Wanawake wanataka ndoa hawapati, ni kweli hamna waoaji?

Wanawake wanataka ndoa hawapati, ni kweli hamna waoaji?

tz2015
Hiyo ndo sababu ndogo kuliko zoote ambazo zingefanya shinikizo la kuoa. Kwa ufupi maadili kwa mabint yamekuwa chini sn, unakuwa na binti lakin bado hata wewe mzaz unajiuliza km atapata mme wa kumuoa maana unaona kabisa yuko kushoto sn.
 
Last edited by a moderator:
selestei

  1. Kujitambulisha ukweni. Hapo utatakiwa uende kijijini alikozaliwa mkeo mtarajiwa ukajitambulishe huko. Kama mfano mkeo anatokea Mwanza, na mnaishi Dar, andaa nauli ya watu wawili, malazi kwa siku mbili, na utagharamia shuhuli hiyo ya utambulisho. We tenga 500,000. Hapo tuna assume mkeo atajitegemea. Otherwise 800,000 itakutoka.
  2. Kumtambulisha mkeo kwenu. Kama nyie nyumbani ni Arusha, utatakiwa umpeleke huko Ngarenanyuki. Sio umlete hapo Tabata mlipopanga. Hapo sio kwenu! Andaa nauli yako na atakaekusindikiza, nauli ya binti na mwenzie, na gharama za vinywaji na chakula siku hiyo. Utahitaji kama 700,000
  3. Kifuatacho ITV ni kuwaalika wakwe zako nyumbani. Uwatoe watu kama nane Mwanza, uwalete Arusha. Wale, walale, wajisaidie, kwa gharama zako. We acha ubishi, tenga 800,000 tu.
  4. Kwani we wazazi wako wanajua unakooa? Sasa je? Wasafirishe kwenda Mwanza! Watu watano. Utahitaji kuwa na 500,000. Beba pia ATM card yako, kuna imejensi.
  5. MAHARI ndio topic inayofuata sasa. Ukiwa mjanja, unganishia kwenye hiyo safari hapo juu uue ndege wawili. Pamoja na hayo, itabidi ubebe 2,000,000.
  6. Sasa kijana unaweza kumvisha mchumba wako pete. Nunua ya kawaida kabisa ya dhahabu. 350,000. Tukio lenyewe la kumvisha pete unaweza ita marafiki wawili watatu ukatumia 200,000. Au fanya sherehe kabisa. Mi simo
  7. Oke, sasa unaweza kuitisha vikao vya harusi. Tengeneza kadi za mwaliko wa kamati kwa 200,000, kikao cha kwanza gharama zote ni juu yako. Andaa 500,000. Swali la kwanza kwenye kikao: "We una shing ngapi?" Sema 1,000,000.
  8. Utahitaji 100,000 ya sms na simu kukumbushia michango. (Shukuru Mungu kuna cheka time)
  9. Wakati vikao vinaendelea, utatuma 200,000 kwa m-pesa ili mambo ya kimila yaendelee kule nyumbani. We unaelewa
  10. "Darling, sasa mi kwenye kitchen party ntavaa nini?" 300,000!
  11. "Darling, kuna mahali nimeona gauni zuri la send…" 400,000!
  12. "Baby, rafiki yangu alinunua gauni la harusi China yani lilimpende….." 700,000!
  13. Wakati huo wewe mwenyewe hujajua utavaa nini, hujanunua pete za harusi, hujamvalisha best man na mkewe. Tuseme unahitaji kama 1,500,000 maana utalia lia sana. Kumbuka, gharama hizi huchangiwi na kamati. Wala hutarudishiwa.
  14. Siku ya send off lazma uende Mwanza. Utaenda mwenyewe? Ndugu wawili watatu na mshenga 600,000. Kwenye send off utatakiwa kutoa sijui blanketi la bibi, vitenge vya mashangazi, na vikorokoro kibao. Nunua hivyo vitu 300,000 uende navyo ili kupunguza gharama. Beba 200,000 za wale mashangazi watakaoibuka ghafla!
  15. Mshonee baba mkwe suti 100,000 mama mkwe yeye atavaa gauni la 50,000.
  16. Fotokopi hiyo hapo juu (namba 15) kwa wazazi wako. 150,000
  17. Watu watakaopenda kuvaa sare wajitegemee! Mimi sina hela! Ila utavishonea nguo vile vitoto kwa 80,000.
  18. Siku mbili kabla ya harusi, utaanza kupokea wageni. Unatakiwa uwatafutie malazi na chakula. Kwa ujumla utahitaji kama 500,000
  19. Jioni watoe auti mashemeji zako ambao hawajawahi kufika Dar ukawanunulie bia ili wakuone wa maana. 200,000
  20. Siku ya harusi bibi harusi na mwenzie na watoto na ma maids watatakiwa wakapambwe saluni. 200,000
  21. We na mwenzio mtaenda kunyoa hapo kwa nanii. Ndevu na nywele 10,000
  22. Siku ya harusi beba sadaka 10,000. Wakati huo umeshamtuma kijana akakulipie hoteli mtakayofikia baada ya harusi. Kamati haitoi hela hiyo, so utalipa malazi ya siku mbili 200,000
  23. Kama mtaenda honeymoon sehemu yoyote nzuri nzuri nje ya mji, si chini ya 800,000 kwa angalau siku 5.
  24. Wakati uko huko honeymoon, huna hata kumi, mwanakamati mmoja ambae hakuchanga anakupigia simu " Sasa tunavunja lini kamati?" Pesa yote iliyochangwa ilitumika kwenye harusi, sasa gharama za kuvunja kamati ni za nani?? 500,000!
  25. SASA MNAANZA MAISHA YA UNYUMBA. 14,150,000 poorer.

https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/198968-gharama-za-harusi-kwa-bwana-harusi.html

NA MIMI NNA SEMA KWA GHARAMA ZOTE HIZO PLUS LIFE LA KIBONGO KUNA KUOA HAPO????
 
Last edited by a moderator:
wanawake wenyewe ndio tatizo...kama unabisha muulize zinc
 
Last edited by a moderator:
wanawake wenyewe ndio tatizo...kama unabisha muulize zinc

Hahaha mpaka uzi tatu zimefungwa na mods.. Kweli itabidi huyo zinc atuweke bayana ni nini hasa..
Tatizo kaeleza nusunusu tuu
 
Last edited by a moderator:
Hahaha mpaka uzi tatu zimefungwa na mods.. Kweli itabidi huyo zinc atuweke bayana ni nini hasa..
Tatizo kaeleza nusunusu tuu

maisha magumu sana mshikaji wangu,wanawake wanaangaika kinoma kutimiza ndoto...Jamaa kapewa darasa la mapenzi kidogo.
 
URL]https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/198968-gharama-za-harusi-kwa-bwana-harusi.html[/URL]

NA MIMI NNA SEMA KWA GHARAMA ZOTE HIZO PLUS LIFE LA KIBONGO KUNA KUOA HAPO????[/QUOTE]

Nashukuru kwa mchango wako,, majuzi nimehudhuria harusi imegharimu milioni 2.5 tuuu na ilifana sana sherehe..
Kwahiyo usikate tamaa kaka penye nia pana njia..
Halafu kuhusu sijui mahari dawa mbona ndogo sana we waweke bayana kuwa huwezi mudu wakupunguzie ukiona wanang'ang'ania wasusie binti uone kama hawajakupa hata bureee...
Hehehe waoaji wenyewe siku hizi hamna.. Wazazi inabidi wabadilike..
 
Hiyo ndo sababu ndogo kuliko zoote ambazo zingefanya shinikizo la kuoa. Kwa ufupi maadili kwa mabint yamekuwa chini sn, unakuwa na binti lakin bado hata wewe mzaz unajiuliza km atapata mme wa kumuoa maana unaona kabisa yuko kushoto sn.
Mkuu nazungumzia kuoa,kama hapa tz hawapo wa kuoa basi oa hata ulaya basi.Tusiwaandame mabinti,pia wanaume tujipime,je sisi tuna sifa za kuoa.Mwanaume na akili kichwani unavaa mlegezo pichu au bukta unayoionyesha chafu
unategemea mtoto wa watu ajitoe mhanga eti kisa kuolewa?
Kama mzazi mwenye watoto ki-ukweli tunaumia unapoona jitu zima halitaki kuoa,ila kesi za kuharibu woto wa watu
zinaongezeka.Acha hizo sababu nyepesi kama hamna hela ya kuolea waombe wazazi wenu tuwalipie muoe.
 
Hahaha........ kiongozi umemaliza kabisa. Ishia hapo hapo usije ukasababisha balaa......
 
Mkuu nazungumzia kuoa,kama hapa tz hawapo wa kuoa basi oa hata ulaya basi.Tusiwaandame mabinti,pia wanaume tujipime,je sisi tuna sifa za kuoa.Mwanaume na akili kichwani unavaa mlegezo pichu au bukta unayoionyesha chafu
unategemea mtoto wa watu ajitoe mhanga eti kisa kuolewa?
Kama mzazi mwenye watoto ki-ukweli tunaumia unapoona jitu zima halitaki kuoa,ila kesi za kuharibu woto wa watu
zinaongezeka.Acha hizo sababu nyepesi kama hamna hela ya kuolea waombe wazazi wenu tuwalipie muoe.

Hehehe nice one
 
unajua ndoa ni matokeo ya kuishi vizuri katika uchumba lakini wadada zetu wanachezea fursa hii shauri yao
 
mi tarajia kuoa nikiwa na miaka 21 au 22 saiz nina mia 18 nina mchumba ambaye 2mepanga kuoana xo mda ukifisha naoa faxta. cha msing ni kuandaana mapema na mpenz wako

sijakuelewa mdogo wangu.lugha gongana
 
..vijana wamekuwa waoga kuingia katika ndoa.
..gharama za kuoa/ mahari na sherehe za arusi zimekuwa juu, vijana wengi wameshindwa kuji commit katika ndoa.
..wadada wanachagua Sana aina gani, uwezo gani, elimu gani, kipato gani alichonacho kijana ili akubali kuolewa nae..
..Vijana nao wanachagua aina ya wadada wa kuoa ili kubeba zigo la maisha pamoja, yaani saivi golikipaz inakwepwa Sana..

Ndio maana kuzalia home kumeongezeka kwa kasi, divorce rate imeongezeka coz wanachotegemea watu sicho wanachokuta ndani.
 
mi tarajia kuoa nikiwa na miaka 21 au 22 saiz nina mia 18 nina mchumba ambaye 2mepanga kuoana xo mda ukifisha naoa faxta. cha msing ni kuandaana mapema na mpenz wako
Kwa mtindo huu wa uandishi usipige kura mwakani itaharibika.
 
Sehemu yoyote ile ambapo kuna mabadiliko ''ima ya kiuchumi au ya kisayansi'' huathiri mila na desturi tulizozizoea. Mm naamini kuoa na kuolewa si suala la kipaumbele kwa jamii ya leo. Hili litaendelea kwa kipindi kirefu kwa sababu leo heshima ya mtu ktk jamii si kuwa na familia yenye kuheshimika bali ni kuwa na vitu[mali]. Wengi walio ktk ndoa wamekuwa watu wa kulialia na kuzilaani ndoa zao kana kwamba ni kitu kisicho na thamani na kinachochangia upotevu wa furaha na amani ndani ya nafsi zao.

unakunywa soda gani nikuletee??
 
ivi wewe ni nani wakuoa mwanamke kiazi.? fesibuku uko wewe unatafuta mchumba,jf wewe,twita na badoo uko alafu unaweka mapicha ya uchi uchi shenzi taipu alafu uje uolewe na nani.?

janmke shenzi shenzi tu hata hofu ya mungu huna.?

kazi kunya mapombe tu kama umezaliwa na tbl... period

janamke linaulizwa na boifilendi wakr vp bebi unalewa pombe... jinsi lilivyo zoba nalo linajibu ... ndio bebi ila biambili tu...

shenzi nani aliekwambia kua bia mbili siopombe.?

nani wakuoa janamke levi.?

au mnazani ndoa ni kichwa chwa chizi kila atakae ananyoa tu..? badirikeni acheni ulimbukeni nawaambia wanawake mkijieshimu kitabia na mavazi lazima wanaume wawafate kuwaomba wawaoe tu.

sasa endelea kukaa uchi uone kama kunamtu ataoa matatizo.
 
Ph-25
Kaka umeongea kwa hasira ila ujumbe umefika..
 
Last edited by a moderator:
..vijana wamekuwa waoga kuingia katika ndoa.
..gharama za kuoa/ mahari na sherehe za arusi zimekuwa juu, vijana wengi wameshindwa kuji commit katika ndoa.
..wadada wanachagua Sana aina gani, uwezo gani, elimu gani, kipato gani alichonacho kijana ili akubali kuolewa nae..
..Vijana nao wanachagua aina ya wadada wa kuoa ili kubeba zigo la maisha pamoja, yaani saivi golikipaz inakwepwa Sana..

Ndio maana kuzalia home kumeongezeka kwa kasi, divorce rate imeongezeka coz wanachotegemea watu sicho wanachokuta ndani.

Mmhhh kazi kweli kweli ndoa za benefits..
 
Back
Top Bottom