Wandwi amshushua Dk Slaa

Kishongo

JF-Expert Member
May 4, 2010
932
64
ALIYEKUWA mgombea wa ubunge Jimbo la MusomaNMjini, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mustafa Wandwi, amemtaka aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa, kuacha kuzungumza mambo ya kuambiwa bali awe na ushahidi wa kutosha.

Pia amesifia uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu kwamba ulikuwa wa haki na huru zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki, alisema kuwa mgombea huyo wa Chadema amekuwa akizungumza mambo ambayo hakuyachambua kwa kina kama kweli yana ukweli wowote na yana madhara gani kwa jamii.

Alisema kitendo alichokionesha Dk. Slaa cha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, sio cha kiungwana kwa kiongozi mkubwa kama yeye ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kubwa ya
nchi.

"Dk. Slaa ana matatizo makubwa ambayo inabidi ajifunze na aache kutumia muda wake kusikiliza mambo ya kuambiwa na kuyaamini, kiongozi mkubwa kama yeye lazima awe na subira na kuyachambua kwa kina yale anayoambiwa kabla ya kuyasema," alisema na kuongeza:

"Mfano kipindi cha kampeni, wakati ule maboksi na karatasi za kupigia kura yakiletwa nchini, alisema kuwa kuna kontena limeingizwa mkoani Mbeya likitokea Afrika ya Kusini likiwa na kura za wizi.

“Serikali ilipofuatilia walikuta ni vipodozi, aache kudanganywa na watu wake wa karibu uongo ni adui mkubwa wa nchi yetu ".

Alisema kuwa kasoro ambazo Dk. Slaa amekuwa akizisema kwa baadhi ya majimbo kuwa maofisa wa usalama waliongia kwenye vituo vya kupigia kura, ni kasoro za kibinaadamu lakini hazikuwa na lengo ya kubadilisha matokeo kwa kuiba kura kama alivyosema mgombea huyo.

"Kasoro ambazo anazisema Dk. Slaa ni za kawaida lakini kama ingekuwa suala hilo lingetokea nchi mzima basi tungesema CCM ameiba kura lakini kitu kingine ambacho Dk. Slaa anashindwa
kujua ni kuamini wakati wa kampeni zake, watu waliokuwa wanajaa kuwa ni kura halisi.

"Kuna wengine tangu wamezaliwa hawajawahi kuiona helkopta kwa kuwa kampeni za kutumia ndege ni chache katika nchi yetu na Bara letu la Afrika pia wengine walikuwa wanahudhuria lakini hawakujiandikisha kupiga kura kura,"alisema.

Alisema kuwa Dk. Slaa ameshindwa kujua kuwa kampeni zake zilijikita zaidi mjini ambapo wapiga kura ni asilimia 20 ikilinganishwa na asilimia 80 ya wapiga kura wengi ambao
wapo vijijini.

"Yeye amesafiri na kufanya kampeni kwa ndege, hakupita vijijini na kuona wapiga kura wake pia mtandao wa Chadema sio mkubwa nchini kama wa CCM na CUF ambao wagombea wao walitumia magari kuwafikia wananchi walio wengi vijijini, “ alisema.

Wandwi alikiri kuwa vijana wameamua kupiga kura na kuwachagua vijana wenzao kwa maana hiyo hana mpango tena kugombea nafasi hiyo mwaka 2015 kwa kuwa sasa wananchi wanahitaji viongozi vijana ambao wanaamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia.
 
Rest In Peace Kamanda Mstaafu. This time jamaa wa musoma wame-ku do kweli. Kura ngapi vile uliambulia?? sio 200 vile??? Pole saana, Ndio maana sishangai wewe kuyasema hayo unayoyasema dhidi ya Dr Slaa.
 
Hayo ni maneno ya wafa maji cuf,washaolewa na ccm na kilichobaki ni kupigwa mimba tu wazalishwe mapacha
 
Wandwi needs to be polite and appreciate slaa's power, hii ya kutafuta u-DC kwa namna hii ngumu bana
 
Anatafuta kaumaarufu kwamba alikuwepo au alitoa maoni..ni haki yake!
 
Haswa tena wameolewa ndoa ya mkeka, nahuyo wa msoma asitafute u supe star kwa jina la Dr Slaa.
 
Mie nasubiri chama kipya kitakachotokana na muungano wa CCM na CUF, maana tayari washa ungana hawa. Hakuna asiyetambua mchango wa Dr. Slaa (Phd) ukombozi wa Taifa hili mikononi mwa CCM.

Ukimsikiliza Wandwi nawe utakua kama yeye. Dr. Slaa ni mtu makini, mwelewa mzalendo wa kweli na mpiganaji asiyeogopa.
 
Wandwi needs to be polite and appreciate slaa's power, hii ya kutafuta u-DC kwa namna hii ngumu bana

subutuuuuu....., nani ampe hiyo kitu? hata kama wamefunga ndoa ya mkeka na ccm hawezi pata hata ukatibu tarafa.
 
mwenzie mahita alisisitiza watu wakipiga kura wakalale nyumbani.......!!!
lengo ilikuwa wakiiba kura zetu tusiwaone kisa tunataka amani.....na hili neno inabidi tuangalie upya kwenye kamusi maana watu wanalimisuse sana....amechapwa viboko na Vincent Kiboko Nyerere anakuja kumchafua Dr Slaa,yeye angeongea yahusuyo ubunge na siyo urais...
naona anajihami ili akirudi ccm kuomba msaada kama dc msaafu anayeumwa asitoswe. serkali ya ccm ni kama shetani,shetani anakuintertain kwa muda fulani halafu anakuacha muda ambao hata hukutegemea na unaaibika kwelikweli. woote wanaoishangilia ccm leo watalia kila mtu kwa melody yake muda wake ukifika. si tumewaona akina Mangula and the likes??!! uovu ni uovu tu, lazima malipo yanayokusitahili uyapate tena hapaha duniani kabla ya moto wa milele.
 
ALIYEKUWA mgombea wa ubunge Jimbo la MusomaNMjini, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mustafa Wandwi, amemtaka aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa, kuacha kuzungumza mambo ya kuambiwa bali awe na ushahidi wa kutosha.

Who is Wandwi in TZ politics?
 
Kweli Vakwavwe hili neno amani inabidi litazamwe matumizi yake kwa sasa, maana sisiemu wamegeuza mtaji.

Pia swala la JK kuimba udini kila siku na ukabila, binafsi sielewi maana yake, maana naona huyu jamaa anapotoka.

Mungu awalaani sisiemu na vizazi vyao vyote kwa kutufanya watanzania masikini. Naamini atasikia maombi yangu.
 
We mzee Wandwi kwani bila kujipendekeza kwa fisadi Kikwete huwezi kuishi? Wacheni wivu nyie Dr Slaa yuko sahihi kulalamika kwani haki haikutendeka, nyie ndiyo mnafanya vyama kama CUF na TLP vionekane kuwa ni CCM-B. Wacheni hizo mnajidharaulisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom