Wanawake waanzisha mgomo wa Ngono! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanawake waanzisha mgomo wa Ngono!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by MAMMAMIA, Jul 16, 2011.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Wakiwa wamechoshwa na hali ya umasikini, ufisadi na wanasiasa wasiowajibika, na hasa kutokana na barabara mbovu isiyopitika, wanawake wa kijiji cha Barbacoas, Colombia, wameamua kuanzisha mgomo waliouita wa "Kubana miguu", wakimaanisha hawatashiriki katika ngono na waume/wanaume wao mpaka hapo barabara ya kijijini hapo itakapotengenezwa. "Hakuna barabara, hakuna mwanamke atakayepanua miguu yake" wamesisitiza wanamama hao wa Barbacoas. Baada ya siku tano tangu kuanza kwa mgomo huo, wanaume wamejibu mapigo kwa kutanganza mgomo wa kutokula. Nani ataibuka mshindi?
  Chanzo: No Road, No Sex, Women Tell Town; Men Respond with Hunger Strike - Fox News Latino
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ahahahaaah!!! Hii kali...... Sophia simba nae aliwahi kutoa ushauri akina mama wa bongo wagome kisa sikumbuki.,..
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mgomo wa ngono umekuwa ukitumika na wanawake kwa karne sasa sasa njia ya amani ya kutatua migogoro inayosababishwa na wanaume. Wanawake wa Kenya, mwaka 2009, waliitisha mgomo wa ngono ili kuwalazimsha wanaume kukaa na kuzungumzia amani, mbinu iliyotumiwa na wanawake wa Kigiriki (Lysistrata - Wikipedia, the free encyclopedia) kwa lengo hilo hilo.
  Hata nchini Belgium ambako daima kumekuweko na mitafaruku ya kisiasa baina kundi la kaskazini linalozungumza Kijerumani na la kusini linalozumza kifaransa, kushindwa kuafikiana kuunda serikali kwa muda mrefu sasa; Seneta mmoja wa kike (Belgian Senator Proposes Sex Strike - The Daily Beast) aliitisha mgomo wa ngono ili wanaume watafakari juu ya mgogoro huu wa kisiasa.
  Tatizo la mbinu hii ni kuwa wakati "wake halali wanafanya mgomo", nyumba ndogo na makahaba huwasaliti wenzao kwa kushabikia tenda.
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hahahah huu mgomo hautekelezeki...kikikubana mwenyewe unakipeleka!
  ila huo mgomo wa msosi kasheshe si unaweza kufa????manake ku duu sio lazima sana ila msosi muhimu.....
   
Loading...