Wanawake zamani VS. Wanawake Sasa

Wanawake zamani VS. Wanawake Sasa

1. Zamani : Mwanamke anakutana na mwanaume kakonda hana mwili, kimoyomoyo " huyu mwanaume hana mtu anayemtunza hadi ana dhoofu afya nipambane niolewe nae nimtunze hadi apendeze"

Sasa : Mmmmhmn MUNGU aniepushe na hiki kikombe, mtu kakondeana kama mti wa dawa afu anajiamini kunitongoza, usikute ana ngoma,hebu ukoo"

2. Zamani: Mwanamke anakutana na mwanaume miaka 30 bachelor hana hata mtoto. "MUNGU kajibu maombi yangu kanipa wa kwangu wa kujehga nae familia from scratch"

Sasa : Mmmmhmn huyu atakuwa ni muhuni,ogopa mwanaume ambaye hajazaa na mtu na hana hata mtoto wa kusingiziwa. Mimi hapana kwakweli ni bora niendelee kuwa single kuliko mtu wa hivi"

3. Zamani: Mwanamke anatongozwa na mume wa mtu. " Mmmmhmn hii si sawa,nitapata laana kuvunja ndoa ya mtu,watoto watateseka wazazi wao wakitengana,na ni dhambi kwa MUNGU wacha tu nisubirie kupata wa kwangu"

Sasa: " ooooh Hallelujah,ngoja niende kwa mwamposa kutoa sadaka kwa kunieletea mwanaume wa ndoto zangu, ana mali, biashara na ananijali,mkewe na watoto wake itabidi wajikaze mimi siwezi kupishana na bahati"

4. Zamani: Mwanamke anakutana na kijana amehitimu masomo ila hana ajira na anajitafuta. " Hongera kwa kumaliza masomo,usijali, MUNGU atatufungulia njia huko mbeleni tutapata mali kwasasa tujibidiishe na maisha".

Sasa : " mmmmmmmmmn sasa mwanaume hauna hela,hauna kazi unanitaka utanihudumiaje kwa mfano, au unataka ukanifubaze nichakae ndio ufurahi? We kuweza"

5. Zamani : mwanamke akienda nyumba ya ibada. " MUNGU baba naomba unilinde na kuniweka mbali na vishawishi na uovu wa shetani,nilinde huu mwili wangu na hiii bikra yangu hadi ndoa niwe mke mwema na kuishi kwa namna ya kukupendeza"

Sasa : " eeeeh Yesu naomba uningezee tako , shepu na rangi ya mtume ili wanaume wakiniona wachanganyikiwe,nisamehe kwa kutoa mimba ya tatu niliogopa kuzaa mtoto asiteseke. Naomba unipe mume handsome,mrefu,rangi nzuri,ajue kuvaa,awe na hela nyingi,kwao wawe matajiri,awe wangu pekee yangu anipende pekee yangu. A

Kwa kifupi wamebadilika sana.
Zamani binti akikojoa ardhi I anachimba kishimo, siku hizi mkojo unasambaa kama umemwagwa kwa ndoo
 
Siku hizi kinachwaharibu wanawake ni vikoba,anaweza kukubali ukiwa huna hela lakini jiandae wakati wa kulala pochi ficha stoo....
 
Lugha zako ni zile zile za kuamini unabishana. Mimi sipo hapa kubishana ila najenga hoja za msingi ili kusadia jamii na kuijenga.

Sasa sijui hapo unapinga wapi
Sasa kwani kubishana maana yake nini au ni wapi ambapo hujanielewa, okay labda niseme kujadiliana japo inashangaza pale ambapo watu wawili mnaenda sambamba kwenye majadiliano halafu mmoja ndio anamuita mwenzie mbishi, sasa kama wewe siyo mbishi basi ungeshaachana na huo mjadala kitendo cha kuendelea kumjibu huyo mtu maana yake wote ni wabishi na hamna tofauti yoyote, wewe huna hoja zozote za kuisaidia jamii labda uwadanganye wasio na elimu wewe hoja zako nyingi hazina uhalisia na zimejikita kuwafariji wanaume tu, tukija kwenye uhalisia sasa hivi hakuna jinsia inateseka kama wanaume ndio maana malalamiko yenu yamejaa mitandaoni na vijiweni ila kama kawaida yenu mnataka muonekane kama mnafanya hayo kwa faida ya wanawake yani kwa kifupi you are in denial
 
Wewe ndo umesema lakini wanawake wa sasa wanachagua. Itabidi mrudi zama za kale ili muwe mnachagua
Hahaha itabidi wafanye Time travelling tu kwakweli maana hakuna namna 🤣🤣
 
Jadda korido za kutisha kama hizi huwa anapita kimya kimya maana anajua akileta fyoko Battalions za combatants wa Masculinity havitamuacha salama kwa mizinga mfululizo.😂😂😂
Huyo ni rafiki yako wa damu😆
 
Wewe ndo umesema lakini wanawake wa sasa wanachagua. Itabidi mrudi zama za kale ili muwe mnachagua
wanawake wakichagua mwanaume wa kuwaoa hukosea sana, watulie wachaguliwe
 
Wanawake tulieni mchaguliwe, nyie hamjui kuchagua mnakosea sana na kujuta kuchagua kwa tamaa zenu
 
Kwamba na sisi tunachagua tunayemtaka, kama hutakiwi unapigwa chini kiroho safi
Sawa ila ndio ukimchagua unaemtaka ukaona kuna vitu hafanyi kwako usilalamike wala kumchukia ,mfundishe hadi ajue.

Imagine kumfundisha mwanaume wako namna ya kukupagawisha kitandani au namna ya kukuletea zawadi na hajisikii. 😂😂😂😂

Ndipo hapo utaelewa kwann wanaume huwa tunatongoza na ninyi wanawake ndio mnatongozwa.
 
Siku hizi kinachwaharibu wanawake ni vikoba,anaweza kukubali ukiwa huna hela lakini jiandae wakati wa kulala pochi ficha stoo....
Unadhani ni uongo mzee. Siku hizi wameanza tabia mbaya za kujitumia pesa kwenye simu au kuchukua kwenye wallet,hiyo tabia ni kichefu chefu.
 
Sasa kwani kubishana maana yake nini au ni wapi ambapo hujanielewa, okay labda niseme kujadiliana japo inashangaza pale ambapo watu wawili mnaenda sambamba kwenye majadiliano halafu mmoja ndio anamuita mwenzie mbishi, sasa kama wewe siyo mbishi basi ungeshaachana na huo mjadala kitendo cha kuendelea kumjibu huyo mtu maana yake wote ni wabishi na hamna tofauti yoyote, wewe huna hoja zozote za kuisaidia jamii labda uwadanganye wasio na elimu wewe hoja zako nyingi hazina uhalisia na zimejikita kuwafariji wanaume tu, tukija kwenye uhalisia sasa hivi hakuna jinsia inateseka kama wanaume ndio maana malalamiko yenu yamejaa mitandaoni na vijiweni ila kama kawaida yenu mnataka muonekane kama mnafanya hayo kwa faida ya wanawake yani kwa kifupi you are in denial
Ubishi ni pale ambapo unajua mada ni kitu fulani na tunalenga kujadili upande fulani halafu wewe unakuja na hoja ambazo zinalenga mada zako wewe kichwani na hata ukiambiwa au kuelekezwa unaona sasa hapa ndio opportunity ya kuanzisha zogo na mabishano ndio maana hata ulivyoanza umesema kubishana badala ya kujadiliana.

Watu wanaojadili vitu huwa wanakuwa na hoja za msingi ambazo zinahusiana na mada mezani. Hatuwezi tukawa tunajadili magari wewe ukaleta hoja za uvuvi na ukalazimisha kuwa ni jambo la msingi pia ukijua wazi hakuna ambaye anajadili uvuvi muda huo bali mjadala ni magari.
 
Back
Top Bottom