Wanawake tuache kujioa, maisha mengine yanawezekana pia

Wanawake tuache kujioa, maisha mengine yanawezekana pia

Umeamini wanaume hamna akili, utu, na mna roho mbaya sana??

ww vp hebu futa kauli yako. Sema baadhi ya wanaume haa! Sijui umekula maharage ya wapi ww.

Lakn huyo jamaa mwache ajifanye mjanja ipo sku hayo machozi ya mwanamke aliyemtelekeza yatamrudia.

Bidada hakuwa na lengo baya wala sio kwamba alijipendekeza bali n mapenz ya kweli kwa jamaa.

Kama huyu jamaa hakuwa tayar kuishi naye kwann alikubali kumtia hasara kiivyo?
 
Hapo analia na mengi ujue. Unawaza una limkopo, kodi, chakula + ulee watoto wawili. Bora hata asingekuwa na hilo deni maskini, ila Mungu yupo tu.

Sasa unadhani huyo mkaka angeweza kusema kuwa hamtaki? Thubutuu si anajua anahudumiwa bure, alikuwa anamtumia tu ili hadi asimame amtose dada wa watu. Mungu ampiganie tu huyo dada maskini

sasa km alikua hamtak aliruhusu vipi wafunge harusi??alikua haoni wakat mwenzake anakopa hela? km angekua kwel mwanaume na anataka kulelewa ange'buy' time mambo yakae sawa ndo amwache kulkua hakuna ulazima wa kufunga nae harusi...

huyu obviously ni mwanaume mvulana,,,hana maturity decision making!! akikua lazima atajutia hiko kitendo!! adhabu ya dhambi ni hapa hapa duniani
 
Lakini nazo social zinaongezea stress Za wadada kutaka kuolewa kwa nguvu: ukienda fb wanaongelea wanawake kuolewa, ukiingia jf wanasema over 30 magume gume, ukiangalia the comedy utasikia masanja anawasema hao hao wasiolewa.

Kama nimeuelewa vizuri Uzi,Dada hakulazimisha. Kujilipia mahari sio kigezo cha Ku force ndoa,pengine alimpenda sana mwanaume na si ajabu walikubaliana. Kilichotokea ni bahati mbaya tu,as hakuna mtu anaeweza kuwa fate teller wa maisha yake mwenyewe.
 
Pole zimfikie huyo dada..ila suala la pressure ya kuolewa kwa wadada ni tatizo kubwa nimegundua sio hapa kwetu tu mpaka nchi za wenzetu..mi ni mpenzi wa movie za kikorea na ukiangalia movie zao nyingi mwanamke asiye olewa au aliyeachwa anadharaulika sana, siku hii mindset ya heshima ya mwanamke ni ndoa itapokuja kupungua itakuwa afadhali kwa kweli....na huyo kaka mwache tu what goes around comes around
 
Kama nimeuelewa vizuri Uzi,Dada hakulazimisha. Kujilipia mahari sio kigezo cha Ku force ndoa,pengine alimpenda sana mwanaume na si ajabu walikubaliana. Kilichotokea ni bahati mbaya tu,as hakuna mtu anaeweza kuwa fate teller wa maisha yake mwenyewe.

tena jamaa alipata mwanamke mwema sana. Kitendo cha mwanamke kuchomoa pesa yake kwaajili ya mwanaume huyo ni wakumheshim. Ningekuwa mm hata kama sikumpenda ningeilazimisha nafsi ingempenda tu....

Maana wanawake wa siku hizi kubabake duuh!
Mda wote wanawaza kukupiga mizinga tu yaan ni majambaz sugu yasiyotumia bunduki wala jambia ila yanatumia tabasam feki na love fake..

Huyo jamaa kuna chamoto kipo mbele yake lakn yeye hajakishtukia tu.
 
Pole yake wajamini duh ngumu kumeza hata kwa kusukumia na maji,bora nijizeeke kwetu kuliko kukutana na vimbwanga kama hivi.

Mwambie apambane hivyo mdogo mdogo atachomoka kimaisha, juhudi zake alizozionyesha kutafuta mahari azifanye na sasa asibweteke. Mungu amfanikishe
 
Okay alikosea, lakini she should teach that lunatic a lesson. Like how could she let it pass just like that?
Go burn that house down
 
Me ni mwanaume lakini huyo mume wa huyo Dada anamtindio wa akili na ni aina ya wale wanaume marioz
 
Huyu dada mwenye mtoto mmoja na mimba ya miezi 6, dada huyu kabla hawajafunga ndoa mmewe alikuwa hayupo vizuri kipesa, kutokana na hilo suala la ndoa lilikuwa linapigwa danadana siku hadi siku, kwakua bidada alikuwa anafanya kazi akaamua kuchukua mkop kazini kwake, akampa kiasi bwana yule akamlipie mahari, na nyingine yakuanzishia vikao, kweli mambo ya yakaenda bidada akajigharamia kila kitu hadi pete alinunua yeye.

Baada ya ndoa bidada akabeba mimba ya kwanza akazaa, na mwaka huo ndio mbwembwe zilianza, bidada akikosea kidogo tu, mwanaume anamwambia "kwanza wewe ulinilazimisha kukuoa ndio maana ulijitolea mahari" mwanaume harudi nyumbani hata siku tatu, bidada anavumilia tu, akashika mimba nyingine ina miezi 6 sasa, mwezi uliopita bidada kagundua mwanaume amejenga mbezi mwisho baada yakupekua msg za mmewe, hapo wao wamepanga, akamuuliza mwanaume akamwambia "kweli nimemjengea .......yule ndio chaguo langu. bwana ndani ya wiki kabeba nguo zake kahamia huko makao mapya.

Mwanamke kaachwa na na mtoto na mimba na deni juu la mkopo, analia anatamani kujiua, anahangaika basi atoe mimba ili abaki na mtoto mmoja.

  • Wadada usikimbilie kuolewa tu kwasababu mtaani watu wanaolewa, olewa kwasababu umepata mtu sahihi wakuishi nae, ambaye anafurahi uwepo wako moyoni mwake.

Waambie pia waache kutubambikia mimba ili tuwaoe!!
 
Duuuhh, napenda kumpa POLE huyu dada kwa yale yaliyompata. Ni kipindi kigumu anapitia na kwa kweli anahitaji faraja kutoka kwa watu wa karibu ili aendelee kujiona wa thamani.

Kila siku nasema "SISI WAAFRIKA" tunaishi kwa unafiki. Siku tukikubali kuuweka unafiki pembeni, tutayabadili maisha na kuufanya ulimwengu huu kuwa sehemu salama zaidi ya kuishi.

Kila Mara najiuliza hivi kuongezeka kwa "nyumba" za ibada kila uchwao tafsiri yake nini? Mbona miaka ya nyuma wakati itikadi kali za kiimani hazijashamiri mbona watu walikuwa waungwana kwa maneno na matendo.
NB:Wengi wetu humu ni wazazi/walezi, hebu tuwalee watoto wetu waje kuwa fahari ya jamii na Taifa na sio karaha kwa wengine.
 
Well said...
 
hamna dhambi kubwa kama kutunza mwanaume, mwanaune yoyote ukimtunza lazima akugeuke chunguza vyema

Sio kweli kabisaa mamiii...
Watu wanatofautiana saana, mtunze mtu anaekupenda kwa dhati na sio yule ambae unalazimisha kumpenda huyu atakuliza tuuu.....

Acha kugenerelarize
 
Lakini nazo social zinaongezea stress Za wadada kutaka kuolewa kwa nguvu: ukienda fb wanaongelea wanawake kuolewa, ukiingia jf wanasema over 30 magume gume, ukiangalia the comedy utasikia masanja anawasema hao hao wasiolewa.

Kamwe usikubali kuolewa kwa pressure za umri, za wazazi,za social netwok

Lazima usubiri paka muda ambao mungu ameupanga uolewe

Ni lazima uvishinde vishawishi hivi ili uweze kufanya maaamuzi sahihi,

Usiogope kubezwa kwa aina yeyote, wanaokubeza hawatakuwepo siku ukiwa unaonja shubiri za ndoa mbovu
 
Umeongea kweli tupu, namjua dada mmoja alikua amewatunza Ma boy friend kila Mala aliangua pua. Alikua anawaweka mjini, kuchangia ada ya kidume, kuchangia pesa ya kula chuo. Mwisho wa siku walimuacha kwenye mataaa

Kwani kumchangia pesa ndio lazima akuoe? Kama unatabia mbovu alafu unajificha kwenye kumchangia pesa utaishia kulalamika

Kuna sababu nyingne za mtu kumuoa mtu, sio tuu kunilipia au kunihonga

Acheni kujidanganya
 
Wanaume sisi sometimes tunajibebe laaana za kujitakia huyo nae aliz kupenda umarioo

Pole sana mdada wakat mgumu sana kwako huuu
 
Back
Top Bottom