Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,559
- 860,711
HOFU ni kitu kibaya mno.. Hofu inaua hofu huleta woga, woga huzaa wasiwasi, wasiswasi huleta mashaka na mashaka huzaa mishtuko hata ukisikia yai limevunjika utajua tayari wamefika... Mwisho wa siku unaumba lijitu linalotisha sana
Litakutisha ukitaka kula litakwambia pengine wameshakuwekea sumu
Litakutisha ukitaka kulala
Litakutisha ukiota ndoto
Litakutisha simu ikiita
Litakutisha ukitaka kuangalia habari ama kutazama taarifa mbalimbali mitandaoni
Ukitaka kutoka kwako utajistukia kuhusu gari yako, litakwambia hata hii wanaijua
Nje ya geti lako ama karibu na hapo ukiona mtu kasimama ama gari imepaki litakwambia wanakufuatilia.. Unakosa amani moyoni na unakosa imani hata kwa mtu wako wa karibu kabisa
Nina mifano miwili ya HOFU
Mzee wangu Nanaila Kiula..! Sijui yuko wapi sasa
Wakati wa awamu ya rais Alhasani Mwinyi alikuwa waziri wa ujenzi.. Ikatokea tenda ya kujenga/kuboresha barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo nadhani mpaka Moro na Chalinze mpaka Segera hivi (kumbu kumbu zinanipotea)
Kwenye ujenzi ule ukafanyika ufisadi nadhani ndio ufisadi mkubwa wa kwanza wa ujenzi kufanyika.. Barabaraba ile ikafinywa kila upande nusu mita.. Kwa ukubwa wa ule mradi hayo yalikuwa ni mabilioni ya pesa
Alipoingia Mkapa alianza na akina Kiula na wenzake.. Wakakamatwa na kupandishwa kizimbani.. Kesi ilienda kwa muda mrefu sana sina kumbukumbu sahihi kama Kiula alishinda ile kesi ama aliachiwa tuu.. Lakini baada ya hapo aliishi maisha ya hofu kubwa.. Akawa ni mtu wa kujistukia na kumkimbia kila mtu..!
Mano wa pili
Awamu ya nne kuna watu walipiga pesa ndefu sana kwa njia za mkato.. Jamaa yetu mmoja alikuwa ndio mbebaji kwenye moja ya ishu za upigaji.. Yeye ndio alikuwa anatumwa kuchukua na kugawa kwa wahusika
Baadae wahusika wakaanza kuskamatwa mmoja baada ya mwingine.. Huyu jamaa yetu naye alikuwa kapiga ndefu sana akawa na mali nyingi tu hapa mjini.. Sasa aliposikia washika dau wameanza kunaswa akaanza kuishi kama digidigi, akawa kazitawanya gari zake maeneo mbali mbali ya mji hivyo safari moja ya Gongo la mboto anaweza,kubadili magari mara mbili, kulala kwake ilikuwa kuanzia saa nane usiku na alikuwa ni mtu wa vibar vya vichochotoni kwenye giza
Kuna mtu ameshathibitisha hofu yake..ameshindwa kuficha hisia kaamua kuongea.. Anatafuta huruma lakini pia kujivua lawana nakuonesha anaonewa.. Amajitabiria yajayo..HII NI HOFU ILIYOMJAA..
Hofu na woga vilivyotamalaki na asijue kwa hakika ni nani hasa atammaliza.. Anataja makundi ya watenda maovu kama ndio wanaomtafuta... Lakini anasahau makundi ya aliowaumiza na kuwatendea vibaya.. Ambao hawakuweza hata kujitetea mbele yake..
Wahudumu wa chumba cha wafu wengi huwa walevi mbwa na kama wamedata hivi.. Sio kosa lao ni zile sura za wafu kule mochwari na yale yote yanayotokea kule huwafanya muda wote watake kutoa lock ili akili isiyawaze
Hakuna jambo baya kama kudhulumu uumbaji
Hakuna jambo baya kama kumwaga damu isiyo na hatia
Hakuna jambo baya kama kutesa na kutia kilema uumbaji wa Mungu
Hakuna jambo baya kama kudhulumu mali isiyo yako..
Ni mengi ya kuandika...
Kila jambo huwa na wakati wake... Kila ubaya una malipo yake. Na malipo yake si lazima yatokane na hao uliowatendea mabaya..kuna kitu kinaitwa karma! Haiongopi haikopeshi
Kwa jinsi alivyokuwa kajipenyeza na kuingia mpaka juu na ndani kabisa na 'kuaminiwa' kufanya mengi ni wazi wanajua anajua mengi.. Hawana haraka naye.. Ni mwendo wa timing.. Na kutiwa hofu. Wanajua wakijaribu..atamwaga mboga
Kilichopo ni kumpa hofu kila mahali.. Mwisho hofu ndio inakuwa kitanzi chake.. Soft killing...!
View attachment 2184692