamininika kwa maneno bila vitendo zilishaisha. No research, no right to say!
   
 15. Nyahende Thomas

  Nyahende Thomas Verified User

  #15
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  subutuuuuu....., nani ampe hiyo kitu? hata kama wamefunga ndoa ya mkeka na ccm hawezi pata hata ukatibu tarafa.
   
 16. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mwenzie mahita alisisitiza watu wakipiga kura wakalale nyumbani.......!!!
  lengo ilikuwa wakiiba kura zetu tusiwaone kisa tunataka amani.....na hili neno inabidi tuangalie upya kwenye kamusi maana watu wanalimisuse sana....amechapwa viboko na Vincent Kiboko Nyerere anakuja kumchafua Dr Slaa,yeye angeongea yahusuyo ubunge na siyo urais...
  naona anajihami ili akirudi ccm kuomba msaada kama dc msaafu anayeumwa asitoswe. serkali ya ccm ni kama shetani,shetani anakuintertain kwa muda fulani halafu anakuacha muda ambao hata hukutegemea na unaaibika kwelikweli. woote wanaoishangilia ccm leo watalia kila mtu kwa melody yake muda wake ukifika. si tumewaona akina Mangula and the likes??!! uovu ni uovu tu, lazima malipo yanayokusitahili uyapate tena hapaha duniani kabla ya moto wa milele.
   
 17. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  wandwi kama huna la kuongea ni bora ukachukue kopo ukachambe
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Who is Wandwi in TZ politics?
   
 19. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kweli Vakwavwe hili neno amani inabidi litazamwe matumizi yake kwa sasa, maana sisiemu wamegeuza mtaji.

  Pia swala la JK kuimba udini kila siku na ukabila, binafsi sielewi maana yake, maana naona huyu jamaa anapotoka.

  Mungu awalaani sisiemu na vizazi vyao vyote kwa kutufanya watanzania masikini. Naamini atasikia maombi yangu.
   
 20. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,591
  Likes Received: 4,699
  Trophy Points: 280
  We mzee Wandwi kwani bila kujipendekeza kwa fisadi Kikwete huwezi kuishi? Wacheni wivu nyie Dr Slaa yuko sahihi kulalamika kwani haki haikutendeka, nyie ndiyo mnafanya vyama kama CUF na TLP vionekane kuwa ni CCM-B. Wacheni hizo mnajidharaulisha.
   
Loading...