Wanawake Warefu (Tall Women)

Wafupi tunasoma comments tu.
Dada nimekumiss.
IMG_20190126_184324_014.JPG


The Hate U Give, Little Infants F's Everyone.
 
Habari zenu wadau natumai siku kwenu inaenda vizuri.
Leo ningependa kuongelea kidogo kuhusu sisi wadada warefu ambao tupo wachache Tanzania. Binafsi mimi nina urefu wa 5'9+ (176cm) na hii nimepimwa nikiwa sijavaa chochote miguuni. Nikivaa kiatu chochote au hata ndala, moja kwa moja nakuwa 5'10+. Na nikivaa high heels nakuwa 6'0+.

Sababu kuu ilionifanya niwe mrefu ni "genetics", wazazi wangu wote ni warefu ingawa sio sana. Pia chakula nilichopatiwa nilivokuwa mdogo hasa hasa protein iliyonowezesha kukua mpaka kufikia kimo changu halisi.

Urefu una raha zake kwasababu, watu wanakuheshimu hata kama hawakufahamu vizuri. Wanakuona una busara na unaweza kuwa kiongozi. Pia unaonekana kwa urahisi zaidi kwenye umati wa watu na ukivaa nguo zinakukaa.

Urefu pia una shida zake kama vile, kupata nguo na viatu ni kazi kuliko wanawake wenye maumbo ya kawaida. Nguo hazitoshi na ukikuta inayokutosha mara nyingi kiuno (sana sana kwa suruali) kinakuwa kikubwa. Viatu ndo hata siongei vile vya kidada dada mara nyingi ni vidogo sana na mpaka kuja kupata vinavyonitosha na bei inapanda. Kingine ni kwamba sio kila siku mtu unapenda kuoneka kuna wakati unataka uwe "low profile" lakini hii haiwezekani. Kingine ni kwamba kila mtu akikuona ana penda kutoa maoni yake. Utasikia mara ooo hupati mume, au urefu wako umezidi au kwanini usiwe model hatakama haupendelei hiyo fani.

Hata hivyo napendelea kuwa mrefu na nina pendelea urefu wangu ingawa nilivokuwa mdogo niliuchukia sana. Lakini pia ningekuwa na uwezo wakuubadilisha ningependa kuongezeka nifikie 180cm au zaidi.

Asanteni. Nakaribisha mawazo yenu.

Yaani hamna kitu napenda kama mwanamke mrefu alafu akipiga heels hapo anipite kidogo urefu ....alafu bwana warefu mnakuwaga wapole wanyeyekevu hadi raha...wee achana na hao wasemao sijui ndio maana hujaolewa...njoo kwangu fasta natangaza nia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom