Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,438
- Thread starter
- #41
mengi ya hayo malalamiko huwa yana sababu/chanzo chake, kama nyamayao nimefanya hilo sana tu na sababu zangu zilikuwa kwanini asihudumie familia yake tena kikamilifu anamaliza ngapi kwa huyo "hawara? coz nilijua anae basi huku nyumbani naomba mtoto asipige chafya huduma imefika, kwasasa nimeanza kidogo kidogo kusaidia, nilikuwa sijigusi kwa lolote na ni lazima sio ombi atoe huduma, sema sasa hivi hasira za hawara yake zimeisha naweza kusiadia kidogo kidogo.
Mh! sasa wale wasio na mahawara wanapata adhabu kutokana na dhana hiyo hiyo.
Kumbuka hilo nalo limekuwa ni Mob Psychology, kila mwanamke anaamini kwamba kila mwanaume ni lazima ana nyumba ndogo.
Nilishangaa juzi hapa kwenye MMU Exclusive interview yangu na lara 1, aliponiuliza kama niliwahi kum-cheat mama Ngina nikakanusha, nusura nitobolewe macho, si wanaume wala wanawake wote walinishambulia wakiongozwa na vinara wa humu MMU Babu DC Dark City na ODM Asprin.
Nahukumiwa kwa sababu ya dhana,na sio kwa ushahidi.......!
Wapo baadhi ya wanaume (Wasiojitambua lakini) wanaolazimika kutokana nje ya ndoa zao kwa ule mtindo wa "kama hanaimini ni heri nifanye kweli" baada ya kuchoshwa na kelele za wenzi wao za kutuhumiwa kutoka nje wakati wala hawana hata wazo hilo..........
Tatizo ni kubwa kuliko tunavyofikiria.
Last edited by a moderator: