Wanawake Warefu (Tall Women)

Wordsworth

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
1,177
3,316
Habari zenu wadau natumai siku kwenu inaenda vizuri.
Leo ningependa kuongelea kidogo kuhusu sisi wadada warefu ambao tupo wachache Tanzania. Binafsi mimi nina urefu wa 5'10 1/2 (178cm) na hii nimepimwa nikiwa sijavaa chochote miguuni. Nikivaa kiatu chochote au hata ndala, moja kwa moja nakuwa 5'11+. Na nikivaa high heels nakuwa 6'0+.
Sababu kuu ilionifanya niwe mrefu ni "genetics", wazazi wangu wote ni warefu ingawa sio sana. Pia chakula nilichopatiwa nilivokuwa mdogo hasa hasa protein iliyonowezesha kukua mpaka kufikia kimo changu halisi.
Urefu una raha zake kwasababu, watu wanakuheshimu hata kama hawakufahamu vizuri. Wanakuona una busara na unaweza kuwa kiongozi. Pia unaonekana kwa urahisi zaidi kwenye umati wa watu na ukivaa nguo zinakukaa.
Urefu pia una shida zake kama vile, kupata nguo na viatu ni kazi kuliko wanawake wenye maumbo ya kawaida. Nguo hazitoshi na ukikuta inayokutosha mara nyingi kiuno (sana sana kwa suruali) kinakuwa kikubwa. Viatu ndo hata siongei vile vya kidada dada mara nyingi ni vidogo sana na mpaka kuja kupata vinavyonitosha na bei inapanda. Kingine ni kwamba sio kila siku mtu unapenda kuoneka kuna wakati unataka uwe "low profile" lakini hii haiwezekani. Kingine ni kwamba kila mtu akikuona ana penda kutoa maoni yake. Utasikia mara ooo hupati mume, au urefu wako umezidi au kwanini usiwe model hatakama haupendelei hiyo fani.
Hata hivyo napendelea kuwa mrefu na nina pendelea urefu wangu ingawa nilivokuwa mdogo niliuchukia sana. Lakini pia ningekuwa na uwezo wakuubadilisha ningependa kuongezeka nifikie 180cm au zaidi.
Asanteni. Nakaribisha mawazo yenu.
 
Hongera mama kuwa mrefu ni baraka, na ufupi ni laana mfano ni wa dodoma kichwa kinakua jirani na tumbo kitu kinachopelekea ubongo kuathirika na joto la mavi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha duuh, by the way mimi ni tall na naupenda urefu, the first day i met my hubby alivutiwa na urefu na umbo langu, mpaka sasa guna watoto wanne. Mahandsome boy watatu warefuuu na ka princesa kamoja karefuu kama miss miss world

Najivunia kuwa mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha duuh, by the way mimi ni tall na naupenda urefu, the first day i met my hubby alivutiwa na urefu na umbo langu, mpaka sasa guna watoto wanne. Mahandsome boy watatu warefuuu na ka princesa kamoja karefuu kama miss miss world

Najivunia kuwa mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera mama, mimi ni 192 mtaani naitwa tolu mnyama na mke wangu ana 180 huwa tukipita popote lazima tupate watazamaji wa kutosha tunakuwaga maarufu automatically wengine wanatuuliza nyie ni ndugu huwa tunajibu yees we are

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera mama, mimi ni 192 mtaani naitwa tolu mnyama na mke wangu ana 180 huwa tukipita popote lazima tupate watazamaji wa kutosha tunakuwaga maarufu automatically wengine wanatuuliza nyie ni ndugu huwa tunajibu yees we are

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hata sisi tukipita watu wanadhani sisi mapacha, sema tu rangi tumetofautiana meenzangu ni super black na mimi ni super white, hao watoto sasa ni fireee

Urefu raha jamani ukienda mahali huna haja ya kujitambulisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

52 Reactions
Reply
Back
Top Bottom