Wandwi amshushua Dk Slaa

Ndo tatizo la wanajeshi wastaafu. popote walipo wanahesabika kama majeshi ya akiba.
sishangai yeye kuongea upupu huo.

Anasema uchaguzi ulikuwa wa haki na huru zaidi. huyu kweli ni wa kuhurumiwa.
cheap politician
 
Naomba kuwa na magazeti yanayotusaidia kupeleka comments za wan JF kwa yeyote anayeongea mambo kama haya. Imefika wakati wa kuelimishana bila kuogopana.
Inashangaza mtu kusema maneno ni ya kusikia, bila yeye kuthibitisha jinsi alivyokwenda kushuhudia yote aliyoyasema! Inasikitisha hadi leo nchi imegawanyika kati ya wapenda mabadiliko na wasiotaka mabadiliko kabisaa. Sasa inaeleweka wazi machafuko kwenye nchi husababishwa na kundi hili la watu wenye akili mgando, wanaosindikiza wenzao wachache kuishi maisha bora, kwao kila kitu ni sawa kikabakia na vile alivyokiacha babu yao. Hizi ni pumba za karne ya ishirini na moja.
 
Wandwi kama hio ndio gia ya kutafuta kazi sema tuu. Kuanzia wiki ijayo kuna kazi Dodoma ya kumchambisha Spika mpya wa Bunge Vijisent Chenge.
 
Anatafuta kaumaarufu kwamba alikuwepo au alitoa maoni..ni haki yake!

Mwacheni maana kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake hata kama hatutaki kuyasikia au kuyasoma, mawazo yake hayawezi kutunyima usingizi au kujadili mambo mengine ya msing na maendeleo kwa nchi yeu
 
ALIYEKUWA mgombea wa ubunge Jimbo la MusomaNMjini, kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Mustafa Wandwi, amemtaka aliyekuwa mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Dk. Wilbroad Slaa, kuacha kuzungumza mambo ya kuambiwa bali awe na ushahidi wa kutosha.

Pia amesifia uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu kwamba ulikuwa wa haki na huru zaidi.

Akizungumza na mwandishi wa habari mwishoni mwa wiki, alisema kuwa mgombea huyo wa Chadema amekuwa akizungumza mambo ambayo hakuyachambua kwa kina kama kweli yana ukweli wowote na yana madhara gani kwa jamii.

Alisema kitendo alichokionesha Dk. Slaa cha kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu, sio cha kiungwana kwa kiongozi mkubwa kama yeye ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kubwa ya
nchi.

"Dk. Slaa ana matatizo makubwa ambayo inabidi ajifunze na aache kutumia muda wake kusikiliza mambo ya kuambiwa na kuyaamini, kiongozi mkubwa kama yeye lazima awe na subira na kuyachambua kwa kina yale anayoambiwa kabla ya kuyasema," alisema na kuongeza:

"Mfano kipindi cha kampeni, wakati ule maboksi na karatasi za kupigia kura yakiletwa nchini, alisema kuwa kuna kontena limeingizwa mkoani Mbeya likitokea Afrika ya Kusini likiwa na kura za wizi.

“Serikali ilipofuatilia walikuta ni vipodozi, aache kudanganywa na watu wake wa karibu uongo ni adui mkubwa wa nchi yetu ".

Alisema kuwa kasoro ambazo Dk. Slaa amekuwa akizisema kwa baadhi ya majimbo kuwa maofisa wa usalama waliongia kwenye vituo vya kupigia kura, ni kasoro za kibinaadamu lakini hazikuwa na lengo ya kubadilisha matokeo kwa kuiba kura kama alivyosema mgombea huyo.

"Kasoro ambazo anazisema Dk. Slaa ni za kawaida lakini kama ingekuwa suala hilo lingetokea nchi mzima basi tungesema CCM ameiba kura lakini kitu kingine ambacho Dk. Slaa anashindwa
kujua ni kuamini wakati wa kampeni zake, watu waliokuwa wanajaa kuwa ni kura halisi.

"Kuna wengine tangu wamezaliwa hawajawahi kuiona helkopta kwa kuwa kampeni za kutumia ndege ni chache katika nchi yetu na Bara letu la Afrika pia wengine walikuwa wanahudhuria lakini hawakujiandikisha kupiga kura kura,"alisema.

Alisema kuwa Dk. Slaa ameshindwa kujua kuwa kampeni zake zilijikita zaidi mjini ambapo wapiga kura ni asilimia 20 ikilinganishwa na asilimia 80 ya wapiga kura wengi ambao
wapo vijijini.

"Yeye amesafiri na kufanya kampeni kwa ndege, hakupita vijijini na kuona wapiga kura wake pia mtandao wa Chadema sio mkubwa nchini kama wa CCM na CUF ambao wagombea wao walitumia magari kuwafikia wananchi walio wengi vijijini, “ alisema.

Wandwi alikiri kuwa vijana wameamua kupiga kura na kuwachagua vijana wenzao kwa maana hiyo hana mpango tena kugombea nafasi hiyo mwaka 2015 kwa kuwa sasa wananchi wanahitaji viongozi vijana ambao wanaamini kuwa wana uwezo mkubwa wa kuwatumikia.
This is a quote from the man who held very sensitive positions in previous governments including the post of a Regional Police Commander! Sijui alikuwa anawaongoza vipi maaskari wake kwa jinsi alivyoonyesha poor reasoning hapa.
Ndiyo maana amepoteza kabisa mvuto hadi kufaulu kuwashawishi wapiga kura 253 tu dhidi ya wenzake waliopigiwa kura kwa makumi ya maelfu. Kinyume na mawazo hasi ya Afisa Mstaafu huyu, matumizi ya Helikopta yaliwasaidia sana wagombea kuwafikia wapiga kura wengi na bila shaka kuongeza idadi ya kura walizopata. Si kweli hata kidogo kwamba eti CCM walitumia magari tu, bali ninavyofahamu ni kwamba CCM walitumia Helikopta si moja tu, bali tatu na ndege moja kwa mgombea wao na CHADEMA moja iliyowasaidia kufika mpaka vijijini. Wandwi anajikomba CCM kuwa eti uchaguzi wa safari hii ulikuwa safi na kwamba kasoro zilizotokea zilikuwa za kawaida! Kuzagaa kwa karatasi za kupigia kura hadi majalalani, watu binafsi kukamatwa na malundo ya karatasi zilizokwisha wekwa alama za ndiyo kwa CCM, baadhi ya watu kugundulika wakiwa wamegawiwa karatasi za kupigia kura tatu tatu, ucheleweshaji wa makusudi wa matokeo kwa madhumuni ya "kuchakachua" kura za wapinzani na kuongeza kura "hewa" kwa CCM na ubadilishaji wa takwimu zilizokuwa zikisomwa na Tume kwa ajili ya matokeo ya kura za u-rais vyote hivyo ni kasoro za kawaida?
Wandwi kwa upeo wa kufikiri uliouonyesha una uwezo finyu kabisa wa kuweza kuzikosoa hoja za Dr. Slaa, mbinu alizotumia kufanya kampeni na hata jinsi alivyobaini kuibiwa kura zake halali. Labda unajipendekeza ukiwa na matumaini ya kuokota makombo ya mafisadi hawa, ninachotaka kukuhakikishia ni kwamba CCM si wajinga kiasi hicho kwa maana wanafahamu fika kuwa wewe ni jeshi lililokwisha tumika (spent force) na hawana cha kuwashawishi kukupandia dau kama walivyofanya kwa wenzio kina Tambwe, Nsanzugwanko, Kaburu, Akwilombe na utitiri waliopandiwa dau na ambao polepole wengi wao wanaachwa solemba.
 
rip mustafa wandwi!!na ubunge wa musoma huupati ng'oo,akitoka vincent nyerere nachukua mimi!!!utausikia kwenye bomba tu!
 
Mi naona wandwi ameshindwa kupata kile alichokuwa anakitafuta alipokuwa upinzani sasa anataka kurudi ccm!!!rudi ccm wandwi,ulisha-expire!!!
 
Back
Top Bottom