Historia ya Mwanamuziki wa Reggae, Lucky Philip Dube

NAS1314

Member
Nov 29, 2017
19
7
Lucky Philip Dube (tamka doo-bei) [1] (3 Agosti 1964 - 18 Oktoba 2007) alikuwa mwanamuziki wa reggae kutoka Afrika Kusini. Alirekodi albamu 22 katika lugha ya Kizulu, Kiingereza na Kiafrikaans katika kipindi cha miaka 25-na alikuwa mwanamuziki wa Reggae kutoka Afrika Kusini ambaye aliuza albamu nyingi kabisa. [2] [3] Dube aliuawa katika kitongoji cha Rosettenville huko Johannesburg jioni ya 18 Oktoba, mwaka 2007. [3] [4] [5]

Lucky Dube
Jina la kuzaliwa
Lucky Philip Dube
Amezaliwa
3 Agosti 1964
Ermelo, Transvaal
(now Mpumalanga), Afrika Kusini
Amekufa
18 Oktoba 2007 (umri 43)
Rosettenville, Johannesburg
Gauteng, South Africa
Aina ya muziki
reggae, mbaqanga
Kazi yake
Mwanamuziki
Ala
Sauti, Kinanda
Miaka ya kazi
1982 - 2008
Studio
Rycodisc, Gallo Record Company
Ame/Wameshirikiana na
The Love Brothers
Tovuti
Official website
Yaliyomo
Wasifu wake Edit
Maisha Yake ya Utotoni Edit
Lucky Dube alizaliwa Ermelo, zamani lilikuwa eneo la Transvaal ya Mashariki, na sasa ni sehemu ya Mpumalanga, tarehe 3 Agosti 1964. Wazazi wake walitalikiana kabla ya yeye kuzaliwa na alilelewa na mamake, Sarah, ambaye alimpa jina hilo kwa sababu alichukulia kuzaliwa kwake kama bahati baada ya mimba nyingi kutoka. [6] Pamoja na ndugu zake wawili, Thandi na Patrick, kwa kipindi cha muda mrefu utotoni mwake Dube aliishi na nyanyake wakati mamake alihamishwa kufanya kazi sehemu nyingine. Kwenye mahojiano ya mwaka 1999 alimsimulia nyanyake kama "mpenzi wake wa dhati" ambaye "alizidisha vitu vingi kumkuza kuwa mtu wa kuwajibika aliye sasa." [7] [8]

Kuanza Uwanamuziki wake Edit
Utotoni mwake Dube alilima lakini, alipokuwa mtu mzima, na kutambua kwamba hakuchuma pato la kumwezesha kulisha familia yake, alianza kuenda shuleni. Akiwa shuleni alijiunga na kwaya, pamoja na marafiki wengine, na kuunda kikundi chake cha kwanza cha waimbaji kilichoitwaThe Skyway Band. [8] Alipokuwa shuleni aligundua kuhusu harakati za Rastafara. Akiwa na umri wa miaka 18 Dube alijiunga na bendi ya binamu yake, The Love Brothers, iliyoimba muziki wa pop kwa lugha ya Kizulu zilizojulikana kama mbaqanga huku akiyakimu maisha yake kwa kufanya kazi na kampuni ya Hole and Cooke kama mlinzi kwenye mnada wa magari huko Midrand. Bendi hiyo iliinga kwenye mkataba na kampuni ya Teal Record, chini ya Richard Siluma (Baadaye Teal iliunganishwa na Kampuni ya Gallo Record). Ingawa bado Dube alikuwa shuleni, bendi hiyo ilirekodi katika mji wa Johannesburg wakati alikuwa likizoni. Albamu waliotoa iliitwa kwa jima la Lucky Dube and the Supersoul. Albamu ya pili ilitolewa muda mchache baadaye, mara hii kando na kuimba Dube alitunga misitari. Ni wakati huu ambao alianza kujifunza Kiingereza. [8]

Kuhamia rege Edit
Baada ya kwa albamu yake ya tano ya Mbaqanga, Dave Segal (ambaye badaye alikuwa mhandisi wa sauti ya Dube) alimshauri aachane na jina la "Supersoul". Albamu zingine zote zilizofuata zilirekodiwa kama Lucky Dube. Wakati huu Dube alianza kugundua kwamba mashabiki walifurahishwa na baadhi ya nyimbo za rege alizoimba hadharani. Aliweza kuvutiwa na Jimmy Cliff [9] na Peter Tosh, [7] alihisi kwamba ujumbe wa masuala ya kijamii na kisiasa uliohusishwa na rege ya kutoka Jamaica ungefaa kwa hadhira ya Afrika Kusini jamii ambayo ubaguzi wa rangi(usarangi) ulikuwa umekithiri. [9]

Aliamua kujaribu mtindo huu mpya wa muziki na katika mwaka wa 1984, alitoa albamu ndogo ya Rastas Never Die. Mauzo ya rekodi hiyo yalikuwa mabaya - idadi ilikuwa karibu 4000- ikilinganishwa na 30000 ambayo rekodi yake ya mbaqanga zingeuzwa. Serikali iliyoeneza usarangi (ubaguzi wa rangi), ikiwa na nia ya kukomesha harakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, ilipiga marufuku albamu hiyo mwaka 1985. [10] Hata hivyo, hakuvunjika moyo na aliendelea kuimba nyimbo za rege hadharani na akatoa albamu ya pili ya rege. Think About The Children (1985). Ilifanikiwa kupata hali ya mauzo ya zaidi ya milioni na kumfanya Dube kuwa mwanamziki wa rege maarufu Afrika Kusini, mbali na kuvutia watu nje ya nyumbani kwao. [8]

Mafanikio muhimu na ya kibiashara Edit
Dube aliendelea kutoa albamu zilizofanikiwa kibiashara. Mwaka 1989 alishinda tuzo nne za OKTV wimbo wa Prisoner, ulishinda nyingine na wimbo wa Captured Live ulishinda tuzo nyingine mwaka uliofuata na bado wimbo wa House Of Exile ulishinda tuzo mbili mwaka mmoja baadaye. [11] Albamu yake ya mwaka 1993, Victims iliuza zaidi ya nakala milioni moja duniani kote. [2] Mwaka 1995 alipata mkataba wa kurekodi duniani na na kampuni ya Motown. Albamu yake ya Trinity ilikuwa ya kwanza kutolewa na kampuni ya Tabu Records baada ya Motown {1{/1} kujipatia kitambulisho hicho. [11]


Mwaka 1996 alitoa mkusanyiko albamu ya, Serious Reggae Business, ambayo ilimpelekea kuitwa "Mwanamziki wa Kiafrika mwenye mauzo bora zaidi" kwenye Tuzo la Wanamziki Duniani na "Msanii bora wa Mwaka" kwenye Tuzo la Wanamziki nchini. Albamu zake tatu zilizofuata zote zilishinda tuzo kwenye Tuzo la Wanamziki la Afrika Kusini. [11] Albamu yake ya hivi karibuni, Respect, ilipata nafasi ya kutolewa Ulaya na Kampuni ya Muziki ya Warner Musi. [2] Dube alizuru nchi nyingi, na kuimba kwenye jukwaa moja na wasanii kama vile Sinéad O'Connor, Peter Gabriel na Sting. [9] Alishiriki kwenye igizo la rege liitwalo Sunsplash mwaka 1991 (hali ya kipekee mwaka huo, alialikwa jukwaani tena na kuimba kwa muda wa dakika 25 akirudia) na onyesho la hadharani la 8 la mwaka 2005 mjini Johannesburg. [9]


Mbali na kuimba, wakati mwingine dube alikuwa muigizaji, alishiriki kwenye filamu za Voice In The Dark, Getting Lucky na Lucky Strikes Back. [12]

Kifo Edit
Lucky Dube aliuawa katika kitongoji cha Rosettenville mjini Johannesburg tarehe 18 Oktoba 2007, muda mfupi baada ya kuwapeleka watoto wake wawili kati ya wote saba kando ya nyumba ya mjomba wao. |18 Oktoba 2007, muda mfupi baada kuwapeleka watoto wake wawili kati ya wote saba kando ya nyumba ya mjomba wao. [13]]] Dube alikuwa akiendesha gari lake la aina ya Chrysler 300C ambayo kumbe ndiyo wauaji wake walikuwa wanataka. Duru za polisi zinaonyesha kuwa aliuawa kwa kupiga risasi na wezi wa magari. Wanaume watano wametiwa mbaroni kutokana na mauaji hayo [14] Watu watatu wwalishitakiwa na kupatikana na hatia tarehe 31 Machi 2009; wawili walijaribu kutoroka lakini walishikwa. [15] Watu hao walihukumiwa kifungo cha maisha. [16]

Aliacha mjane Zanele na watoto wake saba.

Hiba
Tarehe 21 Oktoba 2008, Rykodisc alitoa albamu ya mkusanyiko kwa jina Retrospective, ambayo ilikuwa na nyimbo nyingi za kuvutia za Dube pamoja na traki nyingine ambazo hazikuwa zimetolea vilevile awali unreleased tracks katika Marekani. Albamu hiyo ilisifia muziki wa Dube na kuadhimisha mchango aliyotoa nchini Afrika ya Kusini. [17]

Diskografia Edit
Mbaqanga Edit
Lengane Ngeyethu (1981)
Kudala Ngikuncenga (1982)
Kukuwe (1983)
Abathakathi (1984)
Ngikwethembe Na? (1985)
Umadakeni (1987)
Kiafrikaans Edit
Help My krap (1986)
Reggae Edit
Rastas Never Die (1984)
Think About The Children (1985)
Slave (1987)
Together As One (1988)
Prisoner (1989)
Captured Live (1990)
House of Exile (1991)
Victims (1993)
Trinity (1995)
Serious Reggae Business (1996)
Tax Man (1997)
The Way It Is (1999)
Ili The Rough Guide Lucky Dube (mkusanyiko) (2001)
Soul Taker (2001)
The Other Side (2003)
Respect (2006)
Mkusanyiko Edit
The Best Lucky Dube wa (2008)
Lucky Dube Live In Uganda (2008)
Retrospective (2008)
Marejeo Edit
Fun Facts, luckydubemusic.com, ilitolewa tarehe 19 Oktoba 2007
[2] ^ Five facts about raggae star Lucky Dube, Reuters, tarehe 19 Oktoba 2007
[3] ^ S. Africa reggae icon shot and killed - radio, Reuters, tarehe 19 Oktoba 2007.
[5] ^ Hijackers gun down Lucky Dube, News24.com, tarehe 19 Oktoba 2007
[6] ^ S African reggae star shot dead, BBC News, tarehe 19 Oktoba 2007,
[7] ^ Car jacker kills reggae star, CNN, tarehe 19 Oktoba 2007.
[8] ^ Luvuyo Kakaza, Getting Lucky, The Mail & Guardian, tarehe 26 Agosti 1999.
[9] ^ Finding reggae, luckydubemusic.com, ilitolewa tarehe 19 Oktoba 2007
[12] ^ Basildon Petain, South African raggae star shot dead in front of his chilldren, The Independent, tarehe 19 Oktoba 2007.
condolences pour in for Lucky Dube, SABC, 19 Oktoba 2007.
[17] ^ Discography, luckydubemusic.com, ilitolewa tarehe 19 Oktoba 2007
[24] ^ Who's Who: Lucky Dube, News24, ilitolewa tarehe 10 Oktoba 2007
Bobb, Scott. "S. African Reggae Star Lucky Dube Killed in Attempted Car-Jacking", VOA News, Voice of America, 19 Oktoba 2007. Retrieved on 2 Januari 2009. Archived from the original on 6 January 2008.
"Five arrests over SA star's death", BBC News, 21 Oktoba 2007.
[29] ^ Three Accused of the Murder of Lucky Dube Found Guilty Habari za Yahoo, 31 Machi 2009
[30] ^ Reggae Star's Killers Get Life Habari za Yahoo, tarehe 2 Aprili 2009
[31] ^ Lucky Dube - Bio|Artist|RYKODISC

Story writter: DPAC MC

======

KWA UFUPI

======

=> Siku ya tar 18/10/2007 ndani ya jiji la JOHANNESBURG, majambazi wa4 walikuwa wakiisaka gari aina ya chrysler 300c. Lengo likiwa ni kuiba gari na kwenda kuiuza walipopajua wao. Baada ya muda kupita, waliiona gari waliyokuwa wakiitafuta ikikatiza kwenye mitaa ya ROSETTENVILLE.

=> Majambazi hao wakaifuata gari hiyo na kuimiminia risasi zilizopelekea kukatisha uhai wa mtu aliyekuwa ndani ya gari hiyo, Mtu huyo ni LUCKY DUBE. Na baada ya kufanya hicho walicho kifanya hawakuiba gari hiyo, bali jambo kubwa waliloliona ni kutokomea kusiko julikana. Baada ya muda Majambazi hawa wakarejea tena eneo la tukio ili kujihakikishia Je Hakukuwa na mtu aliyewaona. Kisha baada ya kujihakikishia hakuna mtu aliyewaona, wakaamua kwenda night club huko wakanywa na kugonga cheers bila hofu.

It seems normal to them

=> Mwaka 1964 ni mwaka ambao LUCKY DUBE aliingia katika vilindi vya dunia hii. Kwa majina ya Document anaitwa LUCKY PHILIP DUBE, Amezaliwa 03/08/1964 huko MPUMALANGA nchini Afrika Kusini. LUCKY DUBE ni mtoto aliyesadikika atakufa ndani ya muda mfupi tu baada ya kuzaliwa.

=> Ilikuwa ni baada ya mama wa LUCKY DUBE kupata watoto kadhaa ambao wote walifariki punde tu walipo zaliwa. Ilipofika zamu ya kujifungua LUCKY DUBE mama huyu hakumpa jina mtoto wake badala yake alimuachia Mungu na kusema.. "ikiwa utamkuza nitampa jina linalo kupendeza"

=> Mwaka Mmoja ukakatika mtoto bado anaishi, mama huyu aliona ajabu maana watoto wote walikufa siku kadhaa baada ya kuzaliwa. Mama huyu akiwa ameshakimbiwa na baba wa mtoto, ndipo alipoamua kumpatia mtoto huyu jina la kizulu la "Inhlanhla" likiwa na maana ya Bahati.

=> Inhlanhla alipoanza kujitambua, aliomba kazi ya kutunza bustani kwa wazungu.
Kazi akapata ila aliulizwa maana ya jina lake, akasema bahati mabosi zake wakamuita Lucky. Mara zote Dube alisikia akiitwa Lucky na mabosi zake, from there ikawa anajitambulisha kwa jina la Lucky.

=> Hata shule alibadilisha jina kutoka Inhlanhla na kuja Lucky. Japo maisha yakwao hayakuwa rafiki LUCKY DUBE alijitahidi kujisukuma kwenda Shule mwenyewe, sababu aliachwa na bibi yake huku mama Yake akiwa amekwenda kutafuta vibarua ndani ya jiji la DURBAN. Dube akiwa na bibi yake, alipambana mara zote ili kuhakikisha analeta kitu nyumbani.

=> Alikuwa na tabia akitoka shule anapitia kwa bosi wake, ambao ndio hao mnawaita makaburu. Siku hiyo alivyo fika kwa bosi, alishangaa anaitwa sebuleni, ni ajabu miaka hiyo mtu mweusi ulikuwa huwezi kukaa sehemu moja na wazungu zaidi hapo Afrika Kusini sababu bado walikuwa wametawaliwa na makaburu.

=> Alipofika sebuleni akaambiwa atoke, DUBE akatoka. Kisha zikapita kama dakika 10 Dube aliitwa tena aende sebuleni alipofika alionyeshwa waya mbili za umeme ambazo zilikuwa zimekatwa. Akaambiwa aishike moja na nyingine kisha akaambiwa azigusanishe, Dube alifanya ivyo kilichotokea Dube alirushwa na umeme mkali uliokuwa kwenye waya hizo, alidondoka chini kwa kishindo.

Alitweta akiitafuta pumzi huku akiwasikia kwa mbali makaburu wakimcheka na kuwaambia watoto wao. "This is how it works" Kwamba LUCKY DUBE alitumika kama mfano kwa watoto wa makaburu kujifunza jinsi umeme unavyo fanya kazi. Tokea hapo Dube aliwaona makaburu na wazungu wote duniani kama maadui, watu wabaya na wenye roho mbaya.

=> Miaka ikakatika na baadae alipata nafasi ya kujiunga kwenye kundi la Sky Way Band. Hapa alianza kuzungumzia maisha kupitia muziki. Dube akiwa ndani ya kundi hili alianza kuimba kwa kutumia Lugha ya kizulu. Maisha yakawa ndio hayo, kanisani aliimba muziki, mtaani aliimba muziki..

=> Akatoa wimbo uitwao "Zulu Soul." Na baadaye kama kundi wakaachia album yenye jina la "Baxoleleni, huku mwimbaji mkubwa akiwa ni DUBE. Hizi ni nyakati ngumu kwa LUCKY DUBE kwani japo alijiunga katika kundi hilo lakini maisha bado yalimpiga. Alijihudumia kila kitu mwenyewe na niwakati huu pia ndio wakati ambao alipaswa kumsaidia mama yake na bibi yake nyumbani. Mama alirudi nyumbani baada ya kusumbuliwa na kifua ivyo hakuweza tena kufanya vibarua, Kwa kifupi familia ikawa inamtazama LUCKY DUBE kama mboni. Licha ya matatizo mengi ya kifamilia kumzonga Dube hakuacha kujifunza muziki kila kukicha

=> Ilipofika Mwaka 1984 Dube alionekana kwenye movie ya GETTING LUCKY. Mwaka uliofuata 1985 akatoa album ya "Rastas Never Die". Hii ikawa chukizo kwa makaburu, album ikafungiwa.

=> 1986 akatoa tena album ya "Think About the Children" or "Born to suffer" Hii ikaenda na hapa taa ya Dube ilianza kuwaka. Na nyakati hizi ndizo alizohamia kwenye mji wa Johannesburg rasmi. Akawa anatoa nyimbo za ukombozi, kutetea haki za watu.

=> Kuna siku askari wa kikaburu walimvamia na kumpiga virungu bila sababu. Dube aligundua source ya kipigo hicho ni nini, alijua wazi ni nyimbo zake zinazoikosoa serikali ndio chazo cha kipigo hicho. Dube hakuacha kuimba kwa lugha laini inayoburudisha, kukosoa na kufundisha.

=> Akatoa nyimbo yake aliyoimba kwa kizulu USIZI. Ilipendwa na LUCKY DUBE taa yake ikazidi kumulika na mara hii hakutaka kabisa kutumia lugha ya kizulu katika nyimbo zake, na badala yake akatumia Lugha ya kiingereza moja kwa moja ili nyimbo zake zisikilizwe duniani kote na si Afrika Kusini pekee.

=> Mwaka 1987 akatoa album ya SLAVE yenye nyimbo kama..

~Slave
~Back to My Roots
~Oh My Son (I'm Sorry)
~Rastaman
~Let Jah Be Praised (Igzebier)
~The Hand That Giveth
~I've Got You Babe

=> Hii album alimpeleka Lucky Dube duniani, akasikilizwa na kila lika na akawa maarufu ndani ya Afrika Kusini na njee ya Afrika Kusini. Dube akabamba, akajitafuta na akajipata, uimbaji wake uliogusa maisha halisi ya watu, ulifanya asikilizwe na watu wengi kutoka pande zote. Historia Alianza kuiandika kwa kujaza watu wengi zaidi kwenye show zake. Sasa akawa anasikika zaidi katika ulimwengu wa muziki wa Reggae huku wasanii kama Peter Tosh, Bob Marley na Jimmy Cliff wakianza kupotea katika mazungumzo ya watu.

=> Kijana huyu kutoka Afrika Kusini sasa akatazamika pengine ndiye mrithi wa Bob Marley. Dube alijitengenezea utofauti fulani katika uimbaji wake. Ni zile sauti za wanawake waliosikika mara kwa mara wakiimba Choruses kwenye nyimbo za DUBE ni Wanawake watatu ambao uongozi wa Dube uliwaita "Mothers of Soweto which never sleeps" Yaani wamama wa Soweto ambao hawalali kamwe. Ni sababu wanawake hao walipohitajika studio saa na muda wowote walifika bila kukosa. Pia Dube alipokwenda kufanya show iwe nje au ndani ya nchi ni wao ndio walipangilia style za uchezaji huku wakiimba kama backing vocalist. Dube aliwaita the voices of revival Akimaanisha sauti za uamsho.

=> Kupitia "OKTV Awards" LUCKY DUBE alishinda tunzo nne kupitia album yake ya PRISONER Yenye nyimbo Kama...

~Prisoner
~Dracula
~False Prophets
~War And Crime
~Remember Me
~Don't Cry
~Jah Live
~Reggae Strong

=> DUBE hakuishia hapo, Mwaka 1991, alitembea nchi tofauti. Kupitia nyimbo zake alichukuliwa Kama mtu anayetangaza amani, upendo na kuoneana huruma Utu. Alikwenda Japan na Australia, alikuwa akihitajika kama source ya kuwaliwaza watu au ufunguzi juu ya taasisi ama tamasha la kitaifa. DUBE akaendelea kusonga mbele kwa bidii zaidi, hakika aliushangaza ulimwengu.

=> Mwaka 1992, Dube alikuwa Mwafrika Kusini wa kwanza kufanya show kwenye tamasha la Sunsplash nchini Jamaica. Wapo wa Jamaica waliosema Dube ana asili ya Jamaica huku wa Zimbabwe nao wakisema Dube ni wa kwao, kwa kudai ya kwamba wazazi wa Dube wana asili ya Zimbabwe.

=> Mwaka 1993 Dube akaja na nyimbo iliyoitwa Remember me. Akijaribu kujizungumzia yeye alivyoachwa na baba yake lakini pia hata watu wengine waliopitia malezi ya kukosa baba. Dube aliendelea kuachia nyimbo kila kukicha, ila mwishoni mwa 1993 matukio ya uhalifu yalikuwa mengi sana Afrika Kusini. Watu walikuwa wakidai uhuru dhidi ya mkaburu aliyekuwa hataki kubanduka ndani ya nchi hiyo. Ila katika kudai uhuru huo watu walipiga pesa na zaidi ni watu weusi wenyewe kwa wenyewe waliibiana na kupelekea wengine mpaka kupoteza uhai wao. Raia walimiliki silaha kiholela holela, jambo lililofanya mauaji kutokea kila kukicha. Uhalifu, madawa ya kulevya na wizi wa silaha ulitawala Afrika Kusini.

=> Tar 27-04-1994 nchi ya Afrika Kusini ilipata uhuru wake kutoka kwa mkaburu aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka mingi. Ila baada ya uhuru kupatikana, matukio ya uhalifu bado yaliendelea hayakukoma. Ndipo 31 March 1995 LUCKY DUBE akajana na album yake ya TRINITY yenye nyimbo Kama..

~Trinity
~Feel Irie
~Puppet Master
~You Got No Right
~Affirmative Action
~Big Boys Don't Cry
~Rasta Man's Prayer
~God Bless the Women
~My Brother, My Enemy

Sasa hii nyimbo ya My Brother, My Enemy, Anazungumzia maisha yake yote jinsi alivyo muona mzungu ni adui yake. Lakini baada ya kuona matukio ya mauaji kila kukicha, tena weusi kwa weusi yaani wao kwa wao, hapo akagundua kwamba hakujua hata mtu mweusi aliyehisi ni ndugu yake kumbe anaweza kumuua, au kumfanyia uhalifu. "Not every black man is my brother Not every white man is my enemy". Dube anaandika tena katika wimbo uliobeba jina la album hiyo Trinity.

=> Katika nyimbo ya Trinity Dube anaandika kwa kumuunga mkono Mandela juu ya kumsamehe mkaburu kwamba "Mkaburu baada ya kusamehewa, asilale na bunduki yake mkononi, akidhani perhaps waafrika kusini wanaweza kumvizia na kumuua, Awe na amani". Mwafrika kusini atamfuata mkaburu ili kujifunza kuhusu watu weupe na mkaburu atamfuata mwafrika kusini kujifunza kuhusu watu weusi. Dube anasisitiza we'll unite" tutaungana" kwamba licha ya yoote yaliyotokea bado wanapaswa kuwa kitu kimoja.

=> Nchi ya Afrika Kusini kwa mara ya kwanza ikapata kamishna mweusi wa Kitaifa wa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini. "First National Commissioner of the South African Police Service". Huyu ni Mzee JACOB JACKIE SELEBI maarufu kama JACKIE SELEBI. Bwana JACKIE SELEBI baada ya kushika wadhifa huo akaanza kufanya kazi yake huku akiwa chini ya Rais THABO MBEKI aliyerithi kiti cha NELSON MANDELA mwaka 1999. Lakini siku baada ya siku matukio ya uhalifu yalizidi kuendelea bila kukoma.

=> Miaka ikakatika na ilipofika mwaka 2007 yaani Siku ya tar 18/10/2007 maisha ya LUCKY DUBE yakakatizwa kwa namna ya ajabu sana. Yaani ghafla majambazi yakatokea na kummiminia risasi, kisha majambazi yakaondoka na baadaye yakarudi tena eneo la tukio eti kuhakikisha kama hayakuonekana. Perhaps hili ndilo kosa kubwa Walilolifanya majambazi hawa. Baada ya tukio kutokea taarifa zikawafikia askari kadhaa wa JOHANNESBURG ambao walikuwa ndani ya mtaa wa ROSETTENVILLE wakifanya doria. Askari hawa wa kikosi cha doria ambao miongoni mwao kulikuwa na shushushu wa Kapteni MLOKO KGOMO

=>Askari haraka wakafika eneo la tukio na kukuta gari ya LUCKY DUBE ikiwa imegonga mti huku DUBE akitazamika kwa ndani akiwa mahututi. Mawasiliano yanafanyika gari za huduma ya kwanza zinafika, Pia kapteni MLOKO KGOMO anawasili eneo la tukio kwa mwendo wa kimbunga. Taarifa hizi za yakuwa DUBE ameshambuliwa na kuuwawa zinavuruga vichwa vya asikari watiifu. Ni wakati huu pia anafika Inspector MICHAEL MUNGADI akiambatana na Kapteni HJ BLIGNAUT,

=> Huyu kapteni HJ BLIGNAUT ni mtaalamu wa vifaa vya ulipuzi, yaani "Ballistics expert" Perhaps ninakuchanganya Ninaposema Ballistics expert. Namaanisha mtaalam wa vifaa vya ulipuzi na bunduki, mara nyingi hawa wataalam huchunguza sampuli kama maganda ya risasi au mabaki yoyote ya baruti ambayo yanaweza kutua pembezoni mwa tukio. Huchunguza vumbi, hatua za miguu, damu, risasi na wakati mwingine huchora michoro eneo la tukio ili kuendelea kudadavua tukio na kupata ushahidi.

=> Jambo kubwa Unalopaswa kufahamu "Ballistics expert" huwa hawi pekeake hufuatana na watu kadhaa ambao humsaidia katika kuchakata taarifa za ushahidi, kati ya watu hao mpiga picha ni muhimu sana, huyu mpiga picha wa matukio ya kihalifu kitaalam tunamuita "FORENSIC PHOTOGRAPHY. FORENSIC PHOTOGRAPHY kazi yake kubwa ni kupiga picha vitu, mwili, bastola, damu, risasi, kisu, au silaha yoyote itakayokutwa eneo la tukio. Huyu husaidia hata wakitoka eneo la tukio, uchunguzi utaendelea maabara kwa kutumia picha zilizopigwa na yeye lakini pia na sampuli zilizochukuliwa na BALLISTICS EXPERT

=> Kupitia Sampuli zilizochukuliwa eneo la tukio, silaha, picha na michoro BALLISTICS EXPERT na team yake wataweza kulisaidia vyema jeshi la polisi na mahakama kugundua namna uhalifu ulivyo fanyika. Sasa ili mambo yasiwe mengi wewe elewa tu Kapteni HJ BLIGNAUT, ndio huyo Ballistics expert ivyo huyu na team yake ni muhimu sana katika tukio hili.

=> Baada ya kufika eneo la tukio askari wa doria wakakutwa wamesha tanda eneo hilo kapteni MLOKO KGOMO, Inspector MICHAEL MUNGADI na Kapteni HJ BLIGNAUT na watu wa huduma ya kwanza kwa pamoja walipatwa na bumbuwazi baada ya kuona mtu aliye ndani ya gari hiyo ni kweli ni LUCKY DUBE. Wakiwa katika mshangao huo, mara watu wa huduma ya kwanza wakavaa vitendea kazi vyao na kuanza kazi yao ya kupigania uhai wa LUCKY DUBE ama kunga'amua je ni kweli amekufa au bado anaishi.

=> Wakati huu Kapteni HJ BLIGNAUT anatazama kwa makini mwili wa Lucky Dube na kugundua alikuwa na jereha kubwa eneo la paja mguu wake wa kulia. Nyakati hizi Kapteni HJ BLIGNAUT alizunguuka zunguuka tu kama mtu aliyekuwa anasubiri kupatiwa agizo fulani au taarifa fulani. Alitembea akiizunguuka gari ya DUBE huku jicho lake likiwa pale kwa watuoa huduma ya kwanza walio onekana kufanya kazi yao kwa juhudi ili kuupigania uhai wa LUCKY DUBE. Kwa haraka sana Kapteni HJ BLIGNAUT anagundua gari ya DUBE haikuwa na tundu la risasi kwa njee.

=> Ni wakati huu pia kapteni MLOKO KGOMO Anaamua kuwatawanya vijana wake, waliovaa sare za polisi waendelee na doria kwa maana wahalifu huenda hawako mbali. Kisha wachache waliovaa nguo za kiraia aliwaambia wabaki eneo la tukio wakae kwa umbali fulani ili kuchunguza Yeyote anayepita mitaa hiyo, ama kusikiliza raia wanasema nini juu ya tukio hilo.

=> Vijana hawa walio pewa kazi ya ushushushu wakaanza kazi yao kwa kujichanganya na rai huku wengine, wakipoz migahawa ya karibu kwa kupata Juice na story 2/3 Wakati huo kapteni MLOKO KGOMO Anashirikiana na watu wa huduma ya kwanza kuendelea kutetea uhai wa LUCKY DUBE lakini kwa bahati mbaya watoa huduma wanasema.. DUBE alishafariki. Hili linamuumiza kichwa kapteni MLOKO KGOMO anapata kiu ya kutaka kufahamu namna tukio lilivyo tokea. Watu wa huduma ya kwanza na askari kadhaa wanaruhusiwa waende Hospital na mwili wa LUCKY DUBE. Kisha kapteni MLOKO KGOMO akabaki na Kapteni HJ BLIGNAUT na Inspector MICHAEL MUNGADI kwa kuchunguza sampuli zinazoweza kuwafikisha kwa wahalifu wa tukio hili.

Uchunguzi ukaanza

=> Kapteni MLOKO KGOMO kwa mahojiano aliyoyafanya harakaharaka na majirani wa eneo hili. Akagundua kabla ya tukio kutokea marehemu Dube alikuwa ametoka kuwaacha watoto wake kwa mjomba wao, ivyo baada ya kutoka kuwaacha watoto, umbali kadhaa tu Dube akavamiwa na kufanyiwa unyama huo. Ndugu wa Lucky Dube ambaye alitoka kuachiwa watoto alisemaa "Nilisikia milio ya risasi nikiwa ndani na watoto, mara watu wakaja kusema ndugu yako amevamiwa na majambazi. ninashangaa hawakuiba chochote" Maelezo haya Yaliyojawa na simanzi kwa ndugu huyu wa Lucky Dube yalimfanya kapteni MLOKO KGOMO akapata huzuni kwa muda.

=> Wakati huu Inspector MICHAEL MUNGADI na kapteni HJ BLIGNAUT walikuwa na kazi ya kuichunguza gari ya marehemu LUCKY DUBE. kapteni HJ BLIGNAUT alifanikiwa kugundua alama za miguu zilizo onekana kukanyaga chini, miguu hii ilitembea umbali fulanii kisha ikaishia kwenye matairi ya gari. Hii inaleta maana perhaps aliyefanya uhalifu huu punde tu alipomaliza alikwenda kupanda gari iliyokuwa ikimsubiri na kutimka zake. Lakini zaidi alikuta risasi kwenye seat ya mbele ya gari, pia sanduku la cartridge kwenye seat ya nyuma.

=> Ninaposema sanduku la cartridge namaanisha Cartridge box yaani kiifadhio cha risasi Sasa Risasi na sanduku la Cartridge zilitazamika kuendana na bastola aina ya Glock19 Lakini kitu kingine alichokuja kugundua kapteni HJ BLIGNAUT ni kwamba. Huenda mtu aliyempiga risasi LUCKY DUBE alikuwa ndani ya gari na alipiga kutokea seat ya nyuma.

=> Why amegundua hili? kapteni HJ BLIGNAUT alikumbuka wakati anautazama mwili wa DUBE aliona jeraha kubwa kwenye paja la mguu wa kulia wa LUCKY DUBE, sasa hapa kapteni HJ BLIGNAUT akaanza kuhisi huenda mtu huyu aliingia ndani ya gari na kufanya uhalifu huo akiwa ndani. Pia akagundua gari ya DUBE ilikuwa na mikwaruzo kwenye dashboard na tundu la risasi chini ya seat ya dereva na pia akagundua hakukuwa na tundu lolote la risasi kwenye vioo vya gari hiyo. Hii ikamfanya a-connect dots na ikazidi kumuongezea udadisi wa kufikiri kwamba mtu aliyempiga risasi LUCKY DUBE, alikuwa ndani ya gari na alipiga kutokea seat ya nyuma. kapteni HJ BLIGNAUT akiwa kama Ballistics expert baada ya kugundua yote haya, yeye na Inspector MICHAEL MUNGADI pamoja na kapteni MLOKO KGOMO.

=> Walitoka na ushahidi kama Risasi alama za nyayo za miguu na sanduku la kuifadhia risasi "cartridge box" na fingerprint za Ndani na nje ya gari hiyo zaidi kwenye milango ya gari. Hivyo baada ya kuvipata vyote hivi na sampuli tofauti, makamanda hawa wakatoka eneo la tukio na kwenda straight mpaka kwenye maabara ya uchunguzi huko Pretoria. Ni muda huu sasa anaonekana kijana mmoja mwenye kugeuka huku na kule, akiwa ndani ya gari moja iliyopaki karibu na eneo la tukio.

=> Kijana huyu alionekana ni mwenye wasiwasi sababu mara zote hakutulia ndani ya gari aligeuka kushoto na kulia nyuma na mbele. Mara ghafla wanakuja vijana wengine wa3 mmoja anaingia kwenye gari ya kijana huyu aliyeonekana kuwa na wasiwasi na wengine wawili wanaingia kwenye gari iliyopaki karibu kisha gari zinawashwa na safari inaanza ya kwenda huko walikokujua wao.

=> Mionekano yao ya sura, mavazi na styles za utembeaji wao, zinakuwa kivutio kwa mashushushu walio tega mitego yao katika mtaa huu wa ROSETTENVILLE. Mashushushu wawili wanavutika na kuanza kuwafuatilia vijana hawa Gari zinakwenda mpaka kwenye night club moja kisha vijana hawa wanatelemka na kuingia ndani ya Club hiyo. Lakini punde anatoka kijana mmoja ambaye alikuwa ni dereva wa gari moja kati ya zile mbili. Kijana huyu aliingia ndani ya gari akiwa pekeake na kuanza safari ya kwenda huko ailipopajua yeye..

=> Mashushushu hawa wawili wakamua kujigawa mmoja akamfuatilia yule kijana na mwingine akabaki eneo la Club. Wakati huu kapteni HJ BLIGNAUT, kapteni MLOKO KGOMO na Inspector MICHAEL MUNGADI wakiwa eneo la maabara Wanapokea simu kutoka kwa mashushushu wao, kuna vijana wameonekana wanavutia kuwadadisi. Makamanda wanawakumbusha mashushushu wao, kwamba ukivutwa jivute. Wakimaanisha wasipuuzie mvuto huo, kwa maana waendelee kuwadadisi vijana hao.

=> Siku ya Tar 19/10/2007 Yaani siku iloyofuata baada ya tukio, Ndani ya Jijini JOHANNESBURG majira ya mchana, watu wakiwa wanapata Chakula na wengine kupiga soga mbili tatu. Ndipo wanasikia taarifa zinazopenya masikioni mwao na kufanya umakini wao wa kusikiliza uhamie katika Kusikiliza taarifa hiyo. Ilikuwa ni baada ya msemaji wa jeshi la polisi aliyefahamika kwa jina la Kapteni CHERYL ENGELBRECHT kuja kwenye vyombo vya habari na kusema.

"Tunasikitika kusema kwamba LUCKY PHILIP DUBE ambaye ni msanii wa music amefariki dunia jana usiku baada ya kuvamiwa na majambazi punde tu alipotoka kuwaacha watoto wake kwa mtu aliyefahamika kuwa ni mjomba wao" Taarifa hii inavuma na kusambaa ndani ya SA na nje ya SA, africa na duniani kote.

=> Mpaka sasa ni mimi na wewe tu! na ndugu wa karibu wa DUBE na majirani wa mitaa ya ROSETTENVILLE na wale wa SUBURB ndio tulikuwa tunajua kuwa LUCKY DUBE amefariki dunia Ila baada ya Kapteni CHERYL ENGELBRECHT kutoa taarifa hii, Afrika na dunia ikajua na waafrika kusini wenyewe ni kama walimwagiwa upupu. Vyama vya siasa navyo vikapata neno la kuongea juu ya utawala mbovu ulioko madarakani Yakwamba utawala ulioko madarakani ni wa rushwa, biashara chafu na Magendo yote unayoyajua wewe.

=> Hili likamfikia Raisi wa nchi THABO MBEKI na kuja kwenye vyombo vya habari na kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya LUCKY DUBE lakini ni Kama alikuwa anatupa jiwe gizani Yakwamba, THABO MBEKI alisema... Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mwanamuziki huyu, ni ndugu yetu hichi ni kifo cha Mwafrika Kusini mwenzetu Ni mashuhuri na kwa hakika tuweke ahadi kwamba, tutaendelea kuwa pamoja kama watu ili kukabiliana na janga hili baya la uhalifu. Na sio kuchochea chuki bali, tutangaze amini na upendo kama alivyo yaishi maisha yake LUCKY DUBE." Haya yalikuwa ni maneno ya Rais wa Afrika kusini THABO MBEKI.

=> Licha ya Rais kuzungumza lakini bado hii siku watu waliendelea kupaza sauti juu ya Utawala mbovu wa THABO MBEKI Wakati huu wote kapteni HJ BLIGNAUT, kapteni MLOKO KGOMO na Inspector MICHAEL MUNGADI walikuwa wanaendelea kuchakata Sampuli lakini fingerprint ziligoma kuonekana kapteni HJ BLIGNAUT alirudi tena eneo la tukio akachukua fingerprint na hizi zikapatikana vyema Zege halilali... Jioni ya siku hii mashushushu wanatoa taarifa kuwa kuna wanandoa wawili wanaonekana kunasa kwenye mfumo wa udadisi wanandoa hawa MPHO MONARENG na THABO MONARENG wanakamwatwa katikati ya jiji la JOHANNESBURG. I've no doubt perhaps haya ni matunda ya mashushushu wale wa usiku uliopita.

=> Baada ya watu hawa kushukiwa kuwa wanahusika na tukio la mauaji ya LUCKY DUBE walikabidhiwa kwa kapteni MLOKO KGOMO kwa mahojiano zaidi.. Sasa hapa Bwana THABO na mkewe MPHO walitaka kuwa wazito kutoa maelezo yaliyonyooka. Hapa ndio walimjua kapteni MLOKO KGOMO na kikosi chake. Akachukuliwa MPHO akapelekwa kwa askari wakike na THABO akapelekwa kwa askari wa kiume kisha wote wakaingizwa kwenye vyumba Kilichoendelea huko, Ni wao wenyewe ndio walijua ila walipokutana kwa pamoja wote walitazamana na kulia.

=> Baada ya hapo wakanyoosha maelezo na hapo ndipo THABO MONARENG alisema yeye alipewa kazi ya kuendesha gari na watu wa3 ambao ni S'FISO MHLANGA, MBUTI MABE na JULIUS GXOWA. Kwamba Ile siku kabla ya tukio mchana wake alipigiwa simu na Rafiki yake MBUTI MABE kwamba kuna kazi ya kuendesha gari. Akiwa kama dereva alikubali.. Na Jioni ya siku hiyo MBUTI alikuja na watu wengine wawili na kudai ni marafiki zake ambao walipaswa kwenda pamoja mitaa ya ROSETTENVILLE huko kuna gari wanatakiwa kwenda kuinunua.

=> Walikwenda na walipofika mitaa hiyo ya ROSETTENVILLE, THABO akaambiwa apaki gari pembeni. Wakiwa hapo ghafla aliwaona S'FISO MHLANGA na JULIUS GXOWA wakitelemka na kusimama kandokando ya barabara. Mara kuna gari aina ya CHRYSLER 300c. ilionekana kukatiza barabara hiyo, MHLANGA na GXOWA wakaisimamisha gari hiyo kisha mazungumzo machache yakafanyika..👇

=> Mwisho MHLANGA na GXOWA wanaingia ndani ya gari hiyo na hapo ndipo milio miwili ya risasi inasikika ndani ya gari hiyo. Kisha MHLANGA na GXOWA wanatoka njee ya gari na kurudi walipopaki kina THABO, wakiwa wanahisi wamesha kamilisha azima yao ya mauaji.

=> Ghafla wanashtushwa We want to know everything, regarding the truth of LUCKY DUBE's death.


CREDIT: Wisdomjaykwa #wisdomjaykwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom