Wanawake wengi hawawataki wanaume maskini

Wanawake wengi hawawataki wanaume maskini

Wengi wa aina hiyo wanakuwa wametokea kwenye familia za kimasikini.

Huwa najiuliza, hivi wao hawajiulizi ni kwanini Mama zao waliwavumilia Baba zao kujenga familia katika hali ya umasikini?

Kama hela ni jambo la muhimu mwanaume kuwa nalo ili kudumisha mahusiano, kwanini Baba zao hawana?

Hapa kuna tabia inajengeka.

Kwamba Mwanamke anaiona thamani ya mwanaume pale tu ambapo huyo mwanaume atakua na hela.

Na sasa mwanaume akiwa na hela unakuwa unamtengenezea mazingira ya kutoona value ya mahusiano kwasababu anajua uko hapo kwasababu ya hela zake.

Automatically hiyo inakuwa inamkata stimu emotionally.
 
Wenyewe watuone waonavyo! Kwahiyo wote wanaanzia chini? Na waliojipata wote hawapo single wameanza moja na wapenzi wao wa zamani?
Hapana na hapo ndipo tunapo ubaini uongo wako, ukweli ni kwamba wanawake wengi ni wenye tamaa na kupenda wanaume wenye uchumi mzuri, hoja ya kwamba masikini huwa anabadilika akijipata na kuwaona wanawake ni makapi haina mashiko wala miguu ya kusimamia.
 
Back
Top Bottom