Hata mie nyingi zimenikalia pembeni sema tu ni vile kuna watu wangu wa karibu wako vizuri kiroho hivyo huwa nawaconsult pale ninapoona nimetoka kapa, ila hilo andiko niliambiwa halina maana hiyo hilo ni fumbo tu limetumiwa kama mfano lakini maana yake halisi ni hii...
Chukulia mwanaume ni mfano wa Mungu halafu mwanamke ni mfano wa kanisa, hapo waliposema wanawake saba watamfuata mwanaume mmoja na kumuambia kila kitu watajitegemea wenyewe ila tu waitwe kwa jina la huyo mwanaume ni kama makanisa ya sasa yanavyofanya kwa Mungu.
Makanisa mengi sasa hivi tunasikia wachungaji wanataja jina Mungu na Yesu na wanawaombea waumini wao kupitia hayo majina lakini kiuhalisia wanatumia nguvu za giza. Kwahiyo hizo siku za manabii wa uongo zilizotabiriwa ndiyo hizi ambazo makanisa yanatumia jina la Mungu na Yesu lakini kiuhalisia wako kivyaovyao wanaoperate chini ya nguvu nyingine ambazo hazihusiki na Mungu muumba wa mbingu na nchi.
Sasa kaka yangu usije ukawa unasubiri wanawake saba wakukimbilie wakuomba uwaoe halafu watajitegemea kwa kila kitu kama ambavyo wale wenzenu wa upande mwingine wanavyosubiri wakifa wakakutane na mabikira 72 peponi teh, wewe endelea kuwatafuta tu huko nje usisubiri wakufuate cha msingi wifi yangu asijue maana inaonekana wanaume kutulia imeshindikana kabisa.