CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
Nionavyo mimi, uchaguzi umekuwa mwingi. Zamani wanawake wengi walikuwa wale wenzangu na mimi, kwa hiyo hata vigezo vya mume vinakuwa vya kawaida.
Jamani tunataka hatutaki status za wanawake siku hizi ziko juu. Sasa kuja kumpata mwanaume anayeendana na status yako inakuwa ngumu kidogo.
Wanaume wa kuoa wapo tena wengi tu ila tatizo viwango vyao unakuta viko chini.
Kitu kingine confidence ya wanaume siku hizi iko chini, kuoa mke mwenye status fulani wanaogopa. Ndio maana wengi wanakimbilia kwenye one night stand au F4 na waalimu wa shule za msingi.
Ngoja mwakani nikasomee ualimu hata ngazi ya cheti tu walau nitapata mume na hii 30+yrs yangu!
