Wanawake wakibeba mimba wanatukomoa

Wanawake wakibeba mimba wanatukomoa

Hahahahaa...poleni mie nakumbuka ujauzito wa wife alikuwa anapenda pespi baridi ile chupa yake inamdomo mwembamba....siku moja ziliisha kwa friji imefika saa tisa usiku akaniamsha mzee tulizunguka baa zote dar nikaja ipatia kona bar sinza toka mbezi kimara....tumerudi om tayari kumekucha...

Ungevunga unaumwa bana
 
Mkuu pole!
Ila ktk ulimwengu wa roho (hayo huwa ni mapepo) kwa iman yangu,
Mungu aliweka ndoa kama jambo la faraja na upendo, ujio wa mtoto ni furaha kwa wote wawili, (iweje mwingine asononeke kwa ujio huo) inafika mahali unajuta,

Mabadiliko ya mwili yapo tena sana tu na ukiyaendekeza ndo huge uka mapepo sasa!

Kitaalamu wanasema mtoto akiwa tumboni anaanza tambua uwepo wa watu wanaomzunguka (siko vizur eneo hilo) that's wazazi, na hapo ndo upendo unapoanzia, hutaki kulala na baba wa mtoto, upendo wa baba mtoto ata sense saa ngapi ilihali kutwa yuko kwenye mihangaiko,

Tangu siku ya kwanza hadi ya mwisho umebeba mimba wewe ni mi hasira tu! Unategemea mtoto atakuwa na upendo? Mtoto ni baraka! Isigeuke karaha

Ni wachache wataliewa hili!!
Tufike mahali tutofautishe mapepo na Mabadiliko ya mwili!

Walokole na nyie mmezidi kila kitu mapepo.
 
Kwa nini ateseke na wewe upo? HAta hao unaowaona wagumu wanatamani kudeka.

Kweli, mimi huwa nina style moja ya kila nachotumwa natekeleza, kila kitu afu najifanya nimechoka sana. Mwisho wa siku nahurumiwa baadhi ya vitu na naonekana niko concerned.
 
Duuu mbona watu mnazaaa hivyoo karibia kila mtu humu mke wake mjamzitoo......duuuuuuuu.....mnabanduaana...
 
Acha hizo zote sasa kuna hii:
Mke wa kaka angu, yeye alikuwa anamwambia kaka akitoka tu kazini mara moja arudi nyumbani, akisharudi anachukua viatu vya kaka anaanza kunusu, akawa anasema akinusa ile harufu ya viatu yeye ndo roho inakuwa kwatu, tena akawa anamwambia kaka asivae soksi. Just imagine takribani miezi 8 kaka hakuvaa soksi.
mbaya zaidi kaka achelewe kurudi nyumbani, patachimbika hapo, akifika tu mlango anasema lete viatu. Duh!

Duh kweli mimba inawapeleka vibaya.
 
Mkuu pole!
Ila ktk ulimwengu wa roho (hayo huwa ni mapepo) kwa iman yangu,
Mungu aliweka ndoa kama jambo la faraja na upendo, ujio wa mtoto ni furaha kwa wote wawili, (iweje mwingine asononeke kwa ujio huo) inafika mahali unajuta,

Mabadiliko ya mwili yapo tena sana tu na ukiyaendekeza ndo huge uka mapepo sasa!

Kitaalamu wanasema mtoto akiwa tumboni anaanza tambua uwepo wa watu wanaomzunguka (siko vizur eneo hilo) that's wazazi, na hapo ndo upendo unapoanzia, hutaki kulala na baba wa mtoto, upendo wa baba mtoto ata sense saa ngapi ilihali kutwa yuko kwenye mihangaiko,

Tangu siku ya kwanza hadi ya mwisho umebeba mimba wewe ni mi hasira tu! Unategemea mtoto atakuwa na upendo? Mtoto ni baraka! Isigeuke karaha

Ni wachache wataliewa hili!!
Tufike mahali tutofautishe mapepo na Mabadiliko ya mwili!

Huyu shetani anasingiziwa vingi sana aisee, mpaka mabadiliko ya mwili? Haya sasa wanawake wakipata ujauzito mapigo ya moyo huongezeka, nalo ni shetani? Ebo! muhurumieni shetani mkizini mkiwa mmelewa yeye na mabadiliko ya mwili yeye daah kaazi kweli kweli
 
Mkuu mimi ke, na naongea vitu ninavovielewa mimi sio lazima nawe uelewe!

Ndo maana nikasema si wote watalielewa hili, maana kama kwa maneno ya kawaida tu hayo umeshindwa kuelewa yajayo ndo kabisaaaaa! So bora tuishie hapa!

Mabadiliko yapo ya kisayansi yanaeleweka, na shetan analeta ya kwake ! Ukishindwa kutofautisha hapo utapelekwa sana tu!!!

Kweli aisee madrama yasizidi sana aisee.Mtu anasumbua mpaka anakera kisa mimba.
Nafurahi kuona baadhi ya wanawake wanaweza ku-ihandle hiyo hali.Big up mummy.
Mwingine anasumbua wakati mimba yenyewe kapewa na mwingine anamu-act-ia tu jamaa kwa drama za ajabu ajabu.
 
Huyu shetani anasingiziwa vingi sana aisee, mpaka mabadiliko ya mwili? Haya sasa wanawake wakipata ujauzito mapigo ya moyo huongezeka, nalo ni shetani? Ebo! muhurumieni shetani mkizini mkiwa mmelewa yeye na mabadiliko ya mwili yeye daah kaazi kweli kweli

Mkuu huwez nielewa unless unauelewa ulimwengu ninaouongelea! !
 
I can feel what they're going through. Wangu hakuwa na mapozi sana lakini mtoto alipofia huko ndani, then yeye akapata massive complications, acha kabisa...hawa watu tuwaheshimu tu, huwa wanapitia kipindi kigumu wakati wa ujauzito.

aisee, pole Mkuu.
mie nlisumbua sana,nilivyoanza kuumwa akawa anahisi ni usumbufu wangu tu ingawa hakuwahi kuonyesha hilo, siku nlivyozima mbele yake na alivyoambiwa mimba imeharibika ndio akili alimkaa sawa. nimepata fahamu namuona mtu anajikaza tu ila hayuko sawa kabisa. baadae nlivyopona ndo anasema eti alidhani namdekea na siumwi kweli
 
Si nafuu wewe mkuu,sitasahau mke wa dingi mdogo alikuwa na mimba yake ya kwanza mwaka 2000,basi mpaka dingi mdg kuna kipindi haendi job na alikuwa anamdekeza haswa...siku moja usiku wa saa 7 akatuamsha tena kwa hasira mimi na binamu yangu eti tukamtungulie mkewe mapera mabichi (japo mti haukuwa mbali) halafu tuje na matembele pia. Na kulikuwa na manyunyu usiku huo huyu binamu yangu alianguka kwny utelezi na kuumia hadi leo ana kovu,asubuhi yake alienda kwao (kwa Aunt yangu).

utanivunja Mbavu mkuu!
 
Mke wangu alipobeba mimba tu akawa hapendi tena harufu ya pafyumu ninayo itumie so imebidi kuacha. Nasubiria akijifungua labda hali itakua shwari tena
 
yaan mmenikumbusha mbali wakati nna mimba nadeki uvungu kila cku chumba kila kona na bado napata harufu kali . ole wa mtu akae karibu nami hajaoga namfukuza! msosi wowote nlikuwa sili labda nanasi tu nlishawahi litafuta sehemu ya mbali pikipiki 5000/ lenyew 3000/ kidogo nife jamaaaaaaan hizi mimba hiziiii
 
Kwenda zenu mnadeka sana! Ata mimi huku sina hamu tena... Asikwambie mtu ananiendesha huku kimimba kidogo sana bado.
Tena asikwambie mtu hizo mimba ndogo ndio zinasumbua mnoo,,jamani hivi mnaona ni rahisi eeeh.
 
Acha hizo zote sasa kuna hii:
Mke wa kaka angu, yeye alikuwa anamwambia kaka akitoka tu kazini mara moja arudi nyumbani, akisharudi anachukua viatu vya kaka anaanza kunusu, akawa anasema akinusa ile harufu ya viatu yeye ndo roho inakuwa kwatu, tena akawa anamwambia kaka asivae soksi. Just imagine takribani miezi 8 kaka hakuvaa soksi.
mbaya zaidi kaka achelewe kurudi nyumbani, patachimbika hapo, akifika tu mlango anasema lete viatu. Duh!
hahahaaa,nimecheka sn jamani
 
Ha ha ha! Haichekeshi lakini inabidi nicheke, mi tulikuwa tunatoka Posta kuelekea Kimara, eti tukifika Ubungo anasema ana hamu na Chipsi za Edo, kwa hiyo inabidi turudi Namanga, dah.

Ila nina swali silielewi, mbona wanafunzi au watu wasio na wanaume around mimba zao hazina matata matata? Yaani unakuta kama demu ana mimba Chuoni maisha yanaenda hadeki wala halalamiki kama hawa wake zetu.

Usemalo km lina ukweli lakini pia labda si kweli sana. Mi nlipatia mimba home na mhusika tulikosana mimba ilimchukia nikamwambia ntalea mwenyewe. So i was strong na nafanya kazi zote. Ila hizo hamu za vitu nlikua napata sana na nlikua nafuata vitafunwa mjini almost 12km kutoka nnakoishi ili ninywe chai otherwise siku haiendi. Ao nahisi mnaona usumbufu coz mnatumwa. Hata mu angekuwepo mwenza wangu hvy vitafunwa ningemtuma badala ya kufuata mwenyewe
 
Mleta Uzi vumilia,ndo mimba complications zilivyo.Yataisha kaka,Mtangulize Mungu awapitishe salama ktk kipindi hiki kigumu.Mie wangu alikuwa hapendi pafyumu so ukifika muda wa kujipiga unyunyu nakimbilia sebuleni kujipigilia.
 
ndio gharama za ubaba hizo vumilia..... utakapokuwaunacheza na mwanao utayasahau yote hayo
Wengi wachangiaji wa maada hii wamesema wajawazito wengine hizi fujo wanazoleta wanaigiza aisee mimi nakataa kabsa,Mimba ni noma kwanza hata akufanyie fuju kiasi gani huwez kumpiga km unabusara lkn,Ila ni muda mzuri sana wa kumliwaza wife kwa kuwa hichi kipind ni kigum sana na inahtaj moyo wa uvumilivu hapo ndio muda wake yy mke kudeka na kuona kama kweli unampenda na kumjali.....hii ndio fursa ingawa tunafukuzwa ndani kwamba Tunanuka ,wanatuchukia ,anakufokea yaani aaah mradi siku ziende tu....Nakumbuka mwaka juzi wife akiwa mjamzito yye alikuwa hatak kbsa kuongea na mimi,nikiwa hom anakula buyu,ila toka hatua moja simu hiyo eeh umeshaenda kwa Malaya zako wakat amekutuma kitu dukani, Ukiwahi kurud unasikia muda wote unashinda ndani siuende nje ukakae na wenzako haya ukienda dk2 simu hiyo utasikia na ulale huko huko. Usiku ndio kazi sasa yaani nikutafuna mchele mbichi na kutafuna barafu....jaman eeehh...Nashukuru nilimvumilia bahat nzuri kaniletea matwins mapenz yamerud km wachumba vile
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom