Wanawake wenye vitambi wamezidi kuongezeka...

Wanawake wenye vitambi wamezidi kuongezeka...

Kaka nimekuelewa Ila sasa katika Jamii zetu hzi tunawezaje kuepuka vyakula vya wanga maana ndio vimejaa kila kona...

Mtu anaweza kujitahidi kula mboga za Majani na matunda Ila wanga lazima tu utazidi na maisha yetu haya dah,Kuna muda diet ni ngumu mno kuzifuata aisee.
Nyama haina shida, maana inaweza cheza part ya wanga kuna namna inatengeneza nishati pia.
 
Wale ndugu wa kule kwenye mlima mrefu afrika ambao wana sura nzuri sana lakini nyuma wamepigwa pasi, wapo kwenye kundi lipi ?
Sitaki kujimu moja kwa moja,good ex. Ya pear body shape ni most somalis,tutsi and ethiopians.
But most bantu are apple body shape sema tumebadilika kiasi kwa kuchanga
 
Sasa nyie mkiwapeleka bar cha kwanza mchemsho wa kuku na castle lite unategemea nini?

Wabadilishieni menu anzeni kuwapa...chai ya rangi na mihogo ya pilipili.
Ushindwe na ulegee. Ili bili ije ndogo?
Ni mwendo wa bia na minyama tu, tuvumiliane tu jamani.
 
Kaka nimekuelewa Ila sasa katika Jamii zetu hzi tunawezaje kuepuka vyakula vya wanga maana ndio vimejaa kila kona...

Mtu anaweza kujitahidi kula mboga za Majani na matunda Ila wanga lazima tu utazidi na maisha yetu haya dah,Kuna muda diet ni ngumu mno kuzifuata aisee.
Hahahah ni kweli changamoto ipo kwa sababu vyakula vya protien kama nyama na maharage ndio common zaidi ila kinachopendwa zaidi ni nyama ambayo ni very expensive.

Sasa hamna jinsi zaidi ya kujiimarisha kula kande tu walau utabalance protien na wanga. Ukiweza kula matunda mixa mchana mjini wanauzaga plate buku tu. Ila wenye uwezo diet kwao rahisi sana maana unaweza nunua masamaki, kuku ama nyama ya ng'ombe ukajaza kwenye freezer.
 
Hivi ni kweli vitambi kwa akina dada vinaletwa na chips tu?
Mbona kwa sasa kila sehemu vitambi vinaongezeka kwa speed ya hatari.
 
Kama me wanavitambi itakuwaje ke akose vitambi;tujitahidi kuepuka vyakula vinavyoongeza mafuta mwilini,mazoezi kwa sana n.k
 
Sasa nyie mkiwapeleka bar cha kwanza mchemsho wa kuku na castle lite unategemea nini?

Wabadilishieni menu anzeni kuwapa...chai ya rangi na mihogo ya pilipili.
🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️🙆🏽‍♂️
 
Kula kama unaenda kunyongwa. Kesho yake hautokuwepo kula tena... Na kuna ile kula kwa sababu saa ya kula imefika. Unakula hata kama umeshiba!
Pia hatari zaidi ipo kwenye vyakula vya kawaida tu kama chapati,mandazi, wali, ugali na ndiyo vyakula vikuu vya watanzania.
Bidada asubuhi anapiga chai na chapati 3 na mandazi 2, mchana ugali mkubwaa mboga kidogo, usiku wali sahani 2 hadi anashindwa kuhema alafu dakika 20 baada ya kula anaenda kulala.

Cha msingi watanzania wajifunze kula kwa nidhamu, wengi ni waroho hasa wanawake.
 
Hivi ni kweli vitambi kwa akina dada vinaletwa na chips tu?
Mbona kwa sasa kila sehemu vitambi vinaongezeka kwa speed ya hatari.
Mtindo wa maisha ndiyo coz, zamani watu wengi walitembea hata mijini esp. toka vituoni mwa daladala kwenda home sasa pikipiki zimeongeza problems.tumekuwa kama kitimoto bandani lazima ufule tu
 
Back
Top Bottom