Wanawake wakibeba mimba wanatukomoa

Wa kwangu kituko chake ni SIMU, yaani nikirudi nyumbani tu kabla ya Salamu keshaidaka simu yangu. Ataipeleleza weee hadi wakati wa kulala. Na ole wako agundue kitu!
 
Si nafuu wewe mkuu,sitasahau mke wa dingi mdogo alikuwa na mimba yake ya kwanza mwaka 2000,basi mpaka dingi mdg kuna kipindi haendi job na alikuwa anamdekeza haswa...siku moja usiku wa saa 7 akatuamsha tena kwa hasira mimi na binamu yangu eti tukamtungulie mkewe mapera mabichi (japo mti haukuwa mbali) halafu tuje na matembele pia. Na kulikuwa na manyunyu usiku huo huyu binamu yangu alianguka kwny utelezi na kuumia hadi leo ana kovu,asubuhi yake alienda kwao (kwa Aunt yangu).

Nimecheka kidogo nilie
 
Ni hali ya kawaida,mi kipindi changu sikutaka kuongea na mwenzangu hd najifungua. Yaan nilikuwa nahisi km donge fulan limenikaba rohon hivyo nafuu yangu ilikuwa ni kutomsemesha. Alikuwa anataman sn kuongea na mm ila ndio hivyo na ht nilipokuwa namjibu basi badae ntahangaika sn kwa kutapika.

Thanks God now mtoto wetu ana mwaka na miezi 6 ila baba ndo hayupo tena......dah kwakweli Mungu ana makusudi yake,hamu yote ya mtoto aliyokuwa imepotea km ndoto. Apumzike kwa amani!

Daah...pole sana
 
I can feel what they're going through. Wangu hakuwa na mapozi sana lakini mtoto alipofia huko ndani, then yeye akapata massive complications, acha kabisa...hawa watu tuwaheshimu tu, huwa wanapitia kipindi kigumu wakati wa ujauzito.

Ubarikiwe japo bado sijazaa
 
Wa kwangu mwili ulikuwa unawasha usiku kucha nikune hapa uwiiiii nikune hapa ayayaya nikune hupo nikimwambia jikune mwenyewe timbwili lake sasa wakuu nilifanya kazi ya kukuna kila siku usiku kucha ajabu mchana anakuwa okk kilichotokea job niliomba likizo ya dharura mpaka alipokuja sister wangu kuokoa jahazi. Kucha zote za mikono yangu taaaaabani
 
Nilishavaa sana mashati na t-shirt nyeupe ili aridhike siku nikivaa rangi nyingine panachimbika,sisahau nililala nje na baridi la Mbeya kisa ndani harufu ya sofa inamfanya atapike na mwendo ulikua kupaka baby care tu haaahaaa inakera ila ina raha yake maana ndani ilikua kama kuna wehu wawili,mbaya zaidi akapata miscarrige mwishoni sana bado naitamani ile hali ila Mungu hajabariki mpaka leo na muda mrefu umepita.
Hongera mkuu Mungu awaongoze wewe vumilia tu yataisha ila navitamani viatu kama vyako.

Kwa wakati wa Mungu atawapa haja ya mioyo yenu! lakini pia ni vizuri mkiwaona wataalam wa haya mambo! poleni sana!
 
Ni hali ya kawaida,mi kipindi changu sikutaka kuongea na mwenzangu hd najifungua. Yaan nilikuwa nahisi km donge fulan limenikaba rohon hivyo nafuu yangu ilikuwa ni kutomsemesha. Alikuwa anataman sn kuongea na mm ila ndio hivyo na ht nilipokuwa namjibu basi badae ntahangaika sn kwa kutapika.

Thanks God now mtoto wetu ana mwaka na miezi 6 ila baba ndo hayupo tena......dah kwakweli Mungu ana makusudi yake,hamu yote ya mtoto aliyokuwa imepotea km ndoto. Apumzike kwa amani!

Pole sana! Mungu akuwezeshe!
 
Huku mie mbavu sina,sijaoa bado hivyo hii tushen inanifunza kuwa mvumilivu.
Halafu huu ni kama mtihani linalo
mpata A usidhani litajirudia kwa BCD.
wote watakuwa tofauti..
Nami pia nadhani itakuwa tofauti kama nilivyoona wakitofautiana wanawake wote..
Pia hongereni kwa ushindi na kuitwa
akina Baba/Mama flan.,,
kumbe kuitwa Baba/Mama sii mchezo eenheee!!
 
Nashukuru sana wachangiaji nimegundua kitu kutoka kwa hawa watu,
kwa maana nipo katika kipindi kigumu kweli,
ila baada ya huu mwezi kuisha nitaitwa baba.
 
Mungu ana sababu zake mkuu..kama ipo ipo tu! Kesho kuila leo ni uroho!..
Asante sana chief bado naishi kwenye subira Mungu ana sababu zake.

Kwa wakati wa Mungu atawapa haja ya mioyo yenu! lakini pia ni vizuri mkiwaona wataalam wa haya mambo! poleni sana!
Yeah ni kweli nimeshafanya mawasiliano na wote tuko poa naamini suala la muda ila nadhani unaelewa ile hamu ya kinda inavyokua.
 
Sijui wanawake wote wakibeba mimba wanakuwa hivi au ni huyu wa kwangu tangia abebe mimba ndani hakukaliki mara nina hamu na kitu fulani ukileta hali, amehama chumbani eti kinatoa halafu mbaya analala kwa housegirl.

Nimejitahidi kufanya usafi lakini wapi hataki hata kuingia humo nimebaki nalala mwenyewe kwa kweli kuna maudhi mengi mpaka nachoka hivi ni kweli hizo mimba zinawafanya hivyo.

Nimejaribu kuongea na marafiki ambao wenzi wao walibeba mimba walichonieleza anayoyafanya huyu wangu ni cha mtoto hivi kweli kwamba mimba huwafanya hivyo au mnatufanyia makusudi.

Hayo masumbufu bora tu kuliko huo uchungu,juzi nilikua na shem wangu sekou toure nimeona tu huo uchungu ni balaa kwahyo hzo kero jaribu kubadilishana na uchungu uone.
 
Ni hali ya kawaida,mi kipindi changu sikutaka kuongea na mwenzangu hd najifungua. Yaan nilikuwa nahisi km donge fulan limenikaba rohon hivyo nafuu yangu ilikuwa ni kutomsemesha. Alikuwa anataman sn kuongea na mm ila ndio hivyo na ht nilipokuwa namjibu basi badae ntahangaika sn kwa kutapika.

Thanks God now mtoto wetu ana mwaka na miezi 6 ila baba ndo hayupo tena......dah kwakweli Mungu ana makusudi yake,hamu yote ya mtoto aliyokuwa imepotea km ndoto. Apumzike kwa amani!

Pole kwa yote dada Mungu ni mwema.
Azid kukutia nguvu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom